Kwa hili la Mtwara, CCM imenifariji...!

Kwa hili la Mtwara, CCM imenifariji...!

NAFARIJIKA...!


Nimepokea kwa furaha na amani tele ndani ya moyo na akili yangu maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Viwanda na Biashara juu ya kuendelea na kufufua upya viwanda vya korosho Mkoani Mtwara ambapo itasiaidia kupanua soko la zao hilo lakini pia kutoa ajira kwa vijana wa Mtwara.


Pia nimeridhika na kukiri kwa dhati kuwa sasa CCM imeamua kufanya kazi yake na wananchi wanapaswa kuunga mkona juhudi hizi, pale Katibu wa Itikadi na Uenezi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye alipotoa maagizo kuwa sasa hakuna tena mtoto kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama mchango wowote mashuleni. Agizo hili litaondoa usumbufu unaojitokeza na manyanyaso wanayoyapata watoto masikini mashuleni.


Kwa kasi, nguvu na ari hii wapinzani watasubiri sana...!
Hapo kwenye RED hivi kwa akili zako NAPE kwa cheo chake anauwezo wa kutoa maagizo yeyote katika shughuli za Serikali, unajidanganya ndugu yangu VUVUZELA huwa linatoa mlio tu lakini halina msaada mkubwa kwa unachotarajia ndo maana hata kwenye mechi ya mpira upulizwa tu hata kama timu imefungwa.
 
wewe ndio utasubiri sana kutoka kwenye huo usingizi mnono unao kufanya usijitambue.ukizaa watoto usitegemee mjomba akusomeshee watoto wako, umewahi kujiuliza kwanini watoto wao hawasomi shule hizi?? watoto wao wako huko ulaya ili wakirudi waendelee kukutawala wewe na kizazi chako milele. utabaki kushangilia na kupiga makofi kwa AHADI HEWA na mwisho wa yote watoto wako watakuwa na elimu isiyo toa ushindani kwao na watoto wao.ZINDUKA!!
 
Maagizo au maelekezo mengi hutolewa kwa mbwembwe na ukali. Utekelezaji ni kama hamna kitu! Tumeshuhudia viongozi wakiagiza kuwa wazee na akina mama wajawazito wahudumiwe bure katika hospitali zetu lakini utekelezaji hamna!i
 
Back
Top Bottom