Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Labda anaweza pia kutufundisha jinsi ya kutajirika kwa kutumia cheo cha serikali bila kugundulika.
 
Labda anaweza pia kutufundisha jinsi ya kutajirika kwa kutumia cheo cha serikali bila kugundulika.

Lowassa siyo tajiri fedha ni tajiri wa watu pia siyo mbadhirifu kipato chake zaidi ya kutoa zaka. Na pale anapotoa sadaka anarudishiwi maradufu!
 
% ndogo ya Watanzania wenzangu wamepandikiziwa na kuziamini Proaganda za kumchafua Lowassa lakini uhalisia wa maisha yake kwa Uadilifu na Uaminifu Mh. sio Fisadi.

Ni nani aliye na ushahidi kuwa Lowassa alikula mabilioni ya EPA & RICHMOND alete hizo taarifa atuwekee hapa.(usituwekee taarifa za Uongo maana kweli itatuweka huru)

Tofauti na Escrow Waheshimiwa wengine wameondoka na bilioni 8,Mwingine bilioni 70 na wengine bilioni 1.6 na wengine milioni 400 wakatia kibindoni.

Fedha alizonazo Eddo ni halali na tujue mtu yeyote mwenye uthubutu wa kuleta changes lazima itamugarimu kutokwa JASHO,MIKAKATI MIZURI,AWE NA UHUSIANO MZURI NA RASILIMALI WATU PIA ZITAMTOKA FEDHA.

Watanzania tuache kuziamini propaganda zenye lengo la kumchafua Lowassa.

Anaendesha siasa zake kwa kuonyesha yeye ni Mtu mzima AMEKOMAA KISIASA.
 
Lowassa siyo tajiri fedha ni tajiri wa watu pia siyo mbadhirifu kipato chake zaidi ya kutoa zaka. Na pale anapotoa sadaka anarudishiwi maradufu!
Hata mtoto wa darasa la nne atakuona wewe punguani kwa kauli hiyo.
 
Edo hana afya ya kuongoza nchi,mnaompigia chepuo awe raisi kwa nini msimshauri akapime afya kwanza.itakuwa jambo LA ajabu kama tutamchagua MTU mgonjwa kuwa rais.
 
wanaukumbi tusiifanyie masihara nchi yetu, mtu fisadi lililokubuhu au mnataka kumkabidhi fisi bucha? huyo mwajiri wenu anatamaa ya kutajirika na kadri anavyo pata pesa ndivyo tamaa ya kutaka zaidi inavyozidi hata kama ni ajira oneni aibu.
 
Nakumbuka vizuri kwenye miaka ya 80 mwisho na miaka ya 90 mwanzo sangasinga WA iliyokuwa Tanganyika bus huko mwanza waliachana na masuala ya usafirishaji na kujenga mahoteli. Mojawapo ya hotel hizo ni Tilapia. Hii hotel no vibanda kadhaa vilivyojengwa katika maji ya ziwa Victoria karibu na mtambo unaosindika maji kwa matumizi ya watu WA Mwanza. Timu ya uhandisi ya Manispaa us. Mwanza kwa wakati ule ilikatalia singasinga hao kuanza kuitumia had I watakapopatia ufumbuzi WA kinyesi kutoka hotelini mwao kutoingia ktk maji ya ziwa hususani ni hotel hiyo kuwa karibu na maji yanayopelekwa kwa wakazi WA jiji kwa matumizi yao ya kupika, kunywa na kadhalika. Kwa kushindwa singasinga hao kudivert kinyesi kisichafue maji wali kutana na Lowassa akiwa waziri WA Ardhi wakati WA ziara take Mwanza na yy bila kuwauliza wahandisi WA manispaa akaagiza hotel ianze kutumika hivyo hivyo. Tuliushangaa uamizi huo na kujiuliza sababu iliyomfanya kufumbia macho suala nyeti kama hilo. No upenzi. wake kwa singasinga au kuna namna? Leo hii anaitwa mchapa kazi kwa manufaa ya NANI? Nipeni mfano WA ubora wake aliwahi uonyesha kwa wakulima ambao no zaidi ya 80% ya wtz. ktk kukuza na masoko ya maxao yao. Leo hii wampendee kitu gani? Kams hakujali kuwalisha mavi watu WA Mwanza atafaa kwa lipi LA kumsifia.
 
Nimeingia kwenye uzi huu nikajua una hoja ya msingi, kumbe bado ni muendelezo wa ushabiki wa kisiasa
 
Mimi ni Mwandishi wa gazeti la Mwananchi. Wiki
mbili zilizopita tulikuwa na mjadala mkali sana
kwenye kikao cha uhariri cha kuamua habari kuu
za gazeti. Mjadala ulikuwa juu ya picha iliyotumwa
na mpiga picha wetu kutoka Dodoma. Kuna baadhi
ya wenzetu walitaka picha hiyo iwekwe ukurasa
wa mbele wa gazeti. Kuna wengine hawakutaka
kabisa iwekwe gazetini kwani gazeti lingeonekana
ni nyenzo ya propaganda za siasa za Urais ndani
ya CCM.
Muafaka ukafikiwa kwamba iwekwe nyuma
kwenye ukurasa wa michezo, ingawa nako
kulikuwa na mjadala kwamba Lowasa ni
mwanamichezo tangu lini. Wengine wakahoji
kwamba tukiulizwa kwamba ilikuwaje gazeti letu
likawa kwenye mazoezi ya Lowassa tutasemaje
kwani huwa hakuna taarifa kwa umma kuhusu lini
Lowasa anafanya mazoezi na anapitia njia zipi.
Baada ya mzozo kuisha, baadhi yetu tukaamua
kufanya uchunguzi wa kina kwamba ilikuwaje
mpiga picha wa gazeti akawa sehemu ya mazoezi
ya Lowasa? Je alialikwa? Je alikutana naye kwa
bahati mbaya? Pia wakati tunajadili kuhusu hii
picha, kulikuwa na presha kubwa sana kutoka
Kwa Mzee Lowasa mwenyewe kuja kwa viongozi
wetu wakuu kwamba kwa gharama yoyote ile
(wengine walisema milioni 10) picha hiyo lazima
itoke ukurasa wa mbele. Bahati nzuri mantiki
ikashinda na tukaliokoa gazeti kutoka kwenye aibu
ambayo tungeipata.
Katika uchunguzi wetu ilibainika kwamba Bwana
Abubakari Liongo, mbeba hela za Lowasa kwa
waandishi, aliwatafuta wapiga picha wetu na
kuwaambia kwamba kuna tukio muhimu la dakika
10 kwa Lowassa. Akatuma gari kumpeleka mpiga
picha alipokuwa anatembea Mzee. Akapiga picha
ya kutembea. Washauri wa Mzee wakamuomba
akimbie kidogo, ikapigwa picha ya kukimbia.
Mpiga picha akaambiwa arudishwe lakini
akaamua kubaki kwakuwa ilikuwa ni karibu na
mahali anapoenda. Akashuhudia Mzee akipanda
gari na kuondoka. Ukitazama picha kwa makini
utaona Landcruiser iko kwa nyuma.
Swali ni kwanini hadaa yote hii? Sababu ni
kwamba ni kweli afya ya Mzee Lowassa
imedhoofika. Kila mwezi anaenda kutibiwa
Ujerumani, mikono inatetemeka na jicho moja
linakaribia kufunga kabisa. Sababu ya kutaka
picha hii itoke kwa gharama kubwa ni kujaribu
kuuonyesha umma kwamba yeye ni mzima. Wapi
wazee wengi wanaofanya mazoezi kila siku lakini
hawahangaiki na kupigwa picha. Mzee Mwinyi
ana miaka 89 na anatembea na kukimbia kila siku.
Dr. Salim anakimbia kila siku. Jenerali Mirisho
Sarakikya ana miaka 80 na anapanda Mlima
Kilimanjaro kila mwaka kwa mwaka wa 30 sasa.
Hatuoni wakihaha kupiga picha na kuzisambaza
mitandaoni. Mazoezi magumu kwa Lowasa ni
kushika kikombe cha chai kwa dakika 3.
Binafsi nimepata woga. Nimepata woga kutokana
na uroho mkubwa wa madaraka ulioonyeshwa na
timu ya Lowassa. Wako tayari kufanya chochote
kupata madaraka. Bahati nzuri hadi sasa mambo
mengi wanayoyafanya ni maigizo tu, ikiwemo hili
la kutengeneza mazoezi feki na kuitengea bajeti
picha ili ichapwe gazetini ni kusambazwa
mitandaoni. Mungu Ibariki nchi yetu
 
Kiukweli tukiacha utani Lowasa hafai kuwa rais kabisa anaumwa taabani lakini anatafuta uongozi kwa gharama yoyote hatuwezi kuwa na rais wa namna hii hapana apumzike jamani wapo viongozi wengi.
 
Lowassa siyo tajiri fedha ni tajiri wa watu pia siyo mbadhirifu kipato chake zaidi ya kutoa zaka. Na pale anapotoa sadaka anarudishiwi maradufu!

dogo utakufa kwa njaa kutetea fusadi... jibu swali hapa chin... !!

Labda anaweza pia
kutufundisha jinsi ya
kutajirika kwa kutumia
cheo cha serikali bila
kugundulika.
 
Kiukweli tukiacha utani Lowasa hafai kuwa rais kabisa anaumwa taabani lakini anatafuta uongozi kwa gharama yoyote hatuwezi kuwa na rais wa namna hii hapana apumzike jamani wapo viongozi wengi.

Jasusi amesema hiviii...
" Labda anaweza pia
kutufundisha jinsi ya
kutajirika kwa kutumia
cheo cha serikali bila
kugundulika.
 
Last edited by a moderator:
Kwa lipi la maana alilolifanya Lowassa hadi apewe nchi?

Kuna sababu nyingi za kusema Lowassa hafai kuwa rais wa nchi hii licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.

Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu?

Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.

Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowassa awe Rais wa awamu ya tano?



Sababu za kutawala Lowasa zipo kwanza muhimu ni yeye katika wanaojinadi hakuna kiongozi saidi yake na pia yako mambo ambayo alihitaji kuyafanya akiwa waziri mkuu so this time ndio nyakati yakee
 
Wanajamvi huu ni ukweli toka ndani ya cc ya ccm ni kwamba lowasa hatopitishwa kugombea urais kwakua anakashfa nyingi lakini pia afya yake sio imara kupambana na ukawa ndani ya siku 90 za kampeni kupita kijiji kwa kitongoji hapa tz,naomba kumbu kumbu hizi tuziweke humu
 
  • Thanks
Reactions: Gor
Wanajamvi huu ni ukweli toka ndani ya cc ya ccm ni kwamba lowasa hatopitishwa kugombea urais kwakua anakashfa nyingi lakini pia afya yake sio imara kupambana na ukawa ndani ya siku 90 za kampeni kupita kijiji kwa kitongoji hapa tz,naomba kumbu kumbu hizi tuziweke humu

Kumbu kumbu za ki... pu.. vu, kaziweke na ma.....ma yako
 
Back
Top Bottom