Kwa hili STRABAG mmechemsha vibaya sana

Kwa hili STRABAG mmechemsha vibaya sana

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Jamani, kila mtu hapa mjini ameona jinsi barabara za mabasi yaendayo kasi zinavyojengwa kwa utaalamu mkubwa na kampuni ya ujenzi wa barabara STRABAG. Pamoja na kujenga miundo mbinu na vituo vya basi vya kisasa, wamechemsha vibaya katika ujenzi wa barabara zao.

Ukiangalia vizuri, njia zao zinaruhusu kupita basi moja tu kwani ni nyembamba sana. Yaani njia ya kwenda na kurudi linatakiwa kutembea gari moja, hakuna kupishana. Ishu ipo hapa; itakuaje iwapo basi moja limearibika njiani au limepata pancha, Je! Basi linalokuja nyuma yake litapita wapi wakati hivi vinjia vina kingo ndefu?

Na ukumbuke kuwa haya mabasi yatakua yakifuatana, sasa la mbele limeharibika njiani la nyuma litapita wapi?

Jamani, mwenzenu mpaka hapa sijapata majibu labda wataalam wa mambo ya barabara waje kutuelewesha.
 
Sijaiona project yote..ila lazima kutakuwa na sehemu za kutolea mabasi kwa dharura...
Sitarajii kampuni ifanye project kubwa kiasi hicho alafu washindwe kufikiria kitu kidogo namna hiyo chances are they have alternative already
 
Huenda kukawa na huduma za kuvuta / kubeba magari yaliyoharibika kila baada ya umbali fulani!
 
Hardman jambo analoongelea hapa Ndugu yetu tumeshalichunguza na jamaa zangu fulani. Ni kwamba hawa wataalamu wetu wamechemsha. Sisi tuliona itakuwa tatizo kubwa sana iwapo bus moja lita breakdown during rush hour
 
Last edited by a moderator:
Hilo hata mimi nimelifikiria, kunaweza kukawa na magari ya breakdown lakini na yenyewe yatapata shida kufika eneo la tukio. Zile kingo wameweka kutuzuia Wabongo tusitumie ile njia lakini ndo wametengeneza tatizo lingine.
 
Yani wewe umejiona una akili nyingi sana kuliko mjerumani?

Ndugu, acha kuchanganya habari. Mjerumani kwani katolewa akili wapi? Mchangiaji kadadavua kuwa kampuni ya Uhandisi Ushauri na mwakilishi wa Client/ Mshitiri( kwa hapo ni Tanroads) walitakiwa walione tatizo hilo na kushauri promptly!
 
Kwa mfumo mkubwa kama huo, lazima uwe na breakdown service. Pia vyombo vinavyotumika ubora wake ni lazima uangaliwe kwa ukaribu na kila siku. Kuna mji mmoja naufahamu wana mfumo Kama huo.

Kwanza ni nadra sana kukuta breakdown maana wako makini na service za vyombo vyao, pia breakdown service ina response ya 5 to minutes. Jiulize jiji Kama London linatumia tube train Na breakdown zinatokea na njia ni moja Kama hiyo hiyo ya DART !!

Unadhani hakuna kusubiria hizo response unity kuondoa tube train iliyo haribika? Kwa taarifa tu, hiyo hutokea kila siku. He sisi ni kina nani kuishi perfect world ? Yaani gharama za ujenzi zilivyo juu mnataka njia pana? Kwa eneno lipi? Na Kwa hela gani? Huo mradi ungekuwa Wa trillions tungeukubali?

Engineer bora atafikiria jinsi breakdown response unity zitasetiwa maana kwenye vituo kuna nafasi Kubwa hivyo magari ya recovery yanaweza park kila baada ya kilometre 15 or 20 kusubiria la kutokea ... lukelo sakafu
 
Last edited by a moderator:
Breakdown services ndio suluhisho. Lakini kubwa zaidi ni kinga kuliko tiba. Magari mabovu yasiruhusiwe barabarani.
Japo emergency zitatokea lakini zitakuwa kidogo sana. Sasa hivi unaweza kusema gari ambazo hazistahili kuwa barabarani zipo nyingi tu zinatembea. Ni matokeo ya rushwa kunemeesha matrafiki.
 
Hardman jambo analoongelea hapa Ndugu yetu tumeshalichunguza na jamaa zangu fulani. Ni kwamba hawa wataalamu wetu wamechemsha. Sisi tuliona itakuwa tatizo kubwa sana iwapo bus moja lita breakdown during rush hour

Tatizo hilo lipo kwenye barabara ya Morogoro, barabara ya Kawawa wameliona na tuta lililokuwa ninatenganisha barabara ya mabasi ya kasi halikujengwa, ukipita utaona wameweka msitari mweusi badala ya tuta. Huenda labda tuta la Morogoro road nalo likaondolewa.
 
Kwa jinsi ninavyojua jamaa wamechemka ndiyo maana barabara ya magomeni hadi moroco wameviondoa vile vikuta vinavyo tenganisha barabara zinazotumiwa na mabasi
 
Sasa tatizo la Strabag ni nini? Kwani yeye ni designer wa hiyo barabara hadi umtupie lawama?
 
lukelo sakafu

Usiwe na shaka. Kuna mtu humu humu JF aliwahi kuuliza na kuna mtu alielezea jinsi maintanance inavyokuwa na jinsi wanavyobadilishana kupita na akaweka picha za barabara kama hizi za malasya. Tulielewa, labda moderator atutafutie tena ile post akuwekee na kwa faida ya wengine.
 
Last edited by a moderator:
Hawa jamaa kwenye michoro ni fail fail kabisa , wamesababisha foleni kuzidi badala ya kupungua. Wamefunga baadhi ya njia za kuanganika na barabara kuu,

Na serikali sio wabunifu hata kidogo , waziri wa uchukuzi sitta kachoka kabisa , na magufuli anajikusanyia vi 10% vyake vya mwisho mwisho.

Hawakonwabunifu kabisa ni mazezeta hawaoni na hawajali haya sio matusi ni sifa ya mtu asiekuwa na uwezo.
Mfano bara bara ya samora ni pana kuweza kupitisha gari 2 ways kama zamani , hakuna haja ya kuruhusu parking eneo hili ziwacheni gari zipite kwena na kurudi.

Kipande cha bara bara ya morogoro kutoka sokoine mpaka Bibi titi kifunguliwe ili gari zitoke mjini hii ni barabara kubwa kuifunga na kuifanya kuwa ya mabasi tu ni kosa kubwa la kiufundi. Kufungwa kwa barabara hii inafanya gari zote zina zokwenda njia ya morogoro kutokea mjini kutumia njia ya magore UPanga ambayo ne feedroad nyembamba.na kusababisha foleni kubwa barabara ya zanaki na magore na agrey kutokea mjini.
Pia bara bara ya sokoine ni mistake kuifanya one way, hii ni barabara pana na ingetumika vizuri sana kupumulisha gari ziendazo kilwa road temeke na airport. Lakini leo gari zinapelekwa zote samora!!

Wakuu wetu hebu kaeni akili kiduchu tu , nchi haiendi masaa ya kazi yana potezwa bara barani,
Pia ni wakati wa kusimamia sheria za barabarani na kuacha kuwatuma ma trafic kukusanya fedha na vitabu vyao feki
 
lukelo sakafu

TransMilenio_Calle_63.jpgJakartaTransjakartaBusspurInDerJalanSudirman.jpg
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom