Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,096
- 5,592
Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaenda kutimiza miaka 48 tangu kuanzishwa kwake vijana wameshauriwa kutumia kwa faida mitandao ya kijamii ili iwanufaishe kwenye shughuli zao na shughuli za kichama.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kusherehekea miaka 48 ya chama hicho iliyoambatana na kufanya usafi kwenye ofisi ya CCM kata ya Shangani, Katibu wa CCM Wilaya ya Mtwara Mjini mkoani Mtwara, Fadhil Mrami amesema mara kadhaa wanawaomba vijana kutumia mitandao kwa maslahi yao binafsi na chama chao kwani mambo mengi yanafanyika kidijiti.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM kata ya Shangani Awazi Silim ametoa rai kwa vijana kutotumika kisiasa na badala yake waungane na kushikamana ili chama chao kizidi kuwa imara na kizidi kuchukua dola.
Mariamu Mohamed, ambaye ni mjumbe amekipongeza chama kwa kutimiza miaka 48 na amewaomba wazee wa chama kuwa karibu na vijana kwaajili ya kuwaelimisha ili vijana hao waendelee kudumisha na kukipa uhai chama chao kwakuwa vijana wengi hawajui wapi chama hicho kimetokea.
Source: Jambo TV