Huku mtaani kwa sasa hakuna mwanasiasa maarufu kuliko Makonda

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Sijui anatumia uchawi gani.
Sijui anatumia mbinu gani za kimedani.
Lakini huyu jamaa kwa sasa hakuna mwanasiasa yoyote ambaye anamsogelea kwa umaarufu hata kwa kilometa mia moja.

Kama ni riadha za siasa tunasema Makonda angeshatangazwa ndiye Mshindi kwa sababu tangu aingie kwenye riadha amewaweka wenzake wote pembeni na sio tuu pembeni bali mbali huko.

Jana kwenye Malumbano ya Hoja, ITV Makonda mbele.
Sokoni huko Makonda.
Bodaboda nao Makonda.
Kwenye Daladala Makonda.

Kwani Makonda kafanyaje?
Nilipofuatilia zaidi wengi wa washangiliaji wake wanasema kuwa Makonda ndiye Mtetezi wao, Makonda ndiye Magufuli wao.
Kwamba kwa nchi hii Watanzania waliowengi wanamchukulia Magufuli ndiye Masihi na sasa mrithi wake ni Makonda. Hayo ni mawazo na mtazamo wa watanzania hasa wa hali ya chini ambao ni zaidi ya asilimia 80 hivi.

Sio Chadema, sio ccm, sio Act hakuna mwanasiasa mashuhuri na mwenye ushawishi kwa Tanzania kumzidi Makonda. Hii inamaanisha nini? Kama hali itaendelea hivi basi Watu wataanza kumpenda na upendo siku zote uko na nguvu kuliko Mauti.

Ingawaje mimi sio mfuasi wa siasa za Makonda lakini nikiri kwa ukweli kuwa yeye ndiye amebeba kwa sasa siasa za nchi yetu. Jina lake likiwa kubwa na lenye kuandikwa na kusemwa na waliowengi.

Wasalamu
 
Mheshimiwa Paul Makonda ndiye mtetezi wa wanyonge ndiye Sauti ya watanzania,kinywa cha Mh Makonda kinazungumza kwa niaba ya mamilioni ya watanzania. Mh makonda ndiye aliyebeba matumaini ya vijana na watanzania ambao wameamua kumpeleka ikulu kwa kishindo ifikapo mwaka 2030.
 
Ngoja niulize tena, hivi wanajf huwa mnaishi mtaa gani maana sometimes mnaongea vitu ambavyo hata sijaexperience hata kwa kuvihisi

Hata hivyo sijui mwanasiasa gani kwa sasa anapata kiasi kile kile cha attention & admiration alichopokea magufuli. Na kama kuna kitu kipo maarufu kwa sasa mtaani bhasi haijaizidi TANESCO, SUKARI na KIFO CHA MAGUFULI
 
Ndio nature ya siasa zetu, wapo wanaomtaja Makonda kwa namna ya kumsifia kwa kile anachofanya, na wapo wanaomtaja Makonda kwa namna ya kumponda kwa kile anachofanya, mwisho wa siku wote tunajikuta tunamtaja Makonda.

Ili kuja kumuondoa Makonda relini, lazima wapinzani waje na tukio lao kama maandamano wanayotarajia kuyafanya, lakini kwa sasa, Makonda ndie ana trend.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Makonda yeye anachokifanya anatumia Magufuli style ambayo watanzania wengi(nazungumzia kajamba nani) ndio wanapenda
 
Ngoja niulize tena, hivi wanajf huwa mnaishi mtaa gani maana sometimes mnaongea vitu ambavyo hata sijaexperience hata kwa kuvihisi

Hata hivyo sijui mwanasiasa gani kwa sasa anapata kiasi kile kile cha attention & admiration alichopokea magufuli. Na kama kuna kitu kipo maarufu kwa sasa mtaani bhasi haijaizidi TANESCO, SUKARI na KIFO CHA MAGUFULI

Kwani wewe unaishi wapi Mkuu?
Kama unaishi hapa nchini na sehemu Watu wanaongea kiswahili basi utaelewa kuwa kwa sasa Makonda yupo namba moja kisiasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom