Kwa kweli wakati mwingine maisha ni ufala sana

Unashindia tembele, watoto wanatembea viatu vinacheka, mwenye nyumba anakugongea kila siku na anatishia kukutolea vyombo nje utatoa wapi furaha? Vitu vingine tunavisema tu lakini ni vya kufikirika
Zaburi 118:24
[24]Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,
Tutashangilia na kuifurahia.

Unapoamka asbh ukiwa na afya njema,.. Furahi kwakua Mungu amekupa siku hiyo uifurahie.. Ukianza kutengeneza mawazo ya kuona siku ukiyopewa ni mbaya kwakua una madeni, watoto wanakula matembele nk.. Hautakaa uwe na furaha, kwani hata wenye pesa wana madeni makubwa benk, wana maadui wengi, wana mambo kibao...
Furaha ni vile ulivyochagua maisha yako ya we na furaha kwa kile kidogo, unatengeneza mawazo ya kupokea na kuona ipo sababu ya kufurahi... Utafurahia.
 
Sawa...
 
Watoto sare zimechakaa, shulen mchango wa chakula, chakula milo miwili mmejitahidi kwa kawada ni mmoja.....

Immposiblle.... Ni kujifariji tu
Unashindia tembele, watoto wanatembea viatu vinacheka, mwenye nyumba anakugongea kila siku na anatishia kukutolea vyombo nje utatoa wapi furaha? Vitu vingine tunavisema tu lakini ni vya kufikirika
 
Ukiwa nazo kwanza, haya yote unayosema yanakuwa kweli
 
We ndiye umeonyesha kwamba kukosa pesa kunaweza kukufanya usiwe na furaha na hata ukamkosea Mungu, ila umenichekesha sana kwa maelezo yako
 


Una mifano ya hovyo sana..uzi mzuri unauchafua..mie ni Me-
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…