Kwa hatua niliofikia hivi sasa naona bora nife kwa maana nimefeli hatua zote katika maisha

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Ifikapo mwakani mwezi wa tatu nitakuwa natimiza miaka 36 na mpaka sasa nimefeli hatua zote muhimu katika maisha.

1.Hatua ya kwanza nina miaka 35 sina familia wala mtoto.

2.Hatua ya pili sina mwenza wa maisha, niliekuwa nae alinikimbia na kuniacha pangu pakavu kisa mwelekeo wa maisha.

3.Hatua ya tatu sina ajira inayoweleka wala shughuli inayoeleweka ya kuniingizia kipato hivyo naishi kwa kubahatisha.

4.Hatua ya nne mpaka sasa miaka 35 bado nipo nyumbani kwa ndugu ninaishi kwa wasiwasi kwa maana nikifukuzwa sina pakwenda.

5.Hatua ya tano sina asset yeyote ninayomiliki zaidi ya vyeti vyangu vya chuo na Nguo za kuvaa.

Ukweli ni kwamba kwa hatua niliofikia naona ni bora nife tuu nimeshangaika vya Kutosha hapa duniani nimekosa wa kunishika mkono kiukweli soon ndugu zangu najiua narudia tena najiua.
 
Man, tafuta wimbo wa Mwaipaja unaitwa NAIONA KESHO.

Hafu man, achana na kifo mzee, kuna maraia wana life gumu wewe hugusi ila wanafaiti hadi kesho.

Nina mfanyakazi mwenzangu ana matatizo kibao ya kifamilia mumewe kamuacha hafu kamzurumu assets zake kwakua walikua wanaandika jina la mwanaume, afu yeye ana faiti cancer ipo stage mbaya ameanza kwenda ocean road anaudhuria chemo sijio mionzi. Aisee. Ila ukikaa nae ana plan hadi za 2035 uko.

Nachokushauri kwa kuanza tu, usikae jukwaa la habari mchanganyiko kakae jukwaa la ajira na nafasi za kazi, kule utatoka kimaisha.
 
Mkuu tafadhali sana nakuomba hiyo ndoto ikatishe na usikate tamaa, duniani huwa kuna vitu huwa vinadumu na pia vingine havidumu kama hili la kwako ni moja ya mambo ambayo hayadumu.

Tadadhali share nasi elimu yako ni ya daraja ipi na unaishi hapa hapa dar au upo nje na huku kwa sasa?.

Natamani tufanye safari moja na wewe katika mahospitali uone watu jinsi walivyo na matatizo lakini wanamatumaini makubwa sana kuiko hili jambo lako na ni suala la muda tu litapita, shukuru Mungu kwa kila jambo na pia usikate tamaa.

Mimi kwa sasa mambo si mazuri sana na pia bado kuna watu wanahitaji msaada wangu light kama ningelikuwa nimewamaliza hawa ningejitahidi nikutafutie kijiajira walau ujishikishe ili maisha yaendelee.

Lakini pia je uwezo wa kufanya vibiashara vidogo dogo walau vya kutanua mawazo na connection zaidi ulishajaribu pia?

Wewe una nafasi kubwa sana ya kujibadilisha na ukaingia kwenye fani ambayo itahitaji muda mfupi kujibasilisha na ukaajirika kiurahisi kwa mujibu wa vyeti vyako.

Nakuomba sana mkuu uachane na hayo mawazo Mwenyezi Mungu akuepushe na huyo roho wa mauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu wewe ni msela wa manzese.hapo manzese kila siku maroli ya mazao yanaingia.manzese kuna wauza mitumba hapo,kuna kila aina ya fursa.
komaa tu utatoboa.ni kweli kama huna password hapa mjini maisha ni magumu.

ila kama riziki yako ipo Mungu ataipambanua ila sio kwa kukaa na kulalama ni mpaka upambane kiume.
Commando unakufaje kizembe!!.
 
Pambana Mkuu, kujinyonga ni kuonyesha umekosa mbinu ya kupambana.

Badili mtazamo wa kushindwa sijui mkosi na takataka kama hzo na maisha yataanza kubadilika pia. Ni kweli mjini bila mchongo ni pagumu na panakatisha tamaa.


AMKA NA TUMAINI, AMINI GIZA TOTORO NDIO MWANZO WA PAMBAZUKO.
 
Kuwaza hayo unayowazia ni kawaida kwa binadamu ila usifanye kweli. Maisha yana changamoto zake na unayopitia ndio hizo changamoto zenyewe.

Hebu fikiria kuna mwenzako ana mke na watoto 3 wote wanasoma, mke ni mgonjwa na yeye pia kapata ajali na kaachishwa kazi na ndugu wote wamemkimbia, ila ukikaa naye anaamini atafanikiwa tu. Mtu anaishi kuombaomba kwa marafiki. Ukijiua kwa hoja hizo utanisikitisha mno mbona ni nyepesi mno.

Toka hapo ulipo ingia mtaani tafuta kibarua hata zege ukisubiria kazi ya vyeti vyako.

Nikupe mfano wangu, nina vyeti mpaka vya nchi namba 1 duniani ila nilirudi nikakaa mwaka bila kazi ya maana ila nilijikuta nipo shamba nalima, nauza malimau na biashara ambazo kwa akili zetu za kibongo watu waliona nimerogwa ila mimi nilijua sijarogwa wala nini na nikiwasikiliza naenda kufa kijinga kisa vyeti na ukumbuke nilikuwa baba wa watoto 3 na nilikuwa nategemewa na wadogo zangu 2 mmoja chuo mwingine sekondari.
Natamani nikulaumu ila nataka nikuambie mwanaume lazima ukubali kupigana mpaka tone la mwisho.
 
Ifikapo mwakani mwezi wa tatu nitakuwa natimiza miaka 36 na mpka sasa nimefeli hatua zote muhimu katika maisha

1.hatua ya kwanza nina miaka 35 sina familia wala mtoto

2.hatua ya pili sina mwenza wa maisha niliekuwa nae alinikimbia na kuniacha pangu pakavu kisa mwelekeo wa maisha

3.hatua ya tatu sina ajira inayoweleka wala shughuli inayoeleweka ya kuniingizia kipato hivyo naishi kwa kubahatisha

4.hatua ya nne mpka sasa miaka 35 bado nipo nyumbani kwa ndugu ninaishi kwa wasiwasi kwa maana nikifukuzwa sina pakwenda

5.hatua ya tano sina asset yeyote ninayomiliki zaidi ya vyeti vyangu vya chuo na Nguo za kuvaa

Ukweli ni kwamba kwa hatua niliofikia naona ni bora nife tuu nimeshangaika vya Kutosha hapa duniani nimekosa wa kunishika mkono kiukweli soon ndugu zangu najiua narudia tena najiua
Mkuu hata kazi ya ulinzi umekosa au ndio unaogopa maneno ya watu ?
Au unasuburi kazi ya heshima na yenye mshahara mkubwa ?

Mimi ni mkristo, katika biblia Mungu anafundisha kwa mtu kuanza na ulicho nacho mkononi.
1. Yesu alibariki mikate 5 na samaki 2 maelfu wakala.
( Unadhani ni kwanini hakutoa chakula hewani tu )

2. Musa aliambiwa na Mungu,umeshika nini mkononi akasema fimbo, hiyo hiyo ikatenda muujiza kwa kugeuka nyoka.

Kwanza elimu ni maarifa ambayo unatakiwa kuwa na uwezo wa kuibadili na kuifanya vyovyote upendavyo. Ukiona elimu yako inamtegemea tena mtu fulani kuleta impact, shtuka mapema.

Nakusihi fanya chochote, anza na ulicho nacho. Nahisi huna tu taarifa sahihi.

Kama utahitaji ushauri zaidi, Inbox
Refer: Graduate ninayefanya kazi ya Ulinzi, niulize chochote kuhusu sekta hii

Naamini ninaweza kukushauri mengi maana:

1. Nimesoma chuo bila mkopo wala kulipiwa ada na yoyote na nikahitimu.

2. Nilienda field Dodoma huku nikiwa sina oa kyfikia wala pesa ila nilimaliza field, 2 months.

3. 2013 Nilitoka Mwanza kuja Dar nikiwa na Tsh mia hamsini mfukoni ( Tsh 150 ) 🤣🤣🤣 na mpaka leo nakaza ile ile💪💪💪
4. Nilipohitimu chuo niliyumba, nikaanza kufikiria kurudi home 🙄🙄 nikakumbuka maneno ya bibi "Wewe ni mtoto kiume, pambana"

So, jambo la msingi kama wewe siyo mbunifu IGA tu, au tumia watu.

Maisha ya mafanikio ni muunganiko wa vitu vidogo vidogo vinavyofanywa kila siku na kwa muda mrefu.
Ukianza Sasa utatoa nafasi kwa compound interest kufanyika in the long run hata kama unachofanya kitakuwa na maslahi kidogo.
 
Ifikapo mwakani mwezi wa tatu nitakuwa natimiza miaka 36 na mpka sasa nimefeli hatua zote muhimu katika maisha

1.hatua ya kwanza nina miaka 35 sina familia wala mtoto

2.hatua ya pili sina mwenza wa maisha niliekuwa nae alinikimbia na kuniacha pangu pakavu kisa mwelekeo wa maisha

3.hatua ya tatu sina ajira inayoweleka wala shughuli inayoeleweka ya kuniingizia kipato hivyo naishi kwa kubahatisha

4.hatua ya nne mpka sasa miaka 35 bado nipo nyumbani kwa ndugu ninaishi kwa wasiwasi kwa maana nikifukuzwa sina pakwenda

5.hatua ya tano sina asset yeyote ninayomiliki zaidi ya vyeti vyangu vya chuo na Nguo za kuvaa

Ukweli ni kwamba kwa hatua niliofikia naona ni bora nife tuu nimeshangaika vya Kutosha hapa duniani nimekosa wa kunishika mkono kiukweli soon ndugu zangu najiua narudia tena najiua
Hapana! Hapana! Usijiue! bado Kuna nafasi ya wewe kufanya vizuri!!hayo unayoyaona ni mapito tu!! na kila mtu huwa anamapito yake!! Nawakati mwingine mapito hutufanya tutafakari. Kuwa kwann nayapitia haya? wapi nimekosea nk! Chakwanza omba toba kwa Babayako wa mbinguni! Kisha omba msaada kwake!! maana ss wengine tutaishia na neno pole! Hivyo Anza na muumba wako, naamini milango mingine itafunguka!! usijiue tafadhali!!
 
Mkuu kuna aina mbili za laana,laana ya kujitamkia na laaana ya kutamkiwa,laana ya kutamkiwa huwa haina nguvu sana maana Mara nyingi hutoka kwa wale tuliowachukiza na kuwakwaza.

Sasa wewe ulichokiandika hapa ni laana ya kujitamkiaa,yaani unajilaani mwenyewe, hii laana ina nguvu sana na lazima huwa inatimia,ogopa kutamka mimi siwezi kitu Fulani ,au mim maisha mwangu sidhani kama nitamiliki kitu Fulani ,hapo unajimaliza mwenyewe

Nikusihi tu kuwa usikate tamaa,usiseme maisha ni magumu,maana naona unasimu na unahela ya kununua bando wakati kuna watu hata hela ya mlo mmoja hawana,so jipe moyo ,one day yes.
 
Back
Top Bottom