Kwa hili STRABAG mmechemsha vibaya sana

Kwa hili STRABAG mmechemsha vibaya sana

Bus ikipata break down inabidi gari ya kuivuta ije mbele ya hiyo iloharibika kwa style ya reverse. halafu inafungwa mnyororo na kuivuta kwenda mbele. nawaza tu
 
Kwa mfumo mkubwa kama huo, lazima uwe na breakdown service. Pia vyombo vinavyotumika ubora wake ni lazima uangaliwe kwa ukaribu na kila siku. Kuna mji mmoja naufahamu wana mfumo Kama huo.

Kwanza ni nadra sana kukuta breakdown maana wako makini na service za vyombo vyao, pia breakdown service ina response ya 5 to minutes. Jiulize jiji Kama London linatumia tube train Na breakdown zinatokea na njia ni moja Kama hiyo hiyo ya DART !!

Unadhani hakuna kusubiria hizo response unity kuondoa tube train iliyo haribika? Kwa taarifa tu, hiyo hutokea kila siku. He sisi ni kina nani kuishi perfect world ? Yaani gharama za ujenzi zilivyo juu mnataka njia pana? Kwa eneno lipi? Na Kwa hela gani? Huo mradi ungekuwa Wa trillions tungeukubali?

Engineer bora atafikiria jinsi breakdown response unity zitasetiwa maana kwenye vituo kuna nafasi Kubwa hivyo magari ya recovery yanaweza park kila baada ya kilometre 15 or 20 kusubiria la kutokea ... lukelo sakafu

Mkuu hii ni tanzania nchi ambayo iko Africa na zaidi ya 90% ya wakazi wake ni waafrica,,, ustaarabu huku bado haujafika. Inaonekana hii barabara inayozungumziwa wewe huijui, hii barabara iko kwenye hatua zake za mwisho kabisa tena nafikili wako kwenye commisioning hivi sasa,, kiukweli sisi watumiaji wa hiyo barabara tunaijua vizuri na tunaona nini kinachoendelea,

barabara ni nyembamba sana na kuna wakati mbele yako kukiwa na lori au basi inabidi ufanye kazi kulipita maana akiyumba kidogo tu basi ajali tayari,,, hata hivi sasa ikitokea kuna gari limeharibika basi utegemee foleni kubwa, na kuna wakati hata namna ya kulitoa hilo gari ni shida mpaka litengemae au lisukumwe maana hiyo breakdown nayo kufika inabidi ikae kwenye foleni nayo....

Dar es salaam ni mji unaokua kwa kasi kwa maana ya population na facilities,, mambo mengi hasa miundombinu huhitaji solution ya moja kwa moja na iwe na life span kubwa na kuwe na standard ambazo zitafuatwa.. Magari private dar es salaam ni mengi na watu wanazidi kuagiza na hakuna namna ya kuwazuia,,, suluhu ni kuwa na miundombinu inayokidhi na itakayokidhi....
 
Hao ndio waliosababisha nyororo refu mjini kila siku.
 
Tunaweza kusema hii ni poor design kwa nchi masikini na kwa mji ambao unakua kwa kasi kama Dar es salaam,, hii ilikuwa ni best design kwa dar es salaam ya mwaka 1988 na si hii ya 2015 - 2030, POpulationa ya watu na magari hukua kila kukicha,

lazima kuwe na standard itakayokwenda miaka 100 bila shida, na lazima kuwe na plan for the next solution ya baada ya miaka 100 mfano good road reserve, clearance for possible flyover roads and tunnel ili vijukuu vyetu navyo vikija visibomoe hii ila vijenge mpya bila ya interference ya day to day public activities....
 
Sijaiona project yote..ila lazima kutakuwa na sehemu za kutolea mabasi kwa dharura...
Sitarajii kampuni ifanye project kubwa kiasi hicho alafu washindwe kufikiria kitu kidogo namna hiyo chances are they have alternative already

mkuu hazipo niamini
 
lukelo sakafu

Mimi nadhani gari zitakazo athitika ni kama gari 10 zilizopo nyuma ya gari iliyo athirika. Gari nyengine zitaingia kwenye barabara ya kawaida kwa dharura.
 
Last edited by a moderator:
Hilo hata mimi nimelifikiria, kunaweza kukawa na magari ya breakdown lakini na yenyewe yatapata shida kufika eneo la tukio. Zile kingo wameweka kutuzuia Wabongo tusitumie ile njia lakini ndo wametengeneza tatizo lingine.

The cheapest and simplest was to use semi-mountable kerbstones to separate the brt lanes.
 
Ndugu, acha kuchanganya habari. Mjerumani kwani katolewa akili wapi? Mchangiaji kadadavua kuwa kampuni ya Uhandisi Ushauri na mwakilishi wa Client/ Mshitiri( kwa hapo ni Tanroads) walitakiwa walione tatizo hilo na kushauri promptly!
Kashauriwa tu
kuwa akili zake zisitumike leo wakati hakuna Basi lililoharibika
Barabara zote zimejengwa na magari yanapigwa jeki safari inaendelea
Hebu tusubiri Basi moja liharibike au Barabara zianze kutumika ndio tutoe mada hizi za kitoto
[h=2]kwa hili STRABAG mmechemsha vibaya sana[/h]
 
Mimi nadhani gari zitakazo athitika ni kama gari 10 zilizopo nyuma ya gari iliyo athirika. Gari nyengine zitaingia kwenye barabara ya kawaida kwa dharura.

mkuu kwani hiyo inakubarika? haitaleta mgogoro na madereva wa daladala?
 
Uko sahihi katika wazo lako , lakini bado huwezi kuwatoa ,Tanroad katika lawama .
Contractor anajenga kile alichoambiwa na mteja wake na si vinginevyo. Mfano wa kuvurunda kwingine kwa Tanroad ni mizani ya vigwaza.. Nayo inakuwa accessed na single lane. Pili mizani midogo tangulizi ipo kwenye barabara Kubwa , hii Ina maana kuwa hata gari ndogo saloon etc nazo zinapima na hii itapelekea mizani ile midogo kutodumu. Kumbuka kila gari inatakiwa ipite 30km/h , kwenye hizo mizani midogo , hii inatapelekea foleni siku zijazo.

Wenzetu wanapojenga mizani Kama ya vigwaza , mizani midogo nayo huwa nje ya barabara Kubwa , faida mojawapo ni kuwa magari ambayo hayahusiki na mizani , yanakuwa huru bila kubugudhiwa.
Concentrate hapo kwenye RED.

Nililazimika kusoma tena hoja ya mleta mada huku nikidhani sijamuelewa na kutaka kujiandaa kukubaliana na wewe! Tatizo la mleta mada sio TANROADS bali STARBAG na ndio maana nikasema ikiwa eneo lenyewe linatosheleza single lane,

hao STRABAG wangefanya nini not mentioning suala zima la mkataba wenyewe! Kama lawama ingekuwa kwa TANROADS nisingesema sana ingawaje nao pia huwezi kuwalaumu! TANROADS is just a government agency, na kama serikali ilikusudia kujenga hizo barabara bila kuongeza additional damages (assuming no budget constraint) ya kubomoa nyumba zingine kando kando ya barabara na hatimae kuwaagiza TANROADS or else kushughulikuwa mchakato uliobaki,

hapo TANROADS wasingekuwa na uwezo wa kutia neno zaidi ya kuishia tu kushauri kv "single lane will create problems with this or that...!" Jibu la serikali lingeweza kuwa simple and clears "the government has no money to build additional lanes...!" or "The government can not go on demolishing houses along Morogoro Rd, so work out as advised...!" Biashara inaishia hapo!
 
Concentrate hapo kwenye RED. Nililazimika kusoma tena hoja ya mleta mada huku nikidhani sijamuelewa na kutaka kujiandaa kukubaliana na wewe! Tatizo la mleta mada sio TANROADS bali STARBAG na ndio maana nikasema ikiwa eneo lenyewe linatosheleza single lane, hao STRABAG wangefanya nini not mentioning suala zima la mkataba wenyewe! Kama lawama ingekuwa kwa TANROADS nisingesema sana ingawaje nao pia huwezi kuwalaumu! TANROADS is just a government agency, na kama serikali ilikusudia kujenga hizo barabara bila kuongeza additional damages (assuming no budget constraint) ya kubomoa nyumba zingine kando kando ya barabara na hatimae kuwaagiza TANROADS or else kushughulikuwa mchakato uliobaki, hapo TANROADS wasingekuwa na uwezo wa kutia neno zaidi ya kuishia tu kushauri kv "single lane will create problems with this or that...!" Jibu la serikali lingeweza kuwa simple and clears "the government has no money to build additional lanes...!" or "The government can not go on demolishing houses along Morogoro Rd, so work out as advised...!" Biashara inaishia hapo!

Naona unawatoa Tanroad kwenye lawama,ila Kama umekiri kuwa ni Tanroad ni government agency yenye uwezo wa kupanga projects kadhaa na yet kukawa na loophole ya kukwepa lawama pindi mambo yanapokwenda mrama kwa kisingizio kuwa yenyewe sio serikali kuu !!!!! basi ni dhahiri kuna tatizo sugu katika utendaji, baina ya serikali na hiyo mamlaka yake!!,
Nilitegemea government agency Kubwa Kama hiyo ,iwe responsible kwa kila itakachopanga , kusimamia au kushauri ili kusiwe na mianya ya kujitetea ambayo practically ndo huchochea rushwa. Hivi kuna maana gani basi kuwa na government agency ambayo ni Kama pambo tu haina maamuzi ??

Ila Kama mtoà mada alikuwa ana nia ya kuwalaumu Strabag basi inawezekana alikuwa hajui mambo ya ujenzi yanavyoratibiwa. Kwa maana kuwa hata Kama hiyo tenda ingechujua kampuni nyingine bado nayo ingefuata maagizo Yale Yale ambayo strabag imefuata.
 
Tukiachana na hoja ya mleta mada, anayepaswa kulaumiwa ni serikali na sio TANROADS! TANROADS inawezekana nae ana nafasi yake lakini katika suala la kuwa na only single lane huwezi kuwalaumu wao wakati wao sio wanao-finance hiyo project! Ikiwa serikali na inaweza kutumia utetezi wa kawaida kabisa kwamba haikuwa na uwezo wa ku-finance multiple lanes ambayo ingehusisha na ubomoaji wa majengo na nyumba nyingine zaidi kote inakopita barabara, sasa TANROADS wangefanya nini? Unataka kusema wangeiambia serikali if you can't finance multiple lanes basi achananeni na mradi wenyewe? Hata ukiwaambia, jibu kwao ni simple tu coz' atakayetoa ushauri kama huo is just a person na ataambiwa leave everything on the desk na wapo watakaokuja kutekeleza mradi; simple as that!
 
Tunaweza kusema hii ni poor design kwa nchi masikini na kwa mji ambao unakua kwa kasi kama Dar es salaam,, hii ilikuwa ni best design kwa dar es salaam ya mwaka 1988 na si hii ya 2015 - 2030, POpulationa ya watu na magari hukua kila kukicha,

lazima kuwe na standard itakayokwenda miaka 100 bila shida, na lazima kuwe na plan for the next solution ya baada ya miaka 100 mfano good road reserve, clearance for possible flyover roads and tunnel ili vijukuu vyetu navyo vikija visibomoe hii ila vijenge mpya bila ya interference ya day to day public activities....

Wakati mwingine design inaweza kuwa proper na inayokwenda na wakati, shida ni wale wanaosimama majukwaani kuomba kupendwa badala ya kuomba kuchaguliwa kutokana na uwezo wao vichwani wanawaburuza wataalamu, na kwakuwa wataalam nao hawana namna wanafanya kutokana na matakwa ya wajinga wachache, barabara inaweza kuwa inahitaji billion moja, wao wanakuja wanasema "tujengee ya nusu billion, nusu nyingine ikatuimarishe sisi...."
 
Jamani, kila mtu hapa mjini ameona jinsi barabara za mabasi yaendayo kasi zinavyojengwa kwa utaalamu mkubwa na kampuni ya ujenzi wa barabara STRABAG. Pamoja na kujenga miundo mbinu na vituo vya basi vya kisasa, wamechemsha vibaya katika ujenzi wa barabara zao.

Ukiangalia vizuri, njia zao zinaruhusu kupita basi moja tu kwani ni nyembamba sana. Yaani njia ya kwenda na kurudi linatakiwa kutembea gari moja, hakuna kupishana. Ishu ipo hapa; itakuaje iwapo basi moja limearibika njiani au limepata pancha, Je! Basi linalokuja nyuma yake litapita wapi wakati hivi vinjia vina kingo ndefu?

Na ukumbuke kuwa haya mabasi yatakua yakifuatana, sasa la mbele limeharibika njiani la nyuma litapita wapi?

Jamani, mwenzenu mpaka hapa sijapata majibu labda wataalam wa mambo ya barabara waje kutuelewesha.

Nikikupa kazi ya kunijengea nyumba na ramani nimekupa nikikukuta umebadilisha hata dirisha la chooni tu haki ya nani nakukata kichwa!

STRABAG wako sahihi maana wao kazi yao ni kutafsiri ramani na kuisimika ardhini, hawawezi kuingilia kazi ya mtu mwingine!! Kwani nani amekwambia hayo mabasi yatakuwa yanafukuzana? Kwa jinsi mradi ulivyo Wa kimataifa lazima kutakuwa na mfumo bora kabisa Wa mawasiliano, hivyo hatutegemei kukuta bus limekwama njiani na kufunga barabara!!
 
STRABAG ni contractor tu na anajenga kutokana na design ilivyo kwenye michoro. Hawezi kwenda kinyume na design. Wakulaumiwa ni consultant na TANROADS

Huo ndio ukweli wenyewe
 
Wakati mwingine design inaweza kuwa proper na inayokwenda na wakati, shida ni wale wanaosimama majukwaani kuomba kupendwa badala ya kuomba kuchaguliwa kutokana na uwezo wao vichwani wanawaburuza wataalamu, na kwakuwa wataalam nao hawana namna wanafanya kutokana na matakwa ya wajinga wachache, barabara inaweza kuwa inahitaji billion moja, wao wanakuja wanasema "tujengee ya nusu billion, nusu nyingine ikatuimarishe sisi...."

Mkuu kitu kikishajengwa maana yake ilianza design kwanza na wanaojenga hufuata hiyo design, ndio maana nikaita poor design... mengine nakubaliana kabisa na wewe, wanasiasa wanaleta hizi shida zote lengo ni kujenga familia na koo zao hakuna lingine, suluhu ya haya yote ni kwa watanzania kubadilika na huwa naamini mabadiliko haya tuyatakayo hayapatikani kwenye box la kura ila yatapatikana tu kwa nguvu ya pamoja ya watanzania wote kukataa kila lililo baya kwenye macho yao hata kama limefanywa na mjomba au shangazi...
 
Kinachozungumziwa ni dharula Kama ikitokea , barabara itajifunga!!!

Halafu nikwambie kitu gari hata liwe jipya huwezi kuli exempt na breakdowns , sema chances za kupata breakdown ndo zinapungua. jiulize kwanini gari mpya zinakuja na hooks , ya kuvuta ,nyingine ya kuvutwa ????
Ikiwa gari litaungua ni shida nyingine , maana huwezi kuvuta gari linaloungua , na litakua limefunga njia.
Umeshaandikiwa humu ndani tena vizuri tu kuwa kuna provisions za diversions and the like ili ku serve vitu kama hivyo. Tatizo tunang'ana tuwe na miundo mbinu inayoendana na mapungufu yetu kama "waswahili".
 
Mkuu kitu kikishajengwa maana yake ilianza design kwanza na wanaojenga hufuata hiyo design, ndio maana nikaita poor design... mengine nakubaliana kabisa na wewe, wanasiasa wanaleta hizi shida zote lengo ni kujenga familia na koo zao hakuna lingine, suluhu ya haya yote ni kwa watanzania kubadilika na huwa naamini mabadiliko haya tuyatakayo hayapatikani kwenye box la kura ila yatapatikana tu kwa nguvu ya pamoja ya watanzania wote kukataa kila lililo baya kwenye macho yao hata kama limefanywa na mjomba au shangazi...

Ofcourse, tabia ya kuingilia wataalamu inaingia mpaka kwenye designing maana huko nako designers wanalipwa gharama za utaalamu wao,
 
sawa great thinker...unajua sana kuliko strabag yenye miaka zaidi ya 100 Kazini
 
Back
Top Bottom