Kwa haya ya kununua umeme toka Ethiopia na Ethiopia kutumia bandari ya Dar es Salaam, nasema hapana

Inaonyesha kabla viroba havijapigwa marufuku ulikuwa umejiwekea akiba ya kutosha. Hivi unalinganishaje gharama ya kusafirisha mizigo na kuunganishwa umeme kutoka sehemu moja mpaka nyingine?
Mwambie Magufuli sasa zile ndege zitakazokuwa zinabeba mizigo ya Ethiopia kutoka bandari ya Dar ndizo hizohizo zitumike kusafirisha umeme kutoka Ethiopia kuja Tanzania
 
Kweli kabisa.bora tukope pesa za kujenga hydroelectric power yetu.kuliko kukopa fedha ili tununue umeme kutoka ethiopia.haya mawazo sijui yametoka wapi tu.

Mkuu ungezungumzia umeme unaozalishawa na Nuclear Power Reactors, Geothermal, Mkaa wa mawe hapo ningekuelewa - kwa nini nasema hivyo: Mkuu umesahau crisis ya kupungua maji kwa kiwango kikubwa katika mabwawa yetu ya kuzalisha umeme huko Mtera na Kihansi, kama tusingekewa na Gasturbine engine driven Generators pamoja na Internal Combustion Engines as prime movers za kulazisha umeme huko Tegeta unafikiri tungekuwa wageni wa nani as a Nation tungekwama kweli kweli - je, unajua I.C engines zilikuwa zinakula lita ngapi za Heavy Oil kwa siku? Taifa lilipoteza fedha kiasi gani kuagiza mafuta including capacity charges za wamiliki mitambo ya kuzalisha umeme? Tulipigwa pesa kweli kweli au umesahau scandal za masuala ya EPA.

Mkuu kumbuka hakuna Serikali yenye watu wenye akili timamu inaweza kuruhusu tena Taifa letu kujingiza kwenye jehanamu ya kutegemea sana uzalishaji wa umeme kwa kutumia nguvu za maporomoko ya maji, tumekwisha pata somo the hard way hatuwezi tena kurudia makosa hayo hayo siku za usoni - ndiyo maana na insist Serikali itafute source nyingine ambazo ni reliable - sina shaka Dk.Magufuli na washauri wake walipo kutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia suala la umeme lilipewa kipa umbele for a good reason namely once beaten twice shy, hatuwezi kuzungumzia masula ya Viwanda bila ya kuwa na umeme wa kuaminika na wa kiwango cha kukidhi peak demand, umeme unoa zalishwa kwenye mto wa Blue Nile huko Ethiopia ni wa kuaminika sana kutokana na sources zinazo feed Lake TANA kuwa nyingi sana.
 
WATANZANIA HATUNA AKILI HIVI KUTOKA MTO RUFIJI MPAKA DSM KM 100 HALAFU UNAKWENDA KUCHUKUA UMEME MAILI 10020000000?TUMEWAACHIA MAMBA WANAOGA TU
 
WATANZANIA HATUNA AKILI HIVI KUTOKA MTO RUFIJI MPAKA DSM KM 100 HALAFU UNAKWENDA KUCHUKUA UMEME MAILI 10020000000?TUMEWAACHIA MAMBA WANAOGA TU

Mkuu mbali na mamba kuogelea kwenye mito yetu.pia vyazo kibao tu vipo.inasikitisha sana.
 

Ethiopia wamejenga SGR au standard gauge railway kwenda Djibouti kwa sababu ya bandari kule Djibouti baada ya sababu za kidiplomasia na kiusalama kuacha kutumia bandari ya Asmara, Eritrea. Hata bandari ya Mombasa kwao ni tatizo bado na ndiyo maana kuna mpango wa LAPSET wa Ethiopia na Kenya kujenga bandari kubwa ya kisasa pale Lamu nchini Kenya kwa ajili ya mizigo ya Ethiopia na Sudan kusini.
Kwa haya inaonyesha kabisa kutumia bandari ya Dar Haiwezekani kiufanisi na kigharama kwa sababu ya umbali na miundombinu mibovu.
Awamu ya tano ni wapuuzi tu
 

Cargo planes hao Ethiopia wanaagiza stationary tu peke yake? Wanadevelop project ya Lapset na Kenya kujenga bandari ya Kimataifa Lamu, Kenya, hata Mombasa tu kwao ni mbali wanatumia Djibouti, Dar wapi na wapi. Hatuko hapa kubishana so usitafute uhalali wa kila tamko la viongozi hawa, angalia uhalisia kama mfanyabiashara na mwekezaji nchini Ethiopia, na angalia harakati gani zinafanywa na serikali yao Kuweka mazingira ya kukuza biashara na uchumi wao kwa kushusha gharama za usafirishaji n.K cargo plane inabeba maziwa,nyama, maua,samaki etc na hivi vyote vinapatikana Kenya kiurahisi kuliko hapa
 
Ethiopia ni mfanikiwa kwa nadharia, kwanza tutapeleka ndege zetu kwa matengenezo kisha watatuuzia umeme ambao utatudumaza akili zetu kwa miongo kadhaa. Kuhusu suala la mizigo labda Serikali tu lkn kwa mfanyabiashara hawezi Ku afford gharama kubwa ya usafiri labda km watapitisha pasipo ushuru. Siku zote wafanyabiashara wanaangalia faida na sio sifa ya mahusiano. Kwa suala hili ni sawa sawa na wewe uishi Morogoro ukashushie mzigo wako Mombasa huku ushuru na ufanisi wa port zote unafanana.
 

Nilicho eleza mwanzo ilikuwa ni kama pre amble, nikiwa na lengo la kuwashauri Watanzania wenzangu tuachane na tabia inayo anza kuota mizizi ya kuchukulia kila kitu kinacho fafanuliwa/tendwa na Serikali ya awamu ya tano kina walakini, hakuna kitu +ve mnacho zungumza kuhusu juhudi ya JPJM na washauri wake - amefanya mambo mangapi ya kujivunia ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake - mengi tu, sasa mnashindwa nini kuamini au kuchukulia seriously makubaliano ya Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais Magufulini - ina maana sisi watu baki tuna akili zaidi na weledi kuliko Viongozi hao wawili au? - tell ME!!

Hapa chini nimebandika tena majibu yangu geared for skeptical mwenzako ambaye hana imani na mipango ya ya awamu ya tano:

M'bang'ang'walu said:
Kwani hiyo mizigo itakuwa inazalishwa hapa TZ? Yaani mizigo itoke huko itokako, ibebwe kwa meli mpaka TZ, Kisha ibebwe kwa ndege tena mpaka Ethiopia. Akili hiyo hata mtoto wa chekechea hawezi kuwa nayo
Hivi unajua gharama za kusafirisha mizigo kwa njia ya anga zikoje? Watu wasingekuwa wanatumia muda mrefu kwa kutumia usafiri mwingine. Jiulize kwa nini hao Ethiopia wasitumie ndege kubeba hiyo mizigo kutoka huko itokako. Halafu mizigo mingi ni ya watu na makampuni binafsi, kwa serikali haiwezi kuwalazimisha watu washushie mizigo yao Tanzania


Mambo mengine tujaribu kuchangamsha akili zetu kidogo kwa ku-analyse mambo in 3Ds, unawezaje ku-equate akili za Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais wetu pamoja na washauri wao kwamba akili zao hazina tofauti na za watoto wa chekechea - hizi dharau aziwezi kutufikisha popote, our leaders knows wanacho kitaka/ kifanya kwa maslahi ya Taifa letu - wajibu wetu ni kuwatia moyo na siyo kuwa bezabeza!!!

Tatizo la baadhi yetu ni obsession ya kukosoa kosoa everything 'Magufuli' sijui hii inatokana na chuki binafsi au nini, hawana time ya ku-analyse mambo wakiwa na akili zilizo tuliazana - mihemuko tu masaa yote.

FYI wa Ethiopia watajenga depot ya mizigo yao hapa Dar, kuhusu Mizigo itapatikana wapi na kwa nini wamefikia hatua ya kuhamua kufanya hivyo, hayo sisi hayatuhusu, Wahabeshi wana uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya usafirishaji, badala ya kushukuru kuhusu ujio wao ambao uta create employment, Serikali itapokea kodi na Dar itakuwa HUB ya kusafirisha mizigo kwenda kwa nchi zinazo tuzunguka and beyond hii ni catalyst tosha ya kuinua Economy ya Taifa letu hayo yote wala nyinyi hamuyaoni!!
 
Namba tatu ni uonga.
1. Maji yanayozalisha umeme Ethiopia HAYATOKI TANZANIA

2. Tanzania inamiliki takriban 49% ya ziwa siyo 3/4.
 
Swali ni kwa nini ununue umeme ethiopia huku wewe una vyanzo lukuki vya umeme-mradi wa umeme wa ethipia ulianza kwa kukopa pesa nadhani ilikuwa bank ya dunia kws nini na sisi tusifanye hivyo???
Ethiopia walinyimwa mkopo na WB. Fuatilia. Ilibidi watu wafe bwawa lijengwe.

Hoja zako zinakosa mashiko kwa sababu unaongea uongo uongo mwingi. Kama huna uhakika na jambo usilitaje. Ungeishia ti kuiliza kwanini kununua umeme wa waabeshi na si kutaja na mengine ya uongo.
 
Unayoyasema yamefanyika hapa TZ kipindi cha Jakaya. REA wana facilitate hizo community projects. Tembelea maeneo ya jimbo la marehemu filikunjombe kuna miradi mingi tu ya mini-hydro na wanavijiji wanafaidi.
 
Umbali ndiyo nini? Kwa taarifa yako nchi za SADC wanautaka huo umeme wa Ethiopia.

Hivi unakumbuka ujenzi wa laini za umeme za 400 Kv kutoka Iringa hadi Arusha na Shinyanga? Umefuatilia kwanini huo mradi ulipewa kipaumbele?

Ni kwamba nchi za waafrika weusi zimeanza kufanya kitu inaitwa GRID INTERCONNECTION. Kila mtu atazalisha na kuuza ziada kwenye gridi kwa mwenzie atakayekuwa anahitaji. Mfano Ethiopia wanazalisha ziada inatumiwa Swazland.

Umbali is nothing on this. Unaijua grid ya USA au Canada? Ni ndefu kiasi gani?
 
Njia tayari imejengwa kaka. Hukumbuki line ya 400kv? Tembelea maandiko ya TANESCO.

Halafu kila nchi inajenga upande wake. Kenya wanajenga kwao. Tunakutana mipakani.
 
Where is a hope to obtain/harness electricity based on mutwara gas projects?
Maana mliwapiga sana na lengo mojawapo lilikuwa ni ufuaji umeme kama sikosei?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…