Kwa haya ya kununua umeme toka Ethiopia na Ethiopia kutumia bandari ya Dar es Salaam, nasema hapana

Achana na hao vibaraka wa wazungu mtambo wa umeme wa Richmond ukibebwa toka marekani kilomita zaidi ya laki moja kuja kutuibia hapa wanaona sawa lakinikulete umeme toka Ethiopia kilometa zisizozidi 5000 sio sawa. Mkuu hao wanaopinga ni vibaka na mawakili wa vibaka usipoteze nao muda
Inaonyesha kabla viroba havijapigwa marufuku ulikuwa umejiwekea akiba ya kutosha. Hivi unalinganishaje gharama ya kusafirisha mizigo na kuunganishwa umeme kutoka sehemu moja mpaka nyingine?
Mwambie Magufuli sasa zile ndege zitakazokuwa zinabeba mizigo ya Ethiopia kutoka bandari ya Dar ndizo hizohizo zitumike kusafirisha umeme kutoka Ethiopia kuja Tanzania
 
Kweli kabisa.bora tukope pesa za kujenga hydroelectric power yetu.kuliko kukopa fedha ili tununue umeme kutoka ethiopia.haya mawazo sijui yametoka wapi tu.

Mkuu ungezungumzia umeme unaozalishawa na Nuclear Power Reactors, Geothermal, Mkaa wa mawe hapo ningekuelewa - kwa nini nasema hivyo: Mkuu umesahau crisis ya kupungua maji kwa kiwango kikubwa katika mabwawa yetu ya kuzalisha umeme huko Mtera na Kihansi, kama tusingekewa na Gasturbine engine driven Generators pamoja na Internal Combustion Engines as prime movers za kulazisha umeme huko Tegeta unafikiri tungekuwa wageni wa nani as a Nation tungekwama kweli kweli - je, unajua I.C engines zilikuwa zinakula lita ngapi za Heavy Oil kwa siku? Taifa lilipoteza fedha kiasi gani kuagiza mafuta including capacity charges za wamiliki mitambo ya kuzalisha umeme? Tulipigwa pesa kweli kweli au umesahau scandal za masuala ya EPA.

Mkuu kumbuka hakuna Serikali yenye watu wenye akili timamu inaweza kuruhusu tena Taifa letu kujingiza kwenye jehanamu ya kutegemea sana uzalishaji wa umeme kwa kutumia nguvu za maporomoko ya maji, tumekwisha pata somo the hard way hatuwezi tena kurudia makosa hayo hayo siku za usoni - ndiyo maana na insist Serikali itafute source nyingine ambazo ni reliable - sina shaka Dk.Magufuli na washauri wake walipo kutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia suala la umeme lilipewa kipa umbele for a good reason namely once beaten twice shy, hatuwezi kuzungumzia masula ya Viwanda bila ya kuwa na umeme wa kuaminika na wa kiwango cha kukidhi peak demand, umeme unoa zalishwa kwenye mto wa Blue Nile huko Ethiopia ni wa kuaminika sana kutokana na sources zinazo feed Lake TANA kuwa nyingi sana.
 
WATANZANIA HATUNA AKILI HIVI KUTOKA MTO RUFIJI MPAKA DSM KM 100 HALAFU UNAKWENDA KUCHUKUA UMEME MAILI 10020000000?TUMEWAACHIA MAMBA WANAOGA TU
 
Jana nilimsikiliza Ndugu rais akielezea wachoongea na waziri mkuu wa ethiopia.ikiwa nipamoja na Tanzania kununua umeme kutoka ethiopia kwa minajili ya kwamba bei yao ni nafuu.kwa hili hatakama wangekuwa wanatoa bure siyo kitu cha sisi kama watanzania kufurahi.kikubwa ni sisi tuanza kuzalisha umeme wetu unaotokana na mazingira yetu na kuuza kwa wateja kwa bei rahisi.kwanini wao wwamewezakwa hili hapana aisee.tujijenge uwezo wetu bwana.siku nyaya hizi zitakazo pitia kenya zikakatwa iitakuwaje
Pia from Tz to Ethiopia ni mbali aisee.labda kuna technologia ya wireless.

Suala la pili ni hili la ethiopia kwa kuwa ni landlocked country eti inampango wa kutumia bandari ya Dar. Hivi kweli from ethiopia to Eritrea, Djiboutsomalia Egypt and Kenya. Despite ya usalama wa nchi husika.

Je nikweli kuna feasibilty ya jambo hili la Addis Abbaba kupokea mizigo yake kutokea Dar es salaam.

Sometime tuache akili zetu zitafakari bila la kuathiriwa na ukada au unazi wa vyama fulani

Ethiopia wamejenga SGR au standard gauge railway kwenda Djibouti kwa sababu ya bandari kule Djibouti baada ya sababu za kidiplomasia na kiusalama kuacha kutumia bandari ya Asmara, Eritrea. Hata bandari ya Mombasa kwao ni tatizo bado na ndiyo maana kuna mpango wa LAPSET wa Ethiopia na Kenya kujenga bandari kubwa ya kisasa pale Lamu nchini Kenya kwa ajili ya mizigo ya Ethiopia na Sudan kusini.
Kwa haya inaonyesha kabisa kutumia bandari ya Dar Haiwezekani kiufanisi na kigharama kwa sababu ya umbali na miundombinu mibovu.
Awamu ya tano ni wapuuzi tu
 
Well said mkuu, kwa bahati mbaya baadhi ya Watanzania wako hivyo, kwao kila kitu akisemacho JPJM kina walakini, na ukichunguza kwa umakini utakuta the most vocal ufahamu wao kuhusu masuala ya biashara, teknolojia, utengamano kwao ni sawa sawa na hakuna, wanafikiri Rais kakurupuka tu kutoa tamko - they can't figure out umeme unawezaje kutoka Ethiopia kuja Tanzania and vice versa au Mizigo ya Ethiopia kutoka Bandarini na kusafirishwa kwa Cargo planes kwenda Adis!!

Cargo planes hao Ethiopia wanaagiza stationary tu peke yake? Wanadevelop project ya Lapset na Kenya kujenga bandari ya Kimataifa Lamu, Kenya, hata Mombasa tu kwao ni mbali wanatumia Djibouti, Dar wapi na wapi. Hatuko hapa kubishana so usitafute uhalali wa kila tamko la viongozi hawa, angalia uhalisia kama mfanyabiashara na mwekezaji nchini Ethiopia, na angalia harakati gani zinafanywa na serikali yao Kuweka mazingira ya kukuza biashara na uchumi wao kwa kushusha gharama za usafirishaji n.K cargo plane inabeba maziwa,nyama, maua,samaki etc na hivi vyote vinapatikana Kenya kiurahisi kuliko hapa
 
Kwa mawazo yako unataka kutwambia Waziri Mkuu wa Ethiopia na Dk.Magufuli hilo hawalijui wamekurupuka tu kufurahisha wananchi?

Hivi umejiuliza inachukua muda gani kusafirisha mzigo by freight trains kutoka bandari ya Djibouti kwenda Adis, na je, Air Cargo planes zinachukua muda gani kutoka uwanja wa ndege wa Dar kwenda Ethiopia? JPJM amesema mizigo itabebwa na ndege za mizigo na siyo malori au freight trains, bila shaka wana sababu za maana kufikia uhamuzi huo - tusijifanye wajuaji kuliko wahusika wenyewe - kumbuka Ethiopia imeanza biashara ya usafiri wa anga tangu 1930s na bado wanadunda kama kawa, watu wenye uzoefu wa zaidi miongo saba awawezi kufanya biashara ambayo hailipi.
Ethiopia ni mfanikiwa kwa nadharia, kwanza tutapeleka ndege zetu kwa matengenezo kisha watatuuzia umeme ambao utatudumaza akili zetu kwa miongo kadhaa. Kuhusu suala la mizigo labda Serikali tu lkn kwa mfanyabiashara hawezi Ku afford gharama kubwa ya usafiri labda km watapitisha pasipo ushuru. Siku zote wafanyabiashara wanaangalia faida na sio sifa ya mahusiano. Kwa suala hili ni sawa sawa na wewe uishi Morogoro ukashushie mzigo wako Mombasa huku ushuru na ufanisi wa port zote unafanana.
 
Cargo planes hao Ethiopia wanaagiza stationary tu peke yake? Wanadevelop project ya Lapset na Kenya kujenga bandari ya Kimataifa Lamu, Kenya, hata Mombasa tu kwao ni mbali wanatumia Djibouti, Dar wapi na wapi. Hatuko hapa kubishana so usitafute uhalali wa kila tamko la viongozi hawa, angalia uhalisia kama mfanyabiashara na mwekezaji nchini Ethiopia, na angalia harakati gani zinafanywa na serikali yao Kuweka mazingira ya kukuza biashara na uchumi wao kwa kushusha gharama za usafirishaji n.K cargo plane inabeba maziwa,nyama, maua,samaki etc na hivi vyote vinapatikana Kenya kiurahisi kuliko hapa

Nilicho eleza mwanzo ilikuwa ni kama pre amble, nikiwa na lengo la kuwashauri Watanzania wenzangu tuachane na tabia inayo anza kuota mizizi ya kuchukulia kila kitu kinacho fafanuliwa/tendwa na Serikali ya awamu ya tano kina walakini, hakuna kitu +ve mnacho zungumza kuhusu juhudi ya JPJM na washauri wake - amefanya mambo mangapi ya kujivunia ndani ya mwaka mmoja wa uongozi wake - mengi tu, sasa mnashindwa nini kuamini au kuchukulia seriously makubaliano ya Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais Magufulini - ina maana sisi watu baki tuna akili zaidi na weledi kuliko Viongozi hao wawili au? - tell ME!!

Hapa chini nimebandika tena majibu yangu geared for skeptical mwenzako ambaye hana imani na mipango ya ya awamu ya tano:

M'bang'ang'walu said:
Kwani hiyo mizigo itakuwa inazalishwa hapa TZ? Yaani mizigo itoke huko itokako, ibebwe kwa meli mpaka TZ, Kisha ibebwe kwa ndege tena mpaka Ethiopia. Akili hiyo hata mtoto wa chekechea hawezi kuwa nayo
Hivi unajua gharama za kusafirisha mizigo kwa njia ya anga zikoje? Watu wasingekuwa wanatumia muda mrefu kwa kutumia usafiri mwingine. Jiulize kwa nini hao Ethiopia wasitumie ndege kubeba hiyo mizigo kutoka huko itokako. Halafu mizigo mingi ni ya watu na makampuni binafsi, kwa serikali haiwezi kuwalazimisha watu washushie mizigo yao Tanzania


Mambo mengine tujaribu kuchangamsha akili zetu kidogo kwa ku-analyse mambo in 3Ds, unawezaje ku-equate akili za Waziri Mkuu wa Ethiopia na Rais wetu pamoja na washauri wao kwamba akili zao hazina tofauti na za watoto wa chekechea - hizi dharau aziwezi kutufikisha popote, our leaders knows wanacho kitaka/ kifanya kwa maslahi ya Taifa letu - wajibu wetu ni kuwatia moyo na siyo kuwa bezabeza!!!

Tatizo la baadhi yetu ni obsession ya kukosoa kosoa everything 'Magufuli' sijui hii inatokana na chuki binafsi au nini, hawana time ya ku-analyse mambo wakiwa na akili zilizo tuliazana - mihemuko tu masaa yote.

FYI wa Ethiopia watajenga depot ya mizigo yao hapa Dar, kuhusu Mizigo itapatikana wapi na kwa nini wamefikia hatua ya kuhamua kufanya hivyo, hayo sisi hayatuhusu, Wahabeshi wana uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya usafirishaji, badala ya kushukuru kuhusu ujio wao ambao uta create employment, Serikali itapokea kodi na Dar itakuwa HUB ya kusafirisha mizigo kwenda kwa nchi zinazo tuzunguka and beyond hii ni catalyst tosha ya kuinua Economy ya Taifa letu hayo yote wala nyinyi hamuyaoni!!
 
Kweli akili za watanzania ni hovyo kuna watu wanamtetea rais kwa uamuzi wake wa kununua umeme kutoka ethiopia,kwa nini tusijiulize haya
1.Katika sera ya serikali ya CCM ilituaminisha kuwa nara mradi wa gas utakapoisha tutazalisha zaidi ya megawati 3000 ziko wapi hizo megawati????
2. Kuna muda mwingine hatupo makini miradi mingi ya umeme imisha anzishwa hapa nchini miradi hiyo uite iko wapi na mbaya zaidi imetumia fedha nyingi sana
3.Hivi kweli tanzania ni ya kununua umemr ethiopia pamoja na vyanzo lukuki tulivyonavyo tunazidiwana ethiopia ambayo ni nchi ya ukame,mradi wa umeme wa ethiopia wanatumia maji ya mto naili ambayo maji yake yanatoka ziwa victoria.eneo kubwa la ziwa victoria karibu 3/4 lipo tanzania-kwa kweli haya ni maigizo
4. Tukirudi kiuchumi-unawezaje kuendesha nchi ya viwanda kwa umeme wa kununua
Namba tatu ni uonga.
1. Maji yanayozalisha umeme Ethiopia HAYATOKI TANZANIA

2. Tanzania inamiliki takriban 49% ya ziwa siyo 3/4.
 
Swali ni kwa nini ununue umeme ethiopia huku wewe una vyanzo lukuki vya umeme-mradi wa umeme wa ethipia ulianza kwa kukopa pesa nadhani ilikuwa bank ya dunia kws nini na sisi tusifanye hivyo???
Ethiopia walinyimwa mkopo na WB. Fuatilia. Ilibidi watu wafe bwawa lijengwe.

Hoja zako zinakosa mashiko kwa sababu unaongea uongo uongo mwingi. Kama huna uhakika na jambo usilitaje. Ungeishia ti kuiliza kwanini kununua umeme wa waabeshi na si kutaja na mengine ya uongo.
 
Mkuu ktk nia nzuri ya kumsaidia Mh. Ktk ujenzi wa taifa nitakupatia stori ya kisiwa kimoja huko Scotland, ni vipi wameweza kupambana na tatizo la umeme, Na njia gani wametumia mpaka kufanikiwa kuzalisha umeme wao nje ya national grid supply yaani kama hii yetu Tanesco kwa kutumia renewable energy.

Eigg ni kisiwa kidogo chenye wakazi wasiozidi 150, yenye eneo za mraba zisizozidi 30, wakazi wa kijiji hiki kwa ushirikiano wao binafsi wameweza kuliondoa tatizo la umeme kwa zaidi ya asilimia 95.

Hawa wanakijiji wameunda kampuni yao binafsi ya kutengeneza umeme kwa kutumia vitu amabvyo sio vingeni kwetu, Jua, upepo na maji au renewable energy to be precise.

Kumbuka kwamba hicho kijiji utokaji wa jua ni mdogo sana kwa mwaka mara nyingi ni wakati wa kiangazi kwa muda wa miezi isiozidi mitatu, upepo wao haufikii wa Tanzania Na mito yao sio yenye ukubwa Na nguvu kama yetu sisi hapa Tanzania. Lakini wameweza kudunduliza umeme kutoka sources zote tatu, Yaani jua, maji Na upepo wakauingiza kwenye community grid Na Kusambaza kwa wakazi Na biashara zao, kwa bei ya chini kabisa.

Watu wa nchi mbali mbali wameshapitia kwenye hichi kisiwa kutaka kufahamu, how they did it, Yaani mpaka Malawi imeshapeleka team Scotland kufanya preliminary studies and fact findings, Yaani Mh. hii Malawi inatupiga bao la mkono siku zote. Lol

Sasa tuje kwa upande wetu,

Naelewa wazi kwa Tz, pesa ya kufanya yote haya hatuna lakini kama serikali itakua smart and willing to innovate, wanaweza kuanzisha hata pilot system on renewable energy in partnership Na private sectors, finding strategic village somewhere ukiondoa chato, lol, and do the right thing, i.e. Community grid of some sort, replicating what's these villagers did in solving their problems, and do exact the same to one of our village by self financing, charging the community at subsidised rate.

In this way once successfully, we will encourage private sectors to enter in some sort of partnership with the government in doing the same for other places.

There is no harm trying Mh.

Second solution, and this can be done now! Let the hybrid technology go mainstream, i.e. Combination of both, electricity generated using solar panels in our roof tops and that coming from the national grid, i.e. tanesco.

The government can help by zero rated on VAT and import charges for a certain period of time to encourage the residents particularly from urban areas to go hybrid.

Tanesco can be given the outright monopoly for now, only for now! I insist, until the understanding of the technology become main stream, regulating technological competency through training and after service sales, this way will create more businesses and encourage innovations.

Allowing colleges with subsidised cost by providing tax incentives to teach our children on renewable energy technologies, in order to make us competency, innovative and renewable in some sort.

You never know, we might have our own wind turbine industry, si ndio sera za Mh, viwanda viwanda, and we will start selling the technology and know how to neighbouring countries.

Mh. Nakuomba uwaalike maintenance team ya community electricity grid kutoka Kisiwa cha Eigg Scotland, ambapo wako watatu mmoja muuza mikate, mmoja mfumaji Na mwengine analima bustani. Hawa watatufunza kitu, achana Na Ethiopia, majibu ya matatizo ya umeme yako nje ya magogoni Na upepo huo.

Halafu yale mahela ya maboeing ahirisha ununuzi, finance hii project ukisaidiana na wanakijiji wa Eigg Scotland.

The small Scottish isle leading the world in electricity
Unayoyasema yamefanyika hapa TZ kipindi cha Jakaya. REA wana facilitate hizo community projects. Tembelea maeneo ya jimbo la marehemu filikunjombe kuna miradi mingi tu ya mini-hydro na wanavijiji wanafaidi.
 
Nyie lumumba mburulaazz kweli, issue hapa ni umbali!! Hivi unajua unapita nchi ngapi ili ufike Ethiopia? Sasa hapo zenj na dar kuna umbali gani? Uta manage vp hiyo transmission? Sizonje akiwadangaya kuwa atanunua umeme Ethiopia na wao watatumia bandari yetu kupitisha mizigo mnafuraaaaahhiiiii!!!!!! Kweli nyie nyumbu!!!!
Umbali ndiyo nini? Kwa taarifa yako nchi za SADC wanautaka huo umeme wa Ethiopia.

Hivi unakumbuka ujenzi wa laini za umeme za 400 Kv kutoka Iringa hadi Arusha na Shinyanga? Umefuatilia kwanini huo mradi ulipewa kipaumbele?

Ni kwamba nchi za waafrika weusi zimeanza kufanya kitu inaitwa GRID INTERCONNECTION. Kila mtu atazalisha na kuuza ziada kwenye gridi kwa mwenzie atakayekuwa anahitaji. Mfano Ethiopia wanazalisha ziada inatumiwa Swazland.

Umbali is nothing on this. Unaijua grid ya USA au Canada? Ni ndefu kiasi gani?
 
Hapa Tanzania tuna vyanzo vingi sana vya kuzalisha umeme sema tu nchi imetawaliwa na mihemko ya kisiasa.
Sioni umuhimu wa kununua umeme toka Ethiopia kwa sababu gharama itakayotumika kujenga njia ya kusafirishia umeme haitakuwa tofauti sana na itakayotumika kujenga power generation hapa nchini.
Kama vipi anaepingana na hili twende kihesabu na kitaalam zaidi ndio tupate jibu kuliko kubishana pasipo jibu.
Njia tayari imejengwa kaka. Hukumbuki line ya 400kv? Tembelea maandiko ya TANESCO.

Halafu kila nchi inajenga upande wake. Kenya wanajenga kwao. Tunakutana mipakani.
 
Jana nilimsikiliza Ndugu rais akielezea wachoongea na waziri mkuu wa ethiopia.ikiwa nipamoja na Tanzania kununua umeme kutoka ethiopia kwa minajili ya kwamba bei yao ni nafuu.kwa hili hatakama wangekuwa wanatoa bure siyo kitu cha sisi kama watanzania kufurahi.kikubwa ni sisi tuanza kuzalisha umeme wetu unaotokana na mazingira yetu na kuuza kwa wateja kwa bei rahisi.kwanini wao wwamewezakwa hili hapana aisee.tujijenge uwezo wetu bwana.siku nyaya hizi zitakazo pitia kenya zikakatwa iitakuwaje
Pia from Tz to Ethiopia ni mbali aisee.labda kuna technologia ya wireless.

Suala la pili ni hili la ethiopia kwa kuwa ni landlocked country eti inampango wa kutumia bandari ya Dar. Hivi kweli from ethiopia to Eritrea, Djiboutsomalia Egypt and Kenya. Despite ya usalama wa nchi husika.

Je nikweli kuna feasibilty ya jambo hili la Addis Abbaba kupokea mizigo yake kutokea Dar es salaam.

Sometime tuache akili zetu zitafakari bila la kuathiriwa na ukada au unazi wa vyama fulani
Where is a hope to obtain/harness electricity based on mutwara gas projects?
Maana mliwapiga sana na lengo mojawapo lilikuwa ni ufuaji umeme kama sikosei?
 
Back
Top Bottom