Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
Watu dhaifu siku zote wanatumia dini kufichia udhaifu wao.. sasa JK sijui tumweke wapi ila sijawahi kuona sehemu anakemea udini zaidi ya kuuchochea. hivi viburi vya akina Ponda lazima vitakuwa na push somewhere!!
 
Mkuu...leo naona tutakesha hapa......what are we doing to arrest the situation....issue ya mwanahalisi na udini are incoherent so to say......mbona hata huyo Kubenea ni muislam sasa?????


Back to topic: Wewe na mimi humu tunafanya nini kukemea dhambi hii maana naona kama you are double barreled....nini focus yako RAIS MDINI au UBAYA WA UDINI????? Nini mbaya zaid hapa......huyu ni Binadam na atapita .............nauliza tena nini tufanye ili kundoa hali hii badala ya kuendelea kunyoosheana vidole mkuu?????
Maybe tunatofautiana kwenye maana ama dhana halisi ya "usalama wa Taifa"

Kama magazeti mfano wa sauti sijui na alnoor yanachochea udini,then na yenyewe ni fair game kufungiwa.Na hili ninalisema kama ni kweli mwanahalisi lilifungiwa kwasababu ya kuhatarisha usalama wa taifa ama uchochezi,sioni tofauti yeyote na kinachofanywa na haya magazeti yenye udini.

Kama ameyaachia hayo ya udini kwa kivuli cha "uhuru wa habari",kulifungia mwanahalisi kunanifanya nijiulize mara mbili mbili kama kweli huyu double standards zake hazina hila.

Je wewe unakubaliana na kauli zake misikitini kuwa achaguliwe kwasababu yeye ni muislam kama wao na atazipigania haki zao?na angeyasema maneno ya aina hiyo kiongozi wa dini nyingine kwenye nyumba zao za ibada wakati wa kampeni kungekalika?

Sasa mbona hamkumwuliza kuwa ni kwanini hapiganii haki zenu wakati aliposema mhesabiwe?ama kuna namna nyingine anayopigania maslahi hayo ambayo hatuijui.Hapo ndo Sheick Ponda anapokuwa muhimu kwa mh Rais.
 
hadi dini zote tukae pamoja, tukubaliane, na tupange mikakati ya kurekebisha tulipokosea.

Vinginevyo hakuna wa kutusimamia.
hakuna hata siku moja tulishawahi kuwa na tatizo la kusema dini zikae pamoja.Kwasbabu tayari tulikuwa na umoja wa kitaifa na agenda za taifa.

Sasa mgombea urais anayekwenda msikitini na kusema mnichaguwe mimi kwasbabu ni muislam mwenzenu na nitapigania haki zenu,alishaulizwa atazipigania kwa njia gani?Hatuna haja ya kukusanyana kwa misingi ya kidini.Tutakusanyana kwa misingi ya utaifa.That's my stand.Mimi ni mtanzania kwanza,mengine ni ya kiroho.Imani yangu mimi itanisaidia tu kuwa mtanzania mwema,lakini kamwe siwezi kujiona niko juu zaidi ya mtanzania mwingine kwasababu ya imani yangu!Tukishaipoteza tu ile dhana ya utaifa,basi tumekwisha.Ile dhana ya nationalism and patriotism ambayo alitujengea mwalimu inamalizwa na huyu kilaza!
 
hakuna hasara kwa taifa kama kuwa na kiongozi wa juu asiye na msimamo wala hajui kwa nini yupo pale.

Wakati anajipanga kuingia madarakani alitumia sana mbinu ya udini, pamoja na nyingine na kufanikiwa kuingia.

Kama kawaida yake hakujua kama itafikia hapa, na hakuwa na njia mbadala ya kunusuru hali pindi mambo yataharibika.

Jukumu au wa kulaumiwa ni sisis watanzania tuliokubali kuingozwa na mtu asiye na uelewa na sisi kukubali kumpa nafasi ya kutugawa.

Mjinga akiwachonganisha werevu wawili, wa kulaumiwa si mjinga, bali ni wale werevu walioshindwa kujua lililo bora kwao.

Badala ya kutumia 'platform' kama hii kunyoosheana vidole, ingekuwa jambo la maana kama tukakubali tofauti zetu na kutafuta 'common ground' ambapo tunaweza kusonga mbele kama taifa moja lililowahi kuwa na wananchi wasiotambuana kwa dini kwa majina yao au kwa uwezo wao katika uongozi.
Kikwete mpaka leo hii , hajaonesha udini wowote ule. Hivyo naomba msimsingizie mambo asiyoyatenda.nakuhakikishia na kusema uwazi, kikwete sio mdini kabisaa na anatawala nchi bila kuonesha udini wowote ule. Udini ni ule alioufanya mwinyi ndio ulikuwa mbaya sana.Mwinyi alileta mihadhala ya kukashifu ukristo na kumfanya Ponda kuwa wa maana sana kwa kukashifu dini ya kikristo pale mwembe chai. Mkapa kamkomoa Ponda kwa kuweka kipengere cha kushtakiwa ukikashifu dini. Ndio maana sasa Ponda alitegemea JK angelegeza kamba, lakini JK kammkazia uzi ponda.
 
THE BEST PRESIDENT AMBAE HAJAWAHI TOKEA TANZANIA.Ukweli ndo huo.
Nataka kipengele, lakini sikubaliani na wewe kwenye hili la JK, anatuzuga sana Waislam, kwani si yeye ndio kasema hicho kipengele ni NO.
 
Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania

web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????

hiyo wikipedia.com/tanzania na wikipedia.com/tanzania ni web rasmi za serikali ya Tanzania? kama mnaona ukweli ulipindishwa kwa nini msiupinge kwa kutoa za kwenu? hii kitu ni aibu kwa watu wasomi kuichukulia kama sababu ya kugomea sensa,
Binafsi ni mwislam lakini katika hili tumepotoshwa tukapotoka na tunaelekea kutumika kwa manufaa ya watu ili wafikie malengo yao
 
Maybe tunatofautiana kwenye maana ama dhana halisi ya "usalama wa Taifa"

Kama magazeti mfano wa sauti sijui na alnoor yanachochea udini,then na yenyewe ni fair game kufungiwa.Na hili ninalisema kama ni kweli mwanahalisi lilifungiwa kwasababu ya kuhatarisha usalama wa taifa ama uchochezi,sioni tofauti yeyote na kinachofanywa na haya magazeti yenye udini.

Kama ameyaachia hayo ya udini kwa kivuli cha "uhuru wa habari",kulifungia mwanahalisi kunanifanya nijiulize mara mbili mbili kama kweli huyu double standards zake hazina hila.

Je wewe unakubaliana na kauli zake misikitini kuwa achaguliwe kwasababu yeye ni muislam kama wao na atazipigania haki zao?na angeyasema maneno ya aina hiyo kiongozi wa dini nyingine kwenye nyumba zao za ibada wakati wa kampeni kungekalika?

Sasa mbona hamkumwuliza kuwa ni kwanini hapiganii haki zenu wakati aliposema mhesabiwe?ama kuna namna nyingine anayopigania maslahi hayo ambayo hatuijui.Hapo ndo Sheick Ponda anapokuwa muhimu kwa mh Rais.

Dont tell me unaamini kuwa ni Rais kwa sababu alisema hayo (kama kweli) msikitini???

Hapo kwenye magaazeti sasa ni wizara husika na majukumu yao.....kama tutaliangalia tatizo hili kwa mapana yake twaweza kuja na suluhu ila tukiendelea this way.......tunaingia shimoni
 
Udini tafsiri yake ni uislamu sio? na by extension viongozi wa juu wakiwa wa dini moja ndio udini? the granted Kikwete mdini so do Mkapa, Rais Mkristo, alie kuwa Waziri Mkuu wake Malecela mkristo, katibu wake mkuu Philip Mangula Mkristo nk same argument utawala Julius Nyerere.

Tatizo lenu wakristo wa Tanzania mna roho mbaya, serikalini mmejaa ninyi, mashirika ya umma ninyi, idara za serikali ninyi na juu ya hapo MOU inaita serikali iyape Makanisa Bil 60 kwa mwaka kwa kisingizio cha huduma za jamii lakini mpaka mishahara ya watumishi wa kiroho inaingizwa na serikali inalipa. Kwenu ninyi kwa sababu wanufaika huo sio udini.
Udini ni pale wanapoteuliwa waislamu wachache kushika madaraka mnalipuka!

Dini maana mki ulizwa leteni ushahidi wa udini mnaishia Said Mwema as if Davis Mwamunyange Muislam, mtasema Othman Rashid lakini Zoka hamumtaji na kurugenzo zote zilizoshikwa na wagala.

Kahesabu mawaziri na manaibu linganisha wengi wepi, nenda kwa Ma RC, MaDC RAS, DAS, DED etc

Ndio maana tunasema mna roho mbaya!
 
Dont tell me unaamini kuwa ni Rais kwa sababu alisema hayo (kama kweli) msikitini???

Hapo kwenye magaazeti sasa ni wizara husika na majukumu yao.....kama tutaliangalia tatizo hili kwa mapana yake twaweza kuja na suluhu ila tukiendelea this way.......tunaingia shimoni

Suluhu ya kwanza, fungia hayo magazeti yenye sumu za kidini,na piga marufuku udini kwenye kampeni.Hilo tunaweza kama tuko serious.

Halafu mkuu haya mambo ya JK kupakazia kila kitu wasaidizi wake hayana mpango wala nini.

Na yes,hilo la kutemba misikitini na kuomba kura kwa madai kwamba yeye ni muislam mwenzao na atapigania haki yao.Huo ni udini at its best,no doubt about it.Ama hakusema hayo maneno?Na kama aliyasema,we unaona ni sawa sawa?
 
Mumezeo kuwazulumu waislam sio? Sasa waislam wameamka na ikibidi mapambano ili kupata haki yao mie siwalaumu hata kidogo.

Chuki yenu iliyopitiliza dhidi ya kikwete ni kutokana na dini yake tu munataka ionekane eti muislam hajui wala hawezi kutawala tanzania. Wacheni unafiki nyie kama si kikwete wengi wenu hadi leo mungekua munaiskia tu degree lkn musingali ipata mana vyuo vilikua kidogo sana.
 
KAMA JK ni FISADI na MDINI basi na WEWE ni MCHAGGA na CHADEMA.
Yea,Dr Slaa alikwenda makanisani akasema achaguliwe kuwa rais kwasababu ni mkristu mwenzao,pia alikwenda uchaggani na kusema hayo hayo kwamba achaguliwe na wachagga kwasababu na yeye ni mchagga.Si ndiyo?
 
Dini nini katika sensa? Kama ni idadi ya waumini wetu tuwapate miskitini au makanisani. Kwa sababu muumini atapatikana anakoswali. Kama we ni mchungaji au sheikh na hujui idadi ya waumini wako hufai. Mtu asiyekuja kusali au kuswali sio muislam wala mkristo.

Tuache kutaka kuendesha nchi kwa mifumo na matakwa ya kidini.
 
acha propaganda zisizo na mashiko, unatoa tuhuma bila hata ushahidi.
Ulisha msikia jk akiwa na waslam mcktn na wanayo ongea?
Unaweza kuyathibitisha au unaleta stori za vijiweni?
Hivi kwa vile ni jk ndo asingiziwe kila kitu?
Mbona hauwakosoi mapadri walisema yeye ni chaguo la mungu?
Mbona hauwakosoi walipoingeza serekali kwa kuwauwa watu ndani ya mckt wa mwembechai na pemba wkt mauaji ya arusha viongozi haohao waliyalaani?
Au arusha ndio kuna watu wenye thamani lkn co dar wala pemba?
Mbona haukukosoa kanisa walipotoa muongozo kwenye uchaguzi mwaka juzi, hawakua wanaingilia yasowahusu na kuleta udini?
Mbona chaguzi zote zilizopita hawakuwa wanafanya hivyo?
Mbona hausemi leo kanisa katoliki linahusishwa na kuifadhili cdm, kwanini usiwashauri wakanushe kwanza kuliko kuendelea kukaa kimya?

Wewe ndio mdina na yote uloandika inaonyeshwa jinsi ulivyo. Unatoa tuhuma nzito zisizo na ushahidi na wadini wenzako wanashabikia tu.
 
Mumezeo kuwazulumu waislam sio? Sasa waislam wameamka na ikibidi mapambano ili kupata haki yao mie siwalaumu hata kidogo.

Chuki yenu iliyopitiliza dhidi ya kikwete ni kutokana na dini yake tu munataka ionekane eti muislam hajui wala hawezi kutawala tanzania. Wacheni unafiki nyie kama si kikwete wengi wenu hadi leo mungekua munaiskia tu degree lkn musingali ipata mana vyuo vilikua kidogo sana.
Tunajuwa udini umeshawapofua na ndo maana hata hamkumgusa aliposema mkahesabiwe.Huyu unafiki wake na udini tutajuuta kumwingiza ikulu.
Hata zile kauli za maaskofu kama zililenga kuleta umoja,kwamba eti ni "chaguo la Mungu",sasa kama hamkujuwa mnafiki,pateni definition!
Hii nchi ni ya watanzania na si waislam ama wakristu.
 
Familia yetu ni ya wakristo na waislamu na tupo imara pamoja kama zamani. Kijiji chetu kina waumini wa dini zote mbili na bado tunazikana kama zamani. Sijui umeandika haya baada ya kufanya utafiti wa kiasi gani?
Mkuu tutajie hilo gazeti lenye kusambaza sumu hizo.


Je kwa mujibu wabutafiti wako wew,ni kwa kiasi gani kijiji chenu kinawakilisha hali ya Taifa zima?
 
hapa nachoona, kwanza, si wote tunaamini tatizo la udini lipo, na kama hatujaliona hatuwezi litatua.

Na kingine, naona kuna dhana ya 'wanaoathiri' na 'walioathiriwa'. Hatuwezi kuingia kwenye mijadala ya kutafuta suluhu kama baadhi watajiona ni victims au less prevelaged sababu hayo maafikiano wengine watajiona wameburuzwa kuyakubali.

Natamani watu wamengemwaga mapweint kuliko kunyoosheana kidole. Tayari tushafika hapa, tunarudije tukikotoka?? Kama ni jahazi tumepanda sote, likizama ndo basi tena.
 
Nchi ilipofikia,credits huwa anapewa rais na serikali yake,kwahili la udini,hakuna ubishi umeshaota mizizi.Na sijawahi kusikia kauli ama vitendo kutoka kwa JK vya kukemea haya mambo ya udini.

Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani.

Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)

Ninamini kabisa kuwa tulipofikia,uwezekano wa kuingia kwenye vurugu na mapigano ya kidini ni mkubwa kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya Tz toka tupate uhuru.

Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive.

Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!....

kwanza wewe ni dini gani mpaka uje kuhubiri ujinga huo hapa JF
 
Watu dhaifu siku zote wanatumia dini kufichia udhaifu wao.. sasa JK sijui tumweke wapi ila sijawahi kuona sehemu anakemea udini zaidi ya kuuchochea. hivi viburi vya akina Ponda lazima vitakuwa na push somewhere!!

Mbona mnapenda sana kongelea udini udini, hamna mada zingine za kuleta humu? Una tofauti gani na PONDA wakati wote mnahubiri udini huo huo. Mtapigana wenyewe na huyo PONDA wenu wengine tutakaa pembeni tunawaangalia mahubiri yenu hayo yatakapoishia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom