masluphill
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 540
- 259
Wana UAMSHO rudini darasani,vinginevyo mtatumiwa saana na CCMizi,hamjajua tu kama mshatumiwa na sasa hamtakiwi kwa kuwa kwa sasa hamna kazi ya kuwafanyia?,we vuta subira mtatakiwa tena senso ikiisha baada ya kuwa mmeorodheshwa kwa lazima mbali na TANGAZO lenu kuwa msilm yeyote atakae he,,sa,,bi,,w.a ni ''KHAFIRI'' Ww vp? siku zinakwisha ushachukua ukhafiri wako?,Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania
web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????
Jk ajaleta udini kama unavyotaka kulazimisha, wewe unasukumwa na chuki za udini bahati nzuri humu JF tunajuana kwa michango yetu wewe ni mdini mkubwa tena una chuki kubwa na Waislam na Uislam kwa ujumla, bora angekuja mtu mwingine kuanzisha hii thread labda tungemulewa lakini sio wewe Mushi, ndio maana unakwepa kumelezea Mtei kuhusu udini wake sababu ni kambi yako, unachofanya kwenye hii thread yako ni kiziba shimo la panya na mkate.
@jmushi1, sasa hapa ndipo unapokosea kuweka mada hii lakini hutaki kusahihishwa kwa sababu ya nimani yako wewe. Nakwambia tu mdini ni wewe na hilo la gazeti la sauti ni tuhuma ambazo nakitaka chama changu kikanushe kama ni uongo maana Chadema sio Dr. Slaa hata siku moja ameingia chama kakikuta kama sisi tulivyokikuta.
Yeye ni binadamu na anaweza kushawishika kwa lolote, hivyo siwezi kuweka dhamana yangu kwa mtu yeyote hata iwe mwanangu wa kumzaa anaweza kushawishika..Sipo Chadema kwa sababu ya Dr. Slaa, Mbowe wala Mnyika isipokuwa naamini ktk kupingana na sera za CCM na tuko mstari mmoja..Kama Chadema watazienzi baadhi ya sera za CCM zinazoendeleza ya mkoloni kwa madai ya Udini wakati elimu na Afya vinadorora nchini sintokubali kuendeshwa.Natanguliza fikra na mawazo yangu yanawakilishwa na chama gani ktk harakati hizi sio kuamini na kushabikia Uchadema..
Siyo lazima uchangie.
jmushi1,Udini uko nchini mwetu kuliko wakati wowote ule toka tupate uhuru.Kwani JK ana agenda ya kusilimisha taifa?Unadhani hata wasio na dini watakubali?hujui kuna wazalendo wa kweli watakaoyachanja makalio ya wadini?kama huamini,subiri tufike huko.Tuna muda na nafasi za kutizama kwa macho ya kizalendo,na kulipigania taifa hili na watu wake.Ninarudia tena,mafisadi wanajificha kwenye mwavuli wa udini,hilo hawataweza.Over our dead bodies,and I'm talking about nationalist and true patriots.
Kwenye uchaguzi wa ubunge kule Igunga, Mashehe waliwaita waandishi wa habari na kutangaza kuwa waislam wasiichague CHADEMA. Huu ni mfano hai wa UDINI.Hatari ya Uchaguzi 2010 kwa Umoja
Naomba nirudie kuelezea kusononeshwa na kusikitishwa kwangu na baadhi ya
viongozi wa dini na wanasiasa waliowataka Watanzania wawachague watu kwa dini zao. Jambo hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila mmoja wetu. Nawaomba viongozi wa kisiasa ambao vitendo hivi vya kibaguzi vilifanywa na vinafanywa kwa niaba yao au kwa kuwanufaisha wao wasikae kimya. Watoe kauli kukemea uovu huu. Hapa nchini Watanzania wenye dini mbalimbali wanafanya kazi pamoja, wanasaidiana, wanashirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii bila kujali dini zao, wanaishi pamoja.
Tusikubali zipandikizwe mbegu za chuki baina ya Watanzania.
Nawapongeza na kuwashukuru Watanzania kwa kukataa kugawanywa kwa misingi ya dini katika uchaguzi huu. Narudia wito wangu kwamba sasa viongozi wote wa siasa, wa dini, wanahabari, viongozi wa kimila, kijamii na wengineo wanaoipenda nchi yetu, tuungane kuziba nyufa na kutibu majeraha yaliyoletwa na uchaguzi huu.
Mjadala siyo jmushi1 hapa,kafungue thread hapa si pahala pake.Mkishindwa hoja ndo mnaleta personal attacks.Mjadala hapa ni mkuu wa nchi na udini wake.Unachotakiwa useme ni kwamba JK si mdini base on so and so...
Wanajihesabu WENYEWE makanisani.Basi na nyie muwaige kwa kujihesabu huko misikitini mtajua IDADI yenu ni ngapi?Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania
web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????
Maneno ya kikwete kwenye uzinduzi wa bunge 2010: Hauhitaji hata kusoma sana katikati ya mistari kuelewa hoja ya jmushi1.
Kwenye uchaguzi wa ubunge kule Igunga, Mashehe waliwaita waandishi wa habari na kutangaza kuwa waislam wasiichague CHADEMA. Huu ni mfano hai wa UDINI.
NasDas, Ritz, Njiwa, Zomba... ni kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo?
Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi hii. Kiongozi anayetakiwa kuonyesha njia kwa vitendo, ameshafanya nini zaidi baada ya kutoa ile kauli 2010 kukemea udini?
Sina hamu ya kudiscuss sana nilikuwa nataka majibu tu hapo...
Nchi ilipofikia,credits huwa anapewa rais na serikali yake,kwahili la udini,hakuna ubishi umeshaota mizizi.Na sijawahi kusikia kauli ama vitendo kutoka kwa JK vya kukemea haya mambo ya udini.
Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani.
Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)
Ninamini kabisa kuwa tulipofikia,uwezekano wa kuingia kwenye vurugu na mapigano ya kidini ni mkubwa kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya Tz toka tupate uhuru.
Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive.
Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!....
Maneno ya kikwete kwenye uzinduzi wa bunge 2010: Hauhitaji hata kusoma sana katikati ya mistari kuelewa hoja ya jmushi1.
Kwenye uchaguzi wa ubunge kule Igunga, Mashehe waliwaita waandishi wa habari na kutangaza kuwa waislam wasiichague CHADEMA. Huu ni mfano hai wa UDINI.
NasDas, Ritz, Njiwa, Zomba... ni kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo?
Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi hii. Kiongozi anayetakiwa kuonyesha njia kwa vitendo, ameshafanya nini zaidi baada ya kutoa ile kauli 2010 kukemea udini?
Sina hamu ya kudiscuss sana nilikuwa nataka majibu tu hapo...
Hayo ni majibu ya kitoto mkuu. Kama wanajihesabu kanisani inamaana na hizo takwimu za waislam walizipata hukohuko kanisani? Hayo ndiyo majibu huketaWanajihesabu makanisani.Basi na nyie muwaige kwa kujihesabu huko misikitini mtajua hesabu yenu ni ngapi?
Ndiyo maana nikauliza, kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo.
kikwete kama Rais wa nchi ana viongozi wa ngazi za chini ambao wanauwezo wa ku handle issue kama hizo .. sio kila jambo aongee kikwete! sasa kazi ya wakuu wa mikoa .. mawaziri.. etcl itakuwa ni nini..?!
JF sio mali yako hii thread ungeifungulia chumbani kwako kama unachaguwa watu wa kuchangia, JF ni jukwaa huru.