Kwa jibu la mmoja wa wagombea Urais nchini kwetu Tanzania, hivi Katiba ya nchi inasemaje haswa juu ya uhuru wa faragha (privacy)?

Mkuu hatuhitaji kabisa mambo ya kutafsiriana vifungu vya katiba wala sheria zetu, tunataka tubadili mfumo wa kiutawala utakaoheshimu katiba na sheria tulizojiwekea! Kama tunaongozwa na watu wasi heshimu katiba na wanaovunja sheria hadharani haileti maana hata kuzitafsiri sheria hizo wakati haziheshimiwi! Ni bora tumpe kijiti Lissu ambaye angalau anazikumbuka sheria katika popote anapokuwa na hivyo ataongoza nchi kwa misingi na taratibu za kisheria! Penye sheria pana haki, penye haki pana amani! Hatuwezi kamwe kujitapa kuwa tutaendelea kuwa kisiwa cha amani wakati hatufuati sheria, tunakandamiza haki, hapa amani yetu hata kama inaishi basi inaishi kwa kurefusha maisha tu kama mwathirika anayetumia ARV!
 
kuna vitu vinafurahisha humu ila basi TU, sasa maswala ya kikatiba watu wanajibuje kimihemko ya kidini, ama Tz ni nchi inayoongozwa na misingi ya kidini??
 
Back
Top Bottom