Hakuna mkopo kwa diploma holders kwenda degree

Status
Not open for further replies.

MAFIE JR

Senior Member
Feb 20, 2016
117
92
Habari kwa wahitimu wote wa kidato cha sita na wahitimu wote wa stashahada mwaka 2016. Ni dhahiri kumefanyika mabadiliko makubwa Katika bodi ya usajili vyuo vikuu hii imehusisha mabadiliko ya viongozi wa bodi pamoja na baadhi ya miongozo ya usimamizi.

Kwa wahitimu wa kidato cha sita,wanafunzi watakao pata daraja la kwanza na la pili yaan division one na division two ndio watakosajiriwa kwa elimu ya shahada yaan degree na kwa wale watakaomaliza diploma ni wale watakaopata hazini ya ufaulu Kuanzia 3.3 na kuendelea yaani GPA ya 3.3.kwa wahitimu wa kidato cha sita watakaopata daraja la tatu yaani division 3 watasoma stashahada adhiri yaani special diploma hii itachukua na wahitimu wa stashahada ambao hawakukidhi viwango.

Ieleweke wazi hakutakua na usajili wa wahitimu watakao pata daraja la nne na wale watakaopata GPA chini ya 3.3 kwa wahitimu wa stashahada pia hakutakua na mkopo wa wanafunzi wa stashahada adhiri kama ilivyokua awali,Bali patakuwa na punguzo la ada la asilimia 35 kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka 2016/2017.imesainiwa na kupita

KANUSHO: HESLB yakanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii
 
Kama habari hii ikithibitika,itakuwa imewaumiza ndugu zetu wengi sana.

Sioni mantiki kwanini waliopata ufaulu wa daraja la 3 wasidahiliwe chuo kikuu na kwa diploma wenye gpa chini ya 3.3 wasidahiliwe chuo kikuu,utakuwa ni uonevu

Tuje kwenye mkopo,wametumia kigezo gani kusema hawa watu wasipate mkopo?!maisha ya diploma holders na freshers yanafanana except diploma holders ambao wapo kwenye ajira ambao ni wachache sana

Kwa maoni yangu,bora wangeainisha ufaulu wa kupata mkopo kwa diploma na freshers ili kuondoa mkanganyiko
 
Kama habari hii ikithibitika,itakuwa imewaumiza ndugu zetu wengi sana.

Sioni mantiki kwanini waliopata ufaulu wa daraja la 3 wasidahiliwe chuo kikuu na kwa diploma wenye gpa chini ya 3.3 wasidahiliwe chuo kikuu,utakuwa ni uonevu

Tuje kwenye mkopo,wametumia kigezo gani kusema hawa watu wasipate mkopo?!maisha ya diploma holders na freshers yanafanana except diploma holders ambao wapo kwenye ajira ambao ni wachache sana

Kwa maoni yangu,bora wangeainisha ufaulu wa kupata mkopo kwa diploma na freshers ili kuondoa mkanganyiko
Mkuu uko very correct.... Sio watu wote wenye diploma wameajiriwa.... Kati ya 100%utakuta 30% ndo wameajiriwa.....Mimi nafikiri Rais Magufuli alitizame mara mbili ili swala haswa ukizingatia alituahidi kwamba kila mwenye sifa za kusoma atapewa mkopo
 
Kuna vyuo vya uhandisi kama DIT na MUST, vinategemea asilimia kubwa wanafunzi waliopitia Diploma, kuweka masharti kama haya ni uonevu kabisa, na wanafunzi hawa wanakuwa wakichaguliwa moja kwa moja kukoka Sekondari
 
Tuwekee nyaraka rasmi licha ya wazir wa tamisemi aliwahi kugusia mwezi February
 
"can you give us, a SOURCE of your post please..."
Tunaomba source ya post yako hii mkuu,
Unknown source.... Ila hii kitu inazunguka sana kwenye social media....humu kuna watu wako vizuri they can bring more support maana wengi wameona ikizunguka Jana NA leo
 
Wabongo inaonekana hata kusoma post ya kiswahili ni shida....
Wamesema kwa wale ambao watakuwa wanasoma diploma maalum hawatapata mkopo km ilivyokuwa awali badi watapunguziwa tu ada..
Hii haiwahusu waliomaliza diploma kwenda kuchukua degree, mkopo upo palepale.
 
Nimeisha apply chuo mwaka huu. Nimemaliza diploma ya engineering na guidbook ya nacte inasema vigezo ni kuanzia gpa ya 2.7 sasa hiyo 3.3 ni guidbook ipi??
 
Subiria updates... Najua reliable sources na serikali italitolea ufafanuzi au kulipinga kama sio la kweli
 
Nimeisha apply chuo mwaka huu. Nimemaliza diploma ya engineering na guidbook ya nacte inasema vigezo ni kuanzia gpa ya 2.7 sasa hiyo 3.3 ni guidbook ipi??
Ila mkuu navyosikia kua TCU kua Wana update kitabu Chao kila mwaka sasa wewe umeapply vipi na kitabu kipya hakijatoka nauliza tu
 
Naunga mkono hoja...

Kwa miaka ya karibuni vyuo vimepoteza sifa kwa kudahili wanafunzi wasiostahili kudahiliwa kwa ngazi ya degree... Leo imekuwa kawaida mwanafunzi Mwenye ufaulu Wa division 3 anenda kuchukua degree matokeo yake ni kuzalisha kundi la vijana wasiokuwa na uwezo Wa kureason na kuongea logic.. Kwa ambao wamepita vyuon miaka ya hivi karibuni ninaamin watakuwa wameliona hili .. Haiwezekan tuwe taifa la kuzalisha Quantity ya wasomi badala ya Quality ya wasomi... Njia pekee ya kupata wanafunzi Wa vyuo wenye quality ni kuhakikisha tunakuwa na mechanism filter ya kuchuja waliofeli na kupata cream safi ya wanafunzi ili wakasome degree.. Div 1& 2 ndio wawe wanafunzi Watakaochukuliwa kusoma degree...

Kuhusu suala la mkopo naunga hoja mkono..... Kwa kipindi kirefu wanafunzi wanaojiunga na masomo ya degree kwa sifa za diploma wamekuwa wakinunyimwa mikopo kwa sababu zisizo na maana... Ila kwa punguzo la ada kwa 35% itasaidia saaaaana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom