Hakuna mkopo kwa diploma holders kwenda degree

Hakuna mkopo kwa diploma holders kwenda degree

Status
Not open for further replies.
Hizo habari zimesha kanushwa na heslb mkuu hazina ukweli wowote
 
HESLB wamesha kanusha hizo taarifa
 
Habari kwa wahitimu wote wa kidato cha sita na wahitimu wote wa stashahada mwaka 2016.

Ni dhahiri kumefanyika mabadiliko makubwa Katika bodi ya usajili vyuo vikuu hii imehusisha mabadiliko ya viongozi wa bodi pamoja na baadhi ya miongozo ya usimamizi.kwa wahitimu wa kidato cha sita,wanafunzi watakao pata daraja la kwanza na la pili yaan division one na division two ndio watakosajiriwa kwa elimu ya shahada yaan degree na kwa wale watakaomaliza diploma ni wale watakaopata hazini ya ufaulu Kuanzia 3.3 na kuendelea yaani GPA ya 3.3.kwa wahitimu wa kidato cha sita watakaopata daraja la tatu yaani division 3 watasoma stashahada adhiri yaani special diploma hii itachukua na wahitimu wa stashahada ambao hawakukidhi viwango.

Ieleweke wazi hakutakua na usajili wa wahitimu watakao pata daraja la nne na wale watakaopata GPA chini ya 3.3 kwa wahitimu wa stashahada pia hakutakua na mkopo wa wanafunzi wa stashahada adhiri kama ilivyokua awali,Bali patakuwa na punguzo la ada la asilimia 35 kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka 2016/2017.

1f446
1f446
1f446
1f446
1f446
1f446
1f446

Kuna haja ya kupitia taarifa Mara kwa Mara ili kujua nini kinajiri maana unaweza kushangaa haupo kwenye mstari.

Ukipata nafasi itumie mapema maana ipo siku sheria. Taratibu na vigezo hubadilika ghafla na kuwaathiri wengi sana.

Waziri anaweza kufanya mabadiliko kulingana na alivyofaulu yeye.

Pia mabadiliko hayo yaliyo mengi huchochewa na chuo kikuu cha Dar es salaam ambacho serikali huchukulia kuwa ndo chuo pekee hapa nchini na vingine ni vya vilaza.

Ikumbukwe kwamba degree ya udsm na ya vyuo vingine zote ni degree na zina hadhi sawa.

Wakati mwingine vyuo vya kati vinatoa ELIMU na ujuzi wa maana kuliko chuo kikuu cha DSM na vyuo maarufu nchini.

Elimu yetu inayumbishwa na mabadiliko kila kukicha ambayo hayana tija bali kuendelea kuleta hofu nchini Tanzania.

Kuna watu wenye division 3 form 6 kwa sasa hawaruhusiwi kusoma degree.

Kuna wenye diploma na GPA ya 3.0 hawaruhusiwi kusoma degree.

HOFU YANGU
Inawezekana ikaingia hadi kwenye soko la ajira na kuwaathiri wahitimu ambao watajikuta hawaajiriki kwa kuwa na ufaulu mdogo.

Inawezekana hata waliopo kazini wakaathirika na mabadiliko makubwa yasiyo na tija.

Kwahiyo kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi kila kukicha vinginevyo unaweza kupata tatizo kwa kutokujua nini kinaendelea nchini.

Tumwombe sana Mungu mabadiliko hayo yasituathiri bali yatujenge zaidi.

By Mrutu E.M
Taarifa yako sio sahihi na imekanushwa hii leo tembelea heslb mnavyoleta taarifa muwe na visibitisho la sivyo we soma comments za threads nyingine tu
 
KUKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUPITIA MITANDAO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na mara mchakato utakapokamilika, wadau wote watatangaziwa.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016


Copyright © 2016 Higher Education Students' Loans
 
Hii taarifa kuwa chuo kikuu wataenda wenye division one na two ya form six na kutokea diploma gpa ya kuanzia 3.3 zina ukweli kiasi gani? source iko wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom