Kwa hili la Mtwara, CCM imenifariji...!

Kwa hili la Mtwara, CCM imenifariji...!

Mkuu pole sana,
Hivi unajua msimu wa ununuzi wa korosho unaanzaga mwezi wa kumi na hadi sasa korosho hazijanunulia tafakari.

Hivi unajua Nape sio mwajiriwa wa serikali mwenye mamlaka ya kusema aliyoyasema ni waziri wa elimu ama higher authority.

Study nyingi na wataalamu wengi wameishauri serikali kuhusu usindikaji/ubanguaji korosho lakini kuna kundi dogo la vigogo ndio hawataki na wengine wanataka kuwa viongozi waandamizi wa nchi hii hiyo kauli ya kinana haitatekelezwa.
 
Suala la mafanikio ya ziara kama hii tunaweza kuyapima kwa kuyalinganisha na mafanikio ya kwanza ya Mheshimiwa Nape Nnauye katika ziara yake ya kuimarisha chama ambapo alitembelea mikoa ya Sumbawanga na kumaliza kabisa tatizo la Maji mkoani humo, pamoja na ardhi, na pia kukagua na kongeza nguvu ujenzi wa hospitali ya rufaa katika Mkoa wa Singida na sasa hospitali hiyo inakaribia kukabidhiwa kwani tayari imekamilika kwa ujenzi ambao ulikuwa unalegalega ama kusimama kabisa ila baada ya Mheshimiwa Nape kupita kukagua na kuwataka wakandarasi kuendelea na ujenzi kwa spidi mpya na hivyo kufanikisha mradi huo mkubwa wenye msaada mkubwa kwa wakazi wa Singida.

unatumika si bure
 
safi sana endelea kufarijika
1995 walisema Maisha bora kwa kila mtanzania tena wakasisiteza ajira kwa
vijana, vipi umepata? 7yrs ago!

Mnyika kaahidi mangapi aliyotekeleza?
 
NAFARIJIKA...!

Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.

Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maagizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni. Agizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.

Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!
Unajidanganya mwenyewe,mwanao atabaki shule na shuleni hakuna chaki hakuna madawati hakuna vifaa ila anashinda anacheza tu,nawe unafurahia kwa sababu mwanao hayupo nyumbani basi atakuwa anasoma.Mngemuuliza huko shule serikali imetoa kiasi gani cha fedha au ndo hvo hamna kitu,amka usirubunike kwa hzo mbwembwe
 
NAFARIJIKA...!

Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.

Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maagizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni. Agizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.

Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!

mkuu hzo ni mbwe mbwe tu za kutaka kura zetu 2015..ila waambie hatudanganyiki.
 
JK alitoa "maagizo"Kyela mwaka 2005 kuwa barabara ya Nkuyu-Ipinda-Matema ijengwe tena akisisitiza iwe ya kiwango cha rami;lkn hadi leo imebaki miaka 2 tu atoke madarakani HATUJAONA HATA TINGATINGA kusafisha ile ile barabara tuliyo izoea ya vumbi!

CCM kwa "maagizo"ni nambari one lkn utekelezaji ni ziro!
 
Suala la mafanikio ya ziara kama hii tunaweza kuyapima kwa kuyalinganisha na mafanikio ya kwanza ya Mheshimiwa Nape Nnauye katika ziara yake ya kuimarisha chama ambapo alitembelea mikoa ya Sumbawanga na kumaliza kabisa tatizo la Maji mkoani humo, pamoja na ardhi, na pia kukagua na kongeza nguvu ujenzi wa hospitali ya rufaa katika Mkoa wa Singida na sasa hospitali hiyo inakaribia kukabidhiwa kwani tayari imekamilika kwa ujenzi ambao ulikuwa unalegalega ama kusimama kabisa ila baada ya Mheshimiwa Nape kupita kukagua na kuwataka wakandarasi kuendelea na ujenzi kwa spidi mpya na hivyo kufanikisha mradi huo mkubwa wenye msaada mkubwa kwa wakazi wa Singida.

Nape=ni waziri wa maji??, Nape=waziri wa afya??, Nape=waziri wa viwanda?? Nape=waziri wa elimu??
That guy is a politician, more slogans than actions. Karagabaho
 
wala hajafanya kosa huenda viwanda vikafufuliwa kweli na kama vikifufuliwa kweli nyie mnaoponda mtasemaje?? Mtu akisema jema si vibaya kusema na akisema baya ni vibaya kusema, naungan mkono na Ray
 
NAFARIJIKA...!

Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.

Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maagizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni. Agizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.

Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!

Mkuu ungeeleza muktadha.

Wananchi wamehoji juu ya mambo yagusayo maslahi yao, wakapewa majibu ya kisiasa, wakazomea mawaziri, ndio ahadi/maagizo zikatoka.

Wananchi wa Mtwara si wajinga. Ahadi hizi zimekuwepo tangu uhuru (miaka 51) wamechoka kudanganywa. Kwa nini kuanzia leo wakati tangu uhuru chama hicho kiko madarakani na kina wabunge eneo hilo? Kinana na mleta mada mnadhani watu wamelala kiasi hicho?

Kumbuka "mpende akupendaye asiyekupenda achana naye"! Watu hawadanganyiki tena.

soma hapa:
MAWAZIRI watatu wa Rais Jakaya Kikwete juzi walizomewa baada ya kupanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya wa CCM taifa, ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana.

Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Mtwara ambako Kinana na mawaziri hao walikuwa katika ziara ya chama kujibu kero mbalimbali za wananchi.Mawaziri waliokumbwa na dhahama hiyo ni Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Tamisemi) Naibu wake, Aggrey Mwanri.

Chiza ndio alikuwa wa kwanza kukumbana na zomeazomea hiyo, lakini mambo yalikuwa magumu zaidi kwa Ghasia ambaye alizomewa tangu alipoanza kuzungumza mpaka alipomaliza.Ghasia ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Vijijini, alirushiwa makombora na Rukia Ismail Athumani ambaye alimshutumu yeye pamoja na Mbunge wa Mtwara mjini, Asnein Murji kwamba waliruhusu gesi kupelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa mkoa huo hawajafaidika nayo.

"Ghasia na Murji kwanini mnaudanganya umma kwa kupeleka gesi Dar es Salaam, sisi hatuna ubaya na chama ila hatutaki gesi iende huko" alisema Athumani huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.Kabla ya dada huyo kuteka hisia za wananchi kwa kuwasilisha kero hiyo, Kinana alimruhusu mwananchi mwingine, Issa Kambona ambaye pia alieleza kuwa hakubaliani na suala la gesi hiyo kupelekwa Dar es Salaam.

Kinana alisema amesikia hoja hizo za wananchi na kwamba atamueleza Waziri wa Nishati na Madini azungumze na wananchi wa Mtwara kuhusu gesi hiyo.Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu, Ghasia alilazimika kupanda jukwaani kujibu makombora aliyokuwa akirushiwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.

"Sio kweli kwamba hatutetei maslahi yenu, gesi iliyopo ni nyingi hamuwezi kuitumia na kuimaliza, kuna futi za ujazo trilioni 20,000 na tunaweza kuitumia kwa zaidi ya miaka 90, hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini imetoa ofa ya kuwalipia chuo vijana 150 kila mwaka," alisema Ghasia, lakini wananchi hao waliendelea kumzomea."Uongo, uongo, hatutaki, hatutaki, huyoo, huyooo" walisikika wakisema wananchi hao, hali iliyomfanya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kuingilia kati, kujaribu kuwatuliza.

"Kelele unazozisikia dada (Ghasia) zinaashiria kuna jambo, nafasi hizo 150 hawazipati, kama zinatolewa basi kwa upendeleo," alisema Nape huku akishangiliwa na wananchi hao.Baada ya hali kutulia kiasi, Ghasia alijaribu kuendelea kutoa ufafanuzi, lakini kitendo cha kuanza kuzungumza, wananchi hao walianza tena kuzomea.

"Kila mtu amelelewa katika mazingira tofauti, hilo halinihusu…watu wangu wa Mtwara vijijini wamenielewa," alisema Ghasia na kuteremka jukwaani hali iliyozidisha kelele za kumzomea.Nape alisawazisha mambo kwa kusema, hoja ya wananchi hao imechukuliwa na itawasilishwa kwa Serikali ili kuona namna ambavyo inaweza kukaa na wananchi hao na kuweka maslahi yao mbele.

Ilivyoanza

Pazia la zomea zomea lilifunguliwa na Chiza alipopanda jukwaani kujibu hoja ya kuyumba kwa soko la zao la korosho, ambapo wananchi walimpinga baadhi ya kauli alizozitoa."Tatizo la korosho ni baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na wengine ni watendaji wa Serikali …nipo hapa na wala siondoki, nitalishughulikia hili ili korosho zinunuliwe" alisema Chiza huku sauti za wananchi zikimpinga kwa kusema "uongooo".

Hata hivyo, Chiza aliweza kukabiliana na hali ya zomeazomea jukwaani baada ya watuliza wananchi kwa kusisitiza kuwa ataendelea kuwapo Mtwara, kushughulikia tatizo hilo ili ununuzi uendelee.Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwanri alipata wakati mgumu mara alipopanda jukwaani na kuanza kuzungumzia namna ya kumaliza kero ndogondogo zinazoletwa na mamlaka zake, wananchi walikuwa wanazoea "huyoo…hatutaki" lakini baada ya kuanza kuongea alionekana kuiteka hadhira na mambo yakawa shwari. "

"Tumesema wauza vitumbua, wasibughudhiwe … mkurugenzi njoo jukwani, nakuagiza kuanzia leo marufuku wanafunzi kurudishwa shuleni kwa sababu ya michango" alisema Mwanri huku akishangiliwa.Awali Kinana alisema mkutano huo unalenga kuzipatia ufumbuzi kero za wananchi ambazo zinawezakuwa kikwazo kwa chama hicho kuingia madarakani mwaka 2015.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala alisema umefika wakati wa chama kusimamia utendaji wa Serikali kutatua kero za wananchi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni pamoja na kuyumba kwa soko la korosho na gesi."Najua hapa kuna kero kubwa mbili, korosho na gesi, nimekuja na Mawaziri hapa watatoa majibu leo" alisema Kinana huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu ulioudhuria mkutano huo.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

MY TAKE: sUMBAWANGA JE????? aRUSHA WAKIFIKA ITAKUWAJE? mWANZA? sHINYANGA????

Kwanini hatukuambiwa hii mapema? Imetokea Mtwanra na kuandikwa na Mwananchi la leo.

Pamoja na kufanya siasa, tuwe wakweli.
 
Umeona na hili?

NAHUKO SUMBAWANGA MAMBO YALIKUWA HIVI.

Mjini Sumbawanga mambo yalikuwa magumu kwa viongozi wapya wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wao, Kinana, baada ya kukumbana na zomeazomea ya wananchi kwenye mkutano wake.

Kinana aliingia mjini humo jana kwa ndege akiongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Organizesheni Seif Khatib na Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwandri, na kisha kwenda eneo la Isesa kufanya mkutano. Kwa kuwa eneo hilo ni ngome kuu ya CHADEMA, viongozi hao walianza kuzomewa na hivyo wakati wakiondoka wafuasi wao waling'oa bendera na mlingoti kwenye shina la wapinzani wao na hivyo kuzidisha chuki.

Wakiwa katika mkutano wao wa ndani, uliibuka mzozo mkubwa baina ya viongozi na waendesha bodaboda waliokuwa wamekodishwa kubeba bendera kwa ujira wa kujaziwa mafuta na sh 10,000.
"Walitaka kuwageuka vijana wale ambao kimsngi wengi wao si wafuasi wao kwa kuwalipa sh 2,000 badala ya 10,000 lakini baadaye walilazimika kuwalipa kulingana na makubaliano," kilisema chanzo chetu.

Mchana wakiwa kwenye mkutano wa hadhara eneo la Liboli, Nape aliwaudhi baada ya kuanza kutoa matusi ya nguoni na hivyo akazomewa kwa nguvu kiasi cha kudai wanaozomea wana mimba. Hata Mwanri naye alipata wakati mgumu wakati akitoa ufafanuzi wake na hata Mkuu wa Mkoa, Stella Manyanya, alipoitwa na Kinana afafanue naye alizomewa hatua iliyomfanya Katibu huyo kutumia busara ya hali ya juu kuwatuliza wananchi na mkutano ukamalizika.
 
NAFARIJIKA...!

Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maigizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.

Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maigizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni.Igizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.

Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!

Magamba kwa maigizo tu hamjambo.
 
Napata picha kama ambavyo nabembeleza mtoto wangu, Nikimpa pipi au nikimwambia ntakupeleka Ulaya kukutembeza ananyamaza.

Hii ndio namna viongozi wa CCM wanavyotuona watanzania na ndio wanavyotutendea: "Danganya toto..."

Na tunadanganyika kweli.
 
Mkuu, waunge mkono juhudi zipi! Maneno matupu hayavunji mfupa. Hivi na wananchi waanze kusema tunaunga mkono na viowanda vya kubangua korosho vitaanzan kufanya kazi?
Mimi naamini ni Mwenyezi Mungu pekee ayeweza kusema na neno likawa.
Kumbuka viongozi ni kawaida yao kutoa kauli hizi.
 
Daaa yani nlikuwa naifungua kwa hamu kubwa daaaaa, poa lakini umetupata wasomaji wengi japo mada nei kabisa
 
We nimtu wa ajabu sana hivi unafarijika na ahadi?

Kweli wewe wa pekeee sana!

NAFARIJIKA...!

Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.

Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maagizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni. Agizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.

Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!
 
Kweli wewe ni zezeta, kila unachoambiwa au kuaidiwa na makada wa CCM wewe unaamini na kukubali tu.
Jifunze kutumia ubongo wako sawa sawa.
 
Inawezekana mtoa hoja si raia wa Tanzania, au kama ni raia basi unajifanya hamnazo. Kuna cha kufurahia hapo? Hilo la watoto wa shule kusimamishwa masomo kwa kutolipa mchango ndio umelisikia kwa mara ya kwanza kutoka mdomoni mwa wana CCM? Hilo la ahadi ya kuboresha viwanda ndio umelisikia leo? Angalia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010, je, viwanda walivyoahidi kuviboresha kwa mjibu wa Ilani hiyo viko wapi na ni vingapi? Kama watu wa Kanda ya Ziwa waliahidiwa hayo hayo kwa viwanda vyao vya pamba miaka 7 iliyopita na hakuna kiwanda hata kimoja kilichoboreshwa hadi sasa, hao wa Mtwara unawafariji kwa lipi? wewe unafarijika kwa lipi?. Mahaba yakizidi sana, unaweza kuambiwa kula kinyesi, ukala.
 
Mtoa mada ni jinga sana kazi kushabikia mafisadi tena huyu anachangia nchi kuwa katka hali ngumu
 
NAFARIJIKA...!

Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.

Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maagizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni. Agizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.

Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!

sasa kama Raisi mwenyewe kashindwa kusimamia Mkuu wa mkoa ataweza ?

Hajatoa maagizo bali ameto maigizo ?
Je mtu anapaswa kupongezwa kwa kutoa maagizo au kutekeleza tuu?

Yalitolewa maagizo kwa Nape kukamilisha mpango wa kuvua gamba yamefika wapi ?

Je watu wanataka maagizo au utekelezaji wa maagizo?
 
Back
Top Bottom