Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
Binafsi najisikia kinyaa sana jinsi jinsi mnavyoendekeza udini.....nakumbuka kwenye uchaguzi mkuu 2010, JK kwenye mikutano ya kampeni karibu yote, alikuwa anakemea suala la udini....wakatokea wapumbavu wakasema ni hatari sana kwa kiongozi wa nchi kuzungumzia zungumzia udini wakati nchi haina udini....wakafikia hata kusema eti hali hii inaweza kuwafanya hata wale ambao hawakuwa na hisia za udini, wakaanza kuamka....leo, wale wale wanasema JK hakemei UDINI.....watu wa ajabu sana nyinyi!
Mkuu wala hujanijibu...
 
Mkuu wala hujanijibu...

Nijibu nini mkuu wangu?! Yaani nijibu kwanini JK hakuzungumza suala la masheikh wa huko Igunga?! Yaani Rais wa nchi aitishe Press Conference kukemea kilichoongelewa na kikundi cha watu wachache?! Huko Igunga hakuna DC? Hakuna RC? hakuna OCD? hakuna RPC? hakuna waziri husika?! hivi mauupuuzi kama hayo mbona yanafanywa kila uchao na tena na dini zote?! Kwahiyo kila siku uite press conference kukemea as if wahusika wanaotakiwa kufanya hivyo hawapo!!! Na ndio maana nimekupa mfano wa kipindi cha kampeni, ambacho hata wewe umekikwepa kukielezea kwavile unafahamu nini kilitokea!
 
Maneno ya kikwete kwenye uzinduzi wa bunge 2010: Hauhitaji hata kusoma sana katikati ya mistari kuelewa hoja ya jmushi1.

Kwenye uchaguzi wa ubunge kule Igunga, Mashehe waliwaita waandishi wa habari na kutangaza kuwa waislam wasiichague CHADEMA. Huu ni mfano hai wa UDINI.

NasDas, Ritz, Njiwa, Zomba... ni kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo?
Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi hii. Kiongozi anayetakiwa kuonyesha njia kwa vitendo, ameshafanya nini zaidi baada ya kutoa ile kauli 2010 kukemea udini?

Sina hamu ya kudiscuss sana nilikuwa nataka majibu tu hapo...
Wametumwa na JK,huyu mtu ni mdini sijapata ona.Hili jjkwaa,tulikuwa na umoja yani issue ya ufisadi ikija humu,hata wale watetezi hawakuwa wanaleta udini.Lakini kuna watu waliingia kwa kasi ya ajabu,nina uhakika walitumwa na ni mafisadi.Ndo wakaanzisha ya kuwatetea mafisadi eti wanaonewa kwakuwa ni waislam.Sitaki kuwataja kwasbabu hata majina yao yananichefua.Nilifika pahala nikajiuliza kama ni watanzania.Shida wanajificha nyuma ya mwavuli wa "annonymity",na kweli ukitaka kujuwa JF ni reflection ya wananchi,sasa udini uko mtaani.Wamejipanga,na JK ni kinara.Na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Kwenye thread hii,sidhani tunahitaji michango yao.Nchi itajengwa na wenye moyo.Nina marafiki na ndugu waislam lakini si type hii ya mifisadi hii humu ndani.Ningekuwa na uwezo wa kuwaona ningewalima shaba!Kwasababu hao hawataki maelewano,na haina haja ya kujadiliana na type hii ya watu.Hawana akili na kujadiliana nao ni upotevu wa muda.Mnajijuwa nilowataja.
 
Sijadiliani na wadini,we huna mpango wala huna haja ya kujibu posti yangu,changanya masaburi najuwa unamtetea baba yako.Kuna thread nyingi tu,peleka masaburi kwenye ile ya Zomba.

vipi mkuu wangu, mbona jazba?! amekushika pabaya, au?!
 
Mimi siamini kama JK ni mdini, ila ukisema ni mhuni nitakubaliana na wewe. Kwenye hili la udini hapana, ni moderate muslim, mwenda msikitini wa kawaida tu. Na huenda hata maana ya kuwa mdini haijui. Mimi najua mtu mdini anafanya kila linalowezekana kuhakikisha watu wa imani yake wanafaidi uongozi wake. JK amewasaidia nini waislam maskini wa Tanzania hii. Mfano chuo cha waislam morogoro hajawahi hata kukanyaga mguu. Hakichangii fedha. Chuo kimechoka, waalimu wachache, vifaa duni. Angekuwa mdini kweli angefanya mambo wakaenda maprofesa wa maana na kufaidisha watoto wa waislam maskini wasomao pale, kuna maaeneo ambayo uislam umejikita JK ameyafanyia nini, places like Kilwa, lindi, pangani, temeka Dar hapohapo. Hakuna hata dispendary mpya imefunguliwa, shule ni zilezile za Lowasa. Leo hii unamwita JK mdini mdini gani huyu? Sana sana anaabuse uislam kwa kupachika watu wenye majina ya kiislam wengi kwenye serikali yake. Na wao kama yeye hawasaidii waislam wenzake. Polisi kwenye rumande zote hapo dar pita jioni utakuta waislam wengi kuliko wakristu. Yes polisi mkuu ni Mwema na kaweka wachaga na waislam wengi kwene jeshi lake. Uhuni tusiuchanganye na udini
 
sasa mkuu! tukijadili udini wa jk wakati mleta mada yeye mwenyewe ni mdini! ... obvious wakati unaandaa kurusha thread yako ushaweka conclusion kichwani mwako! ... wewe ni mdini umejaribu sana kujificha lakini ndio hivo hisia zako zakuzidi muda mwengine! ... allegations hizi angetoa mtu aliye neutral kungekuwa na cha kujadili
Nimekwambia sema JK si mdini kwasababu hakuna udini Tz,hapo ntakuelewa.
 
Naskitika kuona malengo ya mtoa hoja yameshindwa kujadiliwa na kujibiwa kwa hoja imekuwa shutuma na jazba dhid yake.

Kama kikwete sio mdini inakuwaje anahutubia watu wahesabiwe sensa, ponda kwa upande wa pili anakataza watanzania wasihesabiwe je tunamarais wangapi?

Kama rais ni mmoja kikwete kwanin hajasema lolote kumkemea ponda kama alivofanya kwa mkoba, ulimboka, mgaya nk? Kunasirigan nyuma ya pazia kama sio udin?

Waislam wameilalamikia sana necta. Kama mkuu wa nchi amechukua hatuagan kukemea tatizo la udin sambamba na kufanya mabadiko yenye tija na kuwaleta pamoja watanzania wanoparuana ovyo kwa mising ya iman zao. Amekaa kimya moto unashika kasi kunaajenda gan nyuma ya pazia?

Tunashambuliana vikali kuhusiana na MOU, kama rais kabla raia wake hatujaanza kutoana roho kwanin asitowe ufafanuzi ili sote turidhike, kwakueleweshana sis hatuaminian, yeye tutamuamin si mkuu wa nchi? Kibaya zaid amekaa kimwa kam si malengo ya kutugawa kwa mising ya udin ni nin?

Tunahitaji umoja wetu kama watanzania.
 
Kaka yangu kwanza hongera kwa kuliona hilo na kulitilia hofu. Pili ni kwamba kaka umesahau kusema nini kifanyike. Labda mie niseme kwa ninavyoona.
1.kwanza kabisa serikali iache mara moja upendeleo kwa mujibu wa imani,iache kwa kuvunja mkataba wa kifisadi baina ya makanisa na serikali. Kaka mtoa mada kama kweli umeandika post hii ukiwa huru kifikra basi hili utaliona kama ni tatizo.
2.kanisa liache mara moja kuingilia siasa za nchi.
3.serikali ipige marufuku mara moja watu wa imani nyingine kuingilia maombi ya watu wa imani tofauti pindi waiombapo serikali yao jambo ambalo wao kwa mujibu wa imani yao litawasaidia,hapa mifamo iko wazi (a)mahakama ya kadhi wakristo inawahusu nini? (b)oic,ivi nchi kujiunga na oic kanisa litaathirika nini? Etc
4.serikali ishughulikie zile sehemu zenye kuleta migongano ya moja kwa moja mfano(a)baraza la mitihani NECTA hapo serikali inatakiwa ilivunje na liundwe upya kwa kuzingatia malalamiko yaliyopo. (b) mgawanyo wa madaraka serikalini unaupendeleo wa waziwazi hilo liondoshwe.
5.katika ngazi za kisiasa iwe marufuku kwa mtu yeyote ambaye ni kiongozi wa kiroho au aliyewahi kuwa basi asiruhusiwe kugombea nafasi yoyote ili kuzuwia mifano ya akina mchungaji msigwa bungeni aliposimama kuwatetea wakristo nawakati yeye si mbunge wa wakristo peke yao.
Naomba kwanza niishie hapo. Kama nawewe siyo muathirika wa huo udini naamini utaunga mkono ushauri wangu kwa serikali na watanzania kwa ujumla.
This is exactly what I call Grat thinking.Nashukuru sana kwa bandiko hili mkuu!Ni matumaini wahusika wanayaoana haya.Ningependa tujadiliane kwa njia hii.Huu ni mfano tosha kuwa si waislam wote wenye mawazo kama ya wafuasi wa JK na JK mwenyewe.Huwa tunatofautiana lakini nimeguswa sana na mchango wako huu.Stay blessed.
 
Nijibu nini mkuu wangu?! Yaani nijibu kwanini JK hakuzungumza suala la masheikh wa huko Igunga?! Yaani Rais wa nchi aitishe Press Conference kukemea kilichoongelewa na kikundi cha watu wachache?! Huko Igunga hakuna DC? Hakuna RC? hakuna OCD? hakuna RPC? hakuna waziri husika?! hivi mauupuuzi kama hayo mbona yanafanywa kila uchao na tena na dini zote?! Kwahiyo kila siku uite press conference kukemea as if wahusika wanaotakiwa kufanya hivyo hawapo!!! Na ndio maana nimekupa mfano wa kipindi cha kampeni, ambacho hata wewe umekikwepa kukielezea kwavile unafahamu nini kilitokea!
Ndiyo maana nilijumlisha viongozi wa serikali na yeye mwenyewe kikwete.
Kwani aliposema hapo chini alikuwa anamaanisha nini? kuitisha press conference kila siku??
Jambo hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila mmoja wetu. Nawaomba viongozi wa kisiasa ambao vitendo hivi vya kibaguzi vilifanywa na vinafanywa kwa niaba yao au kwa kuwanufaisha wao wasikae kimya. Watoe kauli kukemea uovu huu.
Ile ya Igunga nimetoa mfano tu. Kuna matukio mengi ya udini yanayopaswa kukemewa...
 
Sijadiliani na wadini,we huna mpango wala huna haja ya kujibu posti yangu,changanya masaburi najuwa unamtetea baba yako.Kuna thread nyingi tu,peleka masaburi kwenye ile ya Zomba.

Umeanza matusi kweli rangi yako ya ukweli inaanza kuonekana huwezi kujibu bila kutukana wafuasi wachadema naona matusi nimoja ya sera zenu
 
Wametumwa na JK,huyu mtu ni mdini sijapata ona.Hili jjkwaa,tulikuwa na umoja yani issue ya ufisadi ikija humu,hata wale watetezi hawakuwa wanaleta udini.Lakini kuna watu waliingia kwa kasi ya ajabu,nina uhakika walitumwa na ni mafisadi.Ndo wakaanzisha ya kuwatetea mafisadi eti wanaonewa kwakuwa ni waislam.Sitaki kuwataja kwasbabu hata majina yao yananichefua.Nilifika pahala nikajiuliza kama ni watanzania.Shida wanajificha nyuma ya mwavuli wa "annonymity",na kweli ukitaka kujuwa JF ni reflection ya wananchi,sasa udini uko mtaani.Wamejipanga,na JK ni kinara.Na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Kwenye thread hii,sidhani tunahitaji michango yao.Nchi itajengwa na wenye moyo.Nina marafiki na ndugu waislam lakini si type hii ya mifisadi hii humu ndani.Ningekuwa na uwezo wa kuwaona ningewalima shaba!Kwasababu hao hawataki maelewano,na haina haja ya kujadiliana na type hii ya watu.Hawana akili na kujadiliana nao ni upotevu wa muda.Mnajijuwa nilowataja.

jmushi1 bhana, kwa danadana tu hujambo!! cheki ulivyopindishapindisha mambo hadi sasa unataka kuonesha kwamba dhima ya wanaopingana na wewe ni kuwalinda mafisadi wa kiislamu!!! Sina shaka kwamba humu tumekuwa pamoja tukipinga ufisadi....lakini hili la leo, hapana mkuu wangu; usituchezee akili....thread yako inahakisi UDINI wako wewe mwenyewe kuliko ambavyo unataka tuamini. hebu weka wazi mkuu wangu....nini base yako hapa?! Kwamba JK ni MDINI au FISADI?! Ni nani hao MAFISADI WA KIISLAMU unaosema huwa wanatetewa na kwamba wanasakamwa ufisadi kwa kuwa ni waislamu?!
 
Mtoa mada unaonesha kuwa wewe ni mdini mkubwa,kuhusu kufungiwa gazeti la mwanahalisi na kuachwa an-nur ni hivi vyombo vya habari vya kiislam havikurupuki huwa ushahidi vinapotoa kitu, sasa wakitaka kujua nguvu ya waislam wafungie redio imani na vyombo vya habari vingine vya waislam
 
Huenda hao nao ni waislamu pia!

kikwete kama rais wa nchi ana viongozi wa ngazi za chini ambao wanauwezo wa ku handle issue kama hizo .. Sio kila jambo aongee kikwete! sasa kazi ya wakuu wa mikoa .. Mawaziri.. Etcl itakuwa ni nini..?!

Ndiyo maana nilijumlisha viongozi wa serikali na yeye mwenyewe kikwete.
Kwani aliposema hapo chini alikuwa anamaanisha nini? kuitisha press conference kila siku??

Ile ya Igunga nimetoa mfano tu. Kuna matukio mengi ya udini yanayopaswa kukemewa...

Usitake kuniambia kwamba umeshasahu mlipodai kwamba JK anazungumzia zungumzia udini kwenye kampeni wakati nchi hii haina udini......au mkuu wangu wakati wa kampeni ulikuwa Alaska nini?!
 
vipi mkuu wangu, mbona jazba?! amekushika pabaya, au?!
kwenye hilo grupu lenu la wadini hakuna wa kunishika pabaya,never!mnajiona eti nyie zaidi ya binadamu wengine.I hate people who wears religion on their sleeve!mmeharibu nchi kwa ufisadi na udini.Mtalipa na kinara wenu JK.
 
Wewe na kanisa Ndio mnaharibu nchi hii
 
Binafsi najisikia kinyaa sana jinsi jinsi mnavyoendekeza udini.....nakumbuka kwenye uchaguzi mkuu 2010, JK kwenye mikutano ya kampeni karibu yote, alikuwa anakemea suala la udini....wakatokea wapumbavu wakasema ni hatari sana kwa kiongozi wa nchi kuzungumzia zungumzia udini wakati nchi haina udini....wakafikia hata kusema eti hali hii inaweza kuwafanya hata wale ambao hawakuwa na hisia za udini, wakaanza kuamka....leo, wale wale wanasema JK hakemei UDINI.....watu wa ajabu sana nyinyi!

Mkuu mim naunga mkono ulichoandika hapo juu.

Swali langu kwako nawengineo ni hili.

Kazi ya kiongozi hasa wa nchi kama kikwete nikuongea tu au nikuongea, kukemea pamoja na kuchukua hatua?

Ww unaongea, mm naongea na yule anaongea tofauti yetu na rais ni nin? Maana na yeye anaongea kama sisi.

Kama aliona huo udin kama ulivokili hapo juu, alichuku/amechukua hatuagan kutustil wtz na balaa inayotukabili? Au anaongea kama mm.
 
Unapojiunga na ukristo unaandikishwa kwenye daftari na unapewa kitambulisho cha ukristo. Je, ni hivyo pia katika dini zingine au?
Pia kuna centralized system of governance katika ukristo, kwa hiyo unapojenga kanisa lazima lifuate taratibu za kuandikishwa na kuonyesha kweli kama kuna haja ya kuwepo na kanisa hapo. Na ujengapo lazima liwe classified, mathalani KIGANGO, PAROKIA au CATHEDRAL (Kanisa la kiaskofu). Sina uhakika kama katika dini zingine hili linafanyika, if I am to ask!
Kwa sasa naona watu wanajenga makanisa holela na si kwa utaratibu uliozoeleka hapo awali, kwa hiyo yanaweza yasiwe na takwimu sahihi za waumini wake. Isipokuwa kwa makanisa kama KKKT na CATHOLIC nina uhakiwa wanabatiza waumini wao wakiwa wadogo na wanawaandikisha katika kitabu cha orodha ya waamini. In this way, ni rahisi sana kujua idadi yao!
Sasa basi, nashauri tunapounganisha nguvu kuondoa umaskini katika nchi yetu; tujitahidi kuacha propaganda zisizo na tija na kuwa focused na maendeleo yetu. Ukitaka kujua mpo wangapi basi tengeneza mfumo utakaosaidia bila kulazimisha wengine nao wakufanyie kazi yako.
MUNGU ATUJALIE HEKIMA TUVUKE SALAMA, KWANI PEPO LA UDINI LINATUZENGEA!
 
Mtoa mada unaonesha kuwa wewe ni mdini mkubwa,kuhusu kufungiwa gazeti la mwanahalisi na kuachwa an-nur ni hivi vyombo vya habari vya kiislam havikurupuki huwa ushahidi vinapotoa kitu, sasa wakitaka kujua nguvu ya waislam wafungie redio imani na vyombo vya habari vingine vya waislam

Kumbe yana ushahidi yale ya gazeti la sauti?ebu uweke hapa hili ni jukwaa huru.Vyombo vya habari vyenye kuchochoe hisia za kidini ni hatari kwa usalama wa taifa kama mlivyo wachochea udini.
 
jmushi1 bhana, kwa danadana tu hujambo!! cheki ulivyopindishapindisha mambo hadi sasa unataka kuonesha kwamba dhima ya wanaopingana na wewe ni kuwalinda mafisadi wa kiislamu!!! Sina shaka kwamba humu tumekuwa pamoja tukipinga ufisadi....lakini hili la leo, hapana mkuu wangu; usituchezee akili....thread yako inahakisi UDINI wako wewe mwenyewe kuliko ambavyo unataka tuamini. hebu weka wazi mkuu wangu....nini base yako hapa?! Kwamba JK ni MDINI au FISADI?! Ni nani hao MAFISADI WA KIISLAMU unaosema huwa wanatetewa na kwamba wanasakamwa ufisadi kwa kuwa ni waislamu?!
Mkuu bandiko langu la kwanza umelisoma vyema?hakuna danadana yoyote,JK ni mdini na hapendi suluhu kabisa.Hii hali iliyopo nchini wala hata hajali.Ndo hapo tunaona anafuraia.Watetezi wake wote kwenye issue za ufisadi,huwa wanalia udini na ni wauwaji wakubwa wa mwalimu humu ndani.Na nimesema hapo nyuma kwamba inawezekana bifu lake ni alipoondolewa kwenye kugombea urais.Akakiuka hata ile miiko ya unofficial,akataka awe rais anyways licha ya kwamba mzee Mwinyi ndo alikuwa kamaliza muda wake.Yeye ni mmojawsapo anaoamini uonevu dhidi ya uislam,na kwahiyo njia aliyoichukuwa kusolve tataizo hilo kama lipo,ni njia mbaya.Na pia nikasema kwasababu ana kashfa kibao za ufisadi,kuchochea kwake udini ndo salama yake kwasababu ni "a divide and rule" tactic.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom