GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,725
- 109,157
Mtazamo Chanya...
1. Bandari itaboreshwa
2. Ufanisi Kuongezeka
3. Biashara Kuimarika
4. Maslahi juu kwa Wafanyakazi
5. Huduma yao itavutia nchi nyingi Jirani
6. Mapato Kuongezeka
7. Urasimu Kupungua
Mtazamo Hasi
1. Mkataba kutokuwa na Ukomo ni Hatari kwa wenye Bandari
2. Vipengele vinachojichanganya Kimaelezo vinaleta Wasiwasi
3. Kwanini hakukuwa na Mchakato mrefu unaohusisha hata Wananchi ili Kuuelewa?
4. Msemaji wa Serikali badala ya Kuelezea Kiundani muda mwingi anautumia Kufoka. Kukosoa na kutuonyesha Watanzania kuwa hana Akili
5. Tunatulizwa kuwa DP World wako hadi Uingereza ila hatuambiwi kwanini katika Mataifa mengine Wameshindwa
6. Wanasiasa kuingilia Kutetea Mpango huu kunaongeza Shaka kuwa huenda tatizo halipo tu katika Mkataba na DP World bali hata Akili za Wanasiasa Wetu ( hasa Wabunge wa CCM ) nazo zina tatizo
7. Spika wa Bunge kutumia muda mwingi Kuvitishia Vyombo vya Habari vya Tanzania juu ya Kuandika kuhusu huu Mkataba wa DP World na Bandari yetu kunaonyesha kuwa huenda Mihimili Mikubwa miwili imeshalainishwa Kifedha na Waarabu ili Kuuza Rasilimali za Watanzania na Watanzania wenyewe
Nini Kifanyike?
1. Mchakato juu ya huu Mkataba uanze upya na uhusishe Watanzania Wote
2. Lugha ya huu Mkataba iwe ya Kiswahili ili hata tusiojua Kiingereza akina GENTAMYCINE tuuelewe
3. Watanzania tuwe Wavumilivu juu ya Ufadanuzi utakaolewa
4. Wanasiasa na Wabunge wasiwe Wasemaji Wakuu wa hili bali Wataalam wasio na upande ndiyo Wasikilizwe
5. Rais, Waziri na Msemaji wa Serikali wasione Aibu kuwaomba Radhi Watanzania juu ya hii Sintofahamu inayoelekea kuzaa Chuki na Hasira kwa Wadau na Wananchi
6. Tubakie na Utanzania Wetu na kamwe tusianze Kubaguana Kimakabila na Kijiografia kwani Sisi sote ni Watanzania
7. Wale Wanaotetea huu Mkataba wa DP World wasionekane ni Maadui kwani nao wana Hoja mahala lakini pia na wale ambao Wanaukosoa huu Mkataba wasipuuzwe, wasidharauliwe bali Hoja zao nazo zipimwe kisha kwa upamoja Wao kupatikane muafaka thabiti ya huu Uwekezaji wa hawa DP World kama Wawekeze au Wasiwekeze.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ubariki Mtandao huu wa JamiiForums
Mungu Mbariki mno GENTAMYCINE
AMINA.