SoC03 Kwa mazoea haya tutatokomeza UKIMWI?

Stories of Change - 2023 Competition

Himbos

New Member
Jul 19, 2023
1
0
Tangu kuingia kwa ugonjwa wa ukimwi mwanzoni mwa miaka ya 80 harakati za kupambana na ugonjwa huu ni kubwa na mapambano yanaongezeka kasi kadri miaka inavyoenda. Ukweli ulio mchungu mpaka hii leo ugonjwa huu hauna dawa, na ulivyoingia ulipukutisha watu maana hakukuwa na kizuizi chochote wengi walikufa kwa Ukimwi na hata watoto wasio na hatia waliupata kupitia kwa wazazi wao ,na hata namna ya kuwauguza wapendwa wetu ilikuwa ni ngumu ,unyanyapaa ulikuwa wa hali ya juu na wengine waliambukizwa bila kujua ama hakika hii leo kila mmoja ameguswa na ugonjwa huu kwa kuondokewa na ndugu jamaa au marafiki.
1690156204813.png



Kubwa la kushukuru leo hii kuna njia nyingi za kupambana na ugonjwa huu ikiwemo matumizi ya dawa za kufubaza virus vya ukimwi ARVs ,Kondom .n.k.

1690157026135.png

1690157246349.png

Mapambano ya kutoambukizwa virus vya ukimwi yamekuwa kukuru kakara kila mmoja anapambana kwa imani yake na uelewa wake,kinachonisikitisha ni mazoea ,ugonjwa umezoeleka miaka isiyopungua 40 sasa sio mchezo hivyo mazoea ya KUPAMBANA na ugonjwa huu yanatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwa tangu uingie nchini Una muda mrefu na dawa wala chanjo haijapatika tuangalie Aina za mazoea katika KUPAMBANA na maambukizi ya VVU.

1-UPAKAJI WA MAFUTA KWA IMANI YA KUTOPATA VIRUS VYA UKIMWI

Idadi kubwa ya vijana wana msemo kuwa "pipi na maganda yake haina ladha" yaani kufanya ngono na kondom hakuna utamu ,wengine wanasema raha ya tendo ni nyama kwa nyama hivyo hawavutiwi na utumiaji wa kondom , wao wanaamini katika kupaka mafuta sehemu za siri wakati wa tendo kwa kuwa kutakuwa na utelezi kipindi wakifanya ngono na hakutakuwa na michubuko kwa maana hiyo watakuwa salama dhidi ya maambukizi ya vvu .KUNDI HILI LA VIJANA HAWAPIMI AFYA ZAO NA NJIA YAO YA KUJIKINGA NI KUPAKA MAFUTA WAKATI WAKUFANYA NGONO.Mazoea haya tutaotokomeza UKIMWI 2030.

UUZWAJI WA VIFAA VYA KUJIPIMA VVU.
Ukienda Duka la dawa za binadamu yapo maduka ambayo wanauza kifaa cha KUJIPIMA VVU na uuzwaji huu ni wa usiri na wengine uhifadhi vifaa hivi stoo nimekuwa shuhuda katika hili Kwa utafiti niliofanya katika baadhi ya maduka maeneo ya buza Dsm ..."dada hizi kipimo sio matangazo unataka lete 5000 nikupe"
yapo madhara ya mtu kununua na kisha KUJIPIMA mwenyewe wako wanaopata sonono,wapo wanaweza hata kujidhuru na wapo wataoamua kuusambaza na ni rahisi kuusambaza Kwa sababu hawatumii ARVs .Nakabla ya kuamua kununua kifaa hiki wengi wao wanakuwa wanakhofu ya kutokana na rafu walizocheza mwingine anahofia kutumia vidonge vya ARVs zipo sababu nyingi lakini je kwanini kifaa hiki kiuzwe ikiwa kuna athari..maana wengi wao hawana ujuzi WA KUJIPIMA wanapata matokeo HASI kumbe wapo CHANYA.Kwa Mazoea haya tutaotokomeza UKIMWI 2030?
3-KUAMINI DAWA ZA MITISHAMBA KUTIBU UKIMWI.

Tunaamini katika tiba ya miti shamba na hii inatokana wazee wametumia Sana miti shamba lakini zama zimebadilika ni wazi yapo maradhi hizi dawa haziwezi KUTIBU ikiwemo VVU na UKIMWI. Lakini cha kusitikisha wapo wanaocha kutumia ARVs wakiamini au kuaminishwa kuwa VVU vitaisha na watakuwa sio waathirika tena
Lakini hawa wauzaji wapo na wanajinadi kuwa dawa zao ni nzuri .kwanini mpaka Leo hii bado watu hawana elimu ya kutosha kuwa dawa sahihi ni za kufubaza vvu na si vinginevyo. KWA MAZOEA HAYA TUTAOTOKOMEZA UKIMWI 2030?

MAOMBI YANAPONYESHA VVU NA UKIMWI
Leo hii kuna nyumba za ibada nyingi ambazo kila mmoja ananamna ya kuvuta wafuasi wake kujaa katika nyumba ya ibada ,sasa kuna hawa ambao wanawaombea na kuwaaminisha kuwa Maombi yanatoka vvu HIVYO waache kutumia dawa za ARVs ,nilimzika bint mmoja aliyezaliwa na vvu ambaye yeye aliacha kutumiwa dawa baada ya kuambiwa maombi ya yametoa vvu katika mwili wake masikini aliumwaa mpaka ikawa haiwezekani tena kuinuka na akafariki ilihali alikuwa anatumia ARVs Kwa miaka 30. hawa watu wapo na matangazo yapo na utasikia shuhuda za watu wakisema walikuwa na VVU na sasa hawana, WAHUSIKA WADHIBITINI KWANI HAMZIONI ATHARI ZAKE... JE KWA MAZOEA HAYA TUTAUTOKOMEZA UKIMWI 2030?
Ukweli ulio mchungu mapambano ya kutokomeza UKIMWI 2030 yatokomeze mazoea HAYA isije kuwa BIASHARA kichaa 2030 sio mbali.

Himbos
0684695698
Picha zote za mitandaoni
 
Back
Top Bottom