Je, kuinuka kwa mbinu za kisaikolojia kunagusa mzizi wa matatizo yetu?

Nov 2, 2023
60
50
Maisha ya zamani haya kuwa na mambo mengi ya kuwachanganya akili waishio. Mahitaji yao yote waliyapata moja kwa moja kutokana na mfumo wao wa kuishi ulikuwa wakawaida. Na hapa kuwa na mategemeo mengi ya mbele wala hakukua na changamoto nyingi za kibinafsi za kifikra zinazo weza kumdhuru mtu kutokana na jamii yake.

Maisha yanabadilika kila siku kwa uzuri na ubaya pia. Tumekuwa na jamii zenye mifumo mingi na mahitaji mengi yanayoweza kutufanya tuchanganyikiwe tusipoweza kuendana nayo. Tumejiwekea vipao mbele kwa utofauti wake vinavyo tutenganisha wenyewe na kuishi kwa makundi. Kila mtu ana angali cha kwake tu awe na vingi zaidi kuliko wenzake wote. Thamani yetu yote imehamia kwenye vitu sio kwenye utu, tumekuwa binadamu wajinga zaidi wenye vitu vingi vya kumiliki bila kujua chamuhimu zaidi kwao nikipi.

Mabadiliko yote haya ya kimifumo katika maisha kwenye jamii zetu, hayajakuwa na faida tu bali ni chanzo kikubwa cha msongo wa mawazo, kuzidi kwa ubinafsi, maisha ya wasi wasi, dini zinatutenganisha bila kujitambua umoja wetu na kupelea kuingia kwenye uraibu na tuna dhoofisha sana afya za miili yetu na akili kutokana na msukumo mkubwa wa jamii jinsi ilivyo kwa sasa.

Imepekea kuishi kwenye jamii kwa furaha iwe kitu kigumu sana. Tumeipata fedha nafasi kubwa na thamani kuliko thamani yetu wenyewe tunavyo jithamini. Kiufupi tumepoteza ladha ya maisha kwa kutojitambua sisi kwanza na ndio tutende ila tumefanya jamii zitutengeneze ndio tutende ina pelekea vya nnje vinatumiza ndani kwa kuwa havina munganiko wa kutugusa ndani zaidi kutufungua furaha zetu.

Na hapa ndipo mbinu za kisaikolojia zilipo anza kuinuka na kupanda chati kwa kutuahidi zinaweza kututuliza na kuondoa matatizo yetu kabisa. Je, hili ni kweli linawezekana au lina tuwekea kapeti tu juu ya matatizo yetu.

Maarifa ya kisaikolojia kwenye shule au mafunzo popote unapo ya pata msingi wake mkuu ni mbinu za kukutiliza tu kiakili. Kutokana na kuwa na jamii zenye mvurugiko mkubwa wa kifikra unao pelekea madhara mengi kwenye jamii zetu zika anzishwa mbinu hizi ili ziwatulize watu kiakili. Na imepekea kuwa wategemezi kwenye hizi taasisi kwa kuziamini moja kwa moja kuwa ndio tegemeo letu kutuweka sawa na kumaliza shida zetu za kimawazo.

Msaada na uaminifu wa muhimu wa kwanza ni mtu anaojipa mwenyewe, kwanza kwa kutambua njia pekee ya kuweza kumaliza matatizo yako ya kisaikolojia kwenye mizizi yake na kutorudi tena kuwa tatizo kwako, ni wewe mwenyewe kujua ni wajibu wake pekee bila msaada wa mtu au mbinu yoyote ile kujionea mwenyewe jinsi chanzo cha matatizo yake kinavyo anza na kukuletea madhara. Ukiweza kuwa na ufahamu wa kuweza kujitazama na kuelewa chanzo cha matatizo yako bila kuwa na ushawishi wowote wakutaka kumaliza tatizo wala kulitafutia njia ya kuliepuka.

Iwapo utakuwa bado hujaelewa chanzo cha mawazo yako mwenyewe si mtu kukwambia na ukaitikia tu kukubali au kukataa hapana, ni wewe mwenyewe kuwa na ufahamu wa jinsi hisia zako za mawazo zinavyo panda na kupotea bila kubugudhi chochote, hapo utapata uelewa mzima wa akili yako kwa jinsi mawazo yanavyo anza kukushawishi na kujitambua kwa tabia zako kwa jinsi mfumo wako wa akili ulivyo jiweka. Ukiweza kuelewa akili yako basi utakuwa huru kwenye mambo yako yanayohusu saikolojia yote.

Utaelewa mambo mengi yanayotupashida ni kutojitambua tu thamani zetu na kuishia kuishi kwa kushindana, kutafuta usalama wetu wa kijamii, kutengana kwa kuoneana wivu, hatuna muda kabisa wakujitathmini, umbwaji wetu una mambo mengi sana lakini hakuna anayewekea umakini hilo. Tunazalisha mambo mengi vichwani mwetu yasiyo na umuhimu wowote ule kwetu na yanatutesa sana na kukimbilia kwa watu wengine watusaidie kifikra bila kujua hilo haliwezi kutoa mzizi wa matatizo yako ni wewe mwenyewe kutojitambua tu.

Nb: Saikolojia pekee ni kukata tawi la mti ila si kutoa mizizi na mafunzo ya mbinu tu. Na mbinu yoyote ina kikomo, haiwezi kushindana na akili zetu zina uwezo mkubwa zaidi wakutafuta njia yakutumiza zaidi. Kama hatujajitambua wenyewe undani wetu na kuweza kupata mabadiliko halisi yatayo tuweka huru kabisa katika maisha yetu basi tutazinguka dunia yote hatutoweza kupata majibu ya matatizo yetu.
 
Back
Top Bottom