Kwa haya ya kununua umeme toka Ethiopia na Ethiopia kutumia bandari ya Dar es Salaam, nasema hapana

Itakusaidia sana ukitumia akili yako kufikiria hata kuanzisha mradi wa kuku ili akili ifikiri jinsi ya kuwalisha kuku kila siku..usipoteze muda kufikiria mambo yaliyo nje ya uwezo wa akili yako.. ufahamu wa mambo ya biashara, teknolojia, utengamano wewe ni ZERO!

Mkuu:
Hivi wewe huu mradi/miradi ya kuku umeidharau sana, hadi kufananisha na mtu asiye kuwa na akili ndio wanao fanya hiyo kazi.
Unapaswa kupata ushauri nasaha, na
Waombe radhi wafugaji vinginevyo una matatizo ya asili.
 
Jaribu kufikiri kidogo, kutoka Djibouti mpaka Addis Ababa ni km 857 na kutoka Dar es salaam hadi Addis Ababa ni km 2370. Ni mfanyabiashara gani aache Djibouti aje bandari salama. Ni wakati wa kusubiri na kuona.

Sure, lets wait and see.
 
Kuna long na short plans katika projects za kimaendeleo,hivyo kusainiwa kwa mikataba yawezekana ni long plan katika Afrika ijayo ie 100 years later.

Si vibaya kuanza kutengeneza mazingira wezeshi ya namna ya kuimplement malengo ya siku zijazo.

Shabaha yetu iwe ni kuanza kutafakali kwa weredi na kufanya tafiti ili kushauri vizuri maono ya wakuu wetu.

Si vibaya kujilidhisha kwa maneno,lakini ni vyema wataalamu wetu wakafanya upembuzi yakinifu kwa plans zote na kuja na alternatives mbalimbali.

Tujifunze kushauri kwa kutoa alternatives ways kuliko kuponda na kuacha watu hewani bila majibu.

Hoja za umbali,usalama wa miundombinu,gharama na muda sio tatizo kuweza kupinga moja kwa moja na kama tutapinga IPI ni alternative iliyo bora na rahisi (mfano Umeme wa makaa ya MAWE,gesi,maji,jua,upepo,geothermal,nuclear au vyovyote),wapi ,lini na mahali gani panafaa.

Umeeleweka vizuri sana mkuu.congrants
 
Mahitaji ya umeme Tanzania umezidi maradufu 28% to 67.3%. Chanzo cha sasa cha gesi kitazalisha 2000MW hakiwezi kukidhi mahitaji ya walengwa wote, istoshe mkuu kacheza akili umeme wanaonunua kutoka kwa symbion na wengine ni ghali ao mkuu anataka kuwakacha akanunue kwa waethiopia. Mimi binafsi sidhani kama ni tatizo na Tanesco itapata faida kutoka na kupata umeme rahisi kutoka ethiopia. Ugumu utakuja kutengeneza powerline kutoka moyale (kenya/ethio border) mpka namanga (ken/tz border) ni kama 850-900km, hizo hela zitatoka wapi? Tz au ethio?

Kwa ethio kutengeneza depo yao ya mizigo mi nahisi ni kitu kizuri... serikali itapokea kodi, wananchi watapata ajira, wa tz watapata fursa ya kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani; hii yote itachochea uchumi wa Tanzania.

Sekta ya utalii ni kitu kizuri kwa Tz kuingia joint venture na ethio kwa sabb watatutangazia utalii wetu kwa kuwa ndege zao zinasafiri sehemu nyingi duniani

Huree Rais Magufuli.
 
Kati ya majirani wetu wa ovyo na wasio aminika na wenye tamaa ni Wakenya.

Kitu muhimu kama umeme kikipitia nchini mwao mbona watatutesa hawa manyang'au. Watatutesa mpaka tuimbe Poh!

Hivi huo umeme wa Stieglers Gorge project una gharimu kiasi gani kuupata mpaka tushobokee kununua umeme nchi ingine?

Na halafu hiyo itasababisha tusikae tuka tumia maji ya ziwa Victoria maana umeme wa Ethiopia chanzo chake hiyo Victoria. Maji yakipungua naamini yatasababisha upungufu wa umeme
 
Tukisema mkulu hana vision wala mission yoyote na nchi hii kuna watu wanakuja kutokwa na mishipa ya shingo kukaidi. Hata mtoto wangu aliye grade 7 hawezi kuwaza eti ethiopia ishushe mizigo yake bandari ya Dar, mmmh! Ushilawadu wa kiwango cha standard gauge. Hili ningeliamini kama tungekuwa na bandari kubwa kama hiyo anayoipiga danadana ya Bagamoyo.

Halafu vitu vingine vinahitaji simple logic tu, biashara hazifanwyi na Serikali, zinafanywa na watu binafsi. Mizigo pekee ambayo ethiopia inaweza kupitisha kutumia bandari ya Dar ni silaha tu, nothing otherwise.
 
Well said mkuu, kwa bahati mbaya baadhi ya Watanzania wako hivyo, kwao kila kitu akisemacho JPJM kina walakini, na ukichunguza kwa umakini utakuta the most vocal ufahamu wao kuhusu masuala ya biashara, teknolojia, utengamano kwao ni sawa sawa na hakuna, wanafikiri Rais kakurupuka tu kutoa tamko - they can't figure out umeme unawezaje kutoka Ethiopia kuja Tanzania and vice versa au Mizigo ya Ethiopia kutoka Bandarini na kusafirishwa kwa Cargo planes kwenda Adis!!
Mkuu naomba niku challenge uteleze kuhusu hayo uliyosema.

Mkuu kitoa hoja za kujibu hoja ni vema ukaonyesha ili tupate ufahamu

Pili, Watanzania ni watu wepesi sana kusahau. Kumbukumbu zinaonyesha serikali ya JK ilishatamka kuwa gesi itamaliza tatizo la umeme na kuwa na wa ziada kuuza nje. Je, mpango huo umeishia wapi?

Tatu, Ethiopia wanawezaje kutengeneza Dams za kutuuzia umeme tukiwa hatujafanya lolote Stiegler gorge na vyanzo vingine ambavyo Tanzania inavyo kwa wingi?
 
Reli ya Ethiopia inaenda mpaka Djibout lengo ni kusafirisha mizigo moja kwa moja. Sasa nashangaa uyu Rais wetu anasema Ethiopia wanataka kutumia bandari yetu,kwa akili za kawaida ni jambo la kushangaza kidogo.
Wameacha bandari zote uko mpaka waje Tanzania?

Unajua kasuku ana tabia moja, kumfurahisha bosi, anamuimbia anachopenda bosi apate kula yake!

Maisha yanaendelea!
 
Mahitaji ya umeme Tanzania umezidi maradufu 28% to 67.3%. Chanzo cha sasa cha gesi kitazalisha 2000MW hakiwezi kukidhi mahitaji ya walengwa wote, istoshe mkuu kacheza akili umeme wanaonunua kutoka kwa symbion na wengine ni ghali ao mkuu anataka kuwakacha akanunue kwa waethiopia. Mimi binafsi sidhani kama ni tatizo na Tanesco itapata faida kutoka na kupata umeme rahisi kutoka ethiopia. Ugumu utakuja kutengeneza powerline kutoka moyale (kenya/ethio border) mpka namanga (ken/tz border) ni kama 850-900km, hizo hela zitatoka wapi? Tz au ethio?

Kwa ethio kutengeneza depo yao ya mizigo mi nahisi ni kitu kizuri... serikali itapokea kodi, wananchi watapata ajira, wa tz watapata fursa ya kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani; hii yote itachochea uchumi wa Tanzania.

Sekta ya utalii ni kitu kizuri kwa Tz kuingia joint venture na ethio kwa sabb watatutangazia utalii wetu kwa kuwa ndege zao zinasafiri sehemu nyingi duniani

Huree Rais Magufuli.

Ukisemacho ni sawa.hebu tujiulize nikipi kilichowawezesha ethiopia kuweza kujenga hilo dam from blue nile.pamoja na kupata vikwazo kibao kutoka kwa Egypt.lakini wakaendelea tu.
Ukilinganisha na sisi ambao jiografia inanaturuhusu kwa kuwa na mito mingi tu ya maporomoko ukiachilia mbali vyazo vingine vya nnishatihili jambo mimi nadhani ni uthubutu tu.tujenge yetu kwa manufaa hata ya kizazi cha tatu.
 
Kati ya majirani wetu wa ovyo na wasio aminika na wenye tamaa ni Wakenya.

Kitu muhimu kama umeme kikipitia nchini mwao mbona watatutesa hawa manyang'au. Watatutesa mpaka tuimbe Poh!

Hivi huo umeme wa Stieglers Gorge project una gharimu kiasi gani kuupata mpaka tushobokee kununua umeme nchi ingine?

Na halafu hiyo itasababisha tusikae tuka tumia maji ya ziwa Victoria maana umeme wa Ethiopia chanzo chake hiyo Victoria. Maji yakipungua naamini yatasababisha upungufu wa umeme

Najaribu tu kuimageni sehemu ambayo miundo mbinu ya huo umeme utakapo pita.Kenyaaa!? Naombeni tusome alama za nyakati aisee.
And generally ni upuuzi kutegemea umeme wa kununua japo tunakila kitu.Mwenyezi Mungu atuhurumie.
 
Kama tu nchi za ukanda wetu hawana mategemezi makubwa na bandari yetu wataweza hao walio mbali na cc? na inakuaje kila mwaka unaisha umeme wa gesi hatuuoni? na huo umeme utakua unatumwa kwa bluetooth cjui maana naona kichaa kapewa rungu lake
 
Ningeshauri kabla Rais hajatoa matamko ajitafakari zaidi na zaidi. Sio lazima ukiongea na mtu jambo likafurahisha ubongo wakati huo huo ukaenda public. Wawape watu walio kwenye hizo field, na wafanyabiashara wafanye assessment kwanza. Haya majigambo ya mwendokasi tutavuna aibu
 
The president should not jump on anything that seems good at a moment. Vision shall guide us. Bila kuwa na dira mambo mengi anayoibua kila uchwao yatapingwa tu. Nchi haiendeshwi kiurahisi urahisi kwa ku-buy any idea that sounds good. Yapo mengi tu ya kupotezea ili tuweze kufanya yale yetu ya msingi. Mwanzoni tulikimbilia Rwanda, tukaaminishwa kuwa Rwanda inaleta wataalam wa IT. Sasa tunapewa mengine bila kupewa mrejesho wa hayo ya nyuma. How are we supposed to believe?
 
However, linking Africa should also be considered, but in a holistic way. Naamini ipo siku high speed trains zitalink cities za Africa. Umeme wa SA utatumika bongo nk. Lakini haya mambo yanahitaji long term plans.
Kwa sasa tutarajie second death of Air Tanzania. Reason: Hii merger kati ya Ethiopian Airline na Air Tanzania ambayo imejificha ndani ya hiyo inayotangazwa kama hub ya mizigo ni uongo. Ethiopian itakuwa na monopoly hapa Dar Airport on local and international routes. The hub business, just forget about it. It is just polishing the real business
 
mleta mada ameamua kupotosha watu kwa makusudi kabisa! hakuna sehemu raisi alisema tutatununua umeme ethiopia, bali alisema watashirikiana katika technolojia ya kuzalisha umeme wa maji!

wataalam wa huko watakuja hapa na wakwetu wataenda huko ethiopia.

jamaa kawakamata watu wengi hapa na wanaendelea kujadili uongo.

kama anabisha aweke clip tumsikiw wenyewe
Alisema tutanunua na ataanza na Megawatts 400, na zitakuwa zinaongezwa.
 
Back
Top Bottom