Kwa matatizo ya gari

Mimi naomba kusaidiwa kitu kimoja ambacho sasa katika gari kimekuwa kinanikera sana.

Tatizo ni battery kudrain bila ya chochote kuwa kinafanya kazi.

Battery indicator inaonesha green. Alternator ina charge battery.

Asubuhi niliamka kutaka kwenda kazini gari ikagoma, nikapandishia battery mnyama kawaka. Nikafunga safari ambayo ni kama lisaa moja ivi, battery guage kwenye dashboard inaonesha iko powa tu. nikasimamishwa na askari, walitaka mashirikiano nikawapa. Nikaingiza gari kituoni, nikaizima kwa ajili ya kwenda kuwapa mashirikiano. baada ya kumaliza hata dakika 5 hazikufika, nawasha gari imegoma kabisa. ikabidi niite msaada kuja kuboost.

Sasa sifahamu kama ndio battery imekwisha (haijafika hata miaka miwala hii battery na bado indicator inaonesha green). Alternator tumeijaribu, nayo inafanya kazi vizuri, maana kawaida ukichomoa battery kama alternator mbovu basi gari itakata moto, au kama umeweka battery basi ile battery itanyonywa yote na gari kukata moto. Nimehakikisha hakuna kitu kinachokaa wazi hata kimoja.

Mwenye kujua wapi pa kuanzia anifahamishe... Mi nahisi ni battery, lakini kama battery kufa kwanini bado inaonesha green indicator kuwa bado ipo good.
Mkuu ulifanikiwa hili,daah kluger yangu wiki sasa inanifanyia huu ujinga na battery nimeweka mpya inanifanyia nachelewa kibaruani
 
Back
Top Bottom