Kwa kweli wakati mwingine maisha ni ufala sana

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,324
2,000
Kuna wakati maisha yanakuwa ni ufala sana kwani ingawaje wanaoyaishi ni binadamu wenyewe lakini hukosa usawa kabisa...

Kuna mtu muda huu anakufa baada ya kukosa elfu tatu ya dawa ya mseto, Kuna mtu analipa 1mil kutunza mbwa wake

Kuna familia watoto wanalia njaa, kuna familia watoto wanalilia kwenda dubai kutembea

Kuna mtu anatafuta mia tano ale, kuna mtu anakula lunch ya laki na ushee

Kuna mtu anatafuta laki 1 kwa mwezi imfae kwa maisha, kuna mzazi anampa mil3 za matumizi mtoto wake kila mwezi

Kuna kajambanani mmoja hapa anauza jogoo wake alipe ada ya mwanae, kuna mtu yupo bank analipa mil 7 za nusu muhula kwa mwanae wa darasa la pili.

Kuna mtu anatafuta kazi hata ya bure mradi ale, kuna mtu anaacha kazi ya mil5 ili apumzikeWALE KINA KAJAMBANANI WANA HISIA GANI MIOYONI MWAO KUHUSU HAWA WA UPANDE WA PILI?

-WIVU
-HAMASA
-HAWANA HISIA ZOZOTE

NA JE! HAWA W KUNDI LA PILI WASIOIJUA SHIDA MNA HISA GANI NA HILI KUNDI LA KWANZA?

-HURUMA
-DHARAU
-HAMNA HISIA ZOZOTE

images-25.jpeg
Screenshot_2019-06-08-15-52-27.jpeg
 
Attachments

  • Screenshot_2019-06-08-15-52-27.jpeg
    File size
    17.3 KB
    Views
    41

Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
412
1,000
Mkuu, ingawa ni kweli kuwa pesa inarahisisha maisha, lakini ujue kuwa pesa zina ukomo zake, na si kila kitu kinaweza kununuliwa:
MONEY ISN'T EVERYTHING
Money can buy you a house but not a home;
Money can buy you a clock but not time;
Money can buy you a bed but not sleep;
Money can buy you food but not appetite;
Money can buy you a book but not knowledge;
Money can buy you medicine but not health;
Money can buy you blood but not life.
 
Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,055
2,000
Hakuna mtu asiyeijua shida mzee.
Ndo maana pamoja na hela alizokuwa nazo but marehem Ruge alilia penzi la Zamaradi na kukosa raha kabisa.... je hiyo sio shida?

kikubwa amani ya moyo ipatikane mkuu.
Na nakuambia pesa ni makaratasi tu mkuu ila hakikisha unakuwa nazo maana daaah
 
Kasomeko

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
443
1,000
Pamoja na tofauti zote hizo!

Linapofika suala la mahala pa kufukiwa wote tunakuwa Sawa!
Tunakua sawa ila vp mfano wewe n baba wa watoto watatu hata la saba hawajamaliza unakufa unawaacha kwenye nyumba ya kupanga wanalalia makusheni ya kupewa na mwenye nyumba. Sijui n uchungu gani utaupata utakapokua kweny hatua za mwisho kukata roho najua lazma utasema wanangu nawaacha mkiwa wadogo bila chochote cha kurithi mtaishi kwa shida na mateso ila msijali Mungu yupo atawasaidia ishini naisha ya kumpendeza Mungu siku moja tutaonana. Sikuunakata roho tu kale kabinti kako kakubwa kanaingizwa ukubwani rasmi ili kamudu kuwatunza wadogo zake. Sasa hapo maisha ya kumpendeza shetani ndio yanaanza.

Acheni wivu na kukariri misemo isiyo na tija eti sote tutakufa, ukifa huzikwi na gari wala ndani ya nyumba yako eti unazikwa nje!! Sawa tajiri atazikwa nje na masikini nje ila jiulize je, tajiri kafa kawaachia nini wanawe? Masikini nae je kawaachaje wapendwa wake? Kama ni faida kuishi kwenye ufukara endelea kupiga uvivu.
 
mizy gajo

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
799
1,000
hatunaga hisia zozote blaza huku kwetu maisha magumu ila hatutamani kufa...!!!
Kuna wakati maisha yanakuwa ni ufala sana kwani ingawaje wanaoyaishi ni binadamu wenyewe lakini hukosa usawa kabisa...

Kuna mtu muda huu anakufa baada ya kukosa elfu tatu ya dawa ya mseto, Kuna mtu analipa 1mil kutunza mbwa wake

Kuna familia watoto wanalia njaa, kuna familia watoto wanalilia kwenda dubai kutembea

Kuna mtu anatafuta mia tano ale, kuna mtu anakula lunch ya laki na ushee

Kuna mtu anatafuta laki 1 kwa mwezi imfae kwa maisha, kuna mzazi anampa mil3 za matumizi mtoto wake kila mwezi

Kuna kajambanani mmoja hapa anauza jogoo wake alipe ada ya mwanae, kuna mtu yupo bank analipa mil 7 za nusu muhula kwa mwanae wa darasa la pili.

Kuna mtu anatafuta kazi hata ya bure mradi ale, kuna mtu anaacha kazi ya mil5 ili apumzikeWALE KINA KAJAMBANANI WANA HISIA GANI MIOYONI MWAO KUHUSU HAWA WA UPANDE WA PILI?

-WIVU
-HAMASA
-HAWANA HISIA ZOZOTE

NA JE! HAWA W KUNDI LA PILI WASIOIJUA SHIDA MNA HISA GANI NA HILI KUNDI LA KWANZA?

-HURUMA
-DHARAU
-HAMNA HISIA ZOZOTE

View attachment 1121720 View attachment 1121813
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom