Rajab_Omar
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 16,480
- 27,185
Habari kwa wahitimu wote wa kidato cha sita na wahitimu wote wa stashahada mwaka 2016. Ni dhahiri kumefanyika mabadiliko makubwa Katika bodi ya usajili vyuo vikuu hii imehusisha mabadiliko ya viongozi wa bodi pamoja na baadhi ya miongozo ya usimamizi.
Kwa wahitimu wa kidato cha sita,wanafunzi watakao pata daraja la kwanza na la pili yaan division one na division two ndio watakosajiriwa kwa elimu ya shahada yaan degree na kwa wale watakaomaliza diploma ni wale watakaopata hazini ya ufaulu Kuanzia 3.3 na kuendelea yaani GPA ya 3.3.kwa wahitimu wa kidato cha sita watakaopata daraja la tatu yaani division 3 watasoma stashahada adhiri yaani special diploma hii itachukua na wahitimu wa stashahada ambao hawakukidhi viwango.
Ieleweke wazi hakutakua na usajili wa wahitimu watakao pata daraja la nne na wale watakaopata GPA chini ya 3.3 kwa wahitimu wa stashahada pia hakutakua na mkopo wa wanafunzi wa stashahada adhiri kama ilivyokua awali,Bali patakuwa na punguzo la ada la asilimia 35 kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka 2016/2017.imesainiwa na kupita
Mtoa Mada Ulichoelezea ni Tofauti na Tittle ya Maelezo yako.
Kichwa Cha Habari Kinasema: "Hakuna mkopo kwa diploma holders kwenda degree"
Lakini Kwenye Maelezo Umeandika hivi: "Ieleweke wazi hakutakua na usajili wa wahitimu watakao pata daraja la nne na wale watakaopata GPA chini ya 3.3 kwa wahitimu wa stashahada pia hakutakua na mkopo wa wanafunzi wa stashahada adhiri kama ilivyokua awali, Bali patakuwa na punguzo la ada la asilimia 35"
Kulingana Na Maelezo Yako Ni Kuwa Hakutakua na Mkopo Kwa Wanafunzi Wale "Watakaodahiliwa Kwa Ajili Ya Kusoma Stashahada adhiri" na Sio Wale Watakao Soma Degree huku wakiwa Wameshahitimu Diploma.
Kwahiyo Ukitaka Kusoma Diploma Maana Yake Ujipange Na Ada Yako Mkononi ila Watapata Punguzo la Ada Kwa asilimia 35% tu.
Lakini Ukiwa Unadiploma na GPA yako ni above 3.3, Basi Utadahiliwa na Kupewa Mkopo.
Tujifunze Kusoma Kwa Ufahamu na Sio Kusoma Kwa Ajili ya Ubishi.