Nifah
Platinum Member
- Feb 12, 2014
- 34,418
- 82,398
Toa magari yenu mabovu barabarani bana, yaani watu watengeneze barabara ili kukidhi haja ya magari mabovu? Nchi ya ajabu hii.
Hahahahahaaa tufanyeje sasa? Ndio nchi yetu hii.
Toa magari yenu mabovu barabarani bana, yaani watu watengeneze barabara ili kukidhi haja ya magari mabovu? Nchi ya ajabu hii.
sawa great thinker...unajua sana kuliko strabag yenye miaka zaidi ya 100 Kazini
watatumia trecta kuyavuta!
wewe ndo una ubishi wa kuzaliwa, na ujanja wa uzeeni... kama hakuna variations kwenye contract, contractor hawezi kujenga otherwise. Ishu ya mabasi kunyanyuliwa au kuwekewa provisions, maana yake DESIGN itakuwa imefanyiwa mabadiliko...una ubishi wa kuzaliwa km ckosei.Kama Jambo hulijui omba ueleweshwe.Kwa akili zako kubwa tuambie hayo Mabas yatanyanyuliwa na crene kuwekwa kwenye njia zake.Acha uhayawani kwa mambo usioyajua.
Hujui kitu subiri mradi uanze,hata kusoma alama huweziJamani, kila mtu hapa mjini ameona jinsi barabara za mabasi yaendayo kasi zinavyojengwa kwa utaalamu mkubwa na kampuni ya ujenzi wa barabara STRABAG. Pamoja na kujenga miundo mbinu na vituo vya basi vya kisasa, wamechemsha vibaya katika ujenzi wa barabara zao.
Ukiangalia vizuri, njia zao zinaruhusu kupita basi moja tu kwani ni nyembamba sana. Yaani njia ya kwenda na kurudi linatakiwa kutembea gari moja, hakuna kupishana. Ishu ipo hapa; itakuaje iwapo basi moja limearibika njiani au limepata pancha, Je! Basi linalokuja nyuma yake litapita wapi wakati hivi vinjia vina kingo ndefu?
Na ukumbuke kuwa haya mabasi yatakua yakifuatana, sasa la mbele limeharibika njiani la nyuma litapita wapi?
Jamani, mwenzenu mpaka hapa sijapata majibu labda wataalam wa mambo ya barabara waje kutuelewesha.
Mkuu hao jamaa wamejenga barabara ya maili kumi korogwe hadi mazinde lakini hata kabla ya mwaka sehemu nyingine zimeshabonyea kama sponji mzee magofuli ikague ujionee maajabu
Yaliyopita si Ndwele...Hahahahahaaa tufanyeje sasa? Ndio nchi yetu hii.
Hardman jambo analoongelea hapa Ndugu yetu tumeshalichunguza na jamaa zangu fulani. Ni kwamba hawa wataalamu wetu wamechemsha. Sisi tuliona itakuwa tatizo kubwa sana iwapo bus moja lita breakdown during rush hour
Mkuu hii ni tanzania nchi ambayo iko Africa na zaidi ya 90% ya wakazi wake ni waafrica,,, ustaarabu huku bado haujafika. Inaonekana hii barabara inayozungumziwa wewe huijui, hii barabara iko kwenye hatua zake za mwisho kabisa tena nafikili wako kwenye commisioning hivi sasa,, kiukweli sisi watumiaji wa hiyo barabara tunaijua vizuri na tunaona nini kinachoendelea,
barabara ni nyembamba sana na kuna wakati mbele yako kukiwa na lori au basi inabidi ufanye kazi kulipita maana akiyumba kidogo tu basi ajali tayari,,, hata hivi sasa ikitokea kuna gari limeharibika basi utegemee foleni kubwa, na kuna wakati hata namna ya kulitoa hilo gari ni shida mpaka litengemae au lisukumwe maana hiyo breakdown nayo kufika inabidi ikae kwenye foleni nayo....
Dar es salaam ni mji unaokua kwa kasi kwa maana ya population na facilities,, mambo mengi hasa miundombinu huhitaji solution ya moja kwa moja na iwe na life span kubwa na kuwe na standard ambazo zitafuatwa.. Magari private dar es salaam ni mengi na watu wanazidi kuagiza na hakuna namna ya kuwazuia,,, suluhu ni kuwa na miundombinu inayokidhi na itakayokidhi....
Yani wewe umejiona una akili nyingi sana kuliko mjerumani?
Uwezekano upo tena mkubwa sana.Yani wewe umejiona una akili nyingi sana kuliko mjerumani?
Mkuu kama unafikili kila mwenye uzoefu zaidi ya miaka 100 basi anaweza kila kitu 100% uko wrong kaka,, "kuna ndege moja walikoseaga design ya engine locks kwenye bawa za ndege na matokeo yake ikawa maafa baada ya engine moja ya upande wa kulia kuanza kufail lock zake mbili na kudondoka angani na kuitwanga engine nyingine, walizuia zile ndege za namna ile zote zisimame na redesign ifanyike" makosa kwenye engineering yanasababishwa na vitu vingi sana kaka na ndio maana suala la bahati mbaya halikubaliki,,, mara ngapi umesikia toyota wanaagiza gari zirudi viwandani??? waulize wataalamu wa makatapila kuna kitu kinaitwa PIP, SERVICE LETTER, SERVICE MAGAZINE NK.. watakuambia ni nini.. Tumeona ile barabara ya mbagara imerudiwa na kajima je nao hawana uzoefu wa 100 year??? pale mbeya meta wachina wamerudia barabara zaidi ya mara mbili, hapo napo ni vipi???
Makampuni kama haya ni kweli yanauzoefu uliotukuka na watalaamu waukweli,, wanafanya kazi zenye weledi kwao Ulaya na sio Africa, ulaya usimamizi ni wa kueleweka na kila kitu kiko under standard bila siasa... Africa usimamizi hakuna na hawa watu huingiliwa na wanasiasa sana mwisho wa siku kazi huharibika kwa maslahi ya waafrica wenyewe... Unawajua GREEN ACRE LTA wako wapi sasa?? walipomaliza kipande chao cha barabara kutoka Tinde-shinyanga to somewhere mpakani na mwanza hawakupewa project nyingine tena na walifanya kazi nzuri, sasa angalia kuanzia walipoishia kwenda mwanza kilichotokea....
Lazima ujuwe STRABAG wanatafuta faida na wao ni binadamu,, msipowasimamia kiweledi na mkaruhusu watu wenu kuwashawishi 20% ipatikane na wanajua hao hao watu wenu watawalinda wafanyeje sasa,, ulishajiuliza kwanini walishindwa KENYA?? 20% toa tukupe kazi lakini standard lazima iwepo, tukizingatia hili tutafanikiwa..