Kwa hili, Chuo Kikuu Ardhi hamjawatendea haki wanafunzi

mzee wa kismati

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
2,292
795
Mlitoa tangazo kwamba mnatoa muda wa siku tano kwamba kuanzia tarehe 11 mpaka tarehe 15 wanafunz wote ambao hawajakamilisha usajiri wawe wamefanya hivyo.
muitikio ulikuwa mkubwa idadi kubwa ya wanafunzi walifanikiwa kusajiriwa

ajabu mi kwamba leo malipo ya awamu ya pili ya pesa za kujikimu yani BOOM yamefika, lakini kwa wanafunzi waliosajiliwa kipindi hiki wengi hawajapata fedha hizo

nimeshuhudia idadi kubwa ya wanafunzi wakilaani kitendo hicho cha kibaguzi wakiwa wamejawa na sura zenye majonzi, mmesababisha usumbufu mkubwa kwani idadi kubwa ya watoto hawa wa wakulima wametumia nauli zao kwenda benki kutoa hela kwa ajili ya kulipa kodi ya nyumba na kuambulia patupu

mimi kama mzazi nalaani sana kitendo hiki cha kibaguzi na kionevu kwanini kuwasumbua vijana hivi yamkini mkijua hamuwapi pesa zao? mmeshindwa hata kutoa taarifa fupi? naomba mamlaka zinazohusika mlishughulikie hili kabla halijafika kwa magufuli
 
Pole sana mzazi, usajiri ni pamoja na ulipaji ada stahili kwa ajili ya kukidhi gharama za masomo kwa term husika, na usipolipa ada ina maana husajiriwi na kuwa hautakuwa tayari kufanya mitihani ya term, kwa jinsi nilivyojifunza suala la ulipaji ada na usajiri ni la lazima sana na si hiari wala kujipangia kuwa nitajisajiri siku za dead line, hivyo basi ikiwa mzazi unatambua kijhana wako yupo Ardhi ni vema ukajipanga mapema kulipa ada ndani ya tarehe zilizopangwa na hata kasma dirisha la usajili likfunguliwa katika kipindi cha rehema basi fanyeni utaratibu wa malipo kwa wakati,.....

Ardhi ni chuo pekee chenye mfumo wa ufundishaji tofauti na vyuo vingine, uhudhuriaji wa vipindi vya lecture madarasani ni kwa local/attendance registry na kwamba ukimiss lecture kadhaa mfululizo hufanyi paper kabisa na wako strict sana.... vyuo vingine uingie usiingie lecture poa tu unajua wewe mwisho wa siku utaandika nini kwa mtihani wako.....
 
Andikeni madaa kwenda waziri husika wakionaga majinayao humu awakai ofisini polensana nakumbuka mwteso Yale
 
Aisee... Yaani kuna idara huko maVyuoni huwa zinasimamiwa na watu ambao huwa utadhani wao hawana ndugu wenye shida au familia zao tayari zishamaliza kila kitu... Hawana utu zaidi ya kujua kupokea ada na sio kuskiliza wateja wao wanashida gani...
 
Back
Top Bottom