Kwa Jinsi CCM inavyopindua meza yake yenyewe, Bado tu Wana-CCM hamuoni umuhimu wa Katiba Mpya?

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,386
Ni mwaka mmoja umepita sasa tangu Mwenyekiti wa CCM atwaliwe na Bwana! Ni kawaida Kwa Nchi yoyote Rais akifia madarakani hutokea mtikisiko!

Hapa kwetu pia kulitokea na Bado kunaenfelea kutikisika!

Hata hivyo huu wa kwetu ni wa kipekee!

Kuna msemo unaitwa kupindua meza ! Labda pengine ulianzishwa kuiga kazi aliyofanya Yesu hekaluni kupindua meza za walamguzi walio badilisha Hekalu kuwa Pango la wahuni'!

Mapema Kabisa Rais alitanabaisha kuwaa yeye na JPM ni kitu kimoja! Na ataendeleza. yote!

Lakini hali ilivyo zilongwa mbali zitendwa mbali'Mama anapindua meza!

CCM inawarudisha viongozi waandamizi waliondolewa kwa kosa usaliti'

Hàta viongozi wa Mashirika ya Umma waliondolewa kwa kile tulichoambiwa ni wezi : wanarudishwa.

Viongozi wanakosoa waziwazi sera za Uchumi za Magufuli ambapo awali Walikuwa wanasifia!

...Cha kushangaza walewale waliokuwa wanashangalia enzi za Magufuli Ndio haohhao wanashangalia meza ikipinduliwa!

Bila shaka CCM imechoka ,kama sio CCM basi ilee cream ya ya Uongozi haina Vision tena ! ZAIDI ya kulenga kukaa madarakani!

Wana CCM wafia Chama hamuoni aibu!Tunahitaji Katiba Mpya itaakayo ruhusu Taifa kuwa Dira inayotuongoza kulekea tunakotaka kwenda!

Haiwezekani miezi 12 iliyopita tulikuwa tunawatukana Wazungu ,kuwa ni Mabeberu leo tunawaendea tunamshangalia mama kuwa anafungua Nchi!

Ilhali naye alikuwaa Makamu wa Rais!
Taifa limejaa unafiki
Woga
Uzandiki
Kutojitambua
Kimbelembele
Uchawa'
Uchumia tumbo
Mnaopinga Kuandikwa Kwa Katiba Mpya Hamuitendei Haki Tanzania!
Nihitimishe kwaneno la Waziri Mkuu Mstafu Frederek Sumaye...Kama Kinana ni kipimo Cha Uadilifu,Mimi ni Mtakatifu'😋
 
Ukweli ni huo. Ila nikwambiee kitu, Chama Tawala kilpukutika nguvu ya wananchi siku nyingi Sana ila Nguzo kuu yao ni Dolar ambayo wameiweka kwapani,siku Hii ikija kudondoka kwapani ndy siku hyo..Hiki chama kitapotea kimoja!!
 
Ukweli ni huo. Ila nikwambiee kitu, Chama Tawala kilpukutika nguvu ya wananchi siku nyingi Sana ila Nguzo kuu yao ni Dolar ambayo wameiweka kwapani,siku Hii ikija kudondoka kwapani ndy siku hyo..Hiki chama kitapotea kimoja!!
Kabisa Mkulima ,tuna viongozi na uongozi wa ajabu kabisa
 
Back
Top Bottom