Kwa kweli wakati mwingine maisha ni ufala sana

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,138
2,000
Kuna wakati maisha yanakuwa ni ufala sana kwani ingawaje wanaoyaishi ni binadamu wenyewe lakini hukosa usawa kabisa...

Kuna mtu muda huu anakufa baada ya kukosa elfu tatu ya dawa ya mseto, Kuna mtu analipa 1mil kutunza mbwa wake

Kuna familia watoto wanalia njaa, kuna familia watoto wanalilia kwenda dubai kutembea

Kuna mtu anatafuta mia tano ale, kuna mtu anakula lunch ya laki na ushee

Kuna mtu anatafuta laki 1 kwa mwezi imfae kwa maisha, kuna mzazi anampa mil3 za matumizi mtoto wake kila mwezi

Kuna kajambanani mmoja hapa anauza jogoo wake alipe ada ya mwanae, kuna mtu yupo bank analipa mil 7 za nusu muhula kwa mwanae wa darasa la pili.

Kuna mtu anatafuta kazi hata ya bure mradi ale, kuna mtu anaacha kazi ya mil5 ili apumzikeWALE KINA KAJAMBANANI WANA HISIA GANI MIOYONI MWAO KUHUSU HAWA WA UPANDE WA PILI?

-WIVU
-HAMASA
-HAWANA HISIA ZOZOTE

NA JE! HAWA W KUNDI LA PILI WASIOIJUA SHIDA MNA HISA GANI NA HILI KUNDI LA KWANZA?

-HURUMA
-DHARAU
-HAMNA HISIA ZOZOTE

View attachment 1121720 View attachment 1121813
Mungu alichotusaidia nikwamba wote tunakufa
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,365
2,000
Sasa hiyo screenshot ya noti ya kizamani ya sh.500 ni yanini, ama ndiyo kiashiria cha fungu la kukosa, fungu la maskini?
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,365
2,000
kuna mtu alikuwa anapeleka fungu la kumi kanisani.. kubwa kweli kweli zaidi ya milioni.. huku mimi nasaka kodi.. nikasema kweli ndio maana wenye nacho wanabarikiwa
Binadamu hatoi baraka kwa binadamu mwenziye bali Mwenyezi Mungu pekee.

Na Mungu hahongeki kwa njia ya matoleo ya fungu la kumi.
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,365
2,000
Mkuu, ingawa ni kweli kuwa pesa inarahisisha maisha, lakini ujue kuwa pesa zina ukomo zake, na si kila kitu kinaweza kununuliwa:
MONEY ISN'T EVERYTHING
Money can buy you a house but not a home;
Money can buy you a clock but not time;
Money can buy you a bed but not sleep;
Money can buy you food but not appetite;
Money can buy you a book but not knowledge;
Money can buy you medicine but not health;
Money can buy you blood but not life.
Mkuu acha kukaririshwa kama kasuku.
Vyote ulivyoorodhesha hapo vinategemeana katika maisha na kwa kiasi kikubwa vinaletwa na pesa.
 

Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
412
1,000
Mkuu acha kukaririshwa kama kasuku.
Vyote ulivyoorodhesha hapo vinategemeana katika maisha na kwa kiasi kikubwa vinaletwa na pesa.
Hebu nieleze kwa nini Steve Jobs, pamoja na mabillioni zake, hakuweza kujinunulia afya, halafu niambie nani anakaririshwa kama kasuku????
Michael Jackson, Whitney Houston, pamoja na utajiri wao, kwa nini hawakuweza kujinunulia furaha na walifariki kwa sababu ya substance abuse ili kupunguza msongo wa mawazo???
 

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,365
2,000
Hebu nieleze kwa nini Steve Jobs, pamoja na mabillioni zake, hakuweza kujinunulia afya, halafu niambie nani anakaririshwa kama kasuku????
Michael Jackson, Whitney Houston, pamoja na utajiri wao, kwa nini hawakuweza kujinunulia furaha na walifariki kwa sababu ya substance abuse ili kupunguza msongo wa mawazo???
Mzee mbona umetolea mfano wa stress za watu kundi la wavuta bhangi na watumiaji wa dawa za kulevya?

Yote uliyoyaandika yana mantiki ya msingi lakini hayana conclution.

Unapokuwa na pesa ndiyo utafanya mambo yatakayokupatia furaha sahihi uitakayo.

Nakupa mfano mdogo tu hapa kwamba, utatamani kuoa mwanamke atakayekupatia furaha, lakini bila pesa hakuna kitu.

Utatamani kula aina fulani ya chakula una hamu nacho, utakipataje bila pesa?

Umetamani kusafiri kukutana na marafiki zako, utasafirije bila pesa?

Mifano hiyo michache lakini ipo mingi sana katika maisha ambayo kuipata furaha yako mpaka uigharamie.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
43,574
2,000
Nimesoma comments zote mwanzo hadi mwisho. Kwa maoni ya wengi humu JF wengi wana furaha(wana pesa) na wengine hawana furaha (hawana pesa).
Mimi naamini kwenye kuridhika,ukiridhika na hali yako utakuwa na furaha.
 

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
53,994
2,000
Nimesoma comments zote mwanzo hadi mwisho. Kwa maoni ya wengi humu JF wengi wana furaha(wana pesa) na wengine hawana furaha (hawana pesa).
Mimi naamini kwenye kuridhika,ukiridhika na hali yako utakuwa na furaha.
Pacha, unalala njaa, unakula mlo mmoja, mwenye nyumba kila asubuhi anakugongea kukusomea risala utasema umeridhika? Basi wenzetu mna roho nzuri
 

Nebukadreza

Member
Dec 31, 2007
24
75
Tatizo la watu/maskini wengi wanadhani wapo kwenye hali hiyo kwa kusababishiwa na matajiri au wenye uwezo. Ni mawazo mgando sana.
Leo hii wape watanzania wote milioni kumi kila mmoja baada ya mwaka mmoja wafuate nakuhakikishia 90% utawakuta hawana hata senti tano na 5% pekee utakuta bado wanazofedha na wamezalisha Zaidi.
Tatizo kubwa la umaskini sio Mungu, sio Serikali, Sio chama chochote, wala sio kupanda wala kushuka kwa uchumi. Tatizo Binadamu(mtanzania) ameshindwa kutumia Mawazo(akili) yake, Nguvu zake, Hisia(emotion)chanya zake na mwili wake kutatua changamoto zake.
Mtaji wa mafanikio yako ni uhai peke yake. Acha kuwaza msaada/ufadhili wa bure, waza kufanya kazi yyt kwa kuanzia upate pa kuanzia hata kama kufagia barabara. Ishi kulingana na hali yako kula kulingana na kipato chako. Jieleze matatizo yako au mahitaji yako utasaidiwa kupata kazi.
Unasubiri kuonewa huruma mtu mzima una viungo vyote salama. Wanaokula chakula cha laki moja wametafuta fedha zao miaka mingi kwa jasho, wakati wenzio wanaamka saa 11 asubuhi ww unaamka saa 4 asubuhi. ana haki ya kwenda kutibiwa mafua uingereza, usion wivu, usiwe mvivu
Maisha yako yapo mikononi mwako, ww ndio utaamua kama yaweje. kwa kukusaidia amini usiamini ukivipangilia vizuri vipaji hivi ambavyo naamini kila mtu anavyo utafanikiwa kila utakacho fanya.
Your mind
Your body
Your Enegy
Your Emotion
 

semper saratoga

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,086
2,000
Ni vigumu mno kuridhika katika limbwi la ufukara… amini usiamini ndoto (mawazo matamanio) ya binadamu karibia wote ni kupiga mkwanja mrefu wale raha.. Sasa kama miaka inasonga tu goma halisomeki leo bora ya jana unaridhikaje mkuu? Hapo ukipita maeneo eneo unakuta watu wanasukuma mikoko ya hatari mno…
Nimesoma comments zote mwanzo hadi mwisho. Kwa maoni ya wengi humu JF wengi wana furaha(wana pesa) na wengine hawana furaha (hawana pesa).
Mimi naamini kwenye kuridhika,ukiridhika na hali yako utakuwa na furaha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom