Tukianza kuangalia historia ya JK kuingia madarakani mwaka 2005 hapa ndio ulipokuwa mwanzo wa CCM kufa kwa sababu hapa ndio rushwa ilivunja rekodi kwa kuweka wasio wasafi madarakani na ni katika kipindi hicho hawa wote wanaopiga kelele za ufisadi walikuwa kitu kimoja mfano Sitta,Membe na wengine wengi tu iweje leo wapige kelele ya kwamba Lowassa fisadi?
Huu ni unafiki mkubwa kabisa na kwa CCM rushwa ni moja ya sera zake sasa leo hii mtu yuko ndani ya CCM anapiga kelele za ufisadi huyo ni muongo tu.
Kwa sasa mafisadi ndio wanaoindesha CCM na ndio wenye final say ndani ya CCM hata m/kiti anajua hilo na hata Mangula alitoa ahadi baada ya miezi sita atatimua mafisadi lakini wapi na unaposema unatoa mafisadi ina maana umeua chama.
Lowassa kuingia ikulu inawezekana kwa sababu mazingira ameshayaandaa muda mrefu, amejenga mtandao wa kuaminika na anachosubiri ni kuteuliwa na chama tu hilo halina ubishi.Kwa sababu yeye na marafiki zake ndio wanaoiongoza CCM kwa sasa.
Kwa hili hata Kikwete limemtia presha na ndio maana kulikuwa na mipango ya kumuweka Pinda ili alinde uchafu wa Kikwete na wapambe wake kwa sababu kimtazamo wao wana hofu kwamba Lowassa akiingia madarakani atawafanya nini na wakati wa Richmond walikula wote.
Tusiwe wasahaulifu ndugu zangu kwa yaliyotokea Igunga,walidai Rostam hafai lakini baadae wakampigia magoti na yeye kweli akagharamia helicopta kwenye uchaguzi ule.
Kumtimua Lowassa toka CCM hatuwezi na tukiweza tumeua chama.
Mwana-CCM kindakindaki