Kwa hii hali bora kuoa

Kwa hii hali bora kuoa

Huu usithubutu.

Hakuna atakayeonyesha tabia yake ilhali anajua unamchunguza tabia mkuu.

Ukimuweka ndani atajua tu na ataonyesha tabia zote ambazo wenye sifa ya kuolewa wanazo.kwa hivyo atajua kabisa anasomwa tabia na hapo atazifufua tabia usishangae akakulamba mpaka mafua yako nawewe ukasema yeees huyu ndo mke.

Wanawake wanajua kama wanaume tunatafuta tabia na hapo ndo wanatumia udhaifu wetu ulee wa sisi kutaka kuzijua tabia kwa mwenye tabia na hapo hao wenye tabia ndo huanza kuigizaaaaa sasaa.

Unatakiwa ufanye ziara ya kushtukiza tuu mkuu,usiicbunguze tabia ya mwanamke moja kwa moja kutoka kwa mwanamke mwenyewe atakuigizia na mwishowe ukaingia mkenge.

Kuoa ni jambo linahitaji busara kuliko tunavyofikiria tena ilikuwa kuchukua hekima za wazee kabisa.

Usichunguze tabia yake kwa kumuweka ndani kwako,hilo ni kosa kubwa.

"USIMUWEKE NDANI KISHA NDO UCHUNGUZE TABIA,BALI CHUNGUZA TABIA KISHA NDO UMUWEKE NDANI(ndoa)"

Mwanamke ni kama bomu,utafiti kwanza ndo unakaa nae,sio unakaa nae then ndo wafanya utafiti hapanaa.
kweli kabisa mkuu,kuna manzi hata mwaka hatujamaliza basi anavyonilazimisha tufunge ndoa wakati hata sijamsoma vizuri basi ni shida tu!
 
Yees mkuu lakini jambo ambalo tunatakiwa kuliepuka ni kumchunguza tabia ambaye anajua tayari kwamba sasa anachunguzwa tabia.

Hatokaa afanye kosa kamweeee mkuu.
Kumchunguza mtu ambaye anajua anachunguzwa huchukua muda mrefu saaaana saaana.

Lakini kumchunguza ambaye hajui kama anachunguzwa ni jambo halichukui muda.

Mimi nilitumia siku moja tu kumcbunguza tabia.
Nilifunga safari nikarenda kwa wazee waaminifu wa mtaani ambao nao niliwachunguza kwamba hawawezi kunipiga chenga,nikaenda nikasmbiwa tabia zake na familia yake wakati huo najuana nae na wala hakujua kama nimeenda kumchunguza.

Kwa hvyo ingelikuwa ana tabia mbovu ningemkaushia kimya kimya tuu pasi na yeye kujuaa lakini ikawa poa,nikamwambia lengo langu akakubali naye mipango ikasoma
 
Mkuu #Safuha
Naomba kama utakua na muda tupe elimu kidogo juu ya kuweza kuishi na mchumba ambae upo mbali nae.( I mean kuepuka mapenzi ya maigizo
Ndiyo mkuu ninaweza kushare nanyi kidogo nikijuacho na nyinyi mkatupatia sisi abc za hapa na pale.

Kwanza kabisa tu ni kwamba mchumba ambae upo nae mbali ni kujua tu labda umempa akiwa mbali nawe au mlikutana mko karibu kisha akapata safarii.ila ni kuwa huwenda pakawa na utofauti kidogo kati ya hayo mawili.

Muhimu zaidi kwanza haitakiwi kufanya kosa katika kumchagua mchumba wa kuoa,kwa sababu ukishakosea huwenda ukaona aibu hata kughairisha.

Mchumba ambaye mumejuana mbali mbali mkatongozana mbali mbali hivyo hivyo basi huyu kwanza ikiwa mtu anawasiliana naye tuu bila ya kumtongoza na kumuambia nia yake basi lazima ukamfanyie utafiti mpaka huko anakoishii,hi huwenda ikachukua muda na pesa lakini ni njia ambayo ikiwa mtu anajua anachotafuta basi pesa na muda sio kitu kwake,pesa na siku tatu nne sio hasara kwa kuwa anaenda kumtafuta wa siku zotee maishani.

Ni kwa sababu tu mtu wa mbali anakuwa huru kufanya atakalo na alipendalo na huwezi jua huwenda anakuigizia tuu mkiwa kwa simu mpaka ukamuamini kwamba ni mtu mzuriii(huwenda si kweli)lakini sekta hii ya mawasiliano muhimu kwa sababu unamsoma kama ana jeuri au hana,ksms ana mdomo mdomo au hana.

Mimi niliwasiliana na mke wangu kabla ya kumchumbia kwa muda wa miezi saba sijamtongoza wala nini,lakini tulizungumza kwa hisia tu,katika miezi saba hiyo hakuwahi kunipiga kirungu(kuomba pesa,hata vocha) hata siku moja,hakuwahi kujibizana na mimi hata siku moja hata nikija juu.

Ikawa naridhika katika nyanja ya mazungumzo kwamba yuko vizuri,ila mwingine hata hujatongoza anakupiga virungu jee ukitongoza? Na jeeee ukija kuoa kabisaaaa? Balaaa linaanza hapo.

Wengine ukiongea nao tuu ukimkaripia kidogo naye anakuja juu kwa maneno ya dharauu n.k haya yote ni yakuyaangalia saaana katika upande wa mazungumzo tuwe makini sana kuchagua kitu ambacho tutaambatana nacho mpaka kaburini(maisha yote)

Ikiwa mtu anasoma miaka zaidi ya 15 kwa ajili ya kupata kazi ambayo atafanya muda flani na kustaafu. Basi usione kazi kumsoma mke mtarajiwa japo kwa mwaka kwa ajili ya kuishi naye milele milele.
 
Ukijiona tayari unaanza kuwaza kuoa oa basi jua wakati wako umeshaingia mkuu,wasi wasi ndo akili mkuu,hapo taratibu unaanza kuona umuhimu wa mwenzio japo kuoa ni zaidi ya kupikiwa na kufuliwa lakini haya nayo yana umuhimu mkubwa ndiyo maaana watu wanaishi kwa kuwafulia wenza nguo(madobi)na wengine wakiishi kwa kuwapikia wenzao(mama ntilie)lakini mmoja tu kaamua kuishi kumfanyia hayo yote mwennziwe(mke)

Hivyo mkuu kuoa ni jambo jema sana heshima yako inaongezeka japo lengo sio kupata heshima,lakini pia na akili inazidi kupanuka kuwajua zaidi wanawake ukiwa bado kijana,sio lijitu lizee miaka 35 ukiliuliza mwanamke akisema sitaki anamaanisha nini linakujibu tu kizobe zobe"ndo hataki huyoo" ingia mapema ikiwa utakosea utajua namna ya kusolve kwa kuwa bado kijana na ikiwa hujakosea basi utainjoi ndoa tokea ujana wako.

Lakini pia ili usikosee epuka kutafta mke sehemu ambazo sio rafiki na ikiwezekana mtume mama mzazi akufanyie kazi ya kukutaftia mke(sio akuchagulie hapana)kwa sababu wanawake wanajuana sana siri zao hivyo ukimuambia mama unataka mke alotulia mzuri akupende na ana tabia njema lazima atajua tu kwamba mtaa fulani na nyumba fulani yupo aliyetulia na hawezi kukosea kukuchagulia mwanaee,then akimpata wewe unamuambia maza tulia kwanza ukamuone pasi na yeye kujua,then ukimridhia unaanza mingo eidha uzoeanne nae au utume mtu moja kwa moja akapose.

Hakika ndoa ni tamu sana mfano wa muwa tu ni mtamu japo kuwa ukiutafuna yale maganda yanaweza kukukata kidogo mdomoni lakini utamu wa muwa huyashinda maumivu,na ndoa iko hivyo ukipata mtu sahihi kaka utaona ndoa tamu japo kuwa kutakuwa na kutoelewana katika baadhi ya mambo lakini utamu wake uko pale pale.

Kuna baadbi ya watu hawataki kuoa eti wanasema hawataki kukkerana na wanawake ilhali hapo alipo anakerana na hawara yake,sasa akimbia nini afanya nini?

Eti hataki kuumizwa ilhali kila siku hawara yake anagombana nae na kumtesa ndo nini?

Bora kutumia mda utafte kwa makini ukioa unatulia zako unapanga maisha mengine...

Napenda kuandika kiurefu mada kama hizi kwa sababu nimekuwa barozi mzuri juu ya suala hili.
Ndg mpendwa... umeniliwaza na uetoa darsa zuri hata huko chuoni hawanazo materials kama hizi.. J putin msikie profesa huyu na ulifanyie kazi somo hii... wish you best of luck and best wife !!
mashkurran
 
Mkuu tupo pamoja kwa kubadilishana mawazo kama hivi.

Nawe unaweza kutia neno lako kuzidi kutia hamasa juu ya jambo takatifu la ndoa.
 
Shukrani saana Mkuu. Kuna maarifa nimeongeza kupitia andiko hili
 
Ukijiona tayari unaanza kuwaza kuoa oa basi jua wakati wako umeshaingia mkuu,wasi wasi ndo akili mkuu,hapo taratibu unaanza kuona umuhimu wa mwenzio japo kuoa ni zaidi ya kupikiwa na kufuliwa lakini haya nayo yana umuhimu mkubwa ndiyo maaana watu wanaishi kwa kuwafulia wenza nguo(madobi)na wengine wakiishi kwa kuwapikia wenzao(mama ntilie)lakini mmoja tu kaamua kuishi kumfanyia hayo yote mwennziwe(mke)

Hivyo mkuu kuoa ni jambo jema sana heshima yako inaongezeka japo lengo sio kupata heshima,lakini pia na akili inazidi kupanuka kuwajua zaidi wanawake ukiwa bado kijana,sio lijitu lizee miaka 35 ukiliuliza mwanamke akisema sitaki anamaanisha nini linakujibu tu kizobe zobe"ndo hataki huyoo" ingia mapema ikiwa utakosea utajua namna ya kusolve kwa kuwa bado kijana na ikiwa hujakosea basi utainjoi ndoa tokea ujana wako.

Lakini pia ili usikosee epuka kutafta mke sehemu ambazo sio rafiki na ikiwezekana mtume mama mzazi akufanyie kazi ya kukutaftia mke(sio akuchagulie hapana)kwa sababu wanawake wanajuana sana siri zao hivyo ukimuambia mama unataka mke alotulia mzuri akupende na ana tabia njema lazima atajua tu kwamba mtaa fulani na nyumba fulani yupo aliyetulia na hawezi kukosea kukuchagulia mwanaee,then akimpata wewe unamuambia maza tulia kwanza ukamuone pasi na yeye kujua,then ukimridhia unaanza mingo eidha uzoeanne nae au utume mtu moja kwa moja akapose.

Hakika ndoa ni tamu sana mfano wa muwa tu ni mtamu japo kuwa ukiutafuna yale maganda yanaweza kukukata kidogo mdomoni lakini utamu wa muwa huyashinda maumivu,na ndoa iko hivyo ukipata mtu sahihi kaka utaona ndoa tamu japo kuwa kutakuwa na kutoelewana katika baadhi ya mambo lakini utamu wake uko pale pale.

Kuna baadbi ya watu hawataki kuoa eti wanasema hawataki kukkerana na wanawake ilhali hapo alipo anakerana na hawara yake,sasa akimbia nini afanya nini?

Eti hataki kuumizwa ilhali kila siku hawara yake anagombana nae na kumtesa ndo nini?

Bora kutumia mda utafte kwa makini ukioa unatulia zako unapanga maisha mengine...

Napenda kuandika kiurefu mada kama hizi kwa sababu nimekuwa barozi mzuri juu ya suala hili.

kumbe miaka 35 ni lizee 🤣🤣🤣 au ndio hawa wanaitwa mzee baba
 
Ndugu wee Oa tu ila usioe ili upikiwe utamwacha mke kaka... maana hawa wake wa siku hizi wapo busy nao kutafuta mkirudi wote hoi. Mwenye njaa ndo atawasha jiko au mtakula take away.
 
Mkuu tupo pamoja kwa kubadilishana mawazo kama hivi.

Nawe unaweza kutia neno lako kuzidi kutia hamasa juu ya jambo takatifu la ndoa.
BarakaAllahu~Fik wa kathir min amthalak (Baraka zake Allah ziwe nawe, na wawepo mithali zako kwa wingi).... Ameen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom