Mawaziri wazomewa mbele ya Kinana, Nape Mkutanoni...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,506
MAWAZIRI watatu wa Rais Jakaya Kikwete juzi walizomewa baada ya kupanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya wa CCM taifa, ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana.

Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Mtwara ambako Kinana na mawaziri hao walikuwa katika ziara ya chama kujibu kero mbalimbali za wananchi.Mawaziri waliokumbwa na dhahama hiyo ni Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Tamisemi) Naibu wake, Aggrey Mwanri.

Chiza ndio alikuwa wa kwanza kukumbana na zomeazomea hiyo, lakini mambo yalikuwa magumu zaidi kwa Ghasia ambaye alizomewa tangu alipoanza kuzungumza mpaka alipomaliza.Ghasia ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Vijijini, alirushiwa makombora na Rukia Ismail Athumani ambaye alimshutumu yeye pamoja na Mbunge wa Mtwara mjini, Asnein Murji kwamba waliruhusu gesi kupelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa mkoa huo hawajafaidika nayo.

"Ghasia na Murji kwanini mnaudanganya umma kwa kupeleka gesi Dar es Salaam, sisi hatuna ubaya na chama ila hatutaki gesi iende huko" alisema Athumani huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.Kabla ya dada huyo kuteka hisia za wananchi kwa kuwasilisha kero hiyo, Kinana alimruhusu mwananchi mwingine, Issa Kambona ambaye pia alieleza kuwa hakubaliani na suala la gesi hiyo kupelekwa Dar es Salaam.

Kinana alisema amesikia hoja hizo za wananchi na kwamba atamueleza Waziri wa Nishati na Madini azungumze na wananchi wa Mtwara kuhusu gesi hiyo.Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu, Ghasia alilazimika kupanda jukwaani kujibu makombora aliyokuwa akirushiwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.

"Sio kweli kwamba hatutetei maslahi yenu, gesi iliyopo ni nyingi hamuwezi kuitumia na kuimaliza, kuna futi za ujazo trilioni 20,000 na tunaweza kuitumia kwa zaidi ya miaka 90, hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini imetoa ofa ya kuwalipia chuo vijana 150 kila mwaka," alisema Ghasia, lakini wananchi hao waliendelea kumzomea."Uongo, uongo, hatutaki, hatutaki, huyoo, huyooo" walisikika wakisema wananchi hao, hali iliyomfanya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kuingilia kati, kujaribu kuwatuliza.

"Kelele unazozisikia dada (Ghasia) zinaashiria kuna jambo, nafasi hizo 150 hawazipati, kama zinatolewa basi kwa upendeleo," alisema Nape huku akishangiliwa na wananchi hao.Baada ya hali kutulia kiasi, Ghasia alijaribu kuendelea kutoa ufafanuzi, lakini kitendo cha kuanza kuzungumza, wananchi hao walianza tena kuzomea.

"Kila mtu amelelewa katika mazingira tofauti, hilo halinihusu…watu wangu wa Mtwara vijijini wamenielewa," alisema Ghasia na kuteremka jukwaani hali iliyozidisha kelele za kumzomea.Nape alisawazisha mambo kwa kusema, hoja ya wananchi hao imechukuliwa na itawasilishwa kwa Serikali ili kuona namna ambavyo inaweza kukaa na wananchi hao na kuweka maslahi yao mbele.

Ilivyoanza

Pazia la zomea zomea lilifunguliwa na Chiza alipopanda jukwaani kujibu hoja ya kuyumba kwa soko la zao la korosho, ambapo wananchi walimpinga baadhi ya kauli alizozitoa."Tatizo la korosho ni baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na wengine ni watendaji wa Serikali …nipo hapa na wala siondoki, nitalishughulikia hili ili korosho zinunuliwe" alisema Chiza huku sauti za wananchi zikimpinga kwa kusema "uongooo".

Hata hivyo, Chiza aliweza kukabiliana na hali ya zomeazomea jukwaani baada ya watuliza wananchi kwa kusisitiza kuwa ataendelea kuwapo Mtwara, kushughulikia tatizo hilo ili ununuzi uendelee.Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwanri alipata wakati mgumu mara alipopanda jukwaani na kuanza kuzungumzia namna ya kumaliza kero ndogondogo zinazoletwa na mamlaka zake, wananchi walikuwa wanazoea "huyoo…hatutaki" lakini baada ya kuanza kuongea alionekana kuiteka hadhira na mambo yakawa shwari. "

"Tumesema wauza vitumbua, wasibughudhiwe … mkurugenzi njoo jukwani, nakuagiza kuanzia leo marufuku wanafunzi kurudishwa shuleni kwa sababu ya michango" alisema Mwanri huku akishangiliwa.Awali Kinana alisema mkutano huo unalenga kuzipatia ufumbuzi kero za wananchi ambazo zinawezakuwa kikwazo kwa chama hicho kuingia madarakani mwaka 2015.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala alisema umefika wakati wa chama kusimamia utendaji wa Serikali kutatua kero za wananchi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni pamoja na kuyumba kwa soko la korosho na gesi."Najua hapa kuna kero kubwa mbili, korosho na gesi, nimekuja na Mawaziri hapa watatoa majibu leo" alisema Kinana huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu ulioudhuria mkutano huo.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

MY TAKE: sUMBAWANGA JE????? aRUSHA WAKIFIKA ITAKUWAJE? mWANZA? sHINYANGA????

Kwanini hatukuambiwa hii mapema? Imetokea Mtwanra na kuandikwa na Mwananchi la leo.
 
the meek will inherit the wotld. hayo ndiyo yanatotokea Mtwara sasa. wizara ya nishati haipaswi kudanganya uuma kuwa unatoa schoraship kwa vijana wa mtwara kusoma vyuoni bure. Pesa hizo zilipaswa kuimalisha miundo mbinu ya jiji la mtwara na ambazo ni nyingi mno kuliko hata hizo za kusomesha watoto bure. Shule ya msingi Mbawala haina mabati wala vyoo vya kisasa,. bara bara ya bandari ya mtwara mpaka mtwara airpotr siyo ya rami. Uwanja wa ndege wa mtwara ni wa kizamani kabisaa na ulijengwa na Keneth Kaunda ili kusafilisha shaba toka zambia mpaka mtwara. serikali hauja update uwanja huo tolea ujengwe.

Pesa za gesi lazima zitumike kuufanya mji wa mtwara na shule za msingi kuwa za kisasa jamani na sio kuwaonea namna hivyo.

Huo uwanja umezungukwa na nyumba zote za nyasi na ambazo zipo karibu karibu kutoka na operesheni vijiji mwaka 1970. Hivyo kama ndege ikiangukia nyumba hizo usiku, atakayepona ni yule aliyeko safarini tuu. serikali lazika iangalie sana hili kabla ya kuwadhulumu mali yao wana mtwara,
 
Yaliyowapata mawaziri mwaka 2007 kuzomewa na kupigwa mawe mikoani baada ya kumtimua Zitto Bungeni kwa sakata la Buzwagi sasa yanarudi tena
 
the meek will inherit the wotld. hayo ndiyo yanatotokea Mtwara sasa. wizara ya nishati haipaswi kudanganya uuma kuwa unatoa schoraship kwa vijana wa mtwara kusoma vyuoni bure. Pesa hizo zilipaswa kuimalisha miundo mbinu ya jiji la mtwara na ambazo ni nyingi mno kuliko hata hizo za kusomesha watoto bure. Shule ya msingi Mbawala haina mabati wala vyoo vya kisasa,. bara bara ya bandari ya mtwara mpaka mtwara airpotr siyo ya rami. Uwanja wa ndege wa mtwara ni wa kizamani kabisaa na ulijengwa na Keneth Kaunda ili kusafilisha shaba toka zambia mpaka mtwara. serikali hauja update uwanja huo tolea ujengwe.

Pesa za gesi lazima zitumike kuufanya mji wa mtwara na shule za msingi kuwa za kisasa jamani na sio kuwaonea namna hivyo.

Huo uwanja umezungukwa na nyumba zote za nyasi na ambazo zipo karibu karibu kutoka na operesheni vijiji mwaka 1970. Hivyo kama ndege ikiangukia nyumba hizo usiku, atakayepona ni yule aliyeko safarini tuu. serikali lazika iangalie sana hili kabla ya kuwadhulumu mali yao wana mtwara,

Ni wazi wananchi sasa wameamka, ile sera ya majimbo ya kwamba utajiri wa jimbo moja unufaishe wakazi wa jimbo husika nadhani inabidi uangaliwe na ufanyiwe kazi. sio kila cha upinzani ni kibaya.
 
Hizo ni rasharasha masika bado wa Tanzania wa sasa sio wale wa jana wakudanganywa kwa kofia na khanga.
Wananchi wamefungulia tu koki ya maji subiri wakigadhabika nakung'oa koki kabisa nani atazuia hiyo tsunami?.
Kikwete alisema eti watu wanadanganywa na wapinzani kwa kudai kuwa CCM imewatelekeza wananchi bila kuwatatulia kero zao as if watu hawana akili zakujua kipi kinachoendelea mpaka waambiwe na vyama vya vya upinzani.Nimeamini madaraka yanalewesha.
 
Tuombe Mungu waendelee kuwa hivi watanganyika wasibadilike ikifika 2014 kwa kofia na kanga na tisheti
 
Ni wazi wananchi sasa wameamka, ile sera ya majimbo ya kwamba utajiri wa jimbo moja unufaishe wakazi wa jimbo husika nadhani inabidi uangaliwe na ufanyiwe kazi. sio kila cha upinzani ni kibaya.

Sera ya Chadema ya Majimboism nadhani sio sera nzuri kwani majimbo hayana uwiano sawa kiuzalishaji na matokeo yake umaskini utazidi na kupanuka zaidi ktk majimbo yenye uzalishaji duni au yasiokuwa na rasilimali za kutosha!

Kwa mfano Mkoa Kilimanjaro unategemea sana zao la kahawa na ndizi kama mazao ya biashara na chakula! Bukoba nao ni hivyo hivyo! lakini bei ya mazao hayo kimataifa inashuka kila siku kwa sababu ya ushindani wa soko la dunia!

Sasa Mtwara, Tanga na mikoa ya Kusini ambao wanamatumaini ya kuzalisha gesi na Petroli wakiegemea upande wa Majimboism matokeo ni hali za maisha kuboreka! bila shaka gesi na petroli zina bei kubwa ktk masoko na bei yake huwa haiteremki ni kupanda tu kwa sababu mahitaji ni ya juu!

Jee, Chadema wakisisitiza sera hii hawaoni kuwa Wananchi wa mikoa ya Kaskazini na Magharibi wataanguka kiuchumi na kuwa maskini wa kutupwa kwa kupitwa na wenzao wa kusini?

Sera ya chama cha CUF ni sera ya haki sawa kwa wote! yaani tunu na utajiri ulioko TZ tugawane sawa sawa bila kujali inatoka jimbo gani au mkoa gani!

Wa TZ lazima tuwe macho sana kuhusu sera za vyama vya kisiasa kwani haitoshi kwa chama kusimama majukwaani kulaani ufisadi tu huku sera zake ni za kutugawa Wa TZ kimakabila na kimajimbo!!
 
Hujaielewa kabisa sera ya Chadema kuhusu majimbo. Kama Mtwara kuna gesi na gesi hiyo italeta neema, ni bora wakazi wa Mtwara wakafaidika na neema hiyo. Watanzania kutoka sehemu nyinginezo pia watafaidika kwa sababu jinsi uchumi wa Mtwara unavyopanukaa, mahitaji yataongezeka na nafasi za ajira kupatikana kwa yeyote iwe ametoka Tabora au Kigoma. Kwa mantiki hii ni kwamba jinsi maendeleo ya Mtwara yatakavyozidi kuongezeka ndivyo hivyo pia nafasi za ajira na sera za majimbo haijasema kuwa Mtwara iajiri wakazi wa Mtwara peke yake. Si hivyo. Sera ya majimbo haina ukabila hata kidogo.
 
Bila CCM kutoka madarakani watanzania mhesabu mmeliwa!! Mtaendelea tu kutongozwa kwa chumvi, kanga na vikofia vya kijani!! Hiyo ndiyo saizi yenu!!!
 
Kadogoo,

..kama alivyobainisha Jasusi, kaskazini kukidorora wananchi wa huko watakuwa na hiari ya kuhamia mikoa ya kusini.

..hata nchi zenye serikali za majimbo kama marekani wananchi wake wana hama kufuata yale majimbo yenye better opportunities.

..hata mimi napinga sera ya majimbo, lakini nadhani hoja zako dhidi ya sera hiyo zina mushkel kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Sera ya Chadema ya Majimboism nadhani sio sera nzuri kwani majimbo hayana uwiano sawa kiuzalishaji na matokeo yake umaskini utazidi na kupanuka zaidi ktk majimbo yenye uzalishaji duni au yasiokuwa na rasilimali za kutosha!

Kwa mfano Mkoa Kilimanjaro unategemea sana zao la kahawa na ndizi kama mazao ya biashara na chakula! Bukoba nao ni hivyo hivyo! lakini bei ya mazao hayo kimataifa inashuka kila siku kwa sababu ya ushindani wa soko la dunia!

Sasa Mtwara, Tanga na mikoa ya Kusini ambao wanamatumaini ya kuzalisha gesi na Petroli wakiegemea upande wa Majimboism matokeo ni hali za maisha kuboreka! bila shaka gesi na petroli zina bei kubwa ktk masoko na bei yake huwa haiteremki ni kupanda tu kwa sababu mahitaji ni ya juu!

Jee, Chadema wakisisitiza sera hii hawaoni kuwa Wananchi wa mikoa ya Kaskazini na Magharibi wataanguka kiuchumi na kuwa maskini wa kutupwa kwa kupitwa na wenzao wa kusini?

Sera ya chama cha CUF ni sera ya haki sawa kwa wote! yaani tunu na utajiri ulioko TZ tugawane sawa sawa bila kujali inatoka jimbo gani au mkoa gani!

Wa TZ lazima tuwe macho sana kuhusu sera za vyama vya kisiasa kwani haitoshi kwa chama kusimama majukwaani kulaani ufisadi tu huku sera zake ni za kutugawa Wa TZ kimakabila na kimajimbo!!

Haya mambo hayaendi kama unavyofikiri. Angalia nchi zote zenye sera ya majimbo halafu uone hilo tatizo linamalizwa vipi. Sera ya majimbo ndo suluhisho la matatizo ya wananchi kwa kuwa uchumi wote wa eneo hilo unabaki kuendesha shughuli za maendeleo. Kunakuwa na % flani ya pesa ambayo inalipwa serikali kuu kama ushuru na pia kunakuwa na % kadhaa ambayo italipwa katika mfuko maalumu (equalization fund) ambayo itatumika kufidia baadhi ya majimbo ambayo yatakuwa disadvantaged. Uzoefu unaonesha kuwa sera hii huchochea zaidi maendeleo na usimamizi wa rasilimali kuliko sasa ambapo pesa nyingi zinarundikana serikali kuu na matokeo yake zinatumika vibaya, zinachochea vitendo vya rushwa na pia haziruki kwa wananchi/wilaya husika kujenga uchumi wa eneo.

Kwahiyo kaka think outside the box.
 
Na hili la zomea zomea Chadema wanahusika?
Kimsingi CCM imelala uzingizi wa pono, pengine wanafikiri Watanzania wa sitini kweusi ni sawia na Watanzania wa karne ya 21. CCM itekeleze ilani yake vinginevyo santuri hii ya waongo, muongo, hatutaki itasikika mno kuelekea 2015.
 
Kwenye nyuzi kama hizi huwa napenda nione michango ya ndugu zangu zomba Ritz Rejao na chama , lakini siwaoni hebu njooni tujadili gesi ya mtwara na hatma ya wana mtwara
 
Last edited by a moderator:
Bila CCM kutoka madarakani watanzania mhesabu mmeliwa!! Mtaendelea tu kutongozwa kwa chumvi, kanga na vikofia vya kijani!! Hiyo ndiyo saizi yenu!!!

Mkuu, kwani wewe sio mtanzania!?
 
Walivyo mbulula basi watsema chadema ndicho kinatuna wanachama wake kuwazomea......na bado wasikanyage MBEYA,maana wataomba ardhi ipasuke na kinana wao...
 
Ni wazi wananchi sasa wameamka, ile sera ya majimbo ya kwamba utajiri wa jimbo moja unufaishe wakazi wa jimbo husika nadhani inabidi uangaliwe na ufanyiwe kazi. sio kila cha upinzani ni kibaya.

Hii sera ya majimbo ni kama sikio la kufa ,cdm wanajimaliza wenyewe kwa hii sera na inashangaza kwa nini hawaoni ukweli huu
 
Haya mambo hayaendi kama unavyofikiri. Angalia nchi zote zenye sera ya majimbo halafu uone hilo tatizo linamalizwa vipi. Sera ya majimbo ndo suluhisho la matatizo ya wananchi kwa kuwa uchumi wote wa eneo hilo unabaki kuendesha shughuli za maendeleo. Kunakuwa na % flani ya pesa ambayo inalipwa serikali kuu kama ushuru na pia kunakuwa na % kadhaa ambayo italipwa katika mfuko maalumu (equalization fund) ambayo itatumika kufidia baadhi ya majimbo ambayo yatakuwa disadvantaged. Uzoefu unaonesha kuwa sera hii huchochea zaidi maendeleo na usimamizi wa rasilimali kuliko sasa ambapo pesa nyingi zinarundikana serikali kuu na matokeo yake zinatumika vibaya, zinachochea vitendo vya rushwa na pia haziruki kwa wananchi/wilaya husika kujenga uchumi wa eneo.

Kwahiyo kaka think outside the box.

Itachukua miaka mia moja ili uweze kuwaelimisha wananchi kuhusu faida za sera ya majimbo,kimsingi cdm inajimaliza yenyewe kwa kueneza sera ambayo ni rahisi kueleweka kwa wananchi wachache wenye elimu nzuri ya kuelewa mambo,asilimia kubwa ya watanzania ni rahisi sana kuwaeleza kuwa serikali ya majimbo ni kwa ajili ya kugawa watanzania na ukweli ndio huo .Cdm endeleeni kulala usingizi wa pono kwa kueneza sera za kugawa watanzania
 
Kama hata Mtwara mmeanza kuzomewa, Magamba mtakimbilia wapi?

Huyu mwandishi atakuwa kakosema sababu Mtwara ipo kaskazini haiwezekani kabisa chama twawala kufanyiwa vile! BADO YAELEKEA PANA MENGI YAJA KABLA YA 2015
 
Back
Top Bottom