13 December 2023
Dar es Salaam, Tanzania
SERIKALI YAKABIDHI ENEO LA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM KWA BANDARI YA DAR ES SALAAM BAADA YA MRADI WA EPZA KUFELI
Eneo lililokuwa maalum kwa uwekezaji chini ya Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) lakabidhiwa kwa bandari ya Dar es Salaam iliyo chini Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA . Eneo hili mwanzo lilitwaliwa na serikali kuwa eneo maalum la uwekezaji wa viwanda
HISTORIA YA ENEO LA EPZA
View: https://m.youtube.com/watch?v=26a9s9_qaog
Waziri Prof. Kitila Mkumbo anaelezea makubwa kama maji, umeme na barabara ili kubadilisha eneo hili kuwa la mfano kimataifa kuwa Kurasini Logistic Centre na Industrial Park kuwa mtaa wa viwanda Business Centre Kurasini.
Bidhaa za kieletroniki zitaunganishwa pia soko maalum la mazao ya Korosho, Chai na mbogamboga ili kuingia katika mfumo wa soko huru la bidhaa Afrika AfCFTA
Mwaka 2009 China na Afrika nchi 4 za kujengwa kituo cha Kimataifa cha Biashara na Logistics, Tanzania ilipochaguliwa ikaamua kutwaa eneo na kuwalipa wananchi kiasi cha bilioni 101 shilingi za kiTanzania kama fidia ya kuhama Kurasini.
2019 18 December
View: https://m.youtube.com/watch?v=7ga5SiU6fPY
WAZIRI INNOCENT BASHUGWA NA EPZA WAJIPANGA KWENDA SAMBAMBA NA RAIS MAGUFULI
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa ameongoza kikao cha bodi ya Wakurugenzi wa Kanda maalumu ya uwekezaji EPZA (Export Processing Zones Authority).Mhe. Innocent Bashungwa ndie Mwenyekiti wa bodi hiyo ya Wakurugenzi.Kikao hicho kimekuwa na malengo ya kuangalia dira na mwelekeo wa EPZA katika kutekeleza mkakati wa Serikali hususani hotuba ya Mheshimiwa Rais Magufuli aliyoitoa tarehe 12/12/2019 kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ambayo ilieleza mkakati wa nchi wa kujenga uchumi wa kati kupitia serikali ya viwanda kwa mwaka 2020 mpaka 2030.Pia bodi imejadili kuhusu ujenzi wa kituo cha kuchakata mazao katika kata ya Kurasini Dar es saalam. Mradi huo utachukua eneo lenye ukubwa wa ekari 61.87 ambalo litahusisha mitaa ya shimo la udongo, Mvinjeni na KiunganiPia bodi hiyo imeunda timu maalum ya kuandaa mkakati mpya ambao utaleta mabadiliko na sura mpya ya EPZA na kuangalia mikakati ya hotuba za Rais na mikakati ya SADC na Viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ili kujenga nchi yenye uchumi wa kati kupitia viwanda
MWAKA 2014
Awali mwaka 2014 serikali ya China kupitia kampuni ya Yiwu Pan-Africa International Investment Corporation na serikali ya Tanzania iliyowakilishwa na EPZA ziliingia mkataba kuanziasha mradi wa eneo maalum la uwekezaji.
Ujenzi wa mradi huo ulitazamiwa utagharimu Dola za Marekani milioni 400 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 660 ambazo zitagharimiwa na serikali ya China.
Tanzania kwa upande wake ilitoa ardhi na kulipa fidia kwa wakazi wa maeneo hayo ambayo yana ukubwa wa ekari 60.4 yaliyotengwa katika kata ya Kurasini ikihusisha mitaa ya Shimo la Udongo, Mivinjeni na Kiungani.
“Tunatarajia kituo hicho kuwa kikubwa Afrika ya Mashariki na kati, ninafuraha kuwajulisha kuwa fedha iliyokuwa imeahidiwa kwenye bajeti, tayari imewasilishwa katika mamlaka ya EPZA kwa ajili ya malipo,” alisema Dk. Kigoda mwaka .
Alisema katika mwaka wa fedha uliopita, serikali ililipa fidia kwa awamu mbili jumla ya Sh. bilioni 45, ambapo awamu ya kwanza zililipwa Sh. bilioni 25 na awamu ya pili zililipwa Sh. bilioni 20.
Alisema mradi huo utaleta manufaa katika nchi kwa kupata bidhaa mbalimbali kutoka China, kuongeza pato la nchi kupitia kodi, kupanua miundombinu katika eneo la mradi, pamoja na kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao hususan mazao ya kilimo na madini.“Mradi huu utatengeneza ajira za moja kwa moja takriban 25, 000,” alisema.
Waziri Kigoda aliongeza kuwa, kupatikana kwa fedha hizo kumetoa mwanya wa kukamilisha mradi huo utakaofanya eneo hilo kuwa kitovu kikubwa cha viwanda na biashara katika eneo la ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA), kwa wakati huo Bw. Adelhelm Meru, alisema tayari taratibu za malipo zimeshaanza na matarajio ni kuwa baada ya wiki mbili au tatu zoezi hilo litaanza.
Alisema ujenzi wa kituo unaweza kuanza baada ya miezi miwili baada ya zoezi la malipo kukamilika na baada ya taratibu muhimu nyingine kukamilika.
Naye Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda na Biashara, Janet Mbene, aliwatoa wasiwasi Watanzania na kusema kuwa kituo hicho kitakuwa na manufaa makubwa kwa nchi.Jumla ya wananchi 1020 wanatakiwa kuhama katika eneo hilo la mradi.
Chanzo: NIPASHE.

24 September 2021
Prof. Kitila akagua eneo la Uwekezaji Kurasini, EPZA yalikabidhi kwa SUMA JKT na BICO kuanza Ujenzi