Kwa hili TCRA imulikeni Azam TV

Kwa hili TCRA imulikeni Azam TV

Local Chanels za bure ni 5 tuu,
  1. TBC-1,
  2. ITV,
  3. Star Tv,
  4. Channel Ten
  5. Na EATV
TV nyingine zote sio bure, wakiwemo hao Azam, ZBC, Clouds TV, Mlimani TV, TV One, Tumaini TV, CTN, Capital, etc.

Kiukweli ZBC ilipaswa kuwa ni ya bure lakini sijui kwa nini sio bure!.

Pasco
Clouds nayo bure hata ZBC 1 na 2 pia ni bure katika kisimbusi cha azam.
 
Hivi hawa wenye cable TV ambao siyo wireless hawahusiki kufungua local channels kama bundle ikiisha? Arusha kuna Milan Cable anatunyanyasa.
 
Clouds nayo bure hata ZBC 1 na 2 pia ni bure katika kisimbusi cha azam.
Mimi nauzungumzia ubure wa TCRA na sio ubure wa Azam TV, unless kama huo ubure wa TCRA umekuwa extended to Clouds na Azam TV.

Pasco
 
Hivi hawa wenye cable TV ambao siyo wireless hawahusiki kufungua local channels kama bundle ikiisha? Arusha kuna Milan Cable anatunyanyasa.
Cable TV zote ni kama umiliki tuu wa decoder za mahotelini, yaani mwenye cable ndio anaamua aonyeshe nini, hawajibiki kwa TCRA!.

Mimi ni mfuatiliaji wa Telemundo kwenye DSTV, kila nikisafiri, kabla sijapanga hoteli huwa nauliza kama wana DSTV ndipo nachukua room. Sio mara moja au mbili napanga hoteli yenye DSTV kumbe wana decoder moja tuu bila extra view, hivyo chanel inayoonyeshwa ni moja kwa vyumba vyote hoteli nzima, hivyo kujikuta siwezi kuangalia Telemundo!.

Pasco
 
Hiyo DSTV yako itakuwa ni DSTV very Special!, kwangu malipo ya DSTV yakiisha ni yameisha inakata kila kitu, hakuna cha bure pale!.

Pasco.

Mimi pia inabaki TBC na Chanel Ten, wengi hamuangalii kama zipo ndio maana mnabisha.
 
Hiyo DSTV yako itakuwa ni DSTV very Special!, kwangu malipo ya DSTV yakiisha ni yameisha inakata kila kitu, hakuna cha bure pale!.

Pasco.

Hapana mkuu kama uko premium hakika muda ukiisha bado utakuta TBC na hiyo Channel Ten yafanya kazi kama kawaida.

Mimi pia inabaki TBC na Chanel Ten, wengi hamuangalii kama zipo ndio maana mnabisha.

Bora umekuja saidia
 
Hakuna channel yoyote inayotakiwa ionekane baada ya bundle yako kwisha kwa wote wanaopata channels kupitia sattelite.
Ukiona bundle imeisha na bado inaonyesha ujue wameacha tu lakini hawabanwi na sheria yoyote ya nchi au kanuni.Hivyo TCRA hawana mamlaka kwa sasa ya kuwalazimisha watoa huduma kuacha local channel yoyote baada ya bundle kwisha.
Wanaolazimishwa na sheria kuacha local channel free tena zile zenye leseni za kitaifa ni wale wote wanaorusha channel zao kwa mfumo wa Antena tu.
Wakati mwingine serikali wanakosea kukaa kimya bila kutoa elimu kwa wananchi wake.
Lakini pia na Watanzania tulio wengi ni wavivu wa kutafuta ukweli.
Kwenda TCRA kuuliza itakugharimu kiasi gani?
 
Hiyo DSTV yako itakuwa ni DSTV very Special!, kwangu malipo ya DSTV yakiisha ni yameisha inakata kila kitu, hakuna cha bure pale!.

Pasco.
Huo utaratibu ulikuwepo zamani ndo ikawa TBC inabaki free lakini now days hakuna cha bure
 
Mimi kinachoniudhi kwenye Azam kuna chanels ziko kwenye list lakini hazionekani.Kama vipi waziondoe tu kwenye list.Lingine kuna chanel ya NTV Kenya na Uganda ziko kwenye list hazionekani nikafuatilia wakasema wao waligoma chanel hiyo isionekane kwenye nchi zingine tofauti na Kenya tu.Sasa kama ni hivyo kwanini wasiziondoe kwenye list yao maaana inaonekana wana chanel nyingi nyingi kumbe ki uhalisia si😵ther chanels nazo ni magumashi tupu.
 
Wewe unaye ilaumu Azam tv je VP kuhusu dstv ambao kifurushi kikiisha na kilakitu kinaka tusipende vya bure. Ww ulinunua king'amuzi ili uangalie bule.
 
Local Chanels za bure ni 5 tuu,
  1. TBC-1,
  2. ITV,
  3. Star Tv,
  4. Channel Ten
  5. Na EATV
TV nyingine zote sio bure, wakiwemo hao Azam, ZBC, Clouds TV, Mlimani TV, TV One, Tumaini TV, CTN, Capital, etc.

Kiukweli ZBC ilipaswa kuwa ni ya bure lakini sijui kwa nini sio bure!.

Pasco
Dstv channel za bure ni zile za kichina kama cctv news etc and dish 100 ... zingine zote ni za kulipia zikiwemo local zote
 
TCRA wamejaa ubabaishaji tu, hakuna kazi yoyote wanayofanya, tunaibiwa kwenye simu, TV ndo hivyo hazieleweki! Hiki kitengo watimuliwe wote, wamezoea kupokea rushwa na kunyamazia matatizo ya jamii. Gharama za kutuma mpesa, tigo pesa ni kubwa kuliko bank kwanini? Wamulikwe hawa
 
Dstv channel za bure ni zile za kichina kama cctv news etc and dish 100 ... zingine zote ni za kulipia zikiwemo local zote
Kiukweli kutokana na kutozoea kabisa vya bure, nikipata tuu ile sms ya kunikumbushia siku ya mwisho, huwa nalipia kabla, na sijawahi ku seach kama kuna bure baada ya kuishiwa!.

But thanks, now I know, ila pia inawezekana hiyo bure inategemea dekoda mtu anayotumia, mimi natumia explora, kiukweli hakuna bure yoyote, ila this time ikiisha nitapitiliza kidogo ni seach!.

Mkuu Pasco ,hapa essence sio vya bure ama vya kulipia ,na sio kwamba wengine tunapenda vya bure,swala ni sera ama kanuni ama sheria za nchi zinasemaje? Je hawa wawekezaji wanazifuata??? au serikali imewekwa mfukoni na hawa wawekezaji?
 
Last edited by a moderator:
TCRA wamejaa ubabaishaji tu, hakuna kazi yoyote wanayofanya, tunaibiwa kwenye simu, TV ndo hivyo hazieleweki! Hiki kitengo watimuliwe wote, wamezoea kupokea rushwa na kunyamazia matatizo ya jamii. Gharama za kutuma mpesa, tigo pesa ni kubwa kuliko bank kwanini? Wamulikwe hawa
Mkuu Mtawala wa Mwisho, hiki ndicho one of the best Watanzania tunachojua!, kulalamika!. Hata mtendewe mazuri vipi hamuoni, badala ya kuwa na shukrani, ni kulaumu tuu!. Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika kuingia kwenye full digitali kwa asilimia 100!. Kinachotakiwa sasa ni kwa sisi Watanzania tutengeneze local contents za kushibisha machaneli bwerere ya digitali kwenye hao multplex operators watatu, yaani soon itaishuhudia Jamiforum TV ikiwa hewani, haya majadiliano yetu humu ambayo ni limited kwa watumia internet tuu, sasa yatakuwa huru kwa wote!.

Kupitia hii technolojia ya Digitali, kutazama TV sasa ni kwenye simu, kwenye gari, kwenye laptop, hakuna tena hata haja ya kununua hizo TV!, tukija kwenye TV Set, ni smart TV, internet kwenye simu, etc!.

Kama una smart phone na uko DSTV, una download DSTV Mobile, unaingiza number ya kadi yako ya DSTV, then DSTV hiyo kwenye simu yako bure!, bila Digitali tungeweza wapi?!.

Nenda pale Regency , Muhimbili, Hindumandali na Aghakan kashuhudie jinsi Telemedicine inavyofanya kazi, operation Dar es Salaam, mabingwa Marekani!, yote haya huyaoni?!.

Nenda kwenye vyuo ushuhudie jinsi mijibu inayopenda dezo, inavyopark magari yao kula net ya bure kwa wanavyuo!.

Nenda shule za msingi ushuhudie jinsi watoto wa shule zetu wanavyoenjoy distance education kupitia internet connectivity!, ila wewe kama wa simu ya toch, haya yote unaweza usiyajue.

Tukija kwenye money transfer, badala ya kushukuru hizi mobile transfer, ndio kwanza unalalamikia viwango?!, si vimeandikwa na vimebandikwa kwenye kila wakala?. Kwani umelazimiashwa kutumia mobile money transfer za kulipia wakati benki ni bure?!, nenda kaendelee kupanga foleni siku nzima, jumlisha na nauli na mafuta!.

Mimi nimepanga jengo la NHC hapa town kodi ni TZS 3,000,000 kwa mwezi, kupitia hii Digital Technology, niko mbioni kufunga ofisi, na kila kitu kufanyia from home, malipo yote ni kwa mpesa, vipindi napeleka on line, studio ni visual iko ndani ya Final Cut Studio program, sasa ofisi ya nini?!.

Kitu ambacho nakubaliana na wewe, Watanzania bado hatujaandaliwa vyema ku utilize fursa za digitali, hivyo kujikuta tuna fursa lakini bado tunaendelea kuoparate kizamani, mfano watu wengi tayari wanatumia mpesa, lakini bado anachoma nauli kwenda benki au kufoleni kwenye ATM atoe pesa aweke kwenye Mpesa ndipo atume, kumbe ukiwa home tena umejilalia kitandani kwako, unaweza kutoa pesa kupitia sim banking na kuziingiza mpesa bila usumbufu na kwa gharama nafuu sana, na kitu kikubwa zaidi you save time!.

Tufike mahali Watanzania tuache kulalamika, tuchangamkie fursa tubadili maisha yetu, tuachane na maisha ya kianolojia twende kwenye digital life!.

Pasco
 
Back
Top Bottom