Kwa kweli wakati mwingine maisha ni ufala sana

LadyRed

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
9,655
2,000
Kuna vitu Mungu aliweka siri kubwa..
Mf kifo,maradhi na madaraja ya kimaisha

Huwa napenda kusoma Hekima za Mfalme Suleiman hazichoshi
Ni uhalisia mtupu wa maisha tangu zamani hakuna jipya
Na yote ni ubatili na kujilisha upepo
 

Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
17,442
2,000
Sisi kajamba nani ndio tukiwaona wanatumia pesa zao tunaumia na kusema "ushamba tu na ulimbukeni unawasumbua".
Na tunavyowalaani wenye pesa zao, kulalamikia ndugu kwamba wameshindwa kutusaidia ili hali na wao hawana, tunavyozaa watoto kila mwaka halafu ada tunalia kwa ndugu watulipie watoto wetu ni shida
 

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,130
2,000
Tena kunakuwa na chuki kubwa kwa wenye nazo na kuwaandama kwa maneno mabaya ili nao waishi kama mashetani.

Sisi kajamba nani ndio tukiwaona wanatumia pesa zao tunaumia na kusema "ushamba tu na ulimbukeni unawasumbua".
 

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,130
2,000
Hbr bob! Hamjambo huko TZ? nimekuja UK mara moja mpaka next week. Ntakuja ntaanzisha uzi nikielezea maisha magumu au gari yangu ya japani inasumbua ntapata wapi fundi ili wadau wengi wachangie kwa furaha. But nikiwaelezea trip zangu za Paris na Leo Uk Watakasirika sana. Ndo ufala wa maisha wenyewe huo.

Kiduku Lilo The Don ...mchango wako ni wa muhimu sana eneo hili.Tunakungoja 😂
 

Machmadem

JF-Expert Member
Jul 9, 2017
487
500
(1) na (2) - Yaani upate usinginzi na hamu ya chakula mpaka umeze vidonge???? Na hizo vidonge zinakuletea matatizo mengine ya kiakili na kiafya. Kidonge kwa ajili ya chakula, kidonge kwa ajili ya usingizi, viagra kwa ajili ya kusimamisha vituz, - jiulizie kati ya tajiri na maskini nani ana maisha bora?!! Kumbuka vidonge ni ishara ya ugonjwa!
(3) - Sio kila jengo ina raha ya nyumba. Nyumba zingine zimejaa ugomvi na balaa mpaka watu wanatafuta "nyumba ndogo". A home is a place where you feel relaxed and happy, where as a house is just a structure with walls and a roof! Kuna mambo mengi kama upendo (haiuzwi madukani) ambayo inafanya jengo (house) iwe nyumba (home)
(4) - Watu wamekuwa mabingwa kwa kujisomea chini ya miti na wangapi wameenda university na kubaki vilaza??? Kama una uwezo wa kununua elimu, lakini huna hamu ya kusoma, utapataje maarifa??? Ukiwa na hamu na kipaji, basi unaweza kuazima vitabu maktaba na kujisomea na baadaye unapata scholarship kusomea zaidi!! Kama huna kipaji na huna hamu ya kusoma, fedha haitakusaidia kitu!!!
(5) - Maskini na tajiri wote muda wao ukifika, hamna ya kubembeleza. Tajiri anaweza kutafuta huduma hapa na pale, lakini mwisho wa siku hela haitamnunulia afya na kumpatia maisha marefu. Halafu lifestyle diseases kama kisukari, BP nk yanashambulia matajiri zaidi kuliko maskini! Pesa inasaidi kufanya maisha yawe nafuu, lakini inalimits!!!!
Mkuu tafuta pesa acha kuchonga sana
 

Prince Mujubu

JF-Expert Member
Jun 7, 2016
344
250
Mkuu, ingawa ni kweli kuwa pesa inarahisisha maisha, lakini ujue kuwa pesa zina ukomo zake, na si kila kitu kinaweza kununuliwa:
MONEY ISN'T EVERYTHING
Money can buy you a house but not a home;
Money can buy you a clock but not time;
Money can buy you a bed but not sleep;
Money can buy you food but not appetite;
Money can buy you a book but not knowledge;
Money can buy you medicine but not health;
Money can buy you blood but not life.
Money also will never betray you.
 

Nebukadreza

Member
Dec 31, 2007
24
75
ujieleze tu utapata kazi? Na hizo kazi zozote unazozungumzia watu wanatafuta na hawapati.tukubali maisha ni kama kiganja cha mkono hatuwezi kuwa sawa hata iweje.
Tatizo lenu kazi mnazani ni ile muajiriwe tu, tena mnachagua siwezi kufanyakazi ya aina Fulani. Kazi ni shughuli yoyote halali itakayokuingizia kipato. Nafasi za kufagia barabara zipo muda wote, saiti zote za kujenga zinanafasi za kazi ya kubeba zege muda wote. Masoko yote yana kazi za kubeba mizigo muda wote n,k, n.k. Nikweli binadamu hatutalingana na haitakiwi tulingane, lakini unashindwa hata kulihudumia tumbo lako.
Kaa na vyeti vyako subiri eti mpaka upate kazi yenye hadhi yako utasubiri sana. Anza chini ukipata mtaji unabadilisha kazi hatua kwa hatua
 

Espy

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
70,110
2,000
Na tunavyowalaani wenye pesa zao, kulalamikia ndugu kwamba wameshindwa kutusaidia ili hali na wao hawana, tunavyozaa watoto kila mwaka halafu ada tunalia kwa ndugu watulipie watoto wetu ni shida
Yaani ni taabu juu ya shida.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom