msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Hulka yetu watanzania tuliowengi hatupendi kulipa kodi kwa hiari ila ni wa kwanza kuilamu serikali pale inaposhindwa kuleta huduma za maendeleo.
Yaani tunafikiri pengine maendeleo yanakuja tu kama mvua ishukavyo kutoka mawinguni au labda kwamba nchi inaweza kujiendesha yenyewe pasipo watu kulipa kodi, jambo ambalo si kweli.
Inashangaza kwamba leo tunalia kwa sababu serikali imetuwekea kodi ya uzalendo kwenye miamala ya simu lakini tunasahau kwamba taifa letu bado ni changa na linakabiliwa na changamoto lukuki zikiwemo changamoto za ubovu wa bara bara mjini na vijijini, changamoto ya maji safi na salama, changamoto ya madawati, changamoto ya walimu, hospitali, madawa, umeme n.k
Kimsingi wa kutatua changamoto hizi ni sisi wenyewe, tusitegemee kwamba kuna mtu kutoka taifa lingine wa kuja kututatulia changamoto zetu. Kumbe sasa inatupasa kufunga mikanda na vibwebwe kisawa sawa ili tuweze kuzitatua, na njia pekee ya kuzitatua ni kupitia kodi.
Hata mataifa yaliyoendelea kama marekani, uingereza, na china hayakufika hapo yalipo hivi hivi nao walipitia ugumu kidogo kama ambavyo sisi tunaona taabu kulipa kodi ya uzalendo kwenye miamala ya simu lakini baada ya muda fulani walizoea na kuona kwamba kulipa kodi ni suala la kawaida na ndio maana wameweza kupiga hatua kubwa kiuchumi na kuwa hapo walipo hii leo. Hata sisi kwakuwa ndio tunaanza mwanzo utakuwa mgumu lakini baadaye tutazoea na hii kodi ya kizalendo tutakuja kuona ni suala la kawaida kabisa.
Nachotaka kuwambia Watanzania wenzangu, tuonyeshe uzalendo tulipe kodi kwa maendeleo ya Taifa letu kwa sababu bila kodi.
• Hakuna bara bara itajengwa
Hakuna hospitali itajengwa,
Hakuna shule itajengwa
• Watoto wetu wataendelea kukaa chini
• Hakutakuwa na pesa za kununua madawa
• Watumishi wa umma watashindwa kupandishwa madaraja ambayo hayajapanda kwa miaka zaidi ya mitano
• Watoto wetu watakosa vipindi kwa sababu serikali haitakuwa na uwezo wa kuajiri walimu
• Mama zetu hospitali watashindwa kujifungua salama kwa sababu serikali haitakuwa na pesa za kuboresha huduma za afya
• Vile vile hata miradi mikubwa tuliyoanzisha kama SGR, SG n.k itakwama kwa sababu ili ikamilike kunahitajika fedha ambazo zinapatikana kupitia wananchi kodi ya wananchi.
Kwahivyo watanzania wenzangu tusione kama serikali haina nia njema na sisi, La hasha! tulipe kodi na tukishalipa kodi sisi kama wananchi tuchukue jukumu la kuisimamia serikali ili kusudi kodi tuliyolipa isipotee bure au kuishia kwenye mifuko ya wachache bali itumike katika malengo yaliyokusudiwa na matunda yake yaonekane.
KODI YA UZALENDO KWA MAENDLEO YA TAIFA.
Naomba kuwasilisha.