kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,871
Bodi ya mkopo wa elimu ya juu wana mpango wa kupeleka sheria bungeni itakayotaka kila mnufaika wa mkopo kuanzia 1994 hadi sasa kukatwa 15% ya mshahara wake kulipia mkopo wake.
Lengo lao la kukata 15% ni kuharakisha malipo hayo ili na wengine wanufaike. Sipingi watu kukatwa ila napinga hii 15%, hii ni pesa nyingi sana na vijana tutajikuta tunakata tamaa ya kufanya kazi maana mwisho wa mwezi vijana watakuwa na hali mbaya.
Bodi wajue kuwa hawa wanufaika wanakatwa kodi PAYE, wanakatwa Bima ya Afya, wanakatwa na mifuko ya mafao mfano NSSF, wanakula maeneo ya kazi, wana familia zinawategemea, wamepanga nyumba, wanalipa maji na umeme. Jumla ya makato halali tu yanakaribia kufika 35% kwa sasa, kama HESLB watakata 15% huenda jumla ya makato yakafika 50% ya mshahara wa hawa wadaiwa.
Naomba kwa hili wabunge watuonee huruma bila kujali vyama vyao au kama nao wanadaiwa au lah. Walau iwe hata 10% ili jumla ya makato yawe chini kidogo, wajue pamoja na kukopwa bado sisi wachache tuliobahatika kupata ajira ni walipaji wa kodi waaminifu. Nashauri bunge liwape HESLB mbinu nyingine ya kuongeza mapato kama kusaka wadaiwa wengine na si kuwanyonga hawa vijana ambao tayari wameshajitokeza.
USHAURI wangu ni kwamba kwa wale ambao tulikopeshwa na hatujaanza kulipa tujipeleke wenyewe tuanze kulipa ili walipaji wawe wengi huenda ikazuia haya makato makubwa yanayopendekezwa.