Kwa haya ya kununua umeme toka Ethiopia na Ethiopia kutumia bandari ya Dar es Salaam, nasema hapana

mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
Nilicho eleza mwanzo ilikuwa ni kama pre amble, nikiwa na lengo la kuwashauri Watanzania wenzangu tuachane na tabia inayo anza kuota mizizi ya kuchukulia kila kitu kinacho fafanuliwa/tendwa na Serikali ya awamu ya tano kina walakini, hakuna kitu +ve mnacho zungumza kuhusu juhudi ya JPJM na washauri wake - amefanya mambo mangapi ya kujivunia ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake - mengi tu, sasa mnashindwa nini kuamini au kuchukulia seriously makubaliano ya Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais Magufulini - ina maana sisi watu baki tuna akili zaidi na weledi kuliko Viongozi hao wawili au? - tell ME!!

Hapa chini nimebandika tena majibu yangu geared for skeptical mwenzako ambaye hana imani na mipango ya ya awamu ya tano:

M'bang'ang'walu said:
Kwani hiyo mizigo itakuwa inazalishwa hapa TZ? Yaani mizigo itoke huko itokako, ibebwe kwa meli mpaka TZ, Kisha ibebwe kwa ndege tena mpaka Ethiopia. Akili hiyo hata mtoto wa chekechea hawezi kuwa nayo
Hivi unajua gharama za kusafirisha mizigo kwa njia ya anga zikoje? Watu wasingekuwa wanatumia muda mrefu kwa kutumia usafiri mwingine. Jiulize kwa nini hao Ethiopia wasitumie ndege kubeba hiyo mizigo kutoka huko itokako. Halafu mizigo mingi ni ya watu na makampuni binafsi, kwa serikali haiwezi kuwalazimisha watu washushie mizigo yao Tanzania

Mambo mengine tujaribu kuchangamsha akili zetu kidogo kwa ku-analyse mambo in 3Ds, unawezaje ku-equate akili za Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais wetu pamoja na washauri wao kwamba akili zao hazina tofauti na za watoto wa chekechea - hizi dharau aziwezi kutufikisha popote, our leaders knows wanacho kitaka/ kifanya kwa maslahi ya Taifa letu - wajibu wetu ni kuwatia moyo na siyo kuwa bezabeza!!!

Tatizo la baadhi yetu ni obsession ya kukosoa kosoa everything 'Magufuli' sijui hii inatokana na chuki binafsi au nini, hawana time ya ku-analyse mambo wakiwa na akili zilizo tuliazana - mihemuko tu masaa yote.

FYI wa Ethiopia watajenga depot ya mizigo yao hapa Dar, kuhusu Mizigo itapatikana wapi na kwa nini wamefikia hatua ya kuhamua kufanya hivyo, hayo sisi hayatuhusu, Wahabeshi wana uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya usafirishaji, badala ya kushukuru kuhusu ujio wao ambao uta create employment, Serikali itapokea kodi na Dar itakuwa HUB ya kusafirisha mizigo kwenda kwa nchi zinazo tuzunguka and beyond hii ni catalyst tosha ya kuinua Economy ya Taifa letu hayo yote wala nyinyi hamuyaoni!!

Umeshaweka assumption ya kwamba kila kitu kunapingwa na hapo tayari umechukua upande wa kuutetea. Nway kila project au proposal ya wakubwa itaundwa timu ya wataalam kufuatilia utekelezaji wake na siyo wanasiasa na hapa utaona kama project ita take off. Ngonjera zingine za kisiasa unaziangalia kiutendaji na kitaalam zaidi. Hata wakiweka Depot yao ya mizigo itatumia njia gani kusafirisha? Kama ni cargo planes kama ulivyoonyesha awali na hizo bidhaa hazitakua heavy capital goods au nyingi kiasi cha kuifanya Tz kua hub kama unavyoonyesha wewe..na kama ni samaki, au maua etc etc havitanufaisha bandari ya Tz wala sub sectors zinazotegemea bandari kwa kiasi kikubwa. Tukubali kutokukubaliana tu.
 
Bepari la bariadi

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
384
1,000

Kabisa ukiangalia haya mambo kiundani zaidi na kiuhalisia.there is no feasibility of it to be implemented.siasa zisitupofishe kabisa.alaaaaa!
 
Kabembe

JF-Expert Member
Feb 11, 2009
2,550
2,000
Yaani kwa kuombaomba ni bora hata serikali ya Mkwere ,hii serikali ya ngosha inaomba ombaomba sana tena mbaya zaidi inaomba hata vitu vya ovyo kabisa. Yaani ni kama baada ya uchaguzi akili ya huyu jamaa imereverse! Kila mtu aneyekuja yeye anaomba tu na si ajabu akija Mugabe ataomba msaada pia.
 
mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,273
1,225
Huo mto wako hauna maji ya kutosha

Stiglers Gorge project katika bonde rufiji ingetengeneza megawatts zaidi ya 1500 ukijumlisha na current capacity ya hydro electric power generation pamoja na haka ka Gas inayotumika kwa umeme you tungekua self sufficient kwa umeme wa bei rahisi na kuachana na hawa walanguzi wanaotumia generator za mafuta na kuifanya Tz ya viwanda kua na uwezekano wa kweli.
Tatizo ni self interest mkimaliza tatizo la umeme wanene Wetu watakula wapi? Maana hizi symbion,iptl, Richmond ndiyo ulaji wenyewe
 
MLALE

Senior Member
Sep 30, 2015
169
500
Mkuu ktk nia nzuri ya kumsaidia Mh. Ktk ujenzi wa taifa nitakupatia stori ya kisiwa kimoja huko Scotland, ni vipi wameweza kupambana na tatizo la umeme, Na njia gani wametumia mpaka kufanikiwa kuzalisha umeme wao nje ya national grid supply yaani kama hii yetu Tanesco kwa kutumia renewable energy.

Eigg ni kisiwa kidogo chenye wakazi wasiozidi 150, yenye eneo za mraba zisizozidi 30, wakazi wa kijiji hiki kwa ushirikiano wao binafsi wameweza kuliondoa tatizo la umeme kwa zaidi ya asilimia 95.

Hawa wanakijiji wameunda kampuni yao binafsi ya kutengeneza umeme kwa kutumia vitu amabvyo sio vingeni kwetu, Jua, upepo na maji au renewable energy to be precise.

Kumbuka kwamba hicho kijiji utokaji wa jua ni mdogo sana kwa mwaka mara nyingi ni wakati wa kiangazi kwa muda wa miezi isiozidi mitatu, upepo wao haufikii wa Tanzania Na mito yao sio yenye ukubwa Na nguvu kama yetu sisi hapa Tanzania. Lakini wameweza kudunduliza umeme kutoka sources zote tatu, Yaani jua, maji Na upepo wakauingiza kwenye community grid Na Kusambaza kwa wakazi Na biashara zao, kwa bei ya chini kabisa.

Watu wa nchi mbali mbali wameshapitia kwenye hichi kisiwa kutaka kufahamu, how they did it, Yaani mpaka Malawi imeshapeleka team Scotland kufanya preliminary studies and fact findings, Yaani Mh. hii Malawi inatupiga bao la mkono siku zote. Lol

Sasa tuje kwa upande wetu,

Naelewa wazi kwa Tz, pesa ya kufanya yote haya hatuna lakini kama serikali itakua smart and willing to innovate, wanaweza kuanzisha hata pilot system on renewable energy in partnership Na private sectors, finding strategic village somewhere ukiondoa chato, lol, and do the right thing, i.e. Community grid of some sort, replicating what's these villagers did in solving their problems, and do exact the same to one of our village by self financing, charging the community at subsidised rate.

In this way once successfully, we will encourage private sectors to enter in some sort of partnership with the government in doing the same for other places.

There is no harm trying Mh.

Second solution, and this can be done now! Let the hybrid technology go mainstream, i.e. Combination of both, electricity generated using solar panels in our roof tops and that coming from the national grid, i.e. tanesco.

The government can help by zero rated on VAT and import charges for a certain period of time to encourage the residents particularly from urban areas to go hybrid.

Tanesco can be given the outright monopoly for now, only for now! I insist, until the understanding of the technology become main stream, regulating technological competency through training and after service sales, this way will create more businesses and encourage innovations.

Allowing colleges with subsidised cost by providing tax incentives to teach our children on renewable energy technologies, in order to make us competency, innovative and renewable in some sort.

You never know, we might have our own wind turbine industry, si ndio sera za Mh, viwanda viwanda, and we will start selling the technology and know how to neighbouring countries.

Mh. Nakuomba uwaalike maintenance team ya community electricity grid kutoka Kisiwa cha Eigg Scotland, ambapo wako watatu mmoja muuza mikate, mmoja mfumaji Na mwengine analima bustani. Hawa watatufunza kitu, achana Na Ethiopia, majibu ya matatizo ya umeme yako nje ya magogoni Na upepo huo.

Halafu yale mahela ya maboeing ahirisha ununuzi, finance hii project ukisaidiana na wanakijiji wa Eigg Scotland.

The small Scottish isle leading the world in electricity
Mkuu,ww umesema vema but people are very different na wenye akili kama zako hawapewi nafasi ya kusikilizwa mawazo yao na hata watu kama ww wakipata nafasi ya uongozi wanasahau ahadi zao na kutumia vema madaraka,even me!watz uzalendo n zero tena zeroo na wakutuletea tena uzalendo washakufa wotee...chukua chako mapema###mwl wa sanaa
 
Bepari la bariadi

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
384
1,000
Stiglers Gorge project katika bonde rufiji ingetengeneza megawatts zaidi ya 1500 ukijumlisha na current capacity ya hydro electric power generation pamoja na haka ka Gas inayotumika kwa umeme you tungekua self sufficient kwa umeme wa bei rahisi na kuachana na hawa walanguzi wanaotumia generator za mafuta na kuifanya Tz ya viwanda kua na uwezekano wa kweli.
Tatizo ni self interest mkimaliza tatizo la umeme wanene Wetu watakula wapi? Maana hizi symbion,iptl, Richmond ndiyo ulaji wenyewe

Hizi MW 1500 za huo mradi wa stigler gorge si haba.maana ni mradi upo nyumbani na utaendelea kuwepo.kuliko kuelekeza akili zetu zote kununua MW za mhabeshi.
 
asaprichie

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
281
250
kuna Mzungu alisema kwmb kwa gesi ile iliyoko mtwara tz inauwezo wa kugaia umeme nchi kubwa 5 na tz ya 6 kwa muda wa miaka 100 bila kukatika ata kdgo....sasa cjui alikua anandanganya au la
 
bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,769
2,000
sawa ni kweli Wahabeshi wanalo shirika la meli na wanazo meli za mafuta na mizigo. Shirika hili lina zunguka duniani na kupark meli zake katika bandari za nje na hasa Djiobuti kwani Eithiopia hawana Bandari ni land locked country.
kutika saini baina ya bandari ya Dar na shirika hilo jambo la kawaida. lakini ujaji wa Meli hizo itategemea mizigo ya Tanzania kwenda Eithiopia mfano Biashara za Viwanda za kwetu na mazao kama Pamba, Karafuu, Kahawa, Korosho na samaki ..kama watakua na soko huko uhabeshi basi meli hizo zitapakia kutoka Dar hadi Eithiopia kupitia Djiobuti.
Pia inaweza kusaidia kwa bidhaa za Eithiopua Kuingia Dar kwa urahisi kwa kutumia meli hizo kutoka Eithipia kuja Dar. Hii ndio faida itayopatikana.

lakini mkataba huu hautofanya Eithiopia Kushusha na kutumia mizigo ya Bandari ya Dar es salaam na kuisafirisha kwa gari kwa siku 15 kwenda eithiopia. Hilo halipo wala halita tokea ni ndoto kama ya April Fool.
Hivyo ipo faida kama nilivo eleza hapo juu ni kwa Watanzania kuangalia uwezekano wa kuingia Eithipia mfano bidhaa za Bakhressa za chakula zinaweza kwenda huko kwa kutumia meli hizo..
 
Bepari la bariadi

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
384
1,000
sawa ni kweli Wahabeshi wanalo shirika la meli na wanazo meli za mafuta na mizigo. Shirika hili lina zunguka duniani na kupark meli zake katika bandari za nje na hasa Djiobuti kwani Eithiopia hawana Bandari ni land locked country.
kutika saini baina ya bandari ya Dar na shirika hilo jambo la kawaida. lakini ujaji wao itategemea mizigo ya Tanzania kwenda Eithiopia mfano Biashara za Viwanda za kwetu na mazao kama Pamba, Karafuu, Kahawa, Korosho na samaki ..kama watakua na soko huko uhabeshi.
Pia inaweza kusaidia kwa bidhaa za Eithiopua Kuingia Dar kwa urahisi. Hii ndio faida itayopatikana.

lakini mkataba huu hautofanya Eithiopia Kushusha na kutumia mizigo ya Bandari ya Dar es salaam na kuisafirisha kwa gari kwa siku 15 kwenda eithiopia. Hilo halipo wala halita tokea ni ndoto kama ya Aril Fool.
Hivyo ipo faida kama nilivo eleza hapo juu ni kwa Watanzania kuangalia uwezekano wa kuingia Eithipia mfano bidhaa za Bakhressa za chakula zinaweza kwenda huko kwa kutumia meli hizo..

Daah wee jamaa yaani bakhressa apakie bidhaa zake kwenye meli za ethiomzi zitakakuwepo pale bandari ya Dar .harafu meli hizo hizo zishushe mzigo hapo hapo Dar kuwaajili ya kusafirishwa sijui kwa ndege kwenda addis ababa.hii haijawahi tokea duniani aisee.labda sijakuelewa.
 
bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,769
2,000
Daah wee jamaa yaani bakhressa apakie bidhaa zake kwenye meli za ethiomzi zitakakuwepo pale bandari ya Dar .harafu meli hizo hizo zishushe mzigo hapo hapo Dar kuwaajili ya kusafirishwa sijui kwa ndege kwenda addis ababa.hii haijawahi tokea duniani aisee.labda sijakuelewa.

asiejua maana haambiwi jawabu soma tena nilicho andika utaelewa...sio kila kitu utemewe kama makinda ya ndege
 
bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,769
2,000
Daah wee jamaa yaani bakhressa apakie bidhaa zake kwenye meli za ethiomzi zitakakuwepo pale bandari ya Dar .harafu meli hizo hizo zishushe mzigo hapo hapo Dar kuwaajili ya kusafirishwa sijui kwa ndege kwenda addis ababa.hii haijawahi tokea duniani aisee.labda sijakuelewa.

nime edit kidogo upate faida
 
Fais12

JF-Expert Member
Jan 31, 2017
284
250
sawa ni kweli Wahabeshi wanalo shirika la meli na wanazo meli za mafuta na mizigo. Shirika hili lina zunguka duniani na kupark meli zake katika bandari za nje na hasa Djiobuti kwani Eithiopia hawana Bandari ni land locked country.
kutika saini baina ya bandari ya Dar na shirika hilo jambo la kawaida. lakini ujaji wa Meli hizo itategemea mizigo ya Tanzania kwenda Eithiopia mfano Biashara za Viwanda za kwetu na mazao kama Pamba, Karafuu, Kahawa, Korosho na samaki ..kama watakua na soko huko uhabeshi basi meli hizo zitapakia kutoka Dar hadi Eithiopia kupitia Djiobuti.
Pia inaweza kusaidia kwa bidhaa za Eithiopua Kuingia Dar kwa urahisi kwa kutumia meli hizo kutoka Eithipia kuja Dar. Hii ndio faida itayopatikana.

lakini mkataba huu hautofanya Eithiopia Kushusha na kutumia mizigo ya Bandari ya Dar es salaam na kuisafirisha kwa gari kwa siku 15 kwenda eithiopia. Hilo halipo wala halita tokea ni ndoto kama ya April Fool.
Hivyo ipo faida kama nilivo eleza hapo juu ni kwa Watanzania kuangalia uwezekano wa kuingia Eithipia mfano bidhaa za Bakhressa za chakula zinaweza kwenda huko kwa kutumia meli hizo..
Asalam
Ndugu maelezo yako ni mazuri na ya kueleweka kabisa. Si kama ya wachangiaji wengine wanaosema ndege ndio sitazochukua mizigo na hawajui ya kwamba ndege inachukua vitu vyenye uzito mdogo na hivyo sifikirii kwamba vina market kubwa huko ethiopia. Na hii fikra ya tz kuwa hub ni ndoto ya mchana kweupe.
 
doama

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
761
1,000
Cha muhimu si wingi wa meli bali ni ushawishi wa wafanyabiashara kwenda nje kununua bidhaa kwa wingi.

Btw say sasa hivi wafanyabiashara wengi wamepunguza importation kwakuwa hawana imani na maamuzi ya badae kutoka mamlaka.

Kuna watu walikua kipindi cha nyuma anaagiza kontena mpaka 30 kwa wakati mmoja lakini siku hizi anakwambia anaagiza kontena 3 angalia hilo gap hapo kisa anasema tra hawaeleweki kwenye tozo zao.

Kwa mfanyabiashara yeyote ili upate faida kubwa unategemea mauzo ya aina mbili;

(i) Uuze kwa bei ya juu sana ambapo effect yake ni kukaa na mzigo kwa muda mrefu sana na hivyo hiyo faida itakuchukua muda mrefu sana kuipata kwa sababu ya bei ya juu ya uuzaji.

(ii)Uuze kwa bei ya chini, nafuu ambayo utauza mali nyingi zaidi kwa kipindi kifupi sana na utapata faida kubwa sana kwa muda mchache, na hapa ndipo logic nzima ya profit maximization ilipo

Nimesema haya kwa sababu serikali inafanya biashara hapo bandarini na wateja ndio hao wanaoagiza bidhaa Uchina, Japan, Uarabuni na kwingine duniani.

Ikipunguza ushuru logically hata mimi mwezi huu ningeuza gari yangu niagize nyingine. We imagine kwamfano ushuru wa salon car ya Cif milioni nane ni shilingi milioni 9 yani imezidi bei ya manununuzi. Lakini inabidi nisubiri miaka mitatu ndo niagize gari nyingine. Sijui wasomi wetu huko mnaishauri vipi serikali?
Mi sina hata degree lakini ninawaza serikali yangu ina madaktari na maprofesa ambao mchango wa mawazo yao ni hasi
 
Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,303
2,000
Jana nilimsikiliza Ndugu rais akielezea wachoongea na waziri mkuu wa ethiopia.ikiwa nipamoja na Tanzania kununua umeme kutoka ethiopia kwa minajili ya kwamba bei yao ni nafuu.kwa hili hatakama wangekuwa wanatoa bure siyo kitu cha sisi kama watanzania kufurahi.kikubwa ni sisi tuanza kuzalisha umeme wetu unaotokana na mazingira yetu na kuuza kwa wateja kwa bei rahisi.kwanini wao wwamewezakwa hili hapana aisee.tujijenge uwezo wetu bwana.siku nyaya hizi zitakazo pitia kenya zikakatwa iitakuwaje
Pia from Tz to Ethiopia ni mbali aisee.labda kuna technologia ya wireless.

Suala la pili ni hili la ethiopia kwa kuwa ni landlocked country eti inampango wa kutumia bandari ya Dar. Hivi kweli from ethiopia to Eritrea, Djiboutsomalia Egypt and Kenya. Despite ya usalama wa nchi husika.

Je nikweli kuna feasibilty ya jambo hili la Addis Abbaba kupokea mizigo yake kutokea Dar es salaam.

Sometime tuache akili zetu zitafakari bila la kuathiriwa na ukada au unazi wa vyama fulani
Safari ya kiongozi huyo (waziri mkuu) toka Ethopia ilikuwa ni kama danganya TOTO.
Namaanisha kwamba ujio wa kiongozi huyo kila kitu kilikwisha pangwa...
Kifupi ilikuwa ni ziara ya KISIASA iliyokuwa na malengo yaleyale ya MKUU WETU WA NCHI....Kutengeneza headline katika kurasa za mbele za Magazeti kutafuta KIKI.....

Ni kwa wale wasioelewa mambo yanavyokwenda ndio wataamini kile alichosema MTUKUFU...

Swali la kujiuliza ni umbali gani tulionao kutoka ETHOPIA hadi TANZANIA....!!

Ni nchi gapi tumezivuka..!? Ama ni zipi ziko karibu zaidi mfano Msumbiji....Zimbabwe...Uganda.. nchi zote hizi zinauza umeme wake nje..

Kama kweli MTUKUFU anamaanisha kile anachoongea..ni kweli haoni ugumu wa mradi huo kuweza kuwa REALITY na sio siasa zenye lengo la kutuhadaa wananchi kwamtindo uleule wa TANZANIA YA VIWANDA wakati hakuna dalili chembe za utekelezaji...!?

Kweli mtukufu wewe ni MSEMA KWELI lakini kwa hili la kutandaza MAGUZO....NYAYA na "MATRANSIFOMA" kutoka ETHOPIA hadi TANZANIA naona ni kama ndoto za ALINACHA......

Nakutakia kila la kheri MKUU WA NCHI na KWAREZIMA njema....

Tujifunze kusema ukweli kwa yale yanayowezekana.
 
clever two

Member
Jan 19, 2017
44
95
Jana nilimsikiliza Ndugu rais akielezea wachoongea na waziri mkuu wa ethiopia.ikiwa nipamoja na Tanzania kununua umeme kutoka ethiopia kwa minajili ya kwamba bei yao ni nafuu.kwa hili hatakama wangekuwa wanatoa bure siyo kitu cha sisi kama watanzania kufurahi.kikubwa ni sisi tuanza kuzalisha umeme wetu unaotokana na mazingira yetu na kuuza kwa wateja kwa bei rahisi.kwanini wao wwamewezakwa hili hapana aisee.tujijenge uwezo wetu bwana.siku nyaya hizi zitakazo pitia kenya zikakatwa iitakuwaje
Pia from Tz to Ethiopia ni mbali aisee.labda kuna technologia ya wireless.

Suala la pili ni hili la ethiopia kwa kuwa ni landlocked country eti inampango wa kutumia bandari ya Dar. Hivi kweli from ethiopia to Eritrea, Djiboutsomalia Egypt and Kenya. Despite ya usalama wa nchi husika.

Je nikweli kuna feasibilty ya jambo hili la Addis Abbaba kupokea mizigo yake kutokea Dar es salaam.

Sometime tuache akili zetu zitafakari bila la kuathiriwa na ukada au unazi wa vyama fulani
Baba yenu ndo mwisho wa akili yake umeishia hapo, anatufanya wote kina bashite
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,180
2,000
Huu ni uongo mkubwa sana!Geographical position ya Ethiopia hawezi ku allow waje kutumia bandari ya TZ!
Kwa nn wasitumie Djibout au Mombasa au hata Sudan ambapo ni pafupi sana?
Mbona Rais alituambia TZ itaanza kuuza umeme nchi za jirani soon?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom