Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
hakuna hata siku moja tulishawahi kuwa na tatizo la kusema dini zikae pamoja.Kwasbabu tayari tulikuwa na umoja wa kitaifa na agenda za taifa.

Sasa mgombea urais anayekwenda msikitini na kusema mnichaguwe mimi kwasbabu ni muislam mwenzenu na nitapigania haki zenu,alishaulizwa atazipigania kwa njia gani?Hatuna haja ya kukusanyana kwa misingi ya kidini.Tutakusanyana kwa misingi ya utaifa.That's my stand.Mimi ni mtanzania kwanza,mengine ni ya kiroho.Imani yangu mimi itanisaidia tu kuwa mtanzania mwema,lakini kamwe siwezi kujiona niko juu zaidi ya mtanzania mwingine kwasababu ya imani yangu!Tukishaipoteza tu ile dhana ya utaifa,basi tumekwisha.Ile dhana ya nationalism and patriotism ambayo alitujengea mwalimu inamalizwa na huyu kilaza!

Namuomba Mungu sana ninyi mnaoota ndoto za vurugu za kidini muwe wa kwanza kuzianzisha na muwe wa kwanza kufa, full stop. Eee Mungu wangu nisikie. Amina
 
Kugomea sensa ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha miezi sita, sasa nawashangaa sana wakina ponda na radio yao wanapata wapi ujasiri wa kushawishi watu kugomea sensa au ndio mkuu yuko nyuma yao.
 
hapa nachoona, kwanza, si wote tunaamini tatizo la udini lipo, na kama hatujaliona hatuwezi litatua.

Na kingine, naona kuna dhana ya 'wanaoathiri' na 'walioathiriwa'. Hatuwezi kuingia kwenye mijadala ya kutafuta suluhu kama baadhi watajiona ni victims au less prevelaged sababu hayo maafikiano wengine watajiona wameburuzwa kuyakubali.

Natamani watu wamengemwaga mapweint kuliko kunyoosheana kidole. Tayari tushafika hapa, tunarudije tukikotoka?? Kama ni jahazi tumepanda sote, likizama ndo basi tena.
Hatuhitaji maafikiano based on religion,nakuhakikishia tukienda huko,kesho tutafwata mawazo ya Sideeq kuwa nchi igawanywe kwa misingi hiyo.Tuna matatizo ya kitaifa ambayo rais ameshindwa kuyapa kipaumbele,badala yake,anataka kuificha failure yake kwenye mwavuli wa udini.Sijakuelwea unaposema hakuna tatizo na hapo hapo unadai eti kuna ambao wako less priveledged?yani kwa misingi ya dini siyo?sasa this double standard,sorry.kwasababu unayohubiri humu ndo hayo wanayoyahubiri wafuasi wa JK humu kila kukicha.Na akiguswa tu,ni hayo ya udini,hata ufisadi alipoguswa,kulizuka mjadala humu eti mafisaid ni watu wa dini flani nk.Yote ni yeye anaya engineer!
 
Last edited by a moderator:
Kugomea sensa ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha miezi sita, sasa nawashangaa sana wakina ponda na radio yao wanapata wapi ujasiri wa kushawishi watu kugomea sensa au ndio mkuu yuko nyuma yaobbbbbbbbbbbbbbbbb
 
Yea,Dr Slaa alikwenda makanisani akasema achaguliwe kuwa rais kwasababu ni mkristu mwenzao,pia alikwenda uchaggani na kusema hayo hayo kwamba achaguliwe na wachagga kwasababu na yeye ni mchagga.Si ndiyo?

natamani kuwa mchaga kwa vile tu sio rahisi kubadilsha kabila..ukienda moshi kule migombani utashangaa baabaangu yaani kuna kila kitu maji umeme barabara za lami yani maendeleo kwenda mbele mjini ndio usiseme pasafi hata ukitupa kichungi cha sigara unakamatwa...
slaa sio mchaga ni mmbulu wa karatu hana tofauti na mama nagu
 
Kikwete mpaka leo hii , hajaonesha udini wowote ule. Hivyo naomba msimsingizie mambo asiyoyatenda.nakuhakikishia na kusema uwazi, kikwete sio mdini kabisaa na anatawala nchi bila kuonesha udini wowote ule. Udini ni ule alioufanya mwinyi ndio ulikuwa mbaya sana.Mwinyi alileta mihadhala ya kukashifu ukristo na kumfanya Ponda kuwa wa maana sana kwa kukashifu dini ya kikristo pale mwembe chai. Mkapa kamkomoa Ponda kwa kuweka kipengere cha kushtakiwa ukikashifu dini. Ndio maana sasa Ponda alitegemea JK angelegeza kamba, lakini JK kammkazia uzi ponda.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Hakuna sababu yoyote ya kumnyoshea kidole mtu yeyoye kuwa anasababisha udini. Ni sisi wenyewe wananchi tunaopandikiza mbegu chafu miongoni mwetu. Si Mwinyi, si Mkapa wala si JK wa kumnyoshea kidole , kwani tukikataa wangetulazimisha? Tuwaache viongozi wetu , na tukae tukijua kuwa dhamana ya amani ya Taifa letu iko mikononi mwetu na si mikononi mwa viongozi. Kitendo hata cha kuweka mada za udini humu JF na katika mitandao mingine ya kijamii na hata katika mihadhara tayari huo ni udini na sisi ndiyo tunapaswa kunyoshewa kidole. Kwani tumeshindwa kumwabia PONDA sisi wenyewe kuwa anatupeleka pabaya mpaka tuanze kuwasingizia viongozi?
 
Nataka kipengele, lakini sikubaliani na wewe kwenye hili la JK, anatuzuga sana Waislam, kwani si yeye ndio kasema hicho kipengele ni NO.

JK mbona tutamkumbuka sana tu. Hakuna Rais mpole, asiyebagua dini, kabila wala rangi kama JK. Mimi naamini kutokuwa na papara kwake katika maamuzi ndiko kunakofanya tunamdharau, kumtukana, kumnyoshea kidole na hata kumdhihaki. Mungu hamtupi mja wake, lazima JK atakuja kukumbukwa tu tena ha wal wale wabaya wake watamuona kama lulu.
 
Nchi ilipofikia,credits huwa anapewa rais na serikali yake,kwahili la udini,hakuna ubishi umeshaota mizizi.Na sijawahi kusikia kauli ama vitendo kutoka kwa JK vya kukemea haya mambo ya udini.

Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani.

Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)

Ninamini kabisa kuwa tulipofikia,uwezekano wa kuingia kwenye vurugu na mapigano ya kidini ni mkubwa kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya Tz toka tupate uhuru.

Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive.

Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!....

jMushi1 Unafiki wa wana CCM ndio unaosababisha yote haya. Kuanzia wabunge na wanachama wake. Katiba ya CCM inasemaje juu ya udini ukabila na mengineyo yenye misingi ya kibaguzi? Kwa vile wana CCM wamekalia kujinufaisha, na rais ndiye mwenye madaraka lukuki, hawawezi kukemea. Kama bunge lililazimisha kuvunjwa kwa baraza la mawaziri inakuwaje mambo maovu kama ya udini rais anakaa kimya tu halafu na wana CCM na wabunge wengine wana kaa kimya manake ni nini? Bahati mbaya sana watanzania tumekuwa na umaskini wa kila hali. Mara nyingi tumekuwa watu wa kutoa hoja nyepesi nyepesi kwenye mambo mazito. Jambo hili la udini ni zito sana lakini kwa wengi linaonekana kuwa ni jepesi. Watanzania wa kawaida tuache kutumiwa na wanasiasa kwa faida zao tutafakari mustakabali wa taifa letu. Mambo yakichafuka Kikwete na wenzake watakuwa ughaibuni watatuacha sisi tunakufa na familia zetu.
 
Kinachonishangaza kupita yote ni jinsi redio imaan inachonganisha na kutukana dini nyingine na hakuna mtu wa kukemea. Nafikiri katiba yetu iko wazi kwamba mtu ana haki ya kuamini dini yoyote maradi asivunje sheria. Sasa kwanini mtu mwingine awe na haki ya kukashifu wengine???
 
tutajipamba hapa kwa maneno, lakini ikitokea vita, tutakaoathirika hasa ni sie tusokuwa na uwezo wa kugharimia familia zetu kwenda kuishi nje.

Wao utakuta familia zote ziko nje.

Waislamu kudai haki zao ndio tatizo mnasema wataleta vita
 
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Hakuna sababu yoyote ya kumnyoshea kidole mtu yeyoye kuwa anasababisha udini. Ni sisi wenyewe wananchi tunaopandikiza mbegu chafu miongoni mwetu. Si Mwinyi, si Mkapa wala si JK wa kumnyoshea kidole , kwani tukikataa wangetulazimisha? Tuwaache viongozi wetu , na tukae tukijua kuwa dhamana ya amani ya Taifa letu iko mikononi mwetu na si mikononi mwa viongozi. Kitendo hata cha kuweka mada za udini humu JF na katika mitandao mingine ya kijamii na hata katika mihadhara tayari huo ni udini na sisi ndiyo tunapaswa kunyoshewa kidole. Kwani tumeshindwa kumwabia PONDA sisi wenyewe kuwa anatupeleka pabaya mpaka tuanze kuwasingizia viongozi?
Na mwanahalisi tungeachiwa wananchi tuamuwe wenyewe,ndo hapo double standards...
 
acha propaganda zisizo na mashiko, unatoa tuhuma bila hata ushahidi.
Ulisha msikia jk akiwa na waslam mcktn na wanayo ongea?
Unaweza kuyathibitisha au unaleta stori za vijiweni?
Hivi kwa vile ni jk ndo asingiziwe kila kitu?
Mbona hauwakosoi mapadri walisema yeye ni chaguo la mungu?
Mbona hauwakosoi walipoingeza serekali kwa kuwauwa watu ndani ya mckt wa mwembechai na pemba wkt mauaji ya arusha viongozi haohao waliyalaani?
Au arusha ndio kuna watu wenye thamani lkn co dar wala pemba?
Mbona haukukosoa kanisa walipotoa muongozo kwenye uchaguzi mwaka juzi, hawakua wanaingilia yasowahusu na kuleta udini?
Mbona chaguzi zote zilizopita hawakuwa wanafanya hivyo?
Mbona hausemi leo kanisa katoliki linahusishwa na kuifadhili cdm, kwanini usiwashauri wakanushe kwanza kuliko kuendelea kukaa kimya?

Wewe ndio mdina na yote uloandika inaonyeshwa jinsi ulivyo. Unatoa tuhuma nzito zisizo na ushahidi na wadini wenzako wanashabikia tu.

ukosawa sawa!!mungu akuzidishie elim!!asante saaan@
 
Ishu iliyopo ni very gunuine huitaji darubini....Madai ya waislamu ni ya msingi kabisa na lazima yatatuliwe...Walikua wapo cool sana japo wametengwa na iyo ipo planned ili wawe second class ktk nchi yao mf Serikali walipotoa takwimu kua wakristu ni wengi kwa 62% according to wikipedia walikua wanamaana gani? na ikumbukwe hatujawahi kufanya sensa ya kidini TZ na ndo tulikua ndo tunaelekea kwenye sensa nini dhamira km hakuna consipiracy zilizopangwa? Mbona vyanzo vingine mf encyclopedia zinaonesha 35% muslims, 30% cristians and 30% indigenous religion ata CIA WORLD FACT BOOK zinaonesha 35% muslims, 30% cristians sasa kwanini hawakutumia hizo takwimu na wakahalalisha za wikipedia? Waaislam hawana udini ila mambo wanayowanyiwa ktk nchi yao ndo sio mf wanapotaka wajiunge na OIC ili waweze kunufaika na misaada maaskofu wanakataa na uku wao wanapata misaada kila kona hiyo ni haki kweli?
 
natamani kuwa mchaga kwa vile tu sio rahisi kubadilsha kabila..ukienda moshi kule migombani utashangaa baabaangu yaani kuna kila kitu maji umeme barabara za lami yani maendeleo kwenda mbele mjini ndio usiseme pasafi hata ukitupa kichungi cha sigara unakamatwa...
slaa sio mchaga ni mmbulu wa karatu hana tofauti na mama nagu

Sitaki kusema lolote kuhusu dini wala kabila la mtu, ila binafsi ninachoamini ni kwamba kwa jinsi ninavyomfahamu SLAA angekuwa yeye ndiye Rais asingeweza kuwa na busara, staha, na hekima kama ambavyo Rais kikwete ameonesha. JK amekuwa mvumilivu, mwenye staha na busara nyingi sana. JK ametukanwa, kukashifiwa, kudharauliwa na hata watu ambao hawana shule lakini yote hayo ameyapotezea kama ambavyo kiswahili cha mtaani kisemavyo. Ni kutokana na ukweli kwamba watu wengi ambao humdhihaki JK na hasa wanasiasa ni wale ambao hawana hekima wala busara kutokana na shule ndogo walizonazo vichwani mwao. Wengine wana msongo wa mawazo kutokana na kupitia maswahibu mbalimbali yakiwemo mapigo kutoka kwa Mungu, wapo walio asi utumishi wao waliyoapia kuutumikia milele, huku wengine wakiwa na dhambi ya kusepa na michango iliyokuwa ikitokana sadaka za waumini na kuzitumia katika masuala yao binafsi. Hakika watu wa aina hii ni lazima watafute mahala pa kuficha makosa yao.
 
Kugomea sensa ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo cha miezi sita, sasa nawashangaa sana wakina ponda na radio yao wanapata wapi ujasiri wa kushawishi watu kugomea sensa au ndio mkuu yuko nyuma yao.

Tujiulize ingekuwa Nyerere asingetoa tamko la kukemea wanaofanya hivyo? Tamko toka kwa rais ni nzito na linabeba ujumbe mzito sana. Rais Kikwete atoe tamko kwa upuuzi huu kama kweli yeye si mdini.
 
Kinachonishangaza kupita yote ni jinsi redio imaan inachonganisha na kutukana dini nyingine na hakuna mtu wa kukemea. Nafikiri katiba yetu iko wazi kwamba mtu ana haki ya kuamini dini yoyote maradi asivunje sheria. Sasa kwanini mtu mwingine awe na haki ya kukashifu wengine???

inaonekana hujui radio imaan!!imaan haina kashfa hiyo!!!!HATA HIVYO UMEIONA RADIO IMAAN TU!!LIVING WATER YA MWANZA HUJAIONA,NA KWANEMA FM YA MWANZA HUJAIONA!!wakristo acheni chuki .waislam tumeamka kutudhulum tena baaasi mwishoooo..
 
natamani kuwa mchaga kwa vile tu sio rahisi kubadilsha kabila..ukienda moshi kule migombani utashangaa baabaangu yaani kuna kila kitu maji umeme barabara za lami yani maendeleo kwenda mbele mjini ndio usiseme pasafi hata ukitupa kichungi cha sigara unakamatwa...
slaa sio mchaga ni mmbulu wa karatu hana tofauti na mama nagu
nashukuru kwa complements za ukweli kuhusiana na maendeleo kwenye maeneo hayo,tunataka the whole country iwe hivyo.

Kuhusu hilo la Dr Slaa,nafahamu yeye ni muiraq,lakini nilikuwa nikimjibu yule aliyesema kwamba "kama JK ni mdini na fisadi,basi mimi ni mchagga na chadema",aliijibu posti yangu niliyokuwa nikilaani kitendo cha JK kupita misikitini na kuwahadaa ndugu zetu wampigie kura kwa vigezo vya dini na wala si kwamba atalifanyia nini taifa.Siasa za hatari kweli kweli.

Na miye ndo nikamwambia Slaa naye alikuja kuomba kura na kusema mimi mchagga?ama alienda makanisani na kuomba kura akisema mimi mkristu mwenzenu?

Kama Slaa angesema maneno kama hayo,ningemwita mdini vilevile.Hapa JF ni jukwaa huru.
 
Anayebisha kuwa udini hakuna aendeleee kusibiri kwani atauona siku za karibuni sana.

Hata nyerere alikuwa mdini na kanisa lake la katoliki. uhuru wa nchi ulitafutwa na waislamu lakini kwa hila za nyerere akawaingiza wa katoliki wenzake madarakani mfano john rupia na wenzake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom