Uchaguzi 2020 Kwa kasi hii ya wagombea Ubunge wa CCM sidhani kama Mbatia na Mzee Cheyo wataachiwa majimbo ya upendeleo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,966
141,975
Kasi imekuwa ni kubwa mno na wagombea ni wengi kuliko ilivyotarajiwa kwa upande wa CCM.

Ikumbukwe kuwa Mzee Cheyo aliomba mbele ya Mwenyekiti wa CCM kwamba waachiwe majimbo mawili au matatu.
Kadhalika NCCR Mageuzi ilitegemewa kupata majimbo kadhaa kuwahifadhi wahamiaji kutoka CHADEMA.

Lakini kiukweli mambo yanaenda kasi kila mtu apambane na hali yake hakuna wa kulaumiwa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wewe hukusikia maombi ya mzee Cheyo kutaka majimbo mawili ili akawatetee wakulima wa pamba bungeni?!
True, lkn amepata courage ya kusema hayo baada ya Boss wako kusema hakuna mpizani atakaye tangazwa. Na hii rush ya kutokeza kwa wingi wanaamini kuwa akishapitishwa, tayari ni mbunge kwa vile hakuna mpinzani atakaye tangazwa. Unknowingly nawe kukakiri
 
True, lkn amepata courage ya kusema hayo baada ya Boss wako kusema hakuna mpizani atakaye tangazwa. Na hii rush ya kutokeza kwa wingi wanaamini kuwa akishapitishwa, tayari ni mbunge kwa vile hakuna mpinzani atakaye tangazwa. Unknowingly nawe kukakiri
Kama hamtatangazwa mbona mnashiriki uchaguzi?!
 
Bila kujali mleta uzi lengo lako ni nini, lakini Mbatia ni mjinga wa kiwango cha juu, yeye alikuwa ni wa kujilegeza kwa jiwe, wakati inafahamika wazi jiwe ni mwanasiasa mlaghai tu?
Amejilegeza akaliwa sio!
 
,
Kasi imekuwa ni kubwa mno na wagombea ni wengi kuliko ilivyotarajiwa kwa upande wa CCM.

Ikumbukwe kuwa mzee Cheyo aliomba mbele ya mwenyekiti wa CCM kwamba waachiwe majimbo mawili au matatu.
Kadhalika Nccr mageuzi ilitegemewa kupata majimbo kadhaa kuwahifadhi wahamiaji kutoka Chadema.

Lakini kiukweli mambo yanaenda kasi kila mtu apambane na hali yake hakuna wa kulaumiwa.

Maendeleo hayana vyama!
CCM Mpya waachie Jimbo,Kata,Kijiji au Kitongoji au nafasi yoyote hao mavuvuzela waliojikatia tamaa ya mapambano?Salama yao ni kukubali kutumika kuwadhoofisha wapinzani wa kweli.

Mambo haya yanawezekana hapa Tanzania tu.Yaani badala ya kwenda field kutafuta uungwaji mkono na kuleta Sera mbadala kuondokana na umaskini wao wanampigia magoti anayedumisha umaskini?Kimsingi hao siyo wapinzani,labda tuwatafutie utambulisho mwingine na msajili arejee uhalali wa hivi vyama.Orodha yao nahisi mnaifahamu.

Wapinzani wa kweli hapa Nchini,wito wangu kwenu ni kuunganisha nguvu zenu kwa lengo kuu LA kuikomboa nchi kwanza,then turuhusu Uandikaji wa Katiba ya Wananchi ambayo itawezesha Sisi kuanza upya kuijenga Tanzania Huru. Bila kuungana hawa wakoloni tulionao sasa hawaondoki maana ni wenzetu Ila wamekengeuka.Tutafute Muafaka wa Kitaifa bila Uonevu,kila moja wetu kwa nafasi yake tujisahihishe.

Uchaguzi huu wa 2020 wapinzani wasipofanikisha hayo niliyoainisha hapo juu,watakaoumia ni Wananchi wa Taifa letu Pendwa la Tanzania. Chukua hatua,tumia kura yako vizuri,tusidanganyike.
 
Back
Top Bottom