Mwita25
JF-Expert Member
- Apr 15, 2011
- 3,831
- 1,164
Kwako Invisible!
Usiku wa kuamkia leo niliamshwa na haja ndogo, na kama kawaida nilikimbilia chooni. Wakati narudi kitandani niligugundua kuwa sina magamba yangu. Looh! Nilistaajabu sana, lakini wakati naendendelea kutafakari niliona gamba moja lipo karibu na ukutani.
Kutahamaki kumbe yote yalikuwa yamechomoka. Nilipojaribu kuyaruridishia, yakawa madogo kuliko mwili wangu, yaani yamenikataa. Huu ukawa mwanzo wa kukatalaliwa na CCM. Sikustaajabu kwa sababu CCM amewakataa watu wengi sana.
Infact, anajikataa hata yeye mwenyewe. Sina maneno mazuri ya kujieleza zaidi ya kusema kuwa ndoa yangu na CCM imeisha leo. Hizi taarifa haziwezi kuingia kwenye kichwa cha Nape, kada nambari moja asiyejua kazi yake zaidi ya kulazimisha watu tuipiganie CCM kwa nguvu zote tena sehemu yoyote.
Taarifa ni chungu zaidi kwa Mwenyekiti wa UVCCM, Dodoma ambaye kucha kutwa anatuma vivocha kwa wanafunzi wa UDOM ili, eti waipiganie CCM! Kwa lipi hasa? Chama ambacho hata Mwenyekiti wake mstaafu anapangiwa maneno ya kuongea jukwaani! Chama ambacho kiko tayari kuua ili kipate kura moja?!
Hiki ndiyo chama kilichoshika hatamu Tanzania! Sina maneno mengi ila kusema kuwa umbumbumbu wangu umefika kikomo. Gamba limeng'ang'ania kwenye godoro na sasa najisikia mwepesi saaaaaana kiasi cha kujuta kwa nini nimeteseka muda wote huo kula chakula cha simba ambaye mwisho wa siku anataka anitafune?
Nimeteseka sana, nimenyanyasika sana na nimehuzunika sana na sasa NAACHIA NGAZI.
People's Power!