Kwa Juhudi Maksudi za Kikwete Leo Tunabeba Kombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Juhudi Maksudi za Kikwete Leo Tunabeba Kombe

Discussion in 'Sports' started by zomba, Dec 12, 2010.

 1. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa juhudi maksudi na za dhamira njema zilizofanywa na JMK za kuinuwa Michezo, Hususan kandanda, leo tutashuhudia Tanzania ikinyakuwa kombe la Challenge baada ya miaka mingi sana.

  Hongera Kilimanjaro Stars, Hongera wa Tanzania wote, Hongera JMK.

  Kazi yako tunaiona ikizaa matunda.
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Ushindi hauba radha kwa sababu ya rais Mwizi ....

   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sure...Angekuwa ameshinda kihalali, na huu ushindi wa leo, basi ingekuwa burdaaani sana...Moyo wangu unasita kabisa juhudi zake huyu mtu.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mwizi mnamjua ninyi?
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 6. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Afadhali hakwenda uwanjani MKWERE ANAGUNDU KAMA NINI?
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,270
  Likes Received: 19,413
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Labda utuelimishe vizuri jinsi JK alivyochakachua mchezo wa jana hadi tukapewa ushindi wa mezani na waamuzi....................penati haikuwa penati........................mlinzi wa Ivory Coast N'goran Kouassi pamoja na kuinua mikono hakuwa ameugusa ule mpira...............Hivyo lile siyo bao.......................

  bao la wazi la Ivory Coast walinyimwa kwa madai mfungaji aliotea wakati yule aliyepigwa mkwaju wa kwanza hakuwa ameotea...............kwa hiyo ule mpira ambao aliutema Juma kaseja mpigaji hakuwa ameotea kwa hivyo aliyelifunga asingeweza kuwa ameotea.............................kwa hiyo kama waamuzi wangelitenda haki.....................Ivory Coast angelishinda mchezo huo......................
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Najuwa, wengi humu JF hamtapenda pindi JK akisifiwa. Mnyonge Mnyongeni, lakini haki yake mpeni.

  Nani asiyejuwa kuwa leo hii, kandanda safi inayotandazwa Tanzania ni juhudi thabit za JK?

  Leo Kilimanjaro stars imetutowa kimaso maso Tanganyika baada ya miaka 16, hii inamaanisha mara ya mwisho kombe lilikuja wakati wa Mwinyi.

  Si Tanganyika tu iliyotolewa kimasomaso bali ni Africa Mashariki nzima, hebu tazama, leo kikombe cha Afrika Mashariki kingekwenda Afrika Magharibi.

  JK anendeleza hamasa kwa leo hii kuwaalika hawa vijana Ikulu.

  Nani asieuona mchango wa JK kwenye Michezo? Hususan kandanda?
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna uchakachuaji JK ni mpenda michezo na ameinua kiwango na ari ya michezo nchini. Slaa hata mechi ya kirafiki tu hatujawahi kumuona, halafu mwasema huyu ndie alikuwa awe rais, TO HELL !!!
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Well said !!!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nikweli mkuu jana ule ushindi siyo lakini si juhudi za Kikwete....nakama watandelea kufanya ujinga kama huu eti juhudi za Kiwete, mashabiki tutaanza kupungua kama zamani wasimba wana shangilia mchezaji wao hivyo hivyo wa yanga.
   
 13. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Watanzania tuna matatizo makubwa zaidi ya kulikosa kombe la Challenge. Watu makini hushughulika na uchumi wa wananchi wengi, si kama ilivyo kwenye sports, just few beneficiaries! Nakumbuka B.W. Mkapa alikuwa anatua na ndege pale JNIA, akakuta kundi kubwa la watu maeneo ya airport. Alipouliza kuna nini leo, akajibiwa Simba inapokelewa kutoka Misri ambapo imetoka kuifunga Zamalek ya huko na kuwaondoa kwenye michuano ya CAF mabingwa watetezi wa Africa na Misri! Mkapa hakuwa na habari kabisa za Simba na Yanga, lakini ameimarisha uchumi wa nchi na leo hii mkwere ametumia hela za Mkapa hadi zimeisha. Kwa ufupi, watanzania wengi hawanufaiki na upenzi wa rais ktk michezo, wanahitaji uhakika wa mkate wao wa kila siku!
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Bora Tenga achie ngazi ili Kiwete awe rais wa TFF maana anaonekana kufanya vizuri ukilinganisha na sehemu zingine mfano ameshindwa kuzibiti ufisadi, mfumko wa bei kila kukicha vitu vinazidi kupanda bei hata hivyo kwangu mimi heri Mkapa alie tujengea uwanja kuruko huyu mwenye nuksi kiala mechi akitia timu tunafungwa
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu, sijaona kidude cha kukugongea Thanks sijui Invisible kashachakachua.....
   
 16. N

  Newvision JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwizi ni mwizi na hana rangi hata kama ni kijani ni mwizi tu kwani weye humjui?
   
 17. N

  Newvision JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo tena mzee! Ushindi i ushindi hata ukiwa mezani weye ulitakaje
   
 18. Isaac

  Isaac JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 627
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  kweli tulipelekeshwa na kama si juhudi binafsi za Kikwete kutokufika uwanjani tungechapwa sana tu!
   
 19. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nadhani tuliangalia huu mchezo kwa jicho moja. Pamoja na ushindi lakini tulibebwa kimtindo.
   
 20. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Big deal....kwani ndiyo mara ya kwanza kwa Tanzania kuchukua hili kombe? Huko nyuma marais waliokuwepo wali-play role gani?

  Anyways, kujisifu kwa mambo ambayo ni non-issues ni hulka ya baadhi yetu wa-TZ. So.....
   
Loading...