Mawaziri wazomewa mbele ya Kinana, Nape Mkutanoni...

Mawaziri wazomewa mbele ya Kinana, Nape Mkutanoni...

Itachukua miaka mia moja ili uweze kuwaelimisha wananchi kuhusu faida za sera ya majimbo,kimsingi cdm inajimaliza yenyewe kwa kueneza sera ambayo ni rahisi kueleweka kwa wananchi wachache wenye elimu nzuri ya kuelewa mambo,asilimia kubwa ya watanzania ni rahisi sana kuwaeleza kuwa serikali ya majimbo ni kwa ajili ya kugawa watanzania na ukweli ndio huo .Cdm endeleeni kulala usingizi wa pono kwa kueneza sera za kugawa watanzania

Wewe ndo peke huielewi, mbona Mtwara wameielewa ndo maana yametokea yalojiri.
 
Itakuwa poa sana DHAIFU na Mzee wa kupindisha nao wakizomewa kwa utendaji wao finyu.
 
Kwanini hatukuambiwa hii mapema? Imetokea Mtwanra na kuandikwa na Mwananchi la leo.

Mawaziri wazomewa mbele ya Kinana Mtwara

MAWAZIRI watatu wa Rais Jakaya Kikwete juzi walizomewa baada ya kupanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya wa CCM taifa, ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana.


Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Mtwara ambako Kinana na mawaziri hao walikuwa katika ziara ya chama kujibu kero mbalimbali za wananchi.Mawaziri waliokumbwa na dhahama hiyo ni Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Tamisemi) Naibu wake, Aggrey Mwanri.

Chiza ndio alikuwa wa kwanza kukumbana na zomeazomea hiyo, lakini mambo yalikuwa magumu zaidi kwa Ghasia ambaye alizomewa tangu alipoanza kuzungumza mpaka alipomaliza.Ghasia ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Vijijini, alirushiwa makombora na Rukia Ismail Athumani ambaye alimshutumu yeye pamoja na Mbunge wa Mtwara mjini, Asnein Murji kwamba waliruhusu gesi kupelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa mkoa huo hawajafaidika nayo.

“Ghasia na Murji kwanini mnaudanganya umma kwa kupeleka gesi Dar es Salaam, sisi hatuna ubaya na chama ila hatutaki gesi iende huko” alisema Athumani huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.Kabla ya dada huyo kuteka hisia za wananchi kwa kuwasilisha kero hiyo, Kinana alimruhusu mwananchi mwingine, Issa Kambona ambaye pia alieleza kuwa hakubaliani na suala la gesi hiyo kupelekwa Dar es Salaam.

Kinana alisema amesikia hoja hizo za wananchi na kwamba atamueleza Waziri wa Nishati na Madini azungumze na wananchi wa Mtwara kuhusu gesi hiyo.Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu, Ghasia alilazimika kupanda jukwaani kujibu makombora aliyokuwa akirushiwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.

“Sio kweli kwamba hatutetei maslahi yenu, gesi iliyopo ni nyingi hamuwezi kuitumia na kuimaliza, kuna futi za ujazo trilioni 20,000 na tunaweza kuitumia kwa zaidi ya miaka 90, hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini imetoa ofa ya kuwalipia chuo vijana 150 kila mwaka,” alisema Ghasia, lakini wananchi hao waliendelea kumzomea.“Uongo, uongo, hatutaki, hatutaki, huyoo, huyooo” walisikika wakisema wananchi hao, hali iliyomfanya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kuingilia kati, kujaribu kuwatuliza.

“Kelele unazozisikia dada (Ghasia) zinaashiria kuna jambo, nafasi hizo 150 hawazipati, kama zinatolewa basi kwa upendeleo,” alisema Nape huku akishangiliwa na wananchi hao.Baada ya hali kutulia kiasi, Ghasia alijaribu kuendelea kutoa ufafanuzi, lakini kitendo cha kuanza kuzungumza, wananchi hao walianza tena kuzomea.

“Kila mtu amelelewa katika mazingira tofauti, hilo halinihusu…watu wangu wa Mtwara vijijini wamenielewa,” alisema Ghasia na kuteremka jukwaani hali iliyozidisha kelele za kumzomea.Nape alisawazisha mambo kwa kusema, hoja ya wananchi hao imechukuliwa na itawasilishwa kwa Serikali ili kuona namna ambavyo inaweza kukaa na wananchi hao na kuweka maslahi yao mbele.

Ilivyoanza

Panzia la zomea zomea lilifunguliwa na Chiza alipopanda jukwaani kujibu hoja ya kuyumba kwa soko la zao la korosho, ambapo wananchi walimpinga baadhi ya kauli alizozitoa.“Tatizo la korosho ni baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na wengine ni watendaji wa Serikali …nipo hapa na wala siondoki, nitalishughulikia hili ili korosho zinunuliwe” alisema Chiza huku sauti za wananchi zikimpinga kwa kusema “uongooo”.

Hata hivyo, Chiza aliweza kukabiliana na hali ya zomeazomea jukwaani baada ya watuliza wananchi kwa kusisitiza kuwa ataendelea kuwapo Mtwara, kushughulikia tatizo hilo ili ununuzi uendelee.Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwanri alipata wakati mgumu mara alipopanda jukwaani na kuanza kuzungumzia namna ya kumaliza kero ndogondogo zinazoletwa na mamlaka zake, wananchi walikuwa wanazoea “huyoo…hatutaki” lakini baada ya kuanza kuongea alionekana kuiteka hadhira na mambo yakawa shwari. “

“Tumesema wauza vitumbua, wasibughudhiwe … mkurugenzi njoo jukwani, nakuagiza kuanzia leo marufuku wanafunzi kurudishwa shuleni kwa sababu ya michango” alisema Mwanri huku akishangiliwa.Awali Kinana alisema mkutano huo unalenga kuzipatia ufumbuzi kero za wananchi ambazo zinawezakuwa kikwazo kwa chama hicho kuingia madarakani mwaka 2015.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala alisema umefika wakati wa chama kusimamia utendaji wa Serikali kutatua kero za wananchi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni pamoja na kuyumba kwa soko la korosho na gesi.“Najua hapa kuna kero kubwa mbili, korosho na gesi, nimekuja na Mawaziri hapa watatoa majibu leo” alisema Kinana huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu ulioudhuria mkutano huo.



MY TAKE: sUMBAWANGA JE????? aRUSHA WAKIFIKA ITAKUWAJE? mWANZA? sHINYANGA????

Kuzomewa waziri wa serikali ya CCM ni sawa na kuzomewa CCM nzima, hapo Kinana na Nape wamezomewa pia!!
 
Huyu Ghasia ni arrogant sana. Hii kauli ya malezi kuwa kila mtu amelelewa katika mazingira tofauti nimeisikia mara ya pili sasa toka kwake. Anaamini kuwa yeye alipewa malezi bora kabisa na wazazi wake.

Kuna wakati Wenje alihoji ufujaji wa pesa ya walipa kodi pale kwa mfano bajeti ya TAMISEMI inaposomwa, na wakuu wa mikoa yote na ma RAS wakaenda huko Dodoma kushuhudia kupitishwa kwa bajeti ya wizara yao. Hakuna umuhimu wa wao kwenda huko, na ni utumiaji mbaya wa rasilimali zetu, lakini Ghasia alimshambulia Wenje kuwa hakulelewa vyema ndiyo maana anatoa maneno kama yale. Sijui alipewa uwaziri kwa vigezo vipi huyu Ghasia.
 
Na hili la zomea zomea Chadema wanahusika?
Kimsingi CCM imelala uzingizi wa pono, pengine wanafikiri Watanzania wa sitini kweusi ni sawia na Watanzania wa karne ya 21. CCM itekeleze ilani yake vinginevyo santuri hii ya waongo, muongo, hatutaki itasikika mno kuelekea 2015.

KAMA CCM HAWAJIFUNZ YATAWAKUTA KM YA KANU AU KAUNDA WA ZAMBIA, IVI HII C NI MIKUTANO YA NDANI? NI AJABU WANAZOMEWA NA MASWAIBA WENZAO IVI WAKITUALIKA NA SIE TSOTAKA ATA KUWASIKIA JAMANI Si TUTAWAPIGA NA KUPEWA MURDER KESI, KWELI 2015 LZM WATUKABIDHI UFUNGUO WA IKULU
 
Kinachoshangaza ni nini kuhusu sera ya majimbo? Mtwara wenyewe wameshaelewa umuhimu wake na nwasihi waendelee kudai rasilimali yao iwanufaishe wao kwanza.

Mkoa huu uko nyuma kwa kila kitu elimu, afya, miundo mbinu na makazi. Gesi isipowanufaisha wao sasa ndio byebye.

Mtwara mjini kwenyewe maji shida sana hela ya kuuza gesi hii ingetatua matatizi mengi sana mtwara.
Sera ya majimbo ni woga tu kwa CCM lakini matokeo yake ni mazuri.

Ufunguo
kaeleza vizuri kabisa.
 
Sera ya Chadema ya Majimboism nadhani sio sera nzuri kwani majimbo hayana uwiano sawa kiuzalishaji na matokeo yake umaskini utazidi na kupanuka zaidi ktk majimbo yenye uzalishaji duni au yasiokuwa na rasilimali za kutosha!

Kwa mfano Mkoa Kilimanjaro unategemea sana zao la kahawa na ndizi kama mazao ya biashara na chakula! Bukoba nao ni hivyo hivyo! lakini bei ya mazao hayo kimataifa inashuka kila siku kwa sababu ya ushindani wa soko la dunia!

Sasa Mtwara, Tanga na mikoa ya Kusini ambao wanamatumaini ya kuzalisha gesi na Petroli wakiegemea upande wa Majimboism matokeo ni hali za maisha kuboreka! bila shaka gesi na petroli zina bei kubwa ktk masoko na bei yake huwa haiteremki ni kupanda tu kwa sababu mahitaji ni ya juu!

Jee, Chadema wakisisitiza sera hii hawaoni kuwa Wananchi wa mikoa ya Kaskazini na Magharibi wataanguka kiuchumi na kuwa maskini wa kutupwa kwa kupitwa na wenzao wa kusini?

Sera ya chama cha CUF ni sera ya haki sawa kwa wote! yaani tunu na utajiri ulioko TZ tugawane sawa sawa bila kujali inatoka jimbo gani au mkoa gani!

Wa TZ lazima tuwe macho sana kuhusu sera za vyama vya kisiasa kwani haitoshi kwa chama kusimama majukwaani kulaani ufisadi tu huku sera zake ni za kutugawa Wa TZ kimakabila na kimajimbo!!

je umasikini wa watu wa kusini kabla ya kugunduliwa gesi kiasi ilikuwa ni kama adhabu kupata uhamisho kwenda Mtwara ilikuwa ni haki sawa kwa wote?
tofauti ya kimaendeleo ya kiuchumi kati ya mikoa ya kaskazini na kusini iliyopo leo hii hiyo ni haki sawa pia? Au kwa kuwa umeishazowea kuwaona wamakonde wakiwa nyuma kimaendeleo sasa unaogopa kuwa wanaweza wakaipita hata hiyo ya kaskazini?
Hata marekani kuna majimbo tajiri na masikini na haijawakwaza nadhani hii sentiment inasababishwa na ubinafsi na roho mbaya.
Na sitetei labda natoka huko.la asili yangu Tabora ambako hadi leo miaka 50 ya uhuru hatujaunganishwa na barabara ya lami,usafiri wa kutegemewa reli is moving from bad to worse baada ya akina Kikwete kuwapa TRC matapeli wenzao wa kihindi.
Cha maana walichoifanyia Tabora ni kutujengea sanamu ya Nyerere,and yet Tabora inaongoza kuwapa kura magamba,nina hasira na hawa wanyamwezi wenzangu we acha tu sijui nani kawaroga
 
CCM ikiendelea na mtindo huu wa kuwapeleka mawaziri kujibu kero za wananchi wananchi watapata matumaini mapya.

Zomezomea hiyo ni kwamba Mawaziri hawakutani ni wananchi kuwapa taarifa na kusikiliza kero zao hadi pale Kinana au Nape wawaongoze kwenda kwa wananchi..... Mawaziri wanamwangusha Rais wameacha Chadema ikizunguka bila kujibu hoja.
 
hii habari imekolezwa na chumvi kidogo.kawaida wananchi hupenda kutoa dukuduku zao kwa viongozi wanapowatembelea kutaka kujua kero zao na namna ya uwasilishaji wa kero huwa kwa hisia lakini si kwa kuzomea, watanzania ni wastaarabu sana hiyo tabia ya kuzomea haipo hata kama hawakubaliani na kiongozi husika
 
CCM ikiendelea na mtindo huu wa kuwapeleka mawaziri kujibu kero za wananchi wananchi watapata matumaini mapya.

Zomezomea hiyo ni kwamba Mawaziri hawakutani ni wananchi kuwapa taarifa na kusikiliza kero zao hadi pale Kinana au Nape wawaongoze kwenda kwa wananchi..... Mawaziri wanamwangusha Rais wameacha Chadema ikizunguka bila kujibu hoja.

MAGAMBA TEAM et al AT WORK, HAWANA JIPYA, STRATEGY YAO C WANATUMIA POLICCM KUWADHIBITI CHADEMA
 
Kwenye nyuzi kama hizi huwa napenda nione michango ya ndugu zangu zomba Ritz Rejao na chama , lakini siwaoni hebu njooni tujadili gesi ya mtwara na hatma ya wana mtwara

Habari yenyewe haina tija kama walimzomea Hawa Ghasia na wakamshangilia Nape sasa hapo pana habari? Wao hawakubaliani na gesi kupelekwa Dar na sio kama hawaitaki CCM; hilo ni suala dogo la kueleweshana kitu ambacho katibu mkuu na Nape watalifanyia kazi>

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hata mimi ngoja nizomee, hayoooo, hayana itikadi wala dira, yamejaa uongo tu.
 
NAHUKO SUMBAWANGA MAMBO YALIKUWA HIVI.

Mjini Sumbawanga mambo yalikuwa magumu
kwa viongozi wapya wa CCM wakiongozwa na
Katibu Mkuu wao, Kinana, baada ya kukumbana
na zomeazomea ya wananchi kwenye mkutano
wake.
Kinana aliingia mjini humo jana kwa ndege
akiongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi,
Nape Nnauye, Katibu wa Organizesheni Seif
Khatib na Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey
Mwandri, na kisha kwenda eneo la Isesa
kufanya mkutano.
Kwa kuwa eneo hilo ni ngome kuu ya
CHADEMA, viongozi hao walianza kuzomewa na
hivyo wakati wakiondoka wafuasi wao waling’oa
bendera na mlingoti kwenye shina la wapinzani
wao na hivyo kuzidisha chuki.
Wakiwa katika mkutano wao wa ndani, uliibuka
mzozo mkubwa baina ya viongozi na
waendesha bodaboda waliokuwa
wamekodishwa kubeba bendera kwa ujira wa
kujaziwa mafuta na sh 10,000.
“Walitaka kuwageuka vijana wale ambao
kimsngi wengi wao si wafuasi wao kwa kuwalipa
sh 2,000 badala ya 10,000 lakini baadaye
walilazimika kuwalipa kulingana na
makubaliano,” kilisema chanzo chetu.
Mchana wakiwa kwenye mkutano wa hadhara
eneo la Liboli, Nape aliwaudhi baada ya kuanza
kutoa matusi ya nguoni na hivyo akazomewa
kwa nguvu kiasi cha kudai wanaozomea wana
mimba.
Hata Mwanri naye alipata wakati mgumu wakati
akitoa ufafanuzi wake na hata Mkuu wa Mkoa,
Stella Manyanya, alipoitwa na Kinana afafanue
naye alizomewa hatua iliyomfanya Katibu huyo
kutumia busara ya hali ya juu kuwatuliza
wananchi na mkutano ukamalizika.
 
Back
Top Bottom