Kwa matatizo ya gari

tairi likikaa wiki mbili linaisha kidogo, ila nikipeleka kwa wa pancha hawaioni
 
Habari za leo kaka,
Sio kawaida au rahisi stabilizer bar kukatika. Kazi yake hua kuzuia kunesa kwa upande mmoja kama pale ukipiga kona ukiwa kasi kidogo. Yaonekana suspension yako iko na tatizo hasa kw shox, arms za upande wa chini au zile links zilizowekwa hazifai.
Gari lako umeweka spacers kw shox?
Ok mkuu nitajaribu kubadili suspension,kuhusu arms na links nilibadili asante kwa ushauri ulionipa
 
Hali kaka,
Pole kw masaibu ya gari.
Tatizo kweli lipo kw mfumo wa oili lakini sidhani ni issue na pump. Engine yenyewe imewekwa pump inayokidhi mahitaji yake. Oili ndio nadhan inakua nyepesi ikipasha joto. Jaribu kutumia oili ya Total Quartz 9000 ya synthetic.
Mimi ninagari aina ya passo yenye piston tatu .Hii gari inatatizo lakuwasha taa ya oil pindi nikisafili safari ndefu kwamfano kutoka wilayani adi mkoan .Na sana San nikiwa na mzigo au nikiwa nimepakiza watu .Nakumbuka niliipeleka garage wakaangalia baadhi ya matatizo pamoja na samplo na pia wakaisafisha oil pump lakin bado tatizo likawa ni lile lile .Nikashauliwa na mafundi ninunue oil pump mpya ya iyo passo lakin kwa bahat mbaya nilitafuta bila mafanikio lakin nikabahatika kununua oil pump used .Na walipo iweka ile used kidogo tatizo likapungua kwa safari za mtaani ikawa pow lakin kwa safari za mbali ikawa vile vile so mpaka Leo siwez safiri safar ndefu naishia wilayan tu na bado sijapata solution japo service nafanyia vizur tu
 
Toyota rav4 j, gari yangu inakula sana mafuta yaani nisaidie kitaalamu nifanyaje
 
habari mkuu, naweza badilisha mfumo wa 4WD ya Mahindra kwenda Toyota/Nissan?
Safi kaka,
Naomba ufafanue kidogo; gari ni mahindra waibadili mfumo au mfumo wa mahindra ndio wataka weka kwingine?
 
Mkuu nimesoma uzi wako, hakika una knowledge ya magari. Hongera pia kwa elimu hii.

Ningependa kujua, air filter inabadilishwa baada ya mda gani? Maana kila service inapofanyika huwa inapulizwa kutoa vumbi tu lakini sijawahi kuambiwa niibadilishe. Je, kama air filter ni mbovu, inasababisha ulaji wa mafuta uongezeke zaidi ya kawaida?
 
Asante kaka.
Air filter ubadilishwa wakati wa service hasaa huku kwetu ambako vumbi ni tele. Yakaa fundi wako ana false-economy, gharama ya filter anayokwepa unailipa maradufu kw mafuta na pia kuchosha engine yako. Ni kweli ikiziba husababisha unywaji zaidi wa mafuta.

Asante kiongozi,
Kwa hiyo kila service ni lazima air filter ibadilishwe?
 
Nisaidie kutofautisha hiace engine ya 1TR na 2RZ na Ipi ni bora katika biashara ya hiace.
 
Asante kiongozi,
Kwa hiyo kila service ni lazima air filter ibadilishwe?
Inategemea, kama mazingira ni ya mashambani kw barabara za vimbi hapo basi ni vyema kuibadilisha kila service. Kama ni mjini hasaa wakati wa mvua au hakuna vumbi sana, waeza enda kama service tatu na ile ile lakini lazima uiangalie kama imekolea na kuipuliza mara kw mara sio wakati wa service tu.
 
Asante kw swali kaka,
Kwanza ni vyema kuzielewa hizi engine vizuri ili kuweza kufanya uamuzi wa busara.
Engine ya 2RZ ni ya kale kiasi na teknolojia yake sio ya kisasa sana - kw Kiingereza sio advanced ! Ikiwa 2RZ-E au 2RZ-FE, inatumia mfumo wa injection kutema mafuta na sio carburetor kama kw 2RZ. Muundo wake sio wa kukanganya sababu inatumia valve mbili kw kila cylinder na camshaft moja; wakati wa overhaul fundi anayestahili hilo jina hawezi shindwa na lolote.
Engine ya 1TR ni mpya kiasi na ina teknolojia kadha za kisasa ili kuniufaisha kw nguvu na unywaji mafuta. Mfumo wake wa valve (valvetrain) hutumia VVTi; hapa kuna maana valve timing yake itakua mbinde kw wengi wanaovaa overall.
Gari au machine yeyote imeundwa kuchapa kazi, la msingi ni mkono unaoitumia ni wa kuiua au kuitunza. Kama utampa dereva anayeitunza gari kama yake, bila shaka engine yeyote itakupa service nzuri zaidi ile ya kisasa yenye consumption na power nzuri sababu ya design na mifumo yake. Gharama za marekebisho na matunzo pia ni swala la kuzingatia.
Tafakari hili; oili ya synthetic ni ghali kuliko ile ya kawaida ila yaenda mara mbili au tatu zaidi ya kawaida, kuna hasara pale kweli!
Nisaidie kutofautisha hiace engine ya 1TR na 2RZ na Ipi ni bora katika biashara ya hiace.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mkuu naelekea hatua za mwisho kujichanga natamani niagize crown athlete siku za usoni unaweza nipa abc kuhusu hiyo ndinga ili nifanye maamuzi yaliyosahihi
 
Mkuu naelekea hatua za mwisho kujichanga natamani niagize crown athlete siku za usoni unaweza nipa abc kuhusu hiyo ndinga ili nifanye maamuzi yaliyosahihi
Asante kw swali kaka,
Uamuzi mzuri huo!
Toyota Crown Athlete ni dinga poa sana ya daraja la executive models. Engine yake ni ya piston sita na inauwezo tosha wa kuibeba ile body kw kasi/nguvu inayofaa. Engine za sasa hazina issue kibao ila makini kw matunzo, spare na matumizi. Hakikisha oil ni synthetic pekee, spare ni genuine na fundi anaielewa gari na mifumo ya kisasa.
Sehemu nyingine ya kutunza ni interior, yaani ndani ya gari. Hazina maana ununue gari executive lakini waitumia kwenda kisimani, sokoni na kuikodisha kama taxi au kw harusi! Utaichukia mapema. Carwash pia kua makini, isiingie maji ndani hata kijiko kimoja, itavunda sana na kuisha starehe.
Magurudumu hakikisha yafanana, yaani identical type, size na tread. Alignment na balancing peleka kw aliye na computerized machine na gari utaweza achilia msukani kw speed ya mia arobaini na ikaenda true kama mshale.
Ukikosa faatilia yote hakikisha issue ya matunzo, fundi na spare umezingatia.
 
IST hua nikiwa kwenye folen/nkipunguza mwendo sana mara nyngin inajizima na nikiwasha inawaka vzur naendelea na safar. Tatzo nn mtaalam wetu?
 
IST hua nikiwa kwenye folen/nkipunguza mwendo sana mara nyngin inajizima na nikiwasha inawaka vzur naendelea na safar. Tatzo nn mtaalam wetu?
Hili litakua tatizo upande wa umeme hasa kw mfumo wa engine idle stabilization. Itakua vyema ukifanya tune-up ya uhakika na pia diagnosis ya engine, gearbox na mfumo wa umeme in general.
 
Back
Top Bottom