Kwa heri CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa heri CCM

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mwita25, Oct 7, 2011.

 1. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwako Invisible!

  Usiku wa kuamkia leo niliamshwa na haja ndogo, na kama kawaida nilikimbilia chooni. Wakati narudi kitandani niligugundua kuwa sina magamba yangu. Looh! Nilistaajabu sana, lakini wakati naendendelea kutafakari niliona gamba moja lipo karibu na ukutani.

  Kutahamaki kumbe yote yalikuwa yamechomoka. Nilipojaribu kuyaruridishia, yakawa madogo kuliko mwili wangu, yaani yamenikataa. Huu ukawa mwanzo wa kukatalaliwa na CCM. Sikustaajabu kwa sababu CCM amewakataa watu wengi sana.

  Infact, anajikataa hata yeye mwenyewe. Sina maneno mazuri ya kujieleza zaidi ya kusema kuwa ndoa yangu na CCM imeisha leo. Hizi taarifa haziwezi kuingia kwenye kichwa cha Nape, kada nambari moja asiyejua kazi yake zaidi ya kulazimisha watu tuipiganie CCM kwa nguvu zote tena sehemu yoyote.

  Taarifa ni chungu zaidi kwa Mwenyekiti wa UVCCM, Dodoma ambaye kucha kutwa anatuma vivocha kwa wanafunzi wa UDOM ili, eti waipiganie CCM! Kwa lipi hasa? Chama ambacho hata Mwenyekiti wake mstaafu anapangiwa maneno ya kuongea jukwaani! Chama ambacho kiko tayari kuua ili kipate kura moja?!

  Hiki ndiyo chama kilichoshika hatamu Tanzania! Sina maneno mengi ila kusema kuwa umbumbumbu wangu umefika kikomo. Gamba limeng'ang'ania kwenye godoro na sasa najisikia mwepesi saaaaaana kiasi cha kujuta kwa nini nimeteseka muda wote huo kula chakula cha simba ambaye mwisho wa siku anataka anitafune?

  Nimeteseka sana, nimenyanyasika sana na nimehuzunika sana na sasa NAACHIA NGAZI.

  People's Power!
   
 2. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  You better check urself before......
  Ice Cube - Check Your Self - YouTube
  Otherwise get this stuff in ur system....
  Lil Scrappy - Get Some Crunk In Yo System (BASSED UP) - YouTube
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwita 25! Ni wewe au kuna mtu kaiba password yako?
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mbona kam siamini Mwita25! Nini kimekisibu au wamekurusha akina Nape ndiyo ukaon hawan maana! Pole lakini kwa kuwa umeomba msamaha huna budi kusamehewa lakini isije n ID nyingine ili kutupiga changa la macho na kuendelea na umbumbu wako ambao umekutesa kwa kipindi.
   
 5. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mhhhhhhhhhhhh, jamani iteni ambulance haraka kuna mgonjwa huku anaweza kupoteza fahamu kama sio maisha muda mfupi ujao. Au ni mashetani haya?
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi pia bado siamini kama huyu ni mwita25 ninayemfahamu humu jf..
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mhhh! kuna mtu kaingia kwenye server ya jf jamani, kiroja!
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Yote kwa yote,tunakupa muda ili tuone michango yako kama imebadilika, halafu hebu weka wazi uovu wa Nape zaidi tumjue huyu jamaa na mbinu zake kama kweli ineokoka na jinamizi la Magamba.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,660
  Likes Received: 1,493
  Trophy Points: 280
  HApa kuna mtu kaiba Password yake tu lazima.

  Ila inafurahisha kuona kwamba unaweza 'kufunguka' hivi wakati mwingine.

  Toa gamba tupa kule, vaa utu upya.
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Hivi MS "nae" alishavua magamba? Kuna siku niliona amekuja kivingine saana baada ya ile hutuba ya JK siku ya eid kule dodoma.
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mwita mimi bado ni Thomaso sijaamini, ngoja nipekue na kesho nipate jibu sahihi!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,660
  Likes Received: 1,493
  Trophy Points: 280
  SL.....maaajabu hayataisha duniani!
   
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kweli aisee. ID ya yule mwita25 kada wa ccm iko kwa herufi ndogo, wakati ya mwita huyu imeanza kwa herufi kubwa! Changa hili.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  subirini, ni mapema mno kuelewa!!!!
   
 15. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hahahaha never trust this information ila kama niza kweli kijana utakuwa umepiga hatua kubwa ya kuwakomboa watanzania wenzako katika mfumo kandamizi.
   
 16. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Na haya inabidi yakaingizwe kwenye guines book..lol.
   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mathomaso tupo wengi, ila nasikitikia wenye ndoa za kudumu na CCM kama mkuu fulani mwenye deni la over a billion Tshs mpaka alipe awe na ubavu wa kuvua gamba, nampa pole!!!!!!!!!!!
   
 18. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Jamani jamani! Mwita25 nimjuae au kuna mtu amehack akaunt yake? NIMECHEKA SANA! U made my day dude!
   
 19. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu kuna thread moja inazungumzia Slaa kukimbia mdahalo, nimewaeleza jinsi Slaa alivyo muhimu kuliko hiyo midahalo yao ya kujiingizia vijisenti. Nimempigia Nape na Mwenyekiti wa UVCCM Dodoma lakini wamenitukana matusi ya nguoni. Hii haizuii uamuzi wangu wa kukubaliana na ukweli badala ya kushindana na ukweli!
   
 20. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hii siku na tarehe tuiweke kumbukumbu CDM waaaaaaaaaaaa!!!!!!!
   
Loading...