Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
hilo la mahakama ya kadhi fanyeni yote hata kukatana mikono kama inawezekana, illa fanyeni/simamieni wenyewe...kitendo cha kutumia vyombo vya dola kama polisi/jela/mahabusu nk kudhibiti watu walioshindwa kutimiza sharia za ibada ya kiislam ni kitu kisichowezekana katika nchi hii...kama mtu anashindwa kufuata ibada ya dini yake(ambacho ni kitu cha hiari), sioni kwanini serikali itumie vyombo vyake kumlazimisha mtu huyo afuate ibada yake...mkitaka hivyo mkubali na sheria za dini nyingine zisimamiwe na serikali na muondoe hicho kisingizio eti sheria hizo hazijaandikwa kwenye biblia...kwa hili, tutakula sahani moja hata kwenye katiba mpya...
 
Mangi jenga hoja kwa kufanya utafiti na kutumia takwimu.Kwa taarifa yako kama ukimfuatilia kwa makini JK hata hiyo dini haswa ya Islam haifahamu kwa kina.Yeye anazungumza kisiasa zaidi lakini hana ufahamu wa kina wa masuala ya dini.Makmba anamzidi sana JK kwa upande wa uelewa wa masuala ya dini.Habari ndio hiyo.
 
huo muda uliopoteza kumhisi kiongozi ni mdini,ndio kiwango cha udini ulionao wewe.pili hayo makasa mnayolishwa huko kanisani yatawaua,mkihubiriwa udini huko changanyeni na akili zenu mkuu.post yako ni kijinga sana

acha upumbavu wewe, fungua macho. anyway akili zako ndio zimefikia hapo sio kosa lako.
 

Takwimu za kuonyesha udini?hizo nitazipataje?chuki zilizoongezeka baina yetu watanzania chini ya utawala wa JK ndo kielelezo tosha.

Halafu kwani nani kakwambia kila "anayeijuwa dini" ni mdini?tofautisha the two.
 
eeeeeh, hutaniwi?

Nilitegemea input yako earlier on mrembo,na busara zako,however bado hujachelewa.

Kwahiyo kumbe ulikuwa unatania?Nilidhani unasapoti alichopost yule member bila kuelekeza kwa yeyote,siwaentertain member wa aina hiyo hata kidogo.Neways basi tuko pamoja.

Ebu mwaga nasaha basi,unajuwa wananchi wote kwa ujumla wetu tunahitajiana kwasana,we realy need each other more than anytime in our country's history.

Ni vyema tusikwepe jukumu la kujadiliana hata zile hoja ambazo tunaona ni ngumu ama sensitive.
 

Well, I wouldnt want to sound stupid by repeating what has been said earlier on.
Ila kwa kusoma tu assumptionyako hapo juu, na swali zinazo fatia, ngoja niseme:
kwanza SIDHANI KAMA Rais Kikwete ni mdini. Mdini ni mtu anae tumia dini ku-promote
kitu ambacho kinamfalia yeye au kundi lake, na kuwafedheesha wengine
He does this by praising one religion, or by criticising negatively another religion. (IMO)

Rais angekua mdini angeshawishi kipengele cha dini kiingie kwenye katiba yetu
Angekua mdini mngeona mambo ya quota yanakuja wakati wa kuteua-teuliwa
angekua mdini mngemuona akisema au akitenda in a way that makes it explicit
kua yeye ni mfwasi wa dini fulani, anaponda dini zisizo zake, huku aki-promote dini yake.
Being of a certain faith does NOT MEAN that Raisi Kikwete amekua mdini.

On the other hand, as the supreme leader, nadhani alitakiwa kuelewa na kuchukua hatua sababu:
This problem didn't appear suddenly. hata enzi za utawala wa Mwalimu, alishtakiwa kua mdini
It is possible that udini umekua juu zaidi leo kuliko wakati wa Mwalimu, ila sio kosa la mtu mmoja.
BAADHI YA WATANZANIA WAMEKUA WADINI. Narudia: Rais sio mdini, BAADHI YA WATANZANIA ARE.

nakubali kua kama kiongozi wa kisiasa, kama Mheshimiwa Rais wa nchi, alitakiwa alione hili
mapemana aanze kutafuta strategies za kupunguza tensions and conflicts among "believers".
But he didn't.Is that a failure in his leadership abilities? probably. Can he be indexed as mdini?
I don't think so.Unaweza kua "udhaifu" wa kawaida tu [no comment] ila sio Udini. Wadini ni waninchi fulani, wala sio yeye!

Tusisahau pia kua we are in a context where any negative action is blamed on the ruling party
and within a party, any negative action is blamed on a faction. Tumeyaona CCM, tumeyaona CDM
Some obnoxious and bellicose politicians blame udini on the current president. Or use it for themselves.
Some other use religion to gather votes, sympathy, praise etc. Siasa ni mchezo mchafu, kila kitu ni silaha.
 
Mwali,nimekupata sawia.

Napenda niseme kwamba,ni ukweli umeidhinisha kuwa, maybe udhaifu wa JK wa kutoyapatia ufumbuzi ama kuyashughulikia matatizo ya wananchi kumetafsiriwa na mimi mleta hoja kwamba ni udini.

Kimantiki,nakubaliana na wewe kwasababu inamake sense kwa jinsi tunavyouona utendaji wake wa kazi.Lakini pia,mada hii ni pana sana na nimejaribu kucover hizo "weaker sides" of my main point kwa kadri ya uwezo wangu.

Kwanza nilifanya hivyo kwa kuhusisha hoja ya JK na watu wake kwamba ameruhusu uhuru wa habari.Na nikasema kuwa,hiyo si kweli,nikatolea mfano wa vyombo vya habari vyenye kueneza chuki za kidini ambavyo vinaachwa vifanye hivyo bila wasiwasi.Na wakati kwa upande mwingine,nilitolea mfano wa gazeti la mwanahalisi kufungiwa kwa kuandika yale yasiyompendeza.Hata mtandao huu walishajaribu kuufanyia kipindi cha nyuma kama sikosei.Hivyo yale anayoyaacha,naweza kuconclude kwamba yanamfurahisha(siyo yote).

Na kwahiyo licha ya kwamba inaonyesha mnaomtetea mnaya attribute haya kwenye udhaifu wa kiutendaji,bado kuna mambo ambayo hajaonyesha udhaifu hata kidogo.Mambo ambayo watu wake wanayafanya yenye kuonyesha ubabe kabisa na ukiukwaji wa haki za kimsingi kabisa za watanzania.

Sasa tunapopima yanayofanyika kwenye taifa letu,na kuona matokeo yake,basi tunajuwa kuwa something is deadly wrong,nchi haiwezi kuwa kwenye chuki za kidini kuliko wakati wowote ule kwenye historia yetu,halafu eti lawama tupeleke kwa mtu alyetawala zaidi ya miaka takriban 30 iliyopita.

Mimi sizungumzi nani analalamika kuhusu udini,nazungumzia chuki za kidini.Kama kuna waliokuwa wakilalamika udini chini ya mwalimu,basi hiyo ni topic nyingine.

Na kwakukusaidia tu,ni kwamba kama Nyerere alikuwa mdini,basi uweke sababu ie kulikuwepo na udini etc.Hilo tutapingana sana tu,kwasababu chini ya utawala wake tulikuwa na mshikamano.Ila maybe unaweza kuitetea pointi yako kwa kuingiza hoja ya mfumo kristo.Hilo lina thread yake limejadiliwa na bado linaendelea kujadiliwa.

Sasa ninapojiuliza ni kwanini hili ama lile,kwa mfano kukiwa na machafuko kwenye taifa,ama uchumi ukiwa mbaya nk,credits kama nilivyosema hapo awali,zinamwendea mkuu wa nchi.

Na kusema ukweli hiyo mifano uliyoitoa,kwamba JK hajasema hiki ama kile against dini nyingine,ukweli ni kwamba hathubutu kusema hayo kwani asingekuwepo madarakani kwa maneno kama hayo.Ila rais anapimwa kwa matokeo.We look at the results.Nchi ikiwa na mshikamano,atapewa credit,and the opposite is also true.

Sasa ngoja nimalizie kwa kusema haya tena kwa mara nyingine.Nilisema kuwa,JK serikali yake ina kashfa za ufisadi,lakini toka hizi hoja za udini zilipoanza,basi huwezi kushangazwa na watu kumtetea fisadi kwenye issue wazi kabisa ya ufisadi bila kusikia wengine wakisema kiongozi huyo anaonewa kwasababu ya dini yake endapo ni muislam.

Yani issue iliyowaunganisha watanzania ya ufisadi,inaangaliwa kwanza kwa basis ama jicho la udini.Na hata JK mwenyewe akishutumiwa kwa hili ama lile,utasikia ni kwasababu ni muislam.Sasa hapo unategemea niseme nani ni mdini endapo watu wake ndo wameanzisha hayo?

Inasemekana kwenye uchaguzi uliopita,alitumia issue hiyohiyo kuwagawa wananchi.Hili ni tatizo kubwa.Kama alikuwa na uwezo wa kulifungia mwanahalisi,anashindwa vipi kukemea vyombo vya habari vyenye mienendo hiyo?

Naomba niseme kwamba,kama huu udini usingemnufaisha yeye,basi nisingemuhusisha nao hata kidogo.Mimi napenda sana kuwa fair,napenda usawa,sipendi ukandamizaji wala uonevu hata kidogo,hiyo siyo character yangu.

Kama anajuwa kuupinga udini kutawaunganisha watanzania dhidi ya mafisadi,basi naamini yeye anafurahia hali hiyo,so siwezi kumwona tofauti na kwamba ni mdini.Regardless of the reason on how it happens.Nimeconnect dots nikafikia kwenye conclusion hii.However nakubaliana kwa kiasi kikubwa na baadhi ya points zako.
 
Last edited by a moderator:
Kikwete si mdini hamjamuelewa tu ,kwanza ameshiliki shuguli nyingi za kilokole kuliko za uamsho ,sasa udini upo wapi ,huo mlionao ni udhaifu wa kumuelewa ,mnasema mpaka kieleweke wakati hamuelewagi !

Nionavyo JK anamaliza muda wake kistaarabu.
 
Mkuu hatima ya TZ iko mikononi mwetu,JK atapita km zilivyopita mamlaka nyingine,
Atakumbukwa kwa kupanda udini,na atasifiwa kwa kuiua CCM.
 

Aisee!! Mara kwa mara nimekuwa nikijiuliza busara inayotumika kwa kesi, say iliyopo Tanzania na kuchukua reference from another country.....inaleta sense for sure....no new crime ambayo inaweza kutokea pahala ambayo haijapata kutokea popote! But unataka kuniambia mashauri yanayofanyika na Wakatoliki ndo yanatumia hizo Common Laws?! And by the way, What is Canon Laws? Nimepata mwanga wa kutosha kuhusu hiyo Common Laws, but bado hapo kwenye Canon Laws.
 

Mkuu wangu umeghafirika wapi?! Ingawaje post yako umeandika kwa ku-quote my post lakini sioni uhusiano wowote wa hiki ulichokiandika na kile nilichokiandika!!!! vipi mkuu wangu!!!!! Vyombo vya serikali gani na kufanya ibada ipi? Nani anataka ibada za Waislamu zisimamiwe na serikali......let me assume ulisoma post yangu huku ukiwa na personal stress.....unaonaje baada ya kutulia ukianza kuisoma upya kisha uchangie!!! Ni ushauri tu
 
Naona kumuuliza muanzisha huu uzi unaweza kunitajia mkiristo mdini, kama ulivyotamja JK ni mdini ebu nitajie na mie nichangie kidogo kutoka na upeo wangu mdogo.
 
Naona kumuuliza muanzisha huu uzi unaweza kunitajia mkiristo mdini, kama ulivyotamja JK ni mdini ebu nitajie na mie nichangie kidogo kutoka na upeo wangu mdogo.
Sijawahi kuona chuki za kidini zimetawala kwa kiasi kikubwa kama under this regime.Hilo liko wazi sana.Uhuru wa kupanda chuki za kidini upo,lakini uhuru wa kusema ukweli haupo.
 
Kikwete si mdini hamjamuelewa tu ,kwanza ameshiliki shuguli nyingi za kilokole kuliko za uamsho ,sasa udini upo wapi ,huo mlionao ni udhaifu wa kumuelewa ,mnasema mpaka kieleweke wakati hamuelewagi !

Nionavyo JK anamaliza muda wake kistaarabu.
Results,na siyo eti kushiriki,hizo ni shughuli tu ambazo zinabeba majukumu ya kuwatumikia wananchi wote wa taifa la Tanzania.Look at the results,uamsho na mataka taka yote happened under his watch,na kwasababu ananufaika yeye na chama chake,then ni mdini.Fisadi siyo fisadi kwasababu ni muislam,huo ni udini.Hakuna rais mwenye agenda za siri anayefanya hayo mambo openly,hizo ni agenda za siri ambazo hufanyika covertly!ukitaka kuzijuwa,haumsikilizi anachosema,unatizama matokeo.
 

Nilikuwa nakujibu hicho hapo chekundu...mahakama ya Kadhi kuwepo kwa mujibu wa sheria za nchi maana yake ni nini? Zitambuliwe kwenye katiba kama sheria za nchi?
Kwenye hayo maswali ndiyo likaja suala la dola maana ni sheria za nchi tu ambazo zinaweza kuwa enforced na vyombo vya dola...
 
Kwakweli udini ni ishu nyeti kwasasa kumekuwa na chuki ya wazi imepandikizwa na rais dhaifu huu ni ukweli mchungu na ndugu zangu waislam wanaangukia katika mtego huu wa udini. Me naona tuungane wakristo na waislam sisi ni ndugu tuikatae hii serikali dhaifu. Adui yetu ni uongozi mmbovu wa serikali ya ccm umaskini wa kutupwa na ufisadi sidhani kama udini utatupeleka mahala salama
 
Maneno mazito hayo Queen Kyusa,mwenye masikio na asikiie...
 
Last edited by a moderator:
Jk si mdini bali ni kiongozi mwenye subira kwa kila jambo sema tu sisi wananchi ndio tuokurupuka-kurupuka tu kwa kila jambo au neno lipitalo masikioni mwetu au machoni petu.sawa vigezi vilitumika katika hili kwa mtazamo wako yaweza kuwa sawa but kwa mtazamo mwingine si sawa.so no conclusion yet to jugde this issue may be after 10yrs to come and not now.
 
Nakubali mkuu,history will judge him...Lakini haina maana kuwa hatuna macho ya kuona na akili ya kufikiri.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…