Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,349
- 6,476
Kuna mgombea mmoja wa kiti cha Urais amekuwa akinukuu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (toleo la 20 Juni, 2005) ibara ya 16 mara anapojibu swali la waandishi wa habari akiwemo yule wa BBC wakati wa hardtalk kuhusu masuala ya ushoga. Ibara hiyo inahusu haki ya faragha na usalama ambayo ipo kwenye fungu la haki ya kuishi. Ibara hiyo inasomeka kama ifuatavyo:
"16.- (1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama wa nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii."
Pia kifungu kidogo cha pili kinatoa ruhusa faragha kuingiliwa.
Kwa mujibu wa sheria zetu, ushoga ni kosa la jinai, hivyo kwa mujibu wa katiba kama jinai inatendeka, basi faragha hiyo itaingiliwa kwa mujibu wa sheria husika zinazoruhusiwa na katiba. Na sio kweli kuwa faragha hiyo haingiliwi kabisa kwa mujibu wa jibu la mgombea huyo.
Yaweza kuwa kumtia hatiani shoga ni ngumu kama rushwa hasa pale wote wawili wanapokubaliana, ila kwa mujibu wa mila na desturi zetu na maana ya maneno yaliyotumika kwenye katiba kama 'unyumba' yawezabainika kwa kiwango fulani. Pia sheria ya ndoa ipo wazi kwenye kutokutambua ushoga, fuatiilia hapa Sheria Kiganjani.
Je, huyo mgombea hakumbuki faragha yake iliingiliwa kisheria pale alipopekuliwa nyumbani kwake Tegeta Dar baada ya kugoma kupimwa mkojo? Na, kwa nini haisomi hiyo nukuu ya ibara ya katiba ili wananchi wanaomsikiliza wasiokuwa na muda au uwezo wa kupambanua katiba waelewe vizuri?
Kuna mfano, ingawaje katiba yao siifahamu vizuri ila ni wazuri kwenye haya mambo ya faragha, huko Uingereza, polisi walifika nyumbani kwa Boris Johnson pale walipozozana na mchumba wake, Carrie Symonds (tazama video hapo chini).