Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,170
- 829,114
Jumamosi mchana nillisikiliza radio Wapo fm inayomilikiwa na Mchungaji Gamanywa wa wa Wapo internatinal
Siku hiyo mchana wote manabii, mitume na wachungaji wanaomiliki makanisa na vituo binafsi vya maombi na maombezi walikuwa wamepanga Foleni redioni wakinadi misa zao za Siku iliyofuata yaani Jumapili.yaani ilikuwa bandika bandua mpaka Usiku
Maneno yao yalifanana woote, Yani ilikuwa ni kama copy n paste, kuwa ibada itakuwa na miujiza ambayo hujawahi kuiona popote, watakaohudhuria wataombewa watoe nuksi,wapate mali,vyeo utajiri nk nk, lakini mwishoni walitaja namba zao za mpesa na tigopesa kwa ajili ya kuchangia huduma
Nikajiuliza mbona Wapo fm inatumika namna hii, lakini nikajua ni biashara hivyo wanapokea matangazo wanalipwa basi life goes on
Jumapili asubuhi kwenye kipindi cha Patapata Mchungaji gamanywa naye akarushwa hewani akaaza kuwaonya wasikilizaji kuwa wawe makini na watu watoao matangazo ya kuvutia watu waende kwenye makanisa yao, akasema wengi ni waongo na hawaaminiki. Kumbuka naye Siku hiyo alikuwa na ibada kwenye kanisa lake hivyo akawa anavutia kwake huku akikandia wenzake
Hii si nzuri; jana yake kachukua pesa ya wenzake, kawarusha hewani wakajinadi, Siku inayofuata kawakejeli huku akijifagilia mwenyewe
Mungu huyu anaona mengi...!