Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

WANAOMCHAFUA LOWASSA NI WALEWALE, HAWAONGEZEKI NA AJENDA ZAO NI ZILEZILE


MUHIMU SANA


Lowassa ndiyo habari ya mjini
Lowassa ndiye anayezungumzwa
Lowassa ndiyo ajenda ya Taifa
Lowassa amewakip bize wahariri wa vyombo vya habari kwani ndiye anayefanya magazeti yauzike
Kila siku ni Lowassa,,Lowassa, Lowassa

Hivi huyu ni nani hasa

Tumekuwa tukiwakumbusha Watanzania kuhusu huyu mtu anayeitwa Lowassa,mtu muungwana,mtu mwenye hofu ya Mungu,mtiifu kwa chama chake cha Mapinduzi,mkarimu, mtanashati,mtu aliyejaliwa kipaji cha uongozi,mtu aliyejaliwa hekima na busara,haropoki na siku zote amejikita katika kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili watu wake,naam ukisikia Lowassa anazungumza basi ujue kuna agenda ya maendeleo mezani


Hata hotuba zake ni authoritative,hotuba zenye mamlaka,akifika mikoani hata hotuba zake huwa ni majawabu na tiba kwa matatizo ya Wananchi

Kamwe hapendi kulia lia,anaamini kulia lia mbele za Wananchi kama afanyavyo Pinda ni laana mbele za Mungu


Kwa bahati mbaya,pamoja na Mungu kumpa vipaji vyote hivyo mh Lowassa kuna Wanasiasa wachovu,waliofilisika ubongo ,ambao kila kukicha mradi wao mkubwa ni kuchafua taswira ya Lowassa katika jamii,na hakika nao wamepata mawakala wao katika shughuli hii ya kishetani

Cha kuchangaza ni kwamba,wanasiasa wanaomchafua ni walewale,mawakala wao ni walewale na ajenda zao ni zilezile

Mawakala wa hawa wanasiasa mufilisi wana changamoto kubwa,nayo ni kutopewa SEMINA ELEKEZI

Mawakala hawa hawana uelewa mpana kuhusiana na kashfa hizo

Leo utasikia,Lowassa alihusika kwenye kashfa ya richmond,baadhi watakwambia alichukua fedha ya richmonda,ukiwauliza ni sh ngapi,hawajui

Kesho wanakuja na agenda ya kimizimu kwamba Mwl Nyerere alimkataa,ukiwauliza wakupe ushahidi wanakusimulia kuhusu Uchaguzi mkuu mwaka 1995 ambapo Mwl alimbeba BEN,ukimwambia mwaka 95 Lowassa alikuwa kijana mno na kwamba Mwl Aliona BEN alikuwa mkomavu zaidi na hivyo alikuwa anatosha kukabidhiwa taasisi ya Urais,wanakimbia

Ukiwaambia Mwl alijua zamu za JL na Lowassa inakuja,wanagota

Wakati fulani watakwambia Huyu mtu ni mgonjwa,hii agenda siji wanaitoa wapi,maana Mwenyezi Mungu ndiye anayejua majaliwa ya Mwanadamu

Wanaokesha kutoa hoja hii potofu,ni walewale ambao mwaka 2005 walizunguka nchi nzima kuwaaminisha Watanzania kwamba Jk ni mgonjwa,na mawakala wao


Hata hivyo,sisi tulio wengi tunaoamini Lowassa anatosha na anafaa kuwa Mrithi wa JK rai yetu ni hii-Nyinyi mnaomchafua Lowassa kila kukicha tengenezeni ground ya kumchafua kwani ajenda zenu zimechakaa,na mmecheewa kwani train imeshafika Dodoma


Chukueni maamuzi mgumu ambao ni-SIMAMENI MUHESABIWE
Mnarudia rudia sana yale yale!Kimsingi jamaa yenu amekwisha kwama!
 
hivi wewe upo dunia ya ngapi.Katika kipindi cha miaka 2 aliyokaa madarakani bwana EL kajenga shule za kata kibao,chuo cha dodoma na mradi wa maji wa ziwa victoria kupeleka mikoa ambayo haikua na maji ya shinyanga,simiyu na Geita.Sasa unvosema hajafanya kitu mie nakushangaa sana na kuhusu ufisadi ile hela walipiga watu wengi sana ila yeye ndiye aliyekua mbuzi wa kafara.

acha kero, acha kurefusha uzi bila sababu za msingi.
 
WANAOMCHAFUA LOWASSA NI WALEWALE, HAWAONGEZEKI NA AJENDA ZAO NI ZILEZILE


huyu mtu anayeitwa Lowassa,mtu muungwana,mtu mwenye hofu ya Mungu,mtiifu kwa chama chake cha Mapinduzi,mkarimu, mtanashati,mtu aliyejaliwa kipaji cha uongozi,mtu aliyejaliwa hekima na busara,haropoki na siku zote amejikita katika kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili watu wake,naam ukisikia Lowassa anazungumza basi ujue kuna agenda ya maendeleo mezani




Wananchi kama afanyavyo Pinda ni laana mbele za Mungu


Inatosha kukujua we ni mtu gani.
 
hakuna kazi aliyotenda zaidi ya kuchakachua..... apumzike tuu.
 
WANAOMCHAFUA LOWASSA NI WALEWALE, HAWAONGEZEKI NA AJENDA ZAO NI ZILEZILE


huyu mtu anayeitwa Lowassa,mtu muungwana,mtu mwenye hofu ya Mungu,mtiifu kwa chama chake cha Mapinduzi,mkarimu, mtanashati,mtu aliyejaliwa kipaji cha uongozi,mtu aliyejaliwa hekima na busara,haropoki na siku zote amejikita katika kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili watu wake,naam ukisikia Lowassa anazungumza basi ujue kuna agenda ya maendeleo mezani




Wananchi kama afanyavyo Pinda ni laana mbele za Mungu


Inatosha kukujua we ni mtu gani.

kweli uzi ni mfupi kuliko wangu hapo juu. Endelea kuandika nyuzi fupi mkuu ili ujulikane nawe unachangia.
 
WANAOMCHAFUA LOWASSA NI WALEWALE, HAWAONGEZEKI NA AJENDA ZAO NI ZILEZILE


huyu mtu anayeitwa Lowassa,mtu muungwana,mtu mwenye hofu ya Mungu,mtiifu kwa chama chake cha Mapinduzi,mkarimu, mtanashati,mtu aliyejaliwa kipaji cha uongozi,mtu aliyejaliwa hekima na busara,haropoki na siku zote amejikita katika kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili watu wake,naam ukisikia Lowassa anazungumza basi ujue kuna agenda ya maendeleo mezani




Wananchi kama afanyavyo Pinda ni laana mbele za Mungu


Inatosha kukujua we ni mtu gani.

kweli uzi ni mfupi kuliko wangu hapo juu. Endelea kuandika nyuzi fupi mkuu ili ujulikane nawe unachangia.
 
nimeshtushwa na wazee wa sebule kuu.
Ni mchana huu baada ya kuhudhuria lunch ''majris''.
Namnukuu mmoja wao.
''safari hii ni zamu ya wakristu.akafinyanga tonge....
Na katika wakristu lowasa tunamkubali.......akameza.......
Maana ameshatuweka sawa.''kimya.......
Nilisikia kizunguzungu na biriani yoote ikayeyuka.
Nikajikausha, kama sijasikia..........
Huyoo nikaosha mikono nikasepa.
 
[h=2]Lowassa ageuzwa mtaji[/h]

Na Mwandishi Wetu

KUONGEZEKA kwa idadi ya watu wanaokwenda kumtembelea mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwa madai ya kwenda kumshawishi agombee urais, inaelezwa wanafuata kiasi kikubwa cha posho wanachopata kutoka kwa mbunge huyo ambaye anawania urais.

Jana mbunge huyo alipokea watu zaidi ya 715 kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao inadaiwa walikwenda kumshawishi agombee urais, ingawa inaelezwa watu hao walilipwa posho na kuponda raha ndani ya jimbo hilo kwa gharama za Lowassa.

Kwamujibu wa kada mmoja wa CCM ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara huo alisema, kabla ya kufikia makubaliano ya kuanza safari ya kwenda Monduli, kila aliyekubali kufanya kazi hiyo, aliahidiwa posho ya shilingi 150,000 ambayo walilipwa baada ya kufika jimboni humo.

Kada huyo ambaye alikuwa mmoja wa walioandaa msafara huo, alisema pia waliandaliwa malazi na kila mmoja alitakiwa kuhakikisha analala kwenye hoteli inayogharimu shilingi 25,000, huku akitakiwa kutumia vinywaji visivyozidi shilingi 40,000 kwa siku tatu watakazokaa Monduli.

Aidha, ndani ya kundi hilo kulikuwa na wazee 15 ambao kila mmoja alilipwa shilingi 300,000, huku bajeti ya mafuta kwa magari binafsi na mabasi yaliyokuwa kwenye msafara huo yakitengewa shilingi 26,500,000 ambapo jumla inayoelezwa kutumika kwa safari hiyo inakadiriwa kufikia shilingi 382,675,000 na inaelezwa kila kundi linalofika hapo linapokea kitita chake kulingana na umbali waliotoka, wingi na umuhimu wao kwa jamii.

"Nikueleze ukweli ndugu yangu hili ni dili, kuna watu walitufuata wakasema tujikusanye twende kwa mheshimiwa Lowassa na yupo tayari kugharamia safari yetu na kila kitu kwa siku tutakazokuwa kule ili ionekane kuna watu wanamuunga mkono kwenye harakati zake za urais, hakuna lolote hapa ni mipango tu ya mjini hii" alisema kada huyo wa CCM kutoka Manyara.

Kada huyo aliendelea kusema: "Unajua huu ndio wakati wa mavuno, ukipita hawa waheshimiwa hawapatikani, sasa watu wanapeana taarifa kwamba mambo yapo Monduli, ndio maana watu wanapishana kila kukicha, wengi wanatamka wazi kwamba nao wanaambulia hela zilizoibwa serikalini na huyu bwana (Lowassa)"

Kundi hilo la watu 715 kutoka mikoa mbalimbali, lilipishana na kundi jingine la wafanyabiashara ndogondogo ambalo nalo kama wengine waliopo kwenye mpango huo, walimpatia Lowassa fedha wanazodai kuchanga kwa ajili ya kuchukulia fomu ya urais, sambamba na kadi ya uanachama na baadaye inaelezwa kiongozi wao alikabidhiwa kitita cha fedha ili kumalizia sehemu ya fedha walizopewa awali kama walivyokubaliana.

"Huu ni mgodi mzee, wacha tupige hela huyu ni fisadi hatuwezi kumpa nchi, kwanza amechoka na tumejionea wenyewe kwa macho, halafu tulikuwa tunasikia watu wanakula hela walau nasisi tumepata chochote" alisema kijana mmoja kutoka kanda ya ziwa.

Hata hivyo, inaelezwa makundi mengine baada ya kusikia watu wanaokwenda Monduli wanalipwa, nao wanajikusanya na kuanza safari ya kulekea jimboni hapo kabla Lowassa hajarudi bungeni kwaajili ya bunge la bajeti.

Taarifa kutoka Mkoani Simiyu zinasema, kundi kubwa la watu linatarajia kuwasili Monduli na tayari wapo watu wanaotembeza daftari kuchangisha fedha za kukodi basi za kuwafikisha huko, huku wachangishaji wakisisitiza wakifanikiwa kufika Monduli fedha hizo zitarudi na watapata na faida.

Watu mbalimbali wanasema, hii ni aina nyingine ya mtindo wa Lowassa kugawa fedha, ambapo kila mwaka amekuwa akiandaa sherehe nyumbani kwake Monduli na kuwakaribisha watu kutoka sehemu mbalimbali nchini ambapo wahudhuriaji wamekuwa wakilipwa posho na kurudishiwa gharama za nauli zao walizotumia ikiwemo mabasi, ndege na usafiri binafsi na kuandaliwa chakula, vinywaji na malazi kwa siku wanazokaa jimboni humo.

Hata hivyo, mwaka jana sherehe hizo hazikufanyika huku sababu za kiafya za mbunge huyo zikitajwa, ambapo licha ya watu kupewa taarifa kusitishwa kwa sherehe hizo, bado waliendelea kumiminika nyumbani kwa Lowassa ambaye hakuwepo jimboni humo.

"Tutarajie wageni wengi zaidi, maana watu wanajua wakifika wanapata chochote ila sidhani kama wote wanamuunga mkono kwa dhati huyu mzee, watu wanapiga hela tu si unawajua wabongo wakijua wapi kuna mteremko wanajaa, kuna sura nimeziona humu nimeziona kwa wagombea wengine, huenda hii ni ajira yao" alisema mmoja wa vijana waliokuwa kwenye msafara huo.
 
Ukiona mtu anamsifia mtu mchafu kama Lowasa basi ujue yeye ni mchafu zaidi mpaka ananuka.
 
anaandaa timu ya kuingia msituni au ikulu??
 
Back
Top Bottom