Kwa hili, Dr. Slaa wewe ni 'Mdini' pia!

Kwa hili, Dr. Slaa wewe ni 'Mdini' pia!

Status
Not open for further replies.
Dr Slaa kaona mbali, dalili zipo wazi kuwa mwaka 2014 na 2015 chama chake kitaambulia kura chache ambazo zitapunguza ruzuku ambayo ni chanzo chake pekee cha ulaji hivi sasa, hivyo ameona njia muafaka ya kisiasa kwake ili aepuke kushindwa ni KUANZISHA maneno ya uchochezi. Watanzania wenye akili timamu na uzalendo kwa nchi yetu, tumeshtuka hatuamini tena kauli za kizushi;
1. Mchakato wa Katiba umeingiliwa na CCM
2. JK ni Mdini
3. TISS wanafuatilia nyendo za Dr. Slaa
 
K:angry:
hahaha hujui maana ya udini?angalia hapa chini.

Siraa:>''baba askofu salama,vipi baba askofu uchaguzi ndo huu umefika mnanisaidiaje wadau'.
Baba askofu-''relax ,tumeshaamua huyu jamaa awe a one term presdent,tutahakikisha anaanguka kwa kuhakikisha waumini wetu hawampi kura..hivi sasa tumepanga kila siku kutoa waraka wa kuikandamiza serikali yake ili waumini wetu waone hafai tena kupewa kura.kwahiyo tukifanikiwa utatusaidia vipi?.
Sraa>aaah,usiwe na wasiwasi baba askofu,kwanza nitaongeza maradufu fungu la MOU,nitahakikisha madaraka yote ya juu nawapa watu wetu,viherehere kama zito nitampangia kazi akae balozi pale bujumbura,suala la kuchinja nitaruhusu waumini wetu kuchinja,na hao jamaa wakileta zao watakumbana na dola,mihadhara ya waislamu marufuku,mtakacho sema mimi ntawafanyia.'
Baba askofu,>''basi consider it done.huyu hapati kura za waumini wetu hata moja,wewe utaona'.

Huo ndo unaitwa udini mkuu.
 
Magamba mtajaribu kufurukuta saaaaana, lakini ukweli ni kwamba ukishazeeka kinachofuata ni kifo hata kama ufanye nini. CCM imeshazeeka na hivyo kinachofuata ni kifo chake. Endeleeni kutapatapa lakini hampo mbali na kaburi. Aliye kufani hata hama atibiwa na madaktari bingwa ni lazima tu atakufa. Buriani CCM.
 
"AHADI YA MAHAKAMA YA KADHI kwenye ilani ya 2005 HAIKUWA YANGU"by PRESDENT KIKWE.
"kwa sababu mgombea huwa hashirikishwi kuandaa ilani,chama ndio kinaandaa ilani"by PRESDENT KIKWETE.
maneno haya aliyaongea raisi KIKWETE kama sikosei 2009,ktk kipindi kilichorushwa live na TBC KIKIENDESHWA NA TIDO MHANDO WAKATI ULE,wananchi walipata nafasi ya kupiga simu na kutuma meseji ili raisi awajibu.
kimsingi majibu ya kikwete yanadhibitisha MOJA KWA MOJA ukweli kuwa mwanzilishi hasa wa udini kupitia ahadi ya MAHAKAMA YA KADHI NI CHAMA CHA MAPINDUZI.
kuahidi na kutaka kutekeleza ahadi hii ya CCM kulileta MJADALA mkubwa,MGAWANYIKO mkubwa,na CHUKI kubwa baina ya UISLAM NA UKRISTO KUTOKA KWA WAISLAMU NA WAKRISTO(PIA SERIKALI NA CCM ZILICHUKIWA NA WAKRISTO KWA KUTAKA KUTEKELEZA AHADI)
KIMSINGI HAKI ZA WAISLAM NA WAKRISTO HAZITAKIWI KWANZA KUWA AJENDA NA AHADI KWENYE KAMPENI KUTOKA VYAMA VYA SIASA.
waislam na wakristo wafanye mambo yao wenyewe kwa gharama zao.IPO SIKU MTADAI KUJENGEWA MISKITI NA MAKANISA KWA PESA YA SERIKALI.
 
Dr Slaa kaona mbali, dalili zipo wazi kuwa mwaka 2014 na 2015 chama chake kitaambulia kura chache ambazo zitapunguza ruzuku ambayo ni chanzo chake pekee cha ulaji hivi sasa, hivyo ameona njia muafaka ya kisiasa kwake ili aepuke kushindwa ni KUANZISHA maneno ya uchochezi. Watanzania wenye akili timamu na uzalendo kwa nchi yetu, tumeshtuka hatuamini tena kauli za kizushi;
1. Mchakato wa Katiba umeingiliwa na CCM
2. JK ni Mdini
3. TISS wanafuatilia nyendo za Dr. Slaa

hiyo 2014-2015 jitahidini tu kwa sababu tangu 2010 katika chaguzi chadema inaongeza kura kwa kasi ya ajabu anasema ukweli CCm wamevamia mchakato wa katiba,JK ni mdini kikweli anafadhali vikundi vya kiislamu kuzunguka nchi nzima,TISS wanafuatiliaa nyendo za DR Slaa
 
Kwanza hakuna ubishi kwamba Dk Slaa ni mdini kama alivyo mtu mwingine kwa sababu amewahi kutumikia dini kwa ahadi kabla hajaamua kusaliti na kurudi uraiani nadhani kwa lengo la kuwatumikisha.

Pili, hakuna ubishi kwamba gazeti la Tanzania daima ni kampeni meneja wa CHADEMA na tatu hakuma ubishi kwamba kuna wimbi kubwa la masuala ya udini.

Ushauri wangu:
Kama kweli hawa viongozi wanataka kututawala na kuongoza nchi hii waache huu ujinga wa kupandikiza udini miongoni mwa watanzania.

Kama kawaida yako, ukiwa CCM ni lazima ushabikie UDINI kwa kuwa hoja zimewaishia
 
Ukweli ni kuwa mwaka 2010 baada ya chadema kumsimamisha aliyekuwa padre slaa, ccm ilihofia kushindwa uchaguzi kwa makandokando waliyofanya kama Epa,RICHMOND, NA hata ufisadi mwingine! Ccm ikaamua kuwatumia waislamu kama ngazi ya kupandia, kwa kuwaambia kwamba dr slaa ni mgombea wa kanisa katoliki, hivyo waislamu wampigie kikwete kura kwa sababu ni mwenzao! Kazi hiyo ilifanyika misikitini, ndo maana baadhi ya waumini wa kiislamu humchukia dr. Slaa bila sababu za msingi, tatizo ni sumu zilizomwagwa misikitini kwa mtazamo hasi kwa dr. Slaa na chadema! Mtakumbuka kauli ya Mufti wetu, kwamba waislamu wasishiriki maandamano ya chadema, na uchaguzi wa igunga. Kikwete hawezi kukwepa juu ya hili analijua vizuri. Mara zote nasisitiza Dini ya Mwenyezi mungu( Allah) hakuna mwenye uwezo wa kuiondoa duniani, waislamu wasidanganywe na maccm yanayotaka kuwatumia kwa mambo ya kisiasa ili kupambana na vyama vya upinzani!
 
Hiki kibabu kinazeeka vibaya,,anadhani na phd yake ya kuhesabu rozali kanisani ndio ataweza kuongoza watanzania????aendee akalee mjukuu wake aliyezaa na mke wa mtu asituvurugie amani yetu
 
Mleta thread ni mdini, tena mwislamu aliyeipigia kura ccm mwaka 2010 kwa sababu tu wagombea wa nafasi za juu wote ni waislamu, huu ni upofu wa akili. Ikiwa Dr. Slaa ni mdini kwanini msimpeleke mahakamani? Serikali makini na safi ingeshawapeleka mahakamani wanaoeneza siasa za udini lakini ccm chini ya Kikwete imeshindwa kwa sababu na wenyewe wanahusika, rejea ilani ya uchaguzi ya ccm 2005.
 
Kwa hili Dr.Slaa amechemsha, Dr. Slaa anaeneza chuki kama Nape, Mwigulu na Ndugai.
 
Kwa kweli yote haya ninamlaumu jk kwa kuwa mkimya sana kwa sababu hawezi kuchukua hatua watu kama hawa.

Alichotakiwa ni kuwakamata watu kama hawa na kuwaweka ndani kwa muda usiojulikana
 
Dr. Slaa ni zao la kanisa, mfuasi wa kanisa, yupo daima kuhakikisha maslahi ya kanisa katoliki yanafikiwa kwa gharama yeyote, Ameapa kutetea maslahi na ukuaji wa kanisa katoliki HIVYO kamwe hawawangusha wakatoliki; Siasa kupitia Chadema ni daraja la ustawi wa kanisa Tanzania. Ikibidi anawatumia waislam; Zito na Arfi kwa nia ya kupata kura za waislam wakati huo huo ruzuku ya chama inaongezeka, yeye akiwa ni mfaidikaje mkuu wa ruzuku ya chama
hivi anapata wapi jeuri ya kuwalabel watu kuwa wadini wakati yeye ndo kinara.walimfanyia Jk rafu mbaya sana kuelekea uchaguzi mkuu 2010,mpaka jk uvumilivu ukamshinda ikabidi aliseme suala la watu kutumia udini katika hotuba yake ya kufungia kampeni.badala yake haohao kina silaa ndo wakamgeuzia ubao eti kwamba jk ndo katumia udini.wapi alitumia udini,msikiti upi?ukweli ni kuwa silaa na maaskofu wao hawakutaka jk amshinde silaa na walipiga sana black campagn kwa slaa.hata kilaini alipotoa matamshi ya kumsifia jk ,walimuona msaliti wao wakamlima transfer akawe mchungaji kule kagera.

Ni bahati tu kuwa watanzania hawakukubali kurubuniwa na nyaraka zenye ajenda za hao jamaa.
 
USHAURI WANGU.
KWANZA CCM IKOME KUHUBIRI WAZIWAZI NA KUVIITA VYAMA VYA UPINZANI VYA UCHAGA,UKASIKAZINI,UKATOLIKI,UKRISTO,UISLAM NA UGAIDI.
kwa maana ccm ilitengeneza propaganda hizi ili ishinde LAKINI DHAHIRI NAJUA SASA CCM MMEONA MADHARA MAKUBWA ZAIDI YANAKUJA,kama msipofunga midomo yenu hasa wale waliopewa vyeo vya UENEZI WA PROPAGANDA.
maana mkiendelea kusema.WALE MNAOWATUHUMU LAZIMA WAJE KUJIBU na mtakuwa mnaendeleza mjadala wa kulipasua taifa kwa uislam na ukristo na ukabila.
NA MKIACHA HATA WAPINZANI WATAACHA KUJIBU.
kama CUF NI CHAMA CHA SIASA CHA UISLAM NA CHADEMA NI CHAMA CHA SIASA CHA UKATOLIKI NA UKRISTO KWA NINI MPAKA LEO TENDWA HAJAVIFUTA?NA KAMA HANA USHAHIDI AWAOMBE CCM WANAO mana haiwekana miaka yote hii viongozi na watu wakubwa wa CCM WANAPAYUKA BILA HATA HAYA KAMA WASINGEKUWA NA USHAHIDI(mtu mzima hovyo).
VINGINEVYO TENDWA KAZI IMEKUSHINDA KAM UMESHINDWA KUZUIA PROPAGANDA ZA CCM ZA UDINI,UKABILA NA UKANDA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
hizi mada za udini malengo yake ni yapi
kama si kuzidi kutugawa watanzania?
mimi nadhani kila mtu ni mdini cha msingi tuvumiliane
mwingine asimdharau
au kumsema mwengine kwa sababu ya dini yake.
dini hatukuzaliwa nazo tumeletewa na hawa wakoloni wa Ulaya na waarabu.
wazee wetu hawakuchekana kwa dini zao za kuabudu kwenye miti au mawe makubwa
wote waliishi kama ndugu katika koo zao na familia zao.
chuki za udini zinapandwa na mabeberu ili tupigane vita na wao wapate fursa nzuri za kutuibia
tusikubali kuwa watumwa wa hawa mabebeberu, tuishi kama ndugu
 
Dr Kaongea ukweli mtupu. Angalia tofauti ya maandishi kwenye Tz daima na uongo na maneno ya uchochezi ya mtoa mada. Kwanza mtoa mada anaongea kuwa Dr Slaa alifanya kampeni makanisani na maaskofu walimfanyia kampeni. Hatoi ushahidi wowote na haupo. Kuna ushahidi tele na zingine zishawekwa hapa JF watu wakimtetea JK misikitini huku wakitukana viongozi na chama cha CDM. Kuna wajinga wamezunguka nchi hii kufanya mihadhara zingine zikionyeshwa kwenye vyombo vya habari wakimtetea JK kuwa ni muislamu ndio maana watu hawapendi uongozi wake. Hii ilitokea hasa baada ya uchaguzi wa 2010 ambapo watu wengi walishuku ushindi wa JK kama kweli ni halali au ni uchaguzi wa tume ya uchaguzi. Kwenye hiyo mihadhara kilichohubiriwa ni chuki dhidi ya CDM, wakristo na mfumo wanaoita mfumo kristo.Wenye akili zetu tulishangaa na kuduwaa jinsi kiongozi wa taifa anavofumbia macho uchochezi wa chuki dhidi ya wakristo na watanzania wengine kwa misingi tu ya kutafuta kisingizio cha chuki toka kwa wananchi dhidi ya utawala wake wa hovyo kabisa. Mtoa mada siwezi kukulaumu kwa kuwa ndivo ulivofundishwa kwenye mihadhara au mikutano ya ccm iliyogeuka mikutano ya kupandikiza chuki dhidi ya CDM bila kujua CDM haina dini wala ukabila ila wananchi wa tanzania wana makabila yao na dini zao. Kwa kutumia propaganda ya udini na ukabila hawa viongozi maslahi wa ccm akili zao za utambuzi zilizibwa na tamaa ya kubaki madarakani wasijue wanagawanya nchi vipande. Sasa leo mkiambiwa mmeleta udini na JK kama kiongozi wa nchi aliweka miwani ya mbao mkibeba kwa udini bila kujali anaangamiza taifa imekuwa nongwa. Huwezi kupanda mhogo ukategemea kuvuna ngano. Mlipanda udini na mjue JK kama kiongozi wenu atavuna tu historia ya kupalilia udini ulioanzishwa na ccm enzi CUF. Hiyo ndAvune tu alichokipanda. Kuleta thread ya kidini kama hii ni matokeo ya udini mliopewa na JK kuwa kinga yake kwa utawala wake mbovu.
 
Kwa kweli yote haya ninamlaumu jk kwa kuwa mkimya sana kwa sababu hawezi kuchukua hatua watu kama hawa.

Alichotakiwa ni kuwakamata watu kama hawa na kuwaweka ndani kwa muda usiojulikana
unafikiri hapendi kuwakamata? Tatizo hawa kina dr. Slaa wanasema ukweli, nakumbuka mwaka 2010 nilikwenda msikiti mmoja siutaji, mada kubwa ilikuwa namna ya kumsaidia jk ili aweze kushinda urais, ndo maana kura za prof. Lipumba zilishuka! Kwa hiyo ni bora akae kimya mh. Jk! Ni upepo utapita!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom