Kwa hili TCRA imulikeni Azam TV

Kwa hili TCRA imulikeni Azam TV

Mkuu Pasco ,hapa essence sio vya bure ama vya kulipia ,na sio kwamba wengine tunapenda vya bure,swala ni sera ama kanuni ama sheria za nchi zinasemaje? Je hawa wawekezaji wanazifuata??? au serikali imewekwa mfukoni na hawa wawekezaji?
Hili nalo neno!, universal law dunia nzima ni "he who pays the piper, may call the tune!", Tanzania sa beggars as we are, unategemea nini?!, lazima tuwekwe mfukono na kujituliza tuli!.

Pasco
 
Mkuu Mtawala wa Mwisho, hiki ndicho one of the best Watanzania tunachojua!, kulalamika!. Hata mtendewe mazuri vipi hamuoni, badala ya kuwa na shukrani, ni kulaumu tuu!. Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika kuingia kwenye full digitali kwa asilimia 100!. Kinachotakiwa sasa ni kwa sisi Watanzania tutengeneze local contents za kushibisha machaneli bwerere ya digitali kwenye hao multplex operators watatu, yaani soon itaishuhudia Jamiforum TV ikiwa hewani, haya majadiliano yetu humu ambayo ni limited kwa watumia internet tuu, sasa yatakuwa huru kwa wote!.

Kupitia hii technolojia ya Digitali, kutazama TV sasa ni kwenye simu, kwenye gari, kwenye laptop, hakuna tena hata haja ya kununua hizo TV!, tukija kwenye TV Set, ni smart TV, internet kwenye simu, etc!.

Kama una smart phone na uko DSTV, una download DSTV Mobile, unaingiza number ya kadi yako ya DSTV, then DSTV hiyo kwenye simu yako bure!, bila Digitali tungeweza wapi?!.

Nenda pale Regency , Muhimbili, Hindumandali na Aghakan kashuhudie jinsi Telemedicine inavyofanya kazi, operation Dar es Salaam, mabingwa Marekani!, yote haya huyaoni?!.

Nenda kwenye vyuo ushuhudie jinsi mijibu inayopenda dezo, inavyopark magari yao kula net ya bure kwa wanavyuo!.

Nenda shule za msingi ushuhudie jinsi watoto wa shule zetu wanavyoenjoy distance education kupitia internet connectivity!, ila wewe kama wa simu ya toch, haya yote unaweza usiyajue.

Tukija kwenye money transfer, badala ya kushukuru hizi mobile transfer, ndio kwanza unalalamikia viwango?!, si vimeandikwa na vimebandikwa kwenye kila wakala?. Kwani umelazimiashwa kutumia mobile money transfer za kulipia wakati benki ni bure?!, nenda kaendelee kupanga foleni siku nzima, jumlisha na nauli na mafuta!.

Mimi nimepanga jengo la NHC hapa town kodi ni TZS 3,000,000 kwa mwezi, kupitia hii Digital Technology, niko mbioni kufunga ofisi, na kila kitu kufanyia from home, malipo yote ni kwa mpesa, vipindi napeleka on line, studio ni visual iko ndani ya Final Cut Studio program, sasa ofisi ya nini?!.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe, Watanzania bado hatujaandaliwa vyema ku utilize fursa za digitali, hivyo kujikuta tuna fursa lakini bado tunaendelea kuoparate kizamani, mfano watu wengi tayari wanatumia mpesa, lakini bado anachoma nauli kwenda benki au kufoleni kwenye ATM atoe pesa aweke kwenye Mpesa ndipo atume, kumbe ukiwa home tena umejilalia kitandani kwako, unaweza kutoa pesa kupitia sim banking na kuziingiza mpesa bila usumbufu na kwa gharama nafuu sana, na kitu kikubwa zaidi you save time!.

Tufike mahali Watanzania tuache kulalamika, tuchangamkie fursa tubadili maisha yetu, tuachane na maisha ya kianolojia twende kwenye digital life!.

Pasco
Mkuu Pasco, umeeongelea maendeleo ya teknolojia, lakini mimi naongelea TCRA kama wasimamizi na watetezi wa wanyonge katika kuangalia mnyonge asinyonywe na hii mitandao ambayo kila ikifika muda wa kuanza kulipa kodi inabadilishwa majina. Kuna kitu gani kina justify mtu ukitoa kuanzia elf kumi ukatwe 1200? Huoni kama 1200 ni hela nyingi sana? Je tumewahi kujiuliza unyonyaji wa makampuni ya simu katika uchumi wa Tanzania? Je TCRA wamefanya nini? Kwenye hiyo 1200 serikali inapata sh ngapi? Kwanini? Kuhusu TV kuwa digital au analogy inamsaidia nini maskini wa kijijini? Sanasana kuna watu wengi zaidi wamekosa fursa ya kuangalia tv kwa kukosa ving'amuzi. Masikini ananufaika vipi kwa kuangalia tv mpaka ionekane anapenda vya bure kwa kukazania inatakiwa free channel ziwepo? Sanasana mwenye tv na mtangaza bidhaa ndo wananufaika zaidi kwa kufikia watu wengi zaidi. TCRA haipo kwa ajili ya maslahi ya umma kama inavyotakiwa, wananyamazia faulo nyingi sana zinazofanywa na hizo corporates ambazo zinaongoza kwa kukwepa kodi na kuibia wananchi makato yasiyoeleweka ya kwenye mitandao ya simu. By the way, hivi zile 650 million dollars ziliibiwa Vodacom hilo sakata limeishia wapi? Au wanataka kutuaminisha kama ilivyokuwa escrow kulikuwa hamna hela ya kodi za umma mle? Na kama zimo TCRA wamefanya nini?
 
Mkuu una uhakika na unachosema ? Unajua Leseni ya Azam na DSTV ina tofauti na kina Startimes, Continental et al.... ambao hawa leseni yao inawabana kuonyesha zile Free to Air Channels (yaani hata ukipata TV yenye internal Decoder bila Kingamuzi chochote unapata hizo channels za Free to Air..

Hawa kina Azam, DSTV na Cable ni tofauti wewe unacholipia ni plus ile connection kwahio pindi unapoacha kulipa connection inakatwa full...,

Kwa ufupi ni kwamba..Azam TV amesajiliwa nje ya nchi lakini ana-operate kazi zake Tanzania. (Malaysia)
 
Mkuu Pasco, umeeongelea maendeleo ya teknolojia, lakini mimi naongelea TCRA kama wasimamizi na watetezi wa wanyonge katika kuangalia mnyonge asinyonywe na hii mitandao ambayo kila ikifika muda wa kuanza kulipa kodi inabadilishwa majina. Kuna kitu gani kina justify mtu ukitoa kuanzia elf kumi ukatwe 1200? Huoni kama 1200 ni hela nyingi sana? Je tumewahi kujiuliza unyonyaji wa makampuni ya simu katika uchumi wa Tanzania? Je TCRA wamefanya nini? Kwenye hiyo 1200 serikali inapata sh ngapi? Kwanini? Kuhusu TV kuwa digital au analogy inamsaidia nini maskini wa kijijini? Sanasana kuna watu wengi zaidi wamekosa fursa ya kuangalia tv kwa kukosa ving'amuzi. Masikini ananufaika vipi kwa kuangalia tv mpaka ionekane anapenda vya bure kwa kukazania inatakiwa free channel ziwepo? Sanasana mwenye tv na mtangaza bidhaa ndo wananufaika zaidi kwa kufikia watu wengi zaidi. TCRA haipo kwa ajili ya maslahi ya umma kama inavyotakiwa, wananyamazia faulo nyingi sana zinazofanywa na hizo corporates ambazo zinaongoza kwa kukwepa kodi na kuibia wananchi makato yasiyoeleweka ya kwenye mitandao ya simu. By the way, hivi zile 650 million dollars ziliibiwa Vodacom hilo sakata limeishia wapi? Au wanataka kutuaminisha kama ilivyokuwa escrow kulikuwa hamna hela ya kodi za umma mle? Na kama zimo TCRA wamefanya nini?
  1. Faida ya Digital kwa Mkulima wa Kawaida-Zamani alilazimishwa kuangalia TV chache, hivyo hata kama ni utumbo utumba, he had no choice!, sasa ana choice kubwa, hivyo options za kuona developmental news ni kubwa kuliko mwanzo.
  2. Zamani alisubiri kupangiwa bei za mazao yake na mnunuzi bila kujua bei ya soko, kupitia digital technology sasa anaewezo wa kujua bei ya soko hivyo kupanga auze bei gani na sio kupangiwa na kwa vile amepatiawa access to masoko, anaweza kuleta mazao yake sokoni na kupata faida kubwa.
  3. TCRA ina majukumu yake na inatoza ada zake, mamlaka nyingine nazo zina majukumu yao na kutoza ada zao, TCRA inakusanya maduhuli na kupeleka serikalini, mwenye jukumu la kukusanya kodi ni TRA, sio kazi ya TCRA kuisanyia kodi TRA, kama TRA haitozi kodi sio kazi ya TCRA kuikusanyia.
  4. Mwenye jukumu la kusimamia money transfer na ndie mwenye kuidhinisha viwango sio tuu vya mobile money transfer had baking transactions zote, kama BOT imeridia viwango hivyo ndio gharama za money transfer, hiyo ni kazi ya BOT, sio jukumu la TCRA kuamua viwango vya money transfer na sio jukumu lao kujua kama makampuni ya simu yanalipa kodi ya hizo money transfer, jukumu la TCRA ni kupanga viwango vya rarrifs za mawasiliano, hayo ya money transfer ni ya BOT, yale ya TAX ni ya TRA na yale ya ubadilishaji umiliki ni ya BRELA, kila mtu na jukumu lake, hakuna kuingiliana. Kama unamalamiko ya tarrifs nenda TCRA, kama una malamiko ya transfer fee, nenda BOT, kama una mashaka na kodi, nenda TRA na kama huna uhakika na hizo changing names mfano toka Celtel-Zain- Aitel kama tanfse fee imelipwa, nenda Brela!
  5. Hizo milioni 650 za Voda, kaulizie TRA, nijuavyo mimi hakuna aliyelalamika kuibiwa so far!.Kama ilivyo escrow, sio fedha za umma bali kodi ni ya umma, kodi huwa inalipwa wakati wowote tuu, ndio maana hujasikia Rugemalila wala PAP akishitakiwa kwa wizi wowote wala ukwepaji kodi wowote!.
NB, mimi sio mtu wa TCRA bali ni communicator, hivyo na deal sana na TCRA na maofisi ya simu na malipo yangu yangu yote siku hizi nayafanya kwa M-Pesa!.

Pasco
 
Wanaosema dstv wanakata TBC ni waongo, dstv muda wa malipo ukiisha basi tbc na channel tena wanakuwa hewani
Mkuu hiyo package yako ya DSTV ni ipi ambayo bundle ikiisha unaona TBC?
 
Duh,sasa huu mkanganyiko wa Local Channel mbona naona utata.

Maana nyingine zinazoitwa kwamba sio Local Channel lakini zimechiwa wazi kama Local Channels
 
Local Chanels za bure ni 5 tuu,
  1. TBC-1,
  2. ITV,
  3. Star Tv,
  4. Channel Ten
  5. Na EATV
TV nyingine zote sio bure, wakiwemo hao Azam, ZBC, Clouds TV, Mlimani TV, TV One, Tumaini TV, CTN, Capital, etc.

Kiukweli ZBC ilipaswa kuwa ni ya bure lakini sijui kwa nini sio bure!.

Pasco

Clouds nayo bure hata ZBC 1 na 2 pia ni bure katika kisimbusi cha azam.

Hapo sasa,maana za bure na zisizo za bure hali inakuwa tata.

Kwa upande wa Azam wadau wamenielewesha vizuri.Maana lugha ya kuita Local Channes ndio kwangi nilikuwa sielewi,na inaonyesha bado tata
 
Services Providers wa TV na wasimamiaji wa Ving`amuzi vyoote.
Wametakiwa kuachia Channels za ndani,Local Channels bure kwa muda maalum baada ya Bundle ya mteja kuisha.
Kwa maelezo ya TCRA hapo awali.

Sasa Azam Tv wao kama Bundle ikiisha,basi Channel zao ambayo ni Local Channel AZAM TV TWO na ONE,huzifunga pia.Nakuziacha nyingine Local Channels kama Star Tv,TBC,ITV,ZBC,EATv.

Sasa je wao sio Local Channels?na wamepewa uwezo wakutoa hadi Taarifa ya Habari.

Sina uhakika kama TCRA walibadilisha huu mfumo.

Acha upotoshaji local channels walizomaanisha na ambazo zilikuwa allowed ni TBC 1,ITV,CHANNEL 10,EATV na STAR TV na siyo local channels zote alafu kingine uwache ubahili sh. 10,000 tu imekushinda kama umeweza kulipia sh.150,000 kwa kisimbuzi unashindwa hiyo monthly subscription?usiwe kama wale wanaonunua gari sh 35,000,000/= alafu wanashindwa kuweka mafuta ya sh. 20,000/= eti unakuta mtu amezimikiwa na bmw x6 barabarani kisa limeisha mafuta ,sasa unamuangalia huyo mtu unashindwa kummaliza alafu unakuta anajitetea asubuhi nilicheki geji ilikuwa inaonesha vizuri.
 
Mkuu hiyo package yako ya DSTV ni ipi ambayo bundle ikiisha unaona TBC?

Mkuu hiyo kitu ipo hata ya kwangu haikuwahi kukata na zile channel za kichina,ila visimbuzi vingine huwa vinakata sasa sijui tofauti ni nini? na ki utaratibu hizo channel ambazo tcra walizi list kama local channels free to air kama tbc , star tv na nyinginezo zinatakiwa kuwa zionekane bure hata kama malipo yatakuwa yamekwisha.
 
Samahani kwa kutoka kidogo nje ya mada, hawa ndugu wa Channel 10 walifanya mabadiliko kidogo juu ya jinsi wateja wanaweza kuipata hii channel kwa Satellite Dish au kwa kupitia ving'amuzi vilivyopo.Sasa kwa wateja wa ving'amuzi vingi wanaendelea kuiona channel ten LAKINI kupitia king'amuzi cha TING channel ten haionekani kabisa, je kuna yeyote mwenye fununu tatizo ni nini? Ahsante
 
wenzie wanatoa kwa imani kansani watapata baadae..we unatoa nakupatahapohapo unalalama YESU SHUKA BWANA
 
Wezi wengine ni ZUKU, yaan bundle likiisha local channels kama ITV,TBC1,CHANNEL10, EATV zote wanakata. TCRA hawasemi lolote
 
Back
Top Bottom